KAMPENI ya kuhamasisha mawasiliano mazuri kwa watu waliopo kwenye mahusiano hasa wake na waume zao, imeanza kwa mafanikio makubwa katika mik...
KAMPENI ya kuhamasisha mawasiliano mazuri kwa watu waliopo kwenye mahusiano hasa wake na waume zao, imeanza kwa mafanikio makubwa katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ikIhusisha baadhi ya wasanii wa bongo fleva, PNC na Betreace.
Baada ya kupata mafanikio makubwa mkoani Mbeya wiki iliyopita, kampeni hiyo iliyopewa jina la Champion ilianza kwa kishindo mkoani Njombe katika wilaya Njombe na juzi na jana ilifanywa mkoani Iringa katika wilaya za Mufindi na Iringa.
Kwa kupitia kampeni hiyo, makundi mbalimbali ya kijamii yanafikiwa na kupata mrejesho wa moja kwa moja kutoka kwao juu ya jinsi kampeni hiyo inavyosaidia kutatua changamoto za mawasiliano katika kuboresha mahusiano yao, huduma za afya kama upimaji wa virusi vya Ukimwi, uzazi wa mpango na elimu ya afya ya uzazi na Ukimwi.
Katika uzinduzi wa kampeni hiyo mjini Iringa, uliofanyika katika ukumbi wa Neema Craft na hatimaye kumaliziwa kwa matamasha yaliyofanyika katika kata mbalimbali za manispaa ya Iringa, Afisa Mradi wa Champion, Dk Yelonimo Mlawa alisema kampeni hiyo yenye kauli mbiu ya Vunja Ukimya Zungumza na Mwenzio ina lengo la kuwahamasisha watu walio katika mahusiano kuwa na mawasiliano mazuri kwa lengo la kudhibiti uwezekano wa kuwa na wapenzi wengi na hatimaye kupunguza maambukizi ya Ukimwi.
Dk. Mlawa alisema wameamua kuzindua kampeni hiyo baada ya utafiti walioufanya kugundua kuwa wenza wengi hawapo wazi juu ya mahusiano yao jambo linalowafanya wawe na wapenzi wengi.
Alisema katika utafiti walioufanya waligundua kutokuwapo kwa mawasiliano mazuri kwa wenza ni sababu kubwa ya watu kutoridhishwa na kutokuwa na furaha katika mahusiano yao jambo linalowafanya wavitafute vitu hivyo sehemu nyingine ambapo ndiyo huwa mwanzo wa kupata maambukizi ya ukimwi.
Dk. Mlawa alisema katika utafiti huo walibaini watu wana hamu ya kuboresha mawasiliano ili kukuza uaminifu katika mahusiano yao kwani mawasiliano ni kiungo muhimu katika kuleta mafanikio.
Alisema kwa kupitia kampeni hiyo, ziara ya Champion itafanywa katika mikoa hiyo na mingine iliyopo katika kampeni hiyo ya Morogoro, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Pwani, Temeke, Ilala, Kinondoni, Lindi na Mtwara.
Alisema kampeni hiyo imeanza kwenye mikoa hiyo kwa kuzingatia viwango vyake vya maambukizi ya Ukimwi ikilenga kuhamasisha umuhimu wa mawasiliano, majadiliano na ushirikiano baina ya wanaume na wanawake katika kujaribu kuimarisha mahusiano, uaminifu na uwazi.
Dk. Mlawa alibainisha kuwa vyombo vya habari vitatumika katika kufikisha ujumbe kwa jamii ambayo inapaswa kuelewa na kutambua matatizo yanayosababishwa na kutokuwapo kwa mawasiliano.
Alisema Champion ni mradi wa miaka mitano wenye lengo la kuhamasisha mjadala wa kitaifa kuhusu majukumu na nafasi ya mwanaume na kuongeza usawa wa kijinsia ili kupunguza uwezekano wa wanawake, watoto na wanaume kuambukizwa Ukimwi na matatizo mengine ya afya ya uzazi.
Alisema mradi wa Champion unatekelezwa hapa nchini chini ya Shirika la EnderHealth kwa kushirikiana na Shirika la Academy For Edecational Development kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani (USAID).
SOURCE:IRINGA PRESS

COMMENTS