Hizi ni ngano za Feruzi na la maana ni ulemavu inakuwaje hatuwekezi huko? soma zaidi

LINI TUTAKUMBUKA KUWEKEZA KWENYE MICHEZO YA WATU WENYE WENYE ULEMAVU? Juzi ilikuwa ni siku ya walemavu duniani. labda uwe na roho ya chum...

LINI TUTAKUMBUKA KUWEKEZA KWENYE MICHEZO YA WATU WENYE WENYE ULEMAVU?




Juzi ilikuwa ni siku ya walemavu duniani. labda uwe na roho ya chuma ndio usingegusswa na yale waliyoyasema. Niliona maadhimisho ya Kibaha kupitia luninga, wakasema hawakumuona kiongozi yoyote yule! Hapa Dar nilimuona Mheshimiwa Margareth Mkanga, Mbunge anayewakilisha watu wenye ulemavu akizindua kitabu chenye Jina la WALIOSAHAULIKA. Nikakumbuka michezo, nikamkumbuka kauli ya Mheshimiwa Bendara aliyoitoa kuhusu michezo kwa wenye ulemavu, nikapata simanzi! Hii ni hoja pana sana.
Nakumbuka siku mpaka tarehe, ilikuwa ni machi, 27 mwaka 2007 wakati Tanzania ilipopokea msaada wa shilingi milioni 26 kutoka Uingereza ikiwa ni sehemu ya ufadhili wa shilingi milioni 61 zilizopangwa kwa ajili ya kuhamasisha na kuendeleza michezo kwa watu wenye ulemavu kwa watu wa njii hii kwa miaka 4 (2006 hadi 2010). Msaada huo umetolewa na Baraza la michezo la Uingereza. British Sports Council. Wenyewe hapa wala habari hatuna.
Nakumbuka pia katika kupokea msaada ule Naibu waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Joel Bendera, (MB) aliishukuru sana Uingereza na kusema kwa msaada ule ungetumika kununulia vifaa vya michezo kwa timu za wenye ulemavu. Hii ni kweli kwa sababu timu nyingi zina ukosefu wa vifaa acha za wenye ulemavu hata za hao walemavu watarajiwa nazo nyingi ziko taabani.
Tunaileta hoja ya umuhimu wa kuwasaidia wanamichezo walemavu kwa kunukuu kauli ya Mheshimiwa Bendera aliyoitoa miaka miwili iliyopita kuwa Watanzania tubadilike tabia na kusaidia au kuwekeza kwenye michezo kwa wasiojiweza. kweli ni nadra sana kupata misaada kama hii. Nakumbuka Mheshimiwa Bendera alisema, sisi (watanzania) mara nyingi kunakwepesha kuingiza fedha zetu kwenye michezo kwa wetu wasiojiweza aghalabu wenye ulemavu. (Hapa niwafundishe kiswahili, neno aghalabu maana yake ni, mara nyingi. Wasukuma wenzangu wa ushirombo wanaposema agalabu huwa wanafikiria wamesema nadra aaah nawasamehe. Kwanza treni zenyewe zimegoma).
Turudi kwenye hoja yetu pana. Pamoja na ukweli kuwa kila mwenye fedha yake anao uhuru wa kuchagua wapi asaidie. Uzoefu unaonesha kuwa wanaosaidia huwa wanatoa misaada ya masharti au kutegemea kitu fulani. Japokuwa huwa haisemwi moja kwa moja lakini ukiangalia kwa hoja pana utaiona tuu! Utaona mathalani mfadhili fulani anadhamini shughuli fulani kwa maganga feruzi ili kesho safu ya hoja irudishe fadhila. Mungu apishie mbali!! Mambo ya posho mbili. Wadhamini kama hao hawawezi kwenda kwa wenye ulemavu kwa sababu wale masikini ya Mungu hawana cha kurudisha zaidi ya dua. Wafadhadili wa aina hiyo wao na mambo ya dua ni mbali mbali. Ashakum kama nimegusa pabaya. Bora iwe hivyo kuliko mguso wa kitabu cha WALIOSAHAULIWA! Kweli tunaweza watanzania wenzangu kuwa tumefika hapa?
Niliwahi wakati fulani kuongea na Komredi Iddi Kibwana, tuliongea kwa njia ya simu. Ilikuwa mwaka 2006 akaniambia mambo mazuri kweli na mipango ambayo Paralyimpics inayo. Paralyimpics ni chama cha michezo kwa wenye ulemavu ambacho ni cha kitaifa lakini kinachofanya shughuli za michezo mpaka ngazi ya mikoa kwa watu wenye ulemavu. Wakati ule aliniambia kuwa walikuwa na mpango wa kuipeleka timu ya taifa Algeria na baadaye akaniambia jinsi michezo ya Kanda inavyoendesha na Waingereza hasa kupeleka michezo mashuleni. Nilifarijika. NILISAHAU?
Zamani pale uwanja wa Uhuru (Taifa zamani) ilikuwa kabla ya mechi ya Ligi kuu kuanza kulikuwa na siku ambapo kulikuwa na mechi za utagulizi kwa watu wenye ulemavu. Ilikuwa mechi nzuri zinazovutia. Alipoondoka kakangu Fred Macha pale, zile mechi zikafa kabisaaa na watu WAKASAHAU. Sasa hivi Fred Macha yupo Wizarani na anaendelea na juhudi za kutafuta wafadhili na misaada kwa ajili ya walemavu. Mara ya mwisho nilipokutana naye ilikuwa ni wakati alipokuwa akitafuta fedha kwa ajili ya michezo kwa watoto wenye mtindio wa ubongo. Sijui kama alifanikiwa. NILISAHAU kumuuliza.
Sitaki kusema mimi binafsi nimefanya nini kuhusu kuchangia au kushauri kuhusu michezo kwa ajili ya wenye ulemavu lakini nimeeleza baadhi ya mambo ambayo nilipaswa kuyafanya lakini NILISAHAU kuyafanya. Wenye ulemavu wanaposema WALIOSAHAULIWA tukubali udhaifu huo lakini tusiwasahau tena! Hii ni kweli.
Hujafa hujaumbika. Hata kama hali hiyo isingekuwepo, bado watu wenye ulemavu ni ndugu, jamaa na rafiki zetu. Wanahitaji faraja na kuburudika kama wanajamii wengine. Mungu asipokupa hili anakupa jingine. Kuna watu wenye ulemavu wana vipaji vikubwa tu katika michezo na wanaweza kuiletea sifa nchii hii. WALISAHAULIWE. Tumengangania kuwekeza kwenye maudhi ya timu zinazofungwa kila siku? Tubadilike. Tuwekeze kwa wale ambao tunajua wanahitaji msaada lakini pengine hawana sauti za kutufikia au hawajui hata kuandika mchanganuo wa mapendekezo na hakuna wa kuwaandikia. Wenye ulemavu wanahitaji fursa tu! Tuwasaidie kwenye michezo kwa ufadili na vifaa ili wafanye mambo.
Machi 12 hadi 21, 2010 dunia itashuhudia michezo ya paralyimpics kwa watu wenye ulemavu itakayofanyika majira ya baridi huko vancourver Kanada. Sina uhakika uhakika wa uwakilishi wa Tanzania katika michuano hiyo ikoje au utakuwaje? Au tumeshindwa kwa sababu ya kukosa mambo muhimu?
Kama mashirika na makampuni yetu yaliyopo yataamua kutoa kiasi kidogo kwa ajili ya kusaidia michezo kwa ajili ya watu wenye ulemavu, nina uhakika tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika kuwainua wanamichezo hawa hapa Tanzania. Niliwahi kushuhudia kupia luninga jinsi watu wenye ulemavu wanavyoweza kutimua mbio kwa kasi ya ajabu hata kushinda wenye miguu na mikono miwili. Nilitamani wanariadha hao kama wangekuwa watanzania.
Michezo ni ajira. Ipo michezo mingi ambayo wenzetu wenye ulemavu wanaweza kuicheza. Kuna kurusha visahani, kurusha vitufe, mikuki, mbio, kunyanyua vitu vizito na kadhalika na kadhalika. Kama Muingereza aliyetutawala bado anakumbuka kutusaidia kwenye hili, seuze sisi ambao sasa ni taifa huru! Inawezekana hoja hii isiwe nzuri sana wala kuvutia lakini habari ndio .magangaferuzi@gmail.com

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,287,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7057,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,739,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,9,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Hizi ni ngano za Feruzi na la maana ni ulemavu inakuwaje hatuwekezi huko? soma zaidi
Hizi ni ngano za Feruzi na la maana ni ulemavu inakuwaje hatuwekezi huko? soma zaidi
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2009/12/hizi-ni-ngano-za-feruzi-na-la-maana-ni.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2009/12/hizi-ni-ngano-za-feruzi-na-la-maana-ni.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy