Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa limetakiwa kutoziachia mzigo mzito nchi ambazo zimejitolea kutekeleza kwa niaba ya jumuia ya Ki...
Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa limetakiwa kutoziachia mzigo mzito nchi ambazo zimejitolea kutekeleza kwa niaba ya jumuia ya Kimataifa, jukumu la kuwapokea, kuwahukumu na kuwafunga maharamia na majangili ya kisomali yanayoendesha uhalifu wao katika pwani ya Somalia na maeneo mengine.
Ushauri huo ambao umeungwa mkono na mataifa mengi, umetolewa na mwakilishi wa serikali ya Uingereza katika Umoja wa Mataifa, Bw. Mark Lyall Grant wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Usalama uliokuwa ukijadili ripoti na mapendekezo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki Moon, kuhusu namna gani jumuia ya kimataifa itakavyoweza kuboresha na kuongeza kasi ya kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria maharamia wa kisomali.
“ Kazi ya kuwahukumu, kuwafunga na kuwahifadhi maharamia na majangili wa kisomali, ni kazi kubwa na nzito, ni mzigo ambao nchi hizo hazitakiwa kuubeba peke yake, Baraza Kuu la Usalama na Jumuia ya Kimtaifa tunapaswa kuwasaidia ni jukumu letu sote” akasema balozi huyo.
Akasema kuwa hadi sasa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayoshughulikia dawa za kurevya na uhalifu (UNODC) na lile linaloshughulika Maendeleo (UNDP), kwa pamoja yamefanya kazi nzuri ya kuzisadia nchi kadhaa zilizo katika ukanda wa bahari ya Hindi kuboresha na kuzifanyia marekebisho sheria zake ili ziweze kubebe jukumu hilo la kuwahukumu wahalifu wa kisomali, kwa kuzingatia sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu.
“ ili juhudi hizo ziwe endelevu nchi hizi na nyingine zinatakiwa kupewa msaada wa kutosha wa hali na mali na nchi yangu ( Uingereza ) iko tayari kusaidia wale wote waliotia sahihi mfumo wa kanuni wa Djibouti kuhusu sheria za kuwahukumu maharamia”.
Baadhi ya nchi hizo zipatato 10 ni pamoja na Kenya, Seychelles, Tanzania, Mauritius na Somali yenyewe. Ingawa Tanzania imerekebisha baadhi ya sheria zake, bado haijaanza rasmi utekelezaji wa jukumu hilo kama ilivyo kwa Kenya na Seychelles.
Karibu kila mjumbe aliyezungumza katika mkutano huo, akiwamo mwakilishi kutoka Tanzania,alitilia mkazo wa kusaidiwa kwa nchi hizo na nyingine zitakazojitokeza kwa kile walichosema athari zitokanazo na uharamia huo ni tishio kwa jumuia yote ya kimataifa.
Aidha baadhi ya wazungumzaji, walibainisha kwamba ni vema pia jumuia ya kimataifa, ikajielekeza katika kutafutia ufumbuzi vyanzo au sababu zinazowafanya baadhi ya wananchi wa Somalia kujihusisha na utekaji wa meli na ujangili wa kutumia silaha bahari.
Wanavitaja vyanzo hiyo kuwa ni hali ngumu na duni kiuchumi na kimaendeleo inayowakabilia wananchi wa Somalia, kutokuwapo kwa dola yenye mamlaka na nguvu na kutokuwapo kwa hali ya amani, usalama na utulivu.
Awali kabla ya katibu Mkuu, Ban Ki Moon kuwasilisha ripoti yake, wajumbe wa Baraza la Usalama walisimama kwa dakika moja kuwakumbuka wahanga wa mlipuko wa bomu uliotokea katika hoteli ya Muna huku Somalia na kuua watu kadhaa wakiwamo wabunge.
Akizungumzia tukio hilo, Katibu Mkuu amesema waliotekeleza uhalifu huo katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, siyo tu kwamba wamewaua raia wasio na hatia, lakini pia wamewakosea na kuwadharirisha waislam na watu wote wenye kupenda amani. Akasema Umoja wa Mataifa unalaani vikali tukio hilo kwa nvugu zake zote.
Akiyataja mapendekezo yake saba ambayo anasema yakitekelezwa yanaweza kusukuma mbele utekelezaji wa kisheria dhidi ya maharamia na majangili ya kisomali. Ban Ki Moon anaeleza kuwa katika kipindi cha miezi saba iliyopita kumekuwa na matukio 136 yanayohusishwa na vitendo vya kiharamia, huku meli zipatazo 30 zilitekwa nyara wakati meli 17 zikiwa na wafanyakazi 450 zilikuwa zimeshikiliwa na maharamia hao wakitaka wapewe mamilioni ya fedha.
Katibu Mkuu alizishukuru jitihada za kimataifa za kupambana na uharamia katika pwani ya Somalia, huku akisisitiza kwamba ingawa matukio ya kiharamia yanaelekea kama kupungua, lakini jumuia ya kimataifa inatakiwa kuongeza juhudi za kupambana na wahalifu hao.
Mapendekezo saba ambayo Ban ki Moon aliyawasilisha mbele ya baraza Kuu ni : baadhi ni kuundwa kwa mahakama ya Somalia, lakini itakayokuwa ikiendesha shughuli zake katika nchi ya tatu itakayokubali kuwa mwenyeji wa mahakama hiyo. kuwapo kwa chemba maalum katika mfumo wa sheria za nchi moja au nchi kadhaa za ukanda wa pwani ya Somalia na pembe ya afrika kwa kushirikiana au kutoshirikiana na Umoja wa mataifa na , kuundwa kwa mahakama ya kikanda kwa kuzingatia makubaliano ya nchi kadhaa huku kukiwa na ushiriki wa Umoja wa mataifa.
Mapendekezo mengine ni, kuundwa kwa mahakama ya Kimataifa kwa kuzingatia makubaliano kati ya nchi itakayojitolea kuwa mwenyeji wa mahakama hiyo kwa kushirikiana na Umoja wa mataifa, na kuwapo kwa mahakama ya kimataifa itakayoundwa na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia ibara ya VII ya katiba ya Umoja wa Mataifa.
Pamoja na mapendekezo hayo, ripoti hiyo pia inajadili faida na hasara zitakazotokana na utekelezaji wa mapendekezo hayo ambayo karibu nchi zote ziliyaunga mkono.
SOURCE:UBALOZI WA TANZANIA NEW YORK

COMMENTS