RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume amesema kuwa juhudi zinazofanywa za kuimarisha miundombinu...
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume amesema kuwa juhudi zinazofanywa za kuimarisha miundombinu ya bandari ya Zanzibar zina lengo la kuwasaidia wananchi kupata ajira pamoja na kuinua uchumi wa nchi yao.
Rais Karume aliyasema hayo leo huko katika Bandari ya Malindi mjini Zanzibar mara baada ya kuzindua vifaa vya shughuli za bandari ikiwemo tagi pamoja na vifaa vya kuchukulia na kunyanyulia makontena bandarini.
Katika maelezo yake Rais Karume alisema kuwa hatua iliyofikiwa hivi sasa bandarini hapo ni nzuri na itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha shughuli za bandari na kazi kubwa iliyobaki hivi sasa kwa Shirika la Bandari ni kutafuta wateja.
Alisema kuwa mbali ya kuimarika kwa huduma za bandari pia suala la ajira nalo litachukua nafasi yake kwa kuongezeka na kuwasaidia wananchi kwa kiasi kikubwa.
“Sasa bandari tunayo na vifaa tunavyo, lililopo hivi sasa ni kwa Shirika la Bandari kutafuta wateja kwa ajili ya kuimarisha shughuli za bandari”,alisema Rais Karume.
Rais Karume pia alisisitiza utunzaji wa vifaa hivyo na vile vya zamani ili viweze kuchukua muda mrefu na kuweza kusaidia shughuli za bandari.
Pamoja na hayo, Rais Karume aliutaka uongozi wa Shirika la Bandari kuandaa programu maalumu kwa ajili ya mafundi wa vifaa vya bandarini hapo kwa lengo la kupata mafunzo ya ndani na nje ya nchi ili wapate kuwa na ujuzi zaidi wa kufanya kazi zao.
Katika maelezo yake kwenye uzinduzi huo, Rais Karume alisema kuwa ujenzi wa bandari sanjari na vifaa vilivyopo hivi sasa kutawasaidia wafanyabiashara kuleta mizigo yao moja kwa moja hapa Zanzibar badala ya kupitia bandari nyengine.
Rais Karume alieleza kuwa pia alitoa changamoto kwa wale wote waliokuwa na imani ndogo ya kuona kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haitakuwa na uwezo wa kujenga bandari sanjari na kununua vifaa kwa ajili ya kuendeshea shughuli za bandarini.
Kutokana na hali hiyo, Rais Karume alisisitiza haja ya kuwa na subira na kueleza kuwa juhudi za makusudi zimekuwa zikichukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha huduma za maendeleo.
Sambamba na hayo, Rais Karume alitoa pongezi kwa Shirika la Bandari kwa kujenga na kuiimarisha bandari hiyo siku hadi siku.
Mapema Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Machano Othman alieleza kuwa hatua za utendaji bandarini hapo zimeimarika ambapo hivi sasa shughuli za uteremshaji makontena bandarini hapo hazichukui zaidi ya siku tatu.
Pia, Waziri Machano alimuhakikishia Rais Karume kuwa vifaa hivyo vitatunzwa ili vidumu na kuweza kufanyiwa kazi kwa muda mrefu.
Alieleza kuwa kuimarika kwa huduma bandarini hapo kumepelekea meli nyingi kuja moja kwa moja badala ya kupitia katika bandari ya Dar-es-Salaam na Mombasa.
Waziri Machano pia aliwataka wafanyabiashara wanaoshusha makontena yao bandarini hapo kutoyaacha kwa muda mrefu na kuifanya bandari kuwa ghala la kuhifadhia mizigo na badala yake waweze kuchukua juhudi ya kuitoa mapema mizigo yao.
Waziri Machano alieleza kuwa vifaa hivyo vimenunuliwa na Shirika la Bandari kupitia mkopo wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).Vifaa vyote kwa pamoja vina thamani ya zaidi ya Shilingi za Tanzania Bilioni 3.7.
Utengenezaji wa Mradi wa ujenzi wa Gati ya Malindi ulianza Julai, 2005 na kukamilika Novemba 2008 chini ya Ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya.
Katika hafla hiyo viongozi mbali mbali wa chama na serikali walihudhiria ambapo Rais Karume alianza uzinduzi kwa kuizindua Tagi mpya iliyotengenezwa na Kampuni ya Damen Shipyards ya Uholanzi na baadae alizindua vifaa vya kuchukulia na kunyanyulia makontena ambavyo vimetengenezwa na Kampuni ya Kalmar ya Sweden.

Pichani Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume,akizungumza na Balozi Mpya wa Indonesia Nchini Yudhistiranto Sungadi,aliyekuja kwa ajili ya kujitambulisha Ikulu Mjini Zanzibar jana.(Picha na Ramadhan Othman).stori ni ya Ikulu Zenj
COMMENTS