Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonya kuwa tabia ya baadhi ya waajiri nchini kuwalipa mishahara kidogo wafanyakazi wao itazua migogoro kati yao...
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonya kuwa tabia ya baadhi ya waajiri nchini kuwalipa mishahara kidogo wafanyakazi wao itazua migogoro kati yao na wafanyakazi wao.
Amesema kuwa ni jambo la kushangaza kuwa waajiri wanawakabidhi wafanyakazi mashine za mamilioni ya fedha, ili wazilinde na kuzitumia, lakini wakati huo wanawalipa mishahara “kiduchu”.
Rais Kikwete ametoa onyo hilo leo, Jumapili, Oktoba 26, 2008 wakati alipokagua kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha New Tabora Textille Mills cha mjini Tabora, na kuzungumza na wafanyakazi na uongozi wa kiwanda hicho, katika siku ya nne ya ziara yake ya siku nane mkoani Tabora kukagua shughuli za maendeleo.
Rais Kikwete ameuambia uongozi wa kiwanda hicho: “Ni jambo gumu kidogo kueleweka hili. Mnawakabidhi wafanyakazi wenu mashine na mitambo ya mamilioni ya fedha, lakini bado mnawalipa mishahara kiduchu.”
Amesema Rais: “Msibane maslahi ya wafanyakazi. Mnaweza kuwalipa mishahara kidogo kwa muda, lakini hatimaye hili litawaingiza katika migogoro na wafanyakazi wenu wenyewe.”
Hata hivyo, Rais ameusifia uongozi wa kiwanda hicho kwa kuonyesha mfano wa nini kinatakiwa kufanywa na viwanda vya nguo nchini.
“Nashukuru na kuwapongeza sana kwa sababu nyie mmeonyesha mfano. Tusiishie kwenye kuchambua pamba tu, tusiishie kwenye ginnery tu. Hatua inayofuata sasa ni kutengeneza nyuzi na hatimaye kutengeneza nguo hapa hapa nchini,” amesema Rais na kuongeza:
“Kwa sababu tunaposafirisha na kuuza pamba nje, tunachofanya ni kumpelekea malighafi mwenye kiwanda kama hiki hiki cha hapa.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Tusijisifie kwa uhodari wa kuwa na viwanda vingi vya nguo na kuuza pamba yetu nje ya nchi. Tuanze sasa safari ya kutengeneza nguo. Lazima tuongeze thamani kwenye malighafi yetu. Nyie mnajua kuwa kilo mbili tu za pamba zinatengeneza shati moja?
Uongozi wa kiwanda umesifia sera za ubinafsishaji na kusema kuwa bila sera hizo, kiwanda hicho kingeendelea kufungwa hata kama mpaka sasa kinazalisha kwa asilimia 50 tu ya uwezo wake.
Kiwanda hicho kilichojengwa mwaka 1981 kikiwa kiwanda cha umma, kilifungwa mwaka 1981 kutokana na matatizo ya menejimenti. Hakikufunguliwa tena hadi mwaka 2004, kiliponunuliwa na watu binafsi.
Tokea wakati huo zaidi ya dola za Marekani milioni tatu zimewekezwa katika kiwanda hicho ambacho kinaajiri watu 355 ambao wanafanya kazi kwa shifti tatu. Kiwanda hicho kinatumia kati ya marobota 900 na 1,000 ya pamba.
Mpaka sasa kiwanda hicho kinasafirisha nyuzi kwenda Italia, Ureno, Uturuki, Colombia na China. “Tunaishukuru Serikali kwa kutuwekea mazingira mazuri yanayotuwezesha kuendelea na uzalishaji katika kiwanda chetu.
Baadaye leo, Rais amezidua mradi wa josho na lambo la maji kwa ajili ya binadamu na mifugo na hata kufungia samaki katika kijiji cha Imalamihayo, nje kidogo ya mji wa Tabora.

COMMENTS