WIZARA ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa ,upungufu wa maji katika miji midogo ya Mikumi, Kilosa , Turiani ,Mvomero na Gairo , huenda lika...
WIZARA ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa ,upungufu wa maji katika miji midogo ya Mikumi, Kilosa , Turiani ,Mvomero na Gairo , huenda likatoweka kabisa iwapo juhudi za Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka zilizopo kwenye maeneo ya miji midogo hiyo zitaunganishwa katika mtandao mmoja wa kusambazaji na kutoa huduma ya maji kwa wananchi wake.
Hato yamebainishwa na Mhandisi wa Wizara ya hiyo, Zefania Mihayo, juzi ,( agosti 20) mjini Mikumi, katika kikao cha uhamasishaji na kukubaliana kuhusu kuunganishwa kwa Mamlaka za maji safi na taka za miji midogo iliyopo Wilaya ya Kilosa, Mvomero na Morogoro.
Katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya , alikuwa mgeni rasmi ambacho kilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya ya Morogoro, Kilosa na Mvomero ,Wakurugenzi wa Halmashauri hizo, Wadau wa Sekta ya Maji , Watendaji mbalimbali wa Serikali ya Mkoa na Wilaya hizo.
Mhandisi hiyo alisema mpango huo utafanikiwa kutokana na mradi wa ushirikiano wa pamoja kati ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji , Mamlaka ya kuthibiti matumizi ya Nishati na Maji ( EWURA), Shirika la Ushirikiano wa Watu wa Ujerumani (GTZ) na Serikali ya nchi hiyo , chini ya ufadhiliwa wa pamoja na Jumuiya ya Ulaya (EU) katika kuunganisha mamlaka ya mji midogo kutasaidia kabisa kuondoa tatizo hilo la maji.
“ uwezekano huo wa kuondokana na tatizo ya upungufu wa maji katika Miji midogo hii , unaweza kufanikiwa kutokana na kuwepo kwa mkakati wa sekta ya maji ulio chini ya sheria ya maji ya mwaka 2009 ya kuzitaka mamlaka za maji katika miji midogo na mijini kuunganishwa ili kuongeza ufanisi wake” alisema Mhandisi huyo.
Kwa mujibu wa Mhandisi huyo wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, umuhimu wakuunganishwa kwa Mamlaka hizo kutaleta mafanikio makubwa endapo kila mdau atawezakushiriki kikamilifu kkweye utekelezaji wa kutoa huduma kwa wananchi.
Wakichangia hoja mbalimbali,kwa nyakati tofauti, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu na mwenzake Wilaya ya Mvomero, Futma Mwassa , walionyesha wasiwasi juu ya uwezo wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka ya Manispaa ya Morogoro (MORUWASA) kuhudu uwezo wake wa kuhudumia miji midogo hiyo.
Walisema kuwa , Moruwasa ambapo katika mpango huo itakuwa imepewa jukumu la kusimamia usambazaji maji na kuendesha mradi huo , bado Mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo yakiwemo ya kutokidhi usambazaji wa maji kwa wadau wake wa sasa.
” ni ukweli usiopingika kuwepo kwa matatizo ndani ya Moruwasa kuna uwezekano mkubwa wa kutokidhi mahitaji yanayokusudiwa ndani ya Manispaa ya Morogoro na hata wadau hawa wapya wa miji midogo” alisema Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.
Wakuu hao walisema,mahitaji ya maji katika miji midogo yanatofautiana , ambapo zipo mamlaka ya miji iliyoanzishwa muda mrefu na bado inaendelea kutoa huduma ya maji na mingine imeanzishwa hivi karibuni ukiwemo wa mji mdogo wa Gairo ambao unahitaji upendeleo zaidi.
Akifungua kikao hicho cha wadau wa Sekta ya Maji, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Machibya, alisema kuwa , moja ya mahitaji muhimu katika kutekeleza sekta ya maji ni mifumo sahihi ya taasisi mbalimbali zinazohusika katika kutekelezaji wa utoaji huduma ya maji kwa wananchi.
Alisema , mifumo sahihi ya taasisi husika inazingatia kutengenisha kati ya utoaji wa huduma na uthibiti wa ubora wa huduma hizo, ili kuhakikisha uwiano miongoni mwa wadau na taasisi mbalimbali kwa kutumia mbinu ambazo zinawiana na sera ya maji ya mwaka 2002 , na maboresho katika serikali za mitaa.
Wakati huo huo, wakazi wa mji mdogo wa Mikumi , Wilayani Kilosa, kwa nyakati tofauti, wakiuzingunzia mpango huyo, walisema hawajui iwapo miradi ya maji inayoanzishwa itakuwa na manufaa kwao .
Walidai kuwa kwa kipindi kirefu wamekuwa wakipata matatizo makubwa ya uhaba wa maji na hivyo kulazimika kununua maji kwa gharama tofauti kila wakati kulingana na upatikanaji wa maji hayo.
Bila kupenda kutaja majina yao hadhalani, wakazi hao walisema kuwa mara nyingi wamekuwa wakinunua maji ya ujazo wa ndoo yenye lita 20 kwa bei ya sh: 200 hadi 300 na ndoo kubwa zenye ujazo wa lita 30 kwa sh
500 hadi 1,000.
SOURCE:JOHN NDITI WA HABARILEO

COMMENTS