KILA mtu anakuwa na sababu kwanini anaanzisha kitu fulani katika maisha yake.Nyingi ya sababu ni kutokana na kukutwa na hali fulani au kuona...

KILA mtu anakuwa na sababu kwanini anaanzisha kitu fulani katika maisha yake.Nyingi ya sababu ni kutokana na kukutwa na hali fulani au kuona hali fulani ambayo haipendi.Adam Kagoye mzaliwa wa Busoka mtaalum wa masuala ya kibenki, uhasibu na utawala alikuwa na kila sababu ya kuachana na shughuli hizo na kujikita katika kutoa elimu. Lukwangule ilizungumza na mtaalumu huyo na kuona kisa kilichompeleka kuwa mjasiriamali.
CYBERTWIGA ilikuwa shughuli yangu ya kwanza ya kutoa huduma ya kielimu kwa watu ni katika hili nilitambua haja kubwa wanayohitaji watanzania, elimu ya kutosha kuweza kuendesha mambo na kuyachambua kutoka katika umri mdogo, Anasema Adam kagoye ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 46 na bado kijana.
CyberTwiga walikuwa ni watu wa kwanza nchini kutoa huduma za mtandao wa kompyuta nchini, watu ambao walifungua njia kwa namna moja au nyingine ya kuwaambia Watanzania angalieni hiki kilichopo na tazameni wenzetu wanavyonufaika navyo.
Katika kampuni hii Adam alikuwa mkuu wa fedha na utawala, hali ambayo ilitokana na ukweli kuwa ni mtaalum wa benki ambaye ana digrii ya benki na fedha kutoka Italia.
Akiwa amezaliwa Busoka, Kahama mkoa wa Shinyanga na kuchukua elimu yake ya sekondari katika shule ya sekondari ya Kibaha, shule ambayo hata Rais wetu Jakaya Kikwete nako alipitia.
Alichukua diploma yake ya uhasibu katika chuo cha maendeleo ya jamii cha Nyegezi(NSTI) ambayo sasa ndiyo chuo kikuu cha wakatoliki cha St Agustine, kabla ya kuondoka nchini kwenda Italia wka elimu ya juu zaidi katika masuala ya benki na uhasibu.
Kagoye amesema ana historia ndefu sana katika maisha yake, historia ambayo imefungua na kuona tatyizo la watanzania wengi, tatizo la elimu ambayo haimbatanani na kasi kubwa iliyopo sasa katika maisha.
Ni hali hiyo iliyomfanya kubadili mwelekeo wake wa maisha na kufikiria kusaidia vijana wadogo kutoka katika msingi kwa kuzingatiazaidi masomo ya sayansi na utatuzi wa matatizo kwa ukomavu zaidi.
"Haikuwa rahisi kujiingiza katika shughuli za elimu, " anasema Adam ambaye uzoefu wake na uendeshaji wa makampuni mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yalimpa mashaka juu ya uwezekano wa kuwa na shule ambayo anaitaka yeye, shule yenye mwelekeo wa kompyuta na stadi za kisayansi.
"hatuna watu wanaojua kuwa komyuta ndio jibu la sasa, ukiweza kutoa watoto wanaoweza kujua matumizi ya teknolojia unaweza kuwa umepiga hatua moja kubwa zaidi katika kuleta hali njema kwa watoto" amesema huku akionyesha dishi kubwa ambalo linatumika kupokea taarifa mbalimbali za dunia kupitia mtandao wa komyuta-intaneti-.
Alikuwa na uzoefu wa kutunza fedha, kushauri katika masuala ya fedha, alikuwa na uhakika kwamba asiposimamia mwenyewe kitu anachotaka kuwa haitakuwa Rahisi sana.
kagoye ambaye ameshapitia taasisi mbalimbali za fedha ikiwemo benki kuu alitumia uzoefu wake mkubwa katika masuala hayo na uendeshaji wa kampuni kubwa ya kununua dhahabu kwa wachimbaji wadogo na kuuza kwa mashirika ya kimataifa kujipeleka katika elimu, kazi inayohitaji uvumilivu na uangalifu mkubwa.
"uwekezaji wa elimu si lelemama, makosa kidogo unaweza kujuta hasa ukitambua kwamba dhamana unayobeba ya kufunza watoto ndio dhamana ambayo hata kwenye Biblia imeandikwa" anasema Adam ambaye pia ni mzee wa kanisa.
Alipoachana na kampuni ya kununua na kuuza dhahabu ya Zahav Trading Limited iliyokuw ana leseni ya Gold master dealer akiwakama afisa mtendaji mkuu akishughulika na manununuzi yua dhahabu, kuzitayarisha na kuziuza nje, alijirejesha kijiji kimoja nje ya Dar es salaam , Mbezi Luisi katika eneo la Msigani na kutulia kufikiria nini kinachoweza kufanyika.
Haraka sana alifikia uamuzi wa maisha aliyotamani, kuchonga watu wapya wenye uelekeo mpya na kasi mpya ya maisha, watoto.
Alitengeneza shule kwa fedha zote alizonazo, akaiibua kutoka katika ndoto zake na kuiweka kweli miaka mitatu iliyopita,Shule ya Sekondari ya Msigani iliyopo Mbezi, nje kidogo ya jiji la dar es salaam ukichepuka kidogo tu kutoka barabara iendayo Morogoro.
"Nilikuwa hapa na ile dhamira yangu ya kuwa na eneo la kufunza watoto kwa namna ninavyofikiria bora ikajikita zaidi... " anasema akitabasamu.
"Nilitamani eneo hili kuwa na shule yake na ndio maana shule hii ya sekondari unayoiona niliamua kuipa jina la kijiji, ikibeba dhamana kubwa ya kuwafanya wazazi wa hapa kusomesha watoto wao" alisema.
Kwa marafiki zake, Adam kuwa na wito wa kufunza watoto kwa namna anavyofikiri kuwa bora, ni kitu ambacho hawakishangai.
Wakati fulani unafikiria kwamba huyu mtu alistahili kuwa padri, si kwa upole wake bali kwa fikira nyingi kuhusu dhana nzima ya maendeleo duniani kwa kuanzia kuelimisha kizazi kilichopo na kile ambacho kinaandaliwa kuendeleza kijacho.
Maneno ya hapo juu si yangu ni ya Robert Kadago , mmoja wa wanafunzi waliokuwepo nyegezi wakichukua diploma ya uandishi wakati Adam anasoma uhasibu.
Je atarudia kazi ya uhasibu?
"sidhani?" anasema Kagoye wakati akijibu swali la kama anaweza kurejea katika taaluma yake na kufanya kweli katika muda huu ambapo biashara ya benki ni nzuri zaidi.
Aanasema ameamua kuwa katika elimu, ataendelea huko kwani anaona anafanyakazi ambayo moyo wake unaridhika na kuifurahia daima.
Pamoja na furaha ya moyo wake, mpangilio wa kuendesha shule si rahisi kama kutoa taarifa za kibenki na mipangilio ya kiutawala ya kibenki, unatakiw akujua mzunguko na kuangalia mahitaji ya watoto kwa namnba ambavyio watafurahia masomo yao.
"Wengi wa wanaokuja hapa wana msingi mbovu kabisa, tunachofanya ni kuwapika, kuwaingiza katika teknolojia mpya ya matumizi ya kompyuta na kuwapa muda wa kutosha wa kuogelea huko" anasema.
Aidha alisema usumbufu mkubwa upo katika wanafunzi kuelewa mustakabali wao katika dunia iliyojaa mipangilio ya kuzidiana, mipangilio ya utandawazi.
Msigani iliyopata hati ya usahili no s.1438 ni tunu yake kwa vijana wanaotaka kuchanja mbuga katika sayansi, anahusudu sayansi na yeye anaingalia juhudi yake hiyo mpya kama mboni.
Pengine bila ya yeye kujua zao hili la Sengerema sekondari,limeamua kufanyakazi isiyoheshimika waziwazi, kazi ya kuandaa viongozi wa baadaye wa taifa hili la Tanzania.
Akiwa ni baba wa familia Kagoye kama watawala wengine duniani bado anapata muda wa kuwa na familia yake kwa maana ya kwamba anaielekeza na kuipatia muda wa mapenzi yake kwao.
Aidha yeye mwenyewe naye anapata nafasi pia ya kuendeleza kipaji chake cha mahesabu kwa wale wanaohitaji msaada.
Kwa habari ya shule hii fungua hapa
COMMENTS