Wanafunzi wa Nyerere tumepotoka, tumemsahau! LEO Watanzania tunatimiza miaka tisa tangu kuondokewa na kiongozi wetu mpendwa Baba wa Taifa, H...

Wanafunzi wa Nyerere tumepotoka, tumemsahau!
LEO Watanzania tunatimiza miaka tisa tangu kuondokewa na kiongozi wetu mpendwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Tunasema kiongozi mpendwa kwa sababu tangu alipotangaza kung’atuka katika uongozi wa nchi na baadaye katika Chama Cha Mapinduzi alichokiasisi, bado aliendelea kuwa baba aliyekemea pale alipoona mambo hayaendi vizuri.
Ni kiongozi mwenye sifa nyingi, lakini kubwa ni ile sifa ya kutopenda makuu. Licha ya madaraka makubwa aliyokuwa nayo, lakini maisha yake yalionekana ya kawaida hivyo kumfanya afanane na wananchi aliowaongoza.
Ndio sifa inayofanya hadi leo Watanzania tuendelee bado kumkumbuka hasa katika kipindi hiki ambacho macho yetu yanashuhudia maadili katika jamii, wakiwamo viongozi wetu, yakiwa yamemong’onyoka.
Viongozi wetu wamepotoka na hata zile tambo za kuahidi kumuenzi mwasisi huyo wa taifa ambazo tulizitoa mbele ya jeneza lake na hata kando ya kaburi lake hazionekani na zimetoweka katika matendo yao.
Leo hii jamii imeshuhudia baadhi ya viongozi wetu na watumishi waandamizi wa umma wakijilimbikizia mali kwa tamaa zao na wengine wamediriki kuiingiza nchi katika mikataba mibovu kwa tamaa na uroho wao wa kutajirika haraka bila kujali athari ambazo taifa litapata.
Vitendo hivi vya kutia aibu enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere hatukuviona na hiyo inatokana na yeye kuipenda nchi yake kwa moyo wake wote na kufanya kila jambo alilofanya atangulize mbele zaidi maslahi ya taifa yake badala ya maslahi binafsi.
Tunapoadhimisha miaka tisa ya kuondokewa na kiongozi huyu ambaye ameendelea kuwa taa yetu katika kipindi hiki cha giza, tunawasihi viongozi wetu waiangalie taa hii iwaangaze na pale wanapoona hawaendani na mafundisho yake waweze kujirudi.
Tunaomba wajirudi ili taifa hili changa aliloliasisi miaka 47 iliyopita liweze kupiga hatua kubwa ya maendeleo.
Tunataka kuona kwa vitendo wanafunzi hawa wa mwalimu wanavyoipigania nchi yao kama ilivyokuwa kwa mwasisi huyu wa taifa letu, ili ile ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuifanya Tanzania iwe moja ya nchi zinazokimbia katika kujiletea maendeleo yake yenyewe iweze kufikiwa.
Tutafikia hatua hii iwapo viongozi wetu, na sisi wengine wote, tutaacha tamaa na uroho wa kujilimbikizia mali na jamii kuichukia rushwa kama alivyoichukua Mwalimu Nyerere.
Viongozi waonyeshe njia na tuonekane kweli kuwa sisi ni wanafunzi wake watiifu tuliofundwa kuichukia rushwa na vitendo vingine vyote ambavyo vinachangia kurudisha nyuma maendeleo yetu.
ends

katuni hii ni ya Fadhili
COMMENTS