SHIRIKISHO la Kimataifa la Maonyesho Duniani (UFI), limeipatia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), hati safi ya ukaguzi b...
SHIRIKISHO la Kimataifa la Maonyesho Duniani (UFI),
limeipatia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
(Tantrade), hati safi ya ukaguzi baada ya kukidhi vigezo
vya kimataifa katika kuandaa maonyesho ya biashara.
Kaimu Mkurugenzi wa Ukuzaji Masoko wa Tan Trade,
Masha Hussein amesema uamuzi wa taasisi hiyo
unatokana na tathmini iliyoifanya katika Maonyesho ya
34 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),
yaliyoandaliwa na Tantrade na kufanyika kwenye
Viwanja vya Maonyesho vya Mwalimu Julius K . Nyerere,
mwezi uliopita.
BPA inatoa huduma ya ukaguzi kwa taasisi mbalimbali
kwa lengo la kuwaunganisha wamiliki wa taasisi hizo na
wateja kwa kuwaeleza uwezo wao wa kuyafikia masoko na
aina ya bidhaa wanazozalisha. Kwa sasa BPA
inahudumia wateja 2,600 katika nchi 25 duniani kote.
" Watendaji wa Kampuni hiyo walifika kwenye
maonyesho yetu yaliyopita na kuyatathmini kwa kina
katika vipengee vyote na kisha kupeleka ripoti inayohusu
matokeo ya tathmini hiyo kwa UFI, yenye makao yake
makuu, mjini Paris Ufaransa"
alisema na kuongeza kuwa, baada ya kuridhishwa na
utendaji wa Tantrade, imekubali viwango vyetu na kutoa
hati safi" alisema.
Maonyesho hayo, ambayo ni ya kwanza kuandaliwa na
Tan Trade, ambayo imechukuwaa nafasi ya iliyokuwa
Halmashauri ya Biashara ya Nje (BET), yalizinduliwa na
Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva na yalifanyika
kati ya Juni 28 na Julai 8 mwaka huu.
Masha alivitaja baadhi ya vigezo vilivyotumiwa katika
tathmini hiyo kuwa ni pamoja na utaratibu watazamaji
kuingia kwenye uwanja wa maonyesho, ikitia maanani
utaratibu wa upatikanaji wa tiketi na muda ambao
mtazamaji anatumia tangu kufikia maeneo ya uwanja
hadi kuingia ndani.
Vingine ni muda kufunguliwa na kufungwa kwa mabanda
ya maonyesho na upatikanaji wa taarifa zinazohusiana na
maonyesho hayo kwenye mtandao na usimamizi kwa wale
wanaotaka kushiriki.
Hata hivyo, Masha alisema taarifa hiyo ya BPA World
Wide imetoa mapendekezo ambapo imesema Tantrade
inatakiwa kuyafanyiakazi ili kukakikisha hadhi ya
Maonyesho hayo ya DITF yanaendelea kubakia katika
viwango vya juu vya ubora wa kimataifa.
Aliyataja mapendekezo hayo kuwa ni pamoja na kuanisha
sula la umri kwenye tiketi za kuingilia uwanjani ili
kuondoa utata juu ya mtoto ni nani au wa umri gani.
Chini ya marekebisho hayo, tiketi hizo zinatakiwa
kuanisha kuwa watoto ni wale wenye umri kati ya mwaka
mmoja hadi minane mpaka 10. "Wale wenye umri wa
miaka 10 hawastahili kuchukuliwa katika kundi la watoto.
mwisho

COMMENTS