Wengine zaidi wadakwa kwa maafa ya Tabora
WATU wengine wawili wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na tukio lililosababisha vifo vya watoto 19 waliokufa wakati wanacheza muziki siku ya Idd Mosi.
Polisi walisema leo kuwa waliokamatwa ni Meneja wa disko la One Ten Teck Jaffar Rashid na Meneja wa Bubbles Night Club, Vituko Salala. Kabla ya kukamatwa kwa mameneja hao, Polisi waliwakamata wamiliki wa madisko hayo ambao ni Projestus Fidelis na Shashikant Manji Patel.
Kwa mujibu wa vyombo vya dola watu hao ndio waliandaa disko la watoto katika siku hiyo ya Idd.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa, alisema leo kuwa wakurugenzi hao na mameneja wanashikiliwa na polisi kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu chanzo cha tatizo lililosababisha watoto hao kupoteza maisha.
Alisema Polisi imempa taarifa rasmi ya kushikiliwa kwa watu hao, huku ikimuarifu kwamba walinzi wa milangoni katika madisko hayo mawili "Mabaunsa" nao wanasakwa ili waweze kuhojiwa kuhusu sakata hilo.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema wakurugenzi hao, watahojiwa pia na Tume huru iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza mkasa huo, ambayo alisema ilianza kazi leo na kuwataka wananchi waipe ushirikiano ili iweze kupata taarifa za ukweli zitakazofanyiwa kazi na serikali.
Juzi watoto 19 walikufa dunia na wengine kulazwa hospitali ya Kitete baada ya kukosa hewa katika kumbi za disko wakatik wa sherehe ya idd.
Sherehe za Idd hufanyika kuadhimisha kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani.


0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
Links to this post:
Create a Link
<< Home