Mwishoni mwa wiki nilipata nafasi ya kutembelewa na kijana mmoja kutoka Unguja ambaye anajulikana kwa jina la Mohamed Juma Shaaban hapa ofis...
Mwishoni mwa wiki nilipata nafasi ya kutembelewa na kijana mmoja kutoka Unguja ambaye anajulikana kwa jina la Mohamed Juma Shaaban hapa ofisisini. Nilikuwa na muda mfupi nay eye lakini alinifanyia hisani ya kuniona baada ya kutoka Idara ya Maelezo kufanya uzinduzi wa kitabu chake cha mashairi kwa lugha ya kizungu.
Kutoka kwa baba na mama wanaocheza na namba (mhasibu na Mkaguzi) kuwa na mtoto ambaye anaondoka katika lugha kwa namna ambavyo Mohammed anafanya , inakupa swali ambalo huwezi kulipenda lakini lipo na nilimuuliza hii ni genetic malfunction au? Alicheka na kusema No, lakini hiyo ndivyo ilivyo.
Mohamed ambaye anasoma darala la 14 au tuseme kidato cha sita katika shule ya kimataifa ya High View akiwa anachukua masomo ya Historia, Kiswahili na Lugha wenyewe mnasema Language ni kijana ambaye ukimuona ghafla unaweza kusema hawezi kuthubutu, lakini ukiuona kazi yake utachoweza kusema ni kuwataka watanzania wengine wamuangalie kijana huyu na kukuza zaidi kipaji chake, amecheza vyema na mashairi yake.
Nilipata nafasi ya mwishoni mwa wiki kwa fasta kupitia kitabu chake cha mashairi yapatayo hamisni na shairi lililonikuna ni la Un Do Me This Hurt. Naam shairi la nama yake uwe unakiri au hukiri.Siwezi kukueleza kila kitu lakini ni vyema kukueleza kuwa kama hujui maana sina sababu yoyote ile ya kukujuza maana.
Nilitaka kujua kwanini ameamua kutunga mashairi ya kizungu. Hakusita kujibu... changamoto ya matumizi ya lugha na kujiueleza katika dunia ya utandawazi utamaduni ambao ni sehemu ya maisha ya mtu wa kawaida katika nchi ya kawaida kama Tanzania. Amepa fursa ya kuangalia maisha ya Watanzania kwa kutumia lugha ya kishairi na kutoa uwanja mpana wa wageni kuutambua utamaduni wa matanzania, mashaka na kuongeza fasihi ambayo bado ina kiu kubwa ya vitabu vya aina mbalimbali.
Ni changamoto kubwa upande wake na kwa taifa kwa ujumla, anasema, kwani kutoka kwa kitabu hicho kunatokana na ukaribu wake na familia ingawa anadhani pasi shaka yoyote kwamba vijana wakiwezeshwa wanaweza kufanya maajabu makubwa.
Kijana amaeogelea katika siasa, uchumi, maendeleo,jamii, na kitu ambacho vijana wengi wanacho ukali wa upanga katika mioyo ya watu kutokana na mapenzi, Un Do Me This Hurt ni mojawapo.
Lakini katika siasa kuna shairi moja nalipenda Non Is perfect. Amezungumzia viongozi waliopo na waliotangulia ambao wote wamekuwa wakisema wanajuhudi za kusaidia kuleta hali bora lakini kwa kukosekana kwa maarifa au pengine wka sababu za kibinadamu juhudi zao zimegonga. Kimsingi hajaridhika kabisa na uongozi na anatoa changamoto kubwa la uzingatifu wa ahadi.
Kuhusu jamii amesema suala la rushwa, Mayor of the Down Town ni wakilishi bora la ubazazi unaofanywa na viongozi na kukwamisha juhudi za kuinua uchumi na maendeleo ya Wananchi.Mohamed amesema wazi kwamba rushw ainayumbisha uchumi na huwezi kuw ana uchumi endelevu kwa watu kama rushwa inaendelea kutawala.
Nia ya kitabu hiki ukikitazama katika kioo cha kijana kutaka mabadiliko mazuri na kupiga hatua ya kuendeleza mbele kwa kuwa na viongozi bora na kuwapa sapoti vijana katika kutengeneza mustakabali wao kama viongozi si wa kesho bali wa leo katika kusukuma gurudumu la maendeleo.
Nilinunua kitabu chake kwa kupiga sapoti kuheshimu kitu alichokifanya, nilimuuliza beiu na akasema anaviuza kwa bei y ash 4000, nilikuwa na fedha yangu ya chakula cha mchana niliamua kukinunua kutokana na jinsi kilivyokuwa kitamu.
Kitabu hiki kw amujibu wa Mohamed kinapatikana Masomo Bookshop kule Zanzibar lakini kwa mtu anayekitaka anaweza kuwasiliana naye kwa e mail mohammedjuma2000@yahoo.com au simu 0714 460595 au kutembelea blogu yake mjcolections.blogspot.com .
Ameitaka serikali kuwakumbuka vijana na kuwawezesha ili waondokane na tabia za kukaa maskani hali inayowafanya kulewa upepo na kuanza matumizi yasiyosahihi ya dawa za kutibu maradhi makubwa ya saratani..
Akiwa anatarajiwa kumaliza kidato cha sita Februari mwakani (2011) katika shule hiyo ya kimataifa iliyopo Chukwani mkoa wa Mjini, wilaya ya Mjini magharibi amesomea shule ya msingi ya Mzinga ya Mombasa kuanzia shule ya awali ; amezaliwa mwaka 1990 mwezi Agosti 30 na anapenda sana tunzi za Mohammed Seif Kharibu na Shabaan Robert hasa kutokana na mashairi yaliyoshiba yanayogusa jamii.
Akiwa ni motto wanne kati ya watoto watano wa mzee Juma Shaaban Juma ambaye ni accountant na mama Fatma Mohamed Said ambaye ni Auditor general amesema anawashukuru wazazi na ndugu zake kwa sapoti waliyoionyesha na kusema ni ndoto kuwa na kitabu lakini hiyo ndoto imefanikishwa nao.
Kitabu hiki kimepitiwa na mwalimu wake wa fasihi Mohamed Othman Dau ambaye pia ni mtunzi wa vitabu.
Ni vyema tu mtu akanunua kitabu hikia mbacho mashairi yake yameweka katika mfumo rahisi na wa kirafiki zaidi na wale wanaopenda nakshi ama hakika kuna nakshi katika kukisoma na kukiangalia.
COMMENTS