KELELE, nderemo na milio ya honi magari vilifunika anga la Dar es Salaam baada ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kupata ...
KELELE, nderemo na milio ya honi magari vilifunika anga la Dar es Salaam baada ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya watani wao wa jadi Simba baada ya ukame wa miaka kibao.
Bao la mapema la Mkenya, Benard Mwalala lililojazwa wavuni dakika ya 16 lilitokana na krosi safi ya mchezaji wa zamani wa Simba, Athumani Iddi. Mpira uliozaa bao hilo ulianzia kwa mfungaji hodari wa Yanga Boniface Ambani.
Mara ya mwisho Yanga kuibuka na ushindi dhidi ya Simba ni Agosti 5 mwaka 2000.
Pamoja na mchezo bomba, mchezo huo ambao ulishuhudia kadi tatu nyekundu zikitolewa na mwamuzi Victor Mwandike.
Mchezaji wa Simba Haruna Moshi ‘Boban’ alikuwa wa kwanza kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 63 kutokana na kumpiga kiwiko mchezaji mmoja, wakati mfungaji wa bao pekee la Yanga Mwalala naye alionyesha kadi hiyo dakika 72 Wakati akiondoka uwanjani ili kumpisha Kigi Makasi lakini alijichelewesha na kumsababisha beki wa Simba Meshack Abel kumsukuma hivyo wote kutolewa kwa kadi nyekundu.
Hali hiyo ilisababisha Simba kumaliza mchezo wakibaki uwanjani wachezaji 8 na Yanga 10, pamoja na kubaki pungufu Simba bado walionekana kucheza na kusaka bao la kusawazisha lakini wachezaji wake Musa Hassan ‘Mgosi’ alipoteza nafasi kadhaa za wazi za kufunga pamoja na Nico .

Katika hatua nyingine mchezo huo wa watani hao wa jadi leo ulijaa vitendo ambavyo vilikuwa vinashiria imani za ushirikina na kupelekea mpira kusimama kwa dakika kadhaa pale mchezaji wa Simba Ulimboka Mwakingwe kwenda golini mwa Yanga na kutoa vitu na kuvitupa nje na kuibua mayowe kwa mashabiki wa Simba na kufanya wapiga picha kukimbilia kupiga picha vitu hivyo.
Na kabla ya mpira kuanza Simba ilingia kwa staili ya aina yake pale Mwenyekiti wa timu hiyo aliongoza na mchezaji Mgosi na kwenda moja kwa moja kwenye goli moja huku akipiga danadana.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo kocha wa Yanga, Dusan Kondic alisema kuwa timu yake ameridhishwa na kiwango cha timu yake na ushindi wa bao 1-0 unatosha baada ya kuwa katika shinikizo kubwa la kutakiwa kushinda kutoka kwa viongozi na mashabiki wa klabu hiyo ambayo imekuwa ikifungwa kwa muda mrefu na Simba.
Wakati kwa upande wa Simba , kocha Benzink alisema mchezo ulikuwa mzuri na kikosi chake kilicheza vizuri mno na kupata nafasi nyingi za kufunga lakini washambuliaji wake walishindwa kuzitumia na wapinzani wao walitumia nafasi hiyo moja ya shambulizi la kushtukiza kupata bao ambalo limewafanya waibuke na ushindi.
Aidha kocha huyo alisema hakuwatumia wachezaji wa timu hiyo kutoka Nigeria Orji Obina na Emeh Izechukwu kutokana na wachezaji hao kutofanya mazoezi kwa sababu ambazo hazijui.

Pichani ni Ulimboka na George Owino wakichuana vikali. Habari kwa hisani ya Betram Lengama ambaye alikuwa uwanjani na picha ni ya Bongo Pix
COMMENTS