Temporary Shelter

CHATROOM

Wednesday, January 26, 2011

NGO ZINAZOJINUFAISHA KUPITIA MATATIZO YA WANAWAKE ZISIPEWE NAFASI-TANZANIA

Na Mwandishi Maalum
Tanzania imeutaka Umoja wa Mataifa kutozikumbatia taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) zinazolenga kujinufaisha kupitia matatizo ya wanawake.
Tanzania imetoa wito huo kupitia Balozi wake katika Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Bodi ya Chombo kipya cha Umoja wa Mataifa, kinachoshughulikia masuala ya wanawake maarufu kama UN-WOMEN.
Akizungumza katika mkutano huo wa siku tatu, ambao Tanzania ni kati ya nchi za kwanza zinazounda Bodi ya UN-WOMEN. Balozi Sefue anasema wakati Tanzania ikiunga mkono na kukaribisha ushirikiano wa wadau mbalimbali zikiwamo NGOs katika kuchagiza maendeleo na haki za wanawake, tahadhari ichukuliwe dhidi ya wale wanaotaka kujinufisha kupitia matatizo ya wanawake.
“tunakaribisha wazo hili la kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwamo NGOs, na hasa wale ambao kweli wamedhamiria kuonyesha kwa vitendo nia hiyo na si wale wanaolenga kujinufaisha wao” akasisitiza Balozi.
Aidha Mwakilishi huyo wa Tanzania katika UN, amekitaka Chombo hicho kipya katika ujumla wake, kuhakikisha kinakidhi kiu na matarajio ya nchi wanachama na hasa wanawake.
Anaeleza kuwa ni vema watendaji wa Chombo hicho ambacho kimechukua majukumu ya taasisi nyingine nne za UN zilizokuwa zikihusika na masuala ya wanawake. Kwamba licha ya kuwa wabunifu na wanaojituma, lakini pia wanapashwa kuyatambua kwa kujielemisha mazingira watakayofanyia kazi.
Anafafanua kwa kusema. Kila nchi inachangamoto zake linapokuja suala la kushughulikia haki, usawa na maendeleo ya wanawake. Na kwamba kila nchi ina mila, desturi na tamaduni zake, hivyo ni vema watendaji wa Chombo hicho wakayajua na kuyazingatia hayo.
Balozi Sefue anaeleza kuwa ni vema pia Chombo hicho katika utekelezaji wa majukumu yake na hasa kwa kuzingatia kwamba kitalenga zaidi kufanya kazi ndani ya kila nchi husika, kwamba kikazingatia mipango mkakati ya kila nchi na vipaumbele ambavyo nchi hizo imevichagua.
“ Kila nchi inachangamoto zake, kila nchi ina mila na taratibu zake, na kila nchi imejipangia program zake na kuchagua vipaumbele vyake, kwa hiyo ni muhimu sana kwa Chombo hiki kufanya kazi kwa ukaribu sana na serikali husika ” akasisitiza Balozi.
Akatumia nafasi hiyo kuelezea hatua mbalimbali za kisera, kisheria na kimipango ambazo zimefanywa na serikali ya Tanzania katika kutatua kero za wanawake.
Akasema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameonyesha utashi mkubwa wa kisiasa katika kushughulika haki za wanawake na kwamba utashi huo hauishi kwa Rais tu bali hata kwa viongozi wengine wa Serikali.
Pamoja na mambo mengine akasema Tanzania imejitahidi sana kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za utoaji wa maamuzi.
Kwa mfano, akasema kupitia juhudi hizo za serikali, Tanzania hivi sasa Spika wake wa Bunge ni mwanamke, imeazisha Benki ya wanawake, pamoja na kutoa nafasi sawa za kielimu kwa watoto wa kike na wakiume.
Hata hivyo amesema pamoja na mafanikio hayo na mengine mengi Tanzania bado ina safari ndefu katika utekelezi wa mipango ya kuwasaidia wanawake.
Akasema ni matumaini ya Tanzania ya kufanya kazi kwa karibu na Chombo hicho katika kuongeza kasi ya kushughulikia matatizo ya wanawake katika Nyanja mbalimbali.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa UN-WOMEN Madam Michelle Bachelete ambaye aliwahi kuwa Rais wa Jamhuri ya Chile. Aliainisha mbele ya wajumbe wa Bodi vipaumbele vinavyotakiwa kutekelezwa katika siku mia moja pamoja na mipango kazi ya baadaye ya Chombo hicho.

Source:high Commission

NGO ZINAZOJINUFAISHA KUPITIA MATATIZO YA WANAWAKE ZISIPEWE NAFASI-TANZANIA

Na Mwandishi Maalum
Tanzania imeutaka Umoja wa Mataifa kutozikumbatia taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) zinazolenga kujinufaisha kupitia matatizo ya wanawake.
Tanzania imetoa wito huo kupitia Balozi wake katika Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Bodi ya Chombo kipya cha Umoja wa Mataifa, kinachoshughulikia masuala ya wanawake maarufu kama UN-WOMEN.
Akizungumza katika mkutano huo wa siku tatu, ambao Tanzania ni kati ya nchi za kwanza zinazounda Bodi ya UN-WOMEN. Balozi Sefue anasema wakati Tanzania ikiunga mkono na kukaribisha ushirikiano wa wadau mbalimbali zikiwamo NGOs katika kuchagiza maendeleo na haki za wanawake, tahadhari ichukuliwe dhidi ya wale wanaotaka kujinufisha kupitia matatizo ya wanawake.
“tunakaribisha wazo hili la kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwamo NGOs, na hasa wale ambao kweli wamedhamiria kuonyesha kwa vitendo nia hiyo na si wale wanaolenga kujinufaisha wao” akasisitiza Balozi.
Aidha Mwakilishi huyo wa Tanzania katika UN, amekitaka Chombo hicho kipya katika ujumla wake, kuhakikisha kinakidhi kiu na matarajio ya nchi wanachama na hasa wanawake.
Anaeleza kuwa ni vema watendaji wa Chombo hicho ambacho kimechukua majukumu ya taasisi nyingine nne za UN zilizokuwa zikihusika na masuala ya wanawake. Kwamba licha ya kuwa wabunifu na wanaojituma, lakini pia wanapashwa kuyatambua kwa kujielemisha mazingira watakayofanyia kazi.
Anafafanua kwa kusema. Kila nchi inachangamoto zake linapokuja suala la kushughulikia haki, usawa na maendeleo ya wanawake. Na kwamba kila nchi ina mila, desturi na tamaduni zake, hivyo ni vema watendaji wa Chombo hicho wakayajua na kuyazingatia hayo.
Balozi Sefue anaeleza kuwa ni vema pia Chombo hicho katika utekelezaji wa majukumu yake na hasa kwa kuzingatia kwamba kitalenga zaidi kufanya kazi ndani ya kila nchi husika, kwamba kikazingatia mipango mkakati ya kila nchi na vipaumbele ambavyo nchi hizo imevichagua.
“ Kila nchi inachangamoto zake, kila nchi ina mila na taratibu zake, na kila nchi imejipangia program zake na kuchagua vipaumbele vyake, kwa hiyo ni muhimu sana kwa Chombo hiki kufanya kazi kwa ukaribu sana na serikali husika ” akasisitiza Balozi.
Akatumia nafasi hiyo kuelezea hatua mbalimbali za kisera, kisheria na kimipango ambazo zimefanywa na serikali ya Tanzania katika kutatua kero za wanawake.
Akasema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameonyesha utashi mkubwa wa kisiasa katika kushughulika haki za wanawake na kwamba utashi huo hauishi kwa Rais tu bali hata kwa viongozi wengine wa Serikali.
Pamoja na mambo mengine akasema Tanzania imejitahidi sana kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za utoaji wa maamuzi.
Kwa mfano, akasema kupitia juhudi hizo za serikali, Tanzania hivi sasa Spika wake wa Bunge ni mwanamke, imeazisha Benki ya wanawake, pamoja na kutoa nafasi sawa za kielimu kwa watoto wa kike na wakiume.
Hata hivyo amesema pamoja na mafanikio hayo na mengine mengi Tanzania bado ina safari ndefu katika utekelezi wa mipango ya kuwasaidia wanawake.
Akasema ni matumaini ya Tanzania ya kufanya kazi kwa karibu na Chombo hicho katika kuongeza kasi ya kushughulikia matatizo ya wanawake katika Nyanja mbalimbali.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa UN-WOMEN Madam Michelle Bachelete ambaye aliwahi kuwa Rais wa Jamhuri ya Chile. Aliainisha mbele ya wajumbe wa Bodi vipaumbele vinavyotakiwa kutekelezwa katika siku mia moja pamoja na mipango kazi ya baadaye ya Chombo hicho.

Source:high Commission

Saturday, January 22, 2011

Chifu Patrick Kunambi afariki dunia

Mwasisi wa TANU, Chama Cha Mpinduzi na taifa la Tanzania, Chifu Patrick Kunambi amefariki dunia leo alfajiri nyumbani kwake Ubungo Msewe.
Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Lucas Kunambi, baba yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo na alikuwa akihudhuria kliniki ya wagonjwa wa moyo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Marehemu chifu Kunambi alikuwa miongoni mwa waasisi 17, na wanne waliokuwa wamebakia hai, baada ya wengine 13 kufariki dunia.
Marehemu Kunambi alizaliwa Agosti 16,1916 Matombo mkoani Morogoro akiwa mtoto wa mwisho miongoni mwa watoto 11 wa Mzee Kunambi. Baba yake, Chifu, Kunambi alifariki mwaka 1955 akiwa na umri wa miaka 145.
Chifu Kunambi ndiye aliyeongoza mkutano wa Tanu mapema 1955 uliotoka na pendekezo la kumtuma mwalimu Nyerere kwenda Umoja wa Mataifa kukabiliana na Waingereza waliotaka kuchelewesha uhuru wa Tanganyika kwa miaka 25.
Chifu Kunambi ambaye alishika nafasi mbalimbali za uongozi nchini, kitaaluma ni mwalimu ambaye alipata mafunzo Chuo cha ualimu Tabora na Chuo kikuu cha Makerere.
Aidha yeye ndiye alikuwa msajili wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kazi aliyopewa baada ya kurejea nchini akitoka masomoni chuo kikuu cha Duqene, Marekani alikoenda kusomea shahada ya uzamili kati ya mwaka 1962-1964.
RIP Mzee

Wednesday, January 19, 2011

JAJI MAPIGANO APUMZISHWA KWA AMANI


Rais Jakaya Kikwete leo jioni aliongoza mamia ya wananchi kumzika Marehemu Jaji Dan Mapigano katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Makamu wa Rais Dr.Mohamed Gharib Bilal,Waziri mkuu Mizengo Pinda,Jaji Mkuu Othman Chande na waziri mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba, walihudhuria Maziko hayo.
Pichani Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Jaji Dan Mapigano .
SOURCE: Freddy Maro.
RIP JAJI MAPIGANO kama jina lako UMEKAMILISHA MAPIGANO

Ras Nas kufanya shoo Belleville, Oslo. 28 Januari


Kiota cha maraha Belleville, Oslo, kitawaka moto mkali wakati Ras Nas na kikosi chake watakapofanya kweli Ijumaa tarehe 28 mwezi huu. Tumbuizo hili ni la kwanza mwaka huu kwa Ras Nas ambaye ameahidi kufanya shoo la kufa mtu. Safu ya wanamuziki safari hii inajumuisha mpiga sax mahiri toka Mozambique, Ivan Mazuze, mkaanga chipsi (drummer) Uriel Seri toka kwa Gbagbo, Ivory Coast, na mkun'guta besi Aristide Milongo tokea Congo Brazzaville. Wengine ni Dag Pierre, gitaa toka Sweden na Thor Erik mpiga kinanda toka Norway. Mwanamuziki Ras Nas ajulikanaye pia kwa jina halisi la Nasibu Mwanukuzi anachanganya mitindo ya reggae na muziki wa dansi. Kama upo Oslo usikose kujionea mwenyewe kwa macho yako. Usingoje kuambiwa!

Tarehe: Ijumaa 28 January
Mahali: Belleville, Cosmopolite (Vogstgate 64)
Shoo: Kuanzia 22.00 hrs

President Dr.Jakaya kikwete Launch the Second Phase of Secondary education Development Programme(SEDPII) at Ubungo Plaza


President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete holds up a booklet containing a summary of Secondary Education Development Programme (SEDPII) shortly after he launched the programme at Ubungo Plaza in Dar es Salaam this morning. From left, clapping, is the Minister for education and Vocational Training Dr.Shukuru Kawambwa,Permanent Secretary in the ministry Prof. Hamisi Dihenga(Second left), Canadian High Commissioner to Tanzania,Robert Orr(third left),World Bank Country Director ,John McIntire(Fifth left),and on the right is the Minister for Regional Administration and Local Governments George Mkuchika.
source:Freddy Maro

Tuesday, January 18, 2011

JUKWAA LA SANAA BASATA LAMPA KAZI SUGU
Jukwaa la Sanaa BASATA limempongeza kwa ushindi wa nafasi ya ubunge na kumpa kazi ya kutetea wasanii Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni mmoja ya waasisi wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu.
Akizungumza Kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa BASATA kwa niaba ya wadau wote,Profesa Amandina Lihamba kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye alikuwa ni Mratibu wa Jukwaa hilo alisema kwamba,wadau wa Jukwaa la Sanaa wanampongeza kwa dhati kwa ushindi wake na wanamtuma bungeni kutetea haki zao na kwamba asiwatupe.
“Tunajua toka ushinde leo ni mara yako ya kwanza kuonana na hadhira ya wasanii hivyo tunachukua fursa hii kukupongeza kwa dhati,uendelee na moyo huo huo wa kuwapigania wasanii na usiwatupe” aliongeza Profesa Lihamba.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba, pamoja na BASATA awali kutuma barua ya pongezi kwake na kwa wabunge wengine wasanii bado Jukwaa la Sanaa lina kila sababu ya kumpongeza na kumtuma kwenda kutetea haki za wasanii na kuhakikisha maslahi ya sekta ya sanaa yanalindwa.

“Naomba niungane na wenzangu
kutambua uwepo wa Joseph Mbilinyi,Mbunge wa Mbeya Mjini,msanii mwenzetu naimani
sasa tunapozungumza hapa katika Jukwaa tunazungumza na mtu ambaye sasa atakuwa
bungeni akiwakilisha wasanii.Pamoja na barua ya kumpongeza tuliyomtumia yeye na
wasanii wengine walioingia bungeni,tunampongeza tena kwa dhati” alisema
Materego.

Naye Mbilinyi aliyeambatana na Katibu wake Fred Maliki maarufu kwa jina la usanii la Mkoloni alimshukuru Materego kwa pongezi zake lakini akapongeza juhudi anazochukua katika kuwahabarisha na kuwapa fursa ya elimu wadau wa sanaa.Aliahidi kuendeleza harakati za kupigania haki za wasanii kwani ndicho kitu ambacho ataanza nacho.

“Harakati za kupigania haki za wasanii nimezianza kwa muda mrefu nawaahidi kwamba sitarudi nyuma na kwa sasa napenda niwaambie kwamba, mapambano ndiyo kwanza yameanza kwani sasa ndiyo tumekabidhiwa rungu” alimalizia Mbilinyi ambaye aliwahi kutamba na nyimbo kama za Mikononi mwa polisi,Deiwaka, Dar moto chini, Wananiita Sugu,Hold On na nyingine nyingi.

Awali kabla ya pongezi kwa Mbilinyi kulikuwa na Darasa maridhawa Juu ya tasnia ya filamu nchini lililoendeshwa na timu wa watu wa wanne ambao ni Profesa Amandina Lihamba, Dkt.Mona Mwakalinga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wasanii Yvone Cherry (Monalisa, Singo Mutambalike(Rich) na Agnes Lukanga,Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho.

Katika darasa hilo la aina yake somo kuhusu historiia ya filamu hapa
nchini lilielezwa na Dkt.Mwakalinga ambapo alisema kwamba ukiacha Afrika
Kusini,Tanzania ni ya kwanza barani Afrika kuanza kutengeneza sinema ambapo kwa
mara ya kwanza sinema nchini ilitengenezwa mwaka 1935 ambayo ilihusu mafunzo
kwa waafrika katika kuwatumikia wakoloni mashambani na zaidi ya nakala 35
zilizalishwa na kusambazwa.

Kwa upande wao, wasanii Monalisa na Rich walisema waziwazi kwamba, kwa sasa tasnia ya filamu inapoteza dira kutokana na kuingiliwa na mdudu wa usambazaji anayejali fedha tu pasipokujali ubora wa filamu bali majina ya washiriki.Walikiri kwamba, filamu zinazotengenezwa zina ubora wa chini na zisizo na maadili hivyo juhudi za makusudi zinahitajika katika kusawazisha hali ya mambo.

Hata hivyo, wadau wengi wa Jukwaa la Sanaa akiwemo Mwalimu Rashid Masimbi waliwapongeza wasanii wa filamu kwa uthubutu wao ambapo walisema kwamba, wameweza kusababisha filamu za kitanzania zizungumziwe na kujadiliwa na huo ni mwanzo mzuri katika kufikia maendeleo ya kweli ya
tasnia.

Monday, January 17, 2011

Chiku abwao akabidhi jezi kwa Mashine tatu


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (Chadema), Chiku Abwao akikabidhi zawadi ya seti moja ya jezi kwa kapteni wa timu ya Mashine Tatu FC, Khareed Fungabreki iliyoibuka mabingwa wa michuano ya kombe la Staff Inni iliyoanza mwaka huu mjini Iringa.
Mdau Iringa

Eucharia Anunobi bado ataka mume


uigizaji mahiri wa Nolywood bibie Eucharia Anunobi amesema bado anayo matumaini ya kumpata mume.
Muigizaji huyo wa kariba ya juu akizungumza katika mahojiano na Nigeriafilms.com, amesema kwamba pamoja na talaka aliyopewa bado ana matumaini makubw aya kumpata mume anayemfaa.
talaka ya mwanamke huyo ilikuw akatika vyombo vya habari kwa miaka kadhaa na anasema hiyo ilitokana na umaarufu wake.
Madai yaka eya talaka yalichukua muda mrefu katika mahakama za hapa katika kile kilichoonekana kiwango kikubwa cha fedha alichokuwa anaidai kama fidia kutoka kwa mume wake.
Mzozo wa talaka ulianzia mwaka 2006 na inasemekana ulityokana na mwanamama huyo kutaka Naira milioni 100 alizodai za kumtunzia mtoto wao wa miaka 13.
Alisema kwamba kuandikwa mno katika magazeti hakumnyimi usingizi kwa kuwa yeye si mtu wa kwanza jambo hilo kumtokea.
Alisema kwamba yeye hakuomba talaka na kwamba anaamini bado ni mama bora na mke bora lakini watu wakati mwingine wanaweza kuoa au kuolewa na mtu ambaye si sawasawa.
Eucharia Anunobi pamoja na kusema maneno hayo alisema ana matumaini makubwa kwamba atampata mtu wa kumfaa na kuendelea na maisha .

Wachina waanza mazungumzo na Tanzania kuwekeza mradi wa Mchuchuma na Liganga


Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la China na Afrika na Mwenyekiti wa kampuni ya Sichuan Hongda Liu Canglong (kati)akisikiliza kwa maini tafsiri ya mkalimani wake wa maneno kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo nchini (NDC) wakati wa siku ya wkanza ya mkutano wa siku nne wa kufuatilia makubaliano yatakayowezesha kampuni hiyo ya kichina kuchimba chuma cha Liganga na makaa ya mchuchuma.
Canglong alisema kampuni yake ina matumaini ya kufanya mradi huo mkubwa nchini kuwa na maana kwa watanzania na majirani zao hasa kutokana na historia za nchi hizi mbili na mahusiano yaliyopo.
Kampuni hiyo itatumbukiza dola za Marekani bilioni tatu katika mradi huo na kitu cha kwanza kufua umeme.
Kampuni ya Kichina ya Sichuan Hongda yenye thamani ya biashara ya mwaka uliopita ya dola za Marekani bilioni 40 imeelezwa kuwa kampuni pekee iliyoeleza wazi kuwa tayari kutumia zaidi ya dola bilioni 3 kufanyikisha mradi wa Mchuchuma na Liganga.

Mke wa Bob Marley alonga


Mke wa mwanamuziki maarufu wa miondoko ya rege duniani Bob Nesta Marley, Rita Marley amesema kwamba atakubali kuolewa tena kama atampata mume wa kumfaa.
Rita ambaye jina lake halisi ni Alpharita Constantia Anderson, alisema hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha Taxi Driver kinachorushwa na Hitz FM.
Muongoza kipindi hicho Blakk Rasta alitaka kujua kama yupo tayari kuolewa tena.Hata hivyo aliongeza kwamba kwa sasa wala hilo halimshughulishi.
Rita aliyezaliwa Julai 25, 1946 huko Santiago de Cuba, aliolewa na Bob Marley Februari 10, 1966 na alifanikiwa kupata watoto watatu. Bob Marley alifariki dunia Mei 11, 1981 kutokana na ugonjwa wa kansa akiwa na umri wa miaka 36.
Rita Marley ambaye wakati mwingine anajulikana kama Nana ana watoto wengine watatu kutoka katika mahusiano yake mengine, akiwamo Sharon, aliyemzaa kabla ya kukutana na Bob Marley. Pia inaaminika kwamba alikuwa anatoka na Pliers wa Chaka Demus na Pliers na watu wengine mashuhuri kadhaa.
Nana, ambaye alikuwa mmoja wa kundi la uimbaji la I Three lililosanifiwa na wanawake watatu lililoundwa mwaka 1974 kumsaidia Bob Marley and The Wailers,amekanusha madai kuwa alishawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Peter Tosh.

Benki ya Azania wakiukaribisha mwaka mpya

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Azania wakijumuika katika sherehe ya
kuukaribisha mwaka mpya waliyoifanya katika meli maalumu na baadaye kujumuika
katika michezo mbalimbali kisiwani Bongoyo, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Picha nyingine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Charles Singili (mwenye fulana ya njano)akionyesha umahiri wake katika kusakata mpira wa miguu alipojumuika na wafanyakazi wengine wa benki hiyo katika Kisiwa cha Bongoyo wakati wa sherehe za
kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam.

Msoga ndani ya bomba la shule za msingi


Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wanafunzi wa darasa la saba katika shule Mpya ya Msingi Msoga iliyojengwa kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China.Rais Kikwete alikagua madarasa hayo muda mfupi baada ya kukabidhiwa na kaimu Balozi wa China Bwana Fu Jijun huko katika kijiji cha Msoga,wilayani Bagamoyo leo asubuhi
SOURCE: Freddy Maro

Saturday, January 15, 2011

Nimekutana na Kenny Victor


Leo majira flani hivi nilitembelewa ofisini na mmoja wa waigizaji na modo wanaochipukia ambao wanafanya vyema mjini hapa anaitwa Kenny Victor. Alikuwapo hapa akaelezea maisha yake na mchumba wake na nini anachofikiria. kazi nzima itatoka katika gazeti la Jumapili sehemu ya Nyota wetu kaeni mkao wa kumjua Kenny ambaye amecheza Best Wife, Binti kikojozi,fair game na House No 44. pamoja na hizo yeye ametoka wapi na nini falsafa yake.

Profesa Mhando azungumzia bongo movieMTAALAMU wa masuala ya filamu anayefundisha chuo kikuu cha Australia cha Murdoch, Profesa Martin Mhando ameishauri serikali ya Tanzania kuchukua hatua za madhubuti kusaidia sekta ya filamu ambayo mchango wake katika burdani na kuondoa umaskini ni mkubwa.
Kauli hiyo aliitoa jana usiku wakati akitoa mada kuhusu filamu za kitanzania katika ukumbi wa utamaduni wa balozi wa Ufaransa mjini Dar es salaam
Profesa Mhando alisema katika kongamano hilo kuwa tasnia ya filamu inahitaji kupata msaada mkubwa kutoka serikalini ili kuweza kwenda vyema.
Katika mada yake ya msingi alizungumzia ukuaji wa filamu za Tanzania na kusema pamoja na kukienzi kiswahili sinema za Tanzania zimechukua mwelekeo wa sinema za Nigeria zikizungumzia zaidi hadithi za watu wa mijini na madhila ya usasa wao.
Kongamano hilo la siku moja la kujadili filamu za Tanzania, Bongo Movie, pia lilitaka wasanii kuungana na kuunda kundi la kushawishi wabunge kuitafadhalisha serikali kusaidia na kuimarisha ukuaji wa tasnia ya sinema nchini.
Kwa ufupi haya ndio maazimio ya mwisho:
Conclusion ilkuwa kuwa
1. Serikali lazima itambue umuhimu wa tasnia hii kwa utramaduni wa
tanzania and kwa uchumi pia.
2. lazima tuwe na lobby group ya kuwasukuma wabunge na serikali waone
umuhimu wa biashara ya filamu na tatizo la piracy.
3. Serikali ianzishe mfuko maalum wa kusaidia utengenezaji wa filamu
ili kuondoa kushikiliwa kwa biasahara hii na wafanya wabiashara
wachache. Film commission ni lazima ili kutoa misaada kwa watengeneza
filamu na wakati huo huo kusaidia kuongoza ufundi wa kuandika na
kutayarisha filam (producing).
4. Serikali itoe saada kwa njia ya msamaha wa kodi ili kuwaondolea
wafanyabiashara ya muziki na filamu kero za piracy- maana wanajitahidi
kukuza biashara ili kuipatia tija nchi lakini pirates wanawavunja
nguvu. Hivyo ni muhimu serikali kutafuta mbinu za kusolve tatizo hilo.
5. lobby group lazima iwe ya wasanii, wadau na wafanya biashara kwa pamoja.

NA HII NDIYO MADA YAKE

BONGO MOVIES:
A CONTEMPORARY ANALYSIS
SEMINAR PURPOSE

• A diagnostic evaluation of the implications of this phenomenon for production and marketing video film in Tanzania,
• Examine the structure of the industry in Tanzania (Panel Discussion)
• Assess the problems encountered by the emerging video film industry, proffer solutions, and assess its prospects. (Discussion)
What’s a Bongo Movie?
• A perception- includes widely perceived factors – Swahili, cheaply made, melodramatic stories, star based, loosely structured genre-based stories.
• Copycats to Nollywood films
• Films that liberates the discussion of African cinema from concerns with decolonization, identity, authenticity, and the construction of film criticism around national models
• The visual dimension, compared with dialog and narrative, is less important than it is in other cinema cultures (Obaseki, 2005)
NOLLYWOOD-The Video Film
• The video film is the most vibrant form of popular art in contemporary Africa.
• The video-films cut across technical medium, class, social sector, and national boundaries.
• The video film in Africa is seen as a hybrid of television and cinema
• Uniquely poignant is the presence of originality that epitomizes this “film genre”


Why Nollywood succeeds
• “Nollywood directly faces the social problems that make life so hellish, operating with an unusual freedom of expression that arises from the structure of an industry in which the only regulatory authority that counts is the actual consumer and films are watched in unregulated domestic spaces.” (Jonathan Haynes, 2010)
• democratization of image production and the emergence of young filmmakers and film technicians in Nigeria.

• They are uniquely aware that they have struck a lucrative and long-neglected market - movies that offer audiences characters they can identify with in stories that relate to their everyday lives.
• Provide stories that are relevant to life in African urban settings, slums and rural areas

Nollywood Genres
• Nollywood plots epitomize themes and situations that Africans easily recognise and probably confront daily; romance, comedy, horror, the occult/religion, Urbanity, and HIV/AIDS.

• Show- “Huba”

DEFINING THEMES
• violence;
• witchcraft and sorcery;
• prostitution/urban inequity
• tradition versus modernity;
• religious fundamentalism;
• debilitating poverty.
CRITICISM OF NOLLYWOOD • Trite plots, poor dialogue, and poor production values.
• Stereotypes about Africans.
• Allied to piracy
• Follows “Lowest Common Factor” (money) without any ethical or cultural concerns

• BUT the question still remains – how come these films outsell well established Hollywood, European and Bollywood products?
• The answer lies in MARKETING not PRODUCTION

MARKETING • Aggressive marketing techniques using posters, trailers, grassroot urban markets and television advertising (Munis, 2004).
• Uniquely structured MERCHANT distribution systems-
• Use of languages of audiences

Industry analysis
• Unlike African art films, which appear on the global film circuit and are commonly financed by European investors, Nollywood films are completely financed by African merchants.
• Utilise the Wamachinga phenomenon in developing countries- RESOURCEFULNESS and ADAPTABILITY

• Many African immigrants consume the Nigerian movies because the movie themes and content make it possible for them to RECOGNISE and cling to small cultural nuances, (Gray, 2003).


VIDEO DISTRIBUTION CULTURE • Enrolled with piracy, works within not outside the piracy structures
• Take advantage of novel local conditions- Wamachinga
• Not just a Nigerian phenomenon. – It is home entertainment mainstay for the world's developing countries (Aderinokun, 2004).
• Utilise “appropriate socially inclusive technologies”

BRANDING AND THE FUTURE OF BONGO FILMS

• http://www.filamucentral.co.tz/
• promotional methods, include
• poster campaigns, trailers, specialist magazine coverage, radio and television coverage, online site like filamucentral, michuziblog etc.
• selling methods (which are truly in touch with their audiences) street stalls, hawkers, links with hair salons, promotional events – use of mobile phone and blogs
• Sponsorship growing

• When developing a new product, branding is an important decision. The brand can add significant value when it is well recognized and has positive associations in the mind of the consumer. This concept is referred to as brand equity. Brand equity is an intangible asset that depends on associations made by the consumer


Bongo star system? • The organized star system means that the actors are a real promotional asset for the movies. This is fuelled by the sensationalist media coverage (UDAKU) that may well be superficial (often focusing on the stars private lives), but which is also very effective

INTERPRETIVE READINGS • The films are and expression of the “ African urban apocalypse“ -the ultimate expression of anarchic urban catastrophe, environmental destruction, and human misery; its "crime, pollution, and overcrowding make it the cliché par excellence of Third World urban dysfunction" (Kaplan 2000:15).
• Enunciation of social coping mechanisms and creative forms of self-expression of a population whose ability to survive defies common sense,
• An argument about the inability of conventional modes of understanding to explain what permits this survival.

4. These shows emphasize the ingenuity of people struggling to survive in the slums and informal economic sector of African cities, the manic energy that pervades city life, and urban artists' creativity Gandy 2005).1

5. The films are about the main problems with African cities.
6. The images reveal the viewpoints and aspirations of the key urban players ie politicians, technocrats, the middle class on the one hand and ordinary people on the other.
7. The films are made so fast, on minuscule budgets and under such unrelenting commercial pressures, that filmmakers have few resources and little time to realize a distinctive vision.Melodramas and society • Melodramatic plots (Haynes 2000:22-29). This is an aesthetic of immediate impact, plunging us into each moment and milking it for everything it is worth, rather than subordinating every element in the film to an overall sense of design (Barber 1987:46-48; Barrot 2005).
• The films respond to anxieties about violent crime. Some films in this genre convey the terror of urbanity with gritty realism; others sympathetically-and melodramatically-explore the social pressures that produce criminals
• The films frequently involves the occult. As Meyer argues, [this] making of spiritual forces visible is a crucial function of the video films where social inequity is perceived as unsolvable

POSITIVE OUTCOMES 1. The industry has also saved the poor the cost of procuring expensive films from the West (the price per film ranges from N200 to N400-about $2.50- Kuna nafasi ya kupunguza bei
Social criticism and fears
• The films also have significant influence on the way that others see us, and hence on the way they relate to us. We cannot but be concerned, therefore, about what they are saying, what attitudes they are promoting, and what image of us they are projecting.
• Worse, some productions seem to celebrate the evil inherent in the themes, with no serious effort to highlight their moral message.


Bongo movies and cinema
• its reception invite consideration of home video cinema, the nature of its productions, its rapport with the audience, its impact and reception, and the fundamental question of films’ participation in representing national /social experiences.
ADVANTAGES OF NOLLY-CINEMAS
• Filmmakers have responded to the audience's demand for creations that favour local representations and focus on familiar socio-political performances and situations
• Films offer low cost of serial productions, as well as the creative individual freedom


• The low cost of serial production, as well as the creative individual freedom, rather than foreign funds puts filmmakers might turn to television by default.

• In a sense, the success Nolly-African cinema is perhaps a strong signal sent by audiences to filmmakers of a certain impatience with the representations of society that have been purveyed by African cinema until now.


ZIFF’S ROLE
• Embrace changing perspectives of the industry
• Encourage growth and sustained development of Tanzanian cinema
• Project the tensions of the industry
• Represent the various projections and articulations
• Articulate role of cinema in society through festival

Friday, January 14, 2011

He kumbe stori ya kweli ya Mwamwindi haikuandikwa duhh!


Niliingia katika blogu ya kaka Mjengwa na nilikutana na hili:...Nikiwa Njombe, jana nilikutana na kuongea na Mzee Hongole (pichani). Mzee huyu alipata kuwa mwandishi wa habari kijana sana wakati tukio la Mwamwindi kumwua Mkuu wa Mkoa wa iringa Dr Kleruu lililopotokea.
Mzee Hongela: " Ndio kwanza nilikuwa nimepangiwa kufanya kazi kama mwandishi wa habari kwenye gazeti la kanisa pale Iringa. Lilikuwa tukio kubwa sana. Kama mwandishi nilitamani kuandika kilichotokea na maoni ya watu wa Iringa na kanda ya nyanda za juu kusini kwa ujumla.
Kwa wakati ule mfumo haukuruhusu kitu kama hicho. Mwamwindi story was an embargoed one. Lakini nataka kukuambia:" Watu wengi wa Iringa hawakumpenda Dr Kleruu kutokana na unyanyasaji wake".
mwisho wa kunukuu.

Kwa mkono mwingine, LukwanguleSina hakika wengine wanalionaje hili. lakini mimi nadhani Mjengwa anatakiwa kufanyakazi yake, kukusanya kwa kadri inavyowezekana maneno ya mwandishi huyu, mazingira ya kifo, unyanyasaji na kutoka na kitabu hata kama cha kurasa sitini akichanganya historia ya iringa na hasa wakazi wake (watani zangu hawa wana hasira sana) wakati huo vuguvugu la ujamaa lilikuwaje? Maisdha ya wakubwa yalikuwa vipi manake tunazungumzia ufisadi wa hela je hawa hawakuwa mafisadi wa aina yake? Nasikia kulikuw ana kitu si kizuri kishosho. Nilitamani Mjengwa kuandika kitabu kutokana na masimulizi ya huyu mwandishi mkongwe na tena akipata bahati ya kuongea na akina Mwamwindi wanasemaje kuhusu hili.
Je ni kweli kuwa Kleruu alikuwa kafara wa ujamaa au?
Lukwangule

BALOZI WETU WA UINGEREZA ALIKUWA IKULU JE SALAMU ZAKE NI KAMA HUU UCHOKOZI?


Rais DK. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh.Peter Kallage ikulu jijini Dar es Salaam .Kuna maslahi mengi ya Tanzania kwa watawala wetu wa zamani. Pamoja na hayo tuna uhusiano wa aina fulani lakini kama kuchokoza kuna suala la rada ambalo vijisenti vyetu vinatakiwa kurejea. Balozi Kalaghe unaweza kumchomekea maneno mengi kuhusu mazungumzo yake na rais ukiangalia mwenendo wa sasa kimataifa na kitaifa. Nilikuwa nachokoza tu. Si unajua jamaa alikuwa mwandishi pale ikulu kabla hajaenda nje basi anaujua utaaluma wa udodosi.

House No 44 i kikaangoni yasubiri kuliwa


Leo mchana wasanii na waandishi wa habari waliiona kwa mara ya kwanza filamu ya kutisha iliyoandaliwa na Pili Pili Entertainment ya House 44 katika ukumbi wa Sun Cirro uliopo Sinza huko Shekilango Dar es Salaam.
Mtengeneza sinema Sajni Srivastava ambaye pia alishatoa filamu nyingine za PayBack na filamu ya Nani hakuwa na mazungumza sana wakati wa kuanza kwa sinema hiyo lakini alimwambia mpenzi mmoja wa sinema kwamba anatumaini watanzania wataipenda sinema hiyo ya aina ya pekee.
Waigizaji wakuu Kenny Victor na Baby Madaha (pichani)walisema ni kitu bomba na mimi nisemeje Lukwangule? Mhh sijui ila nitazungumza kwa staili si unanijua.

HAFLA FUPI YA TUZO ZA FILAMUCENTRAL.CO.TZ BORA ZA 2010


Leo majira ya mchana watu wa Filamucentral.co.tz walitoa tuzo kwa wasanii na watengeneza sinema bora waliopatikana kwa kura zilizopigwa online kwa mwaka 2010 katika kipindi cha mwezi mmoja.
Mtoaji tuzo alikuwa ni mwalimu wa masuala ya filamu Profesa Martin Mhando ambaye kwa sasa yupo nchini katika mapumziko. Profesa Mhando ni mwalimu chuo kikuu cha Murdoch Australia na pia Mkurugenzi wa tamasha kubw ala filamu Afrika Mashariki la nchi za majahazi,ZIFF.
Baada ya kutoa tuzo hizo alipiga nao picha pamoja kama anavyoonekana pichani.Utoaji tuzo huo ulifanyika hoteli ya Tamal,Mwenge jijini Dar.
Kwa mujibu wa watu walioandaa mashindano hayo alisema kwamba kazi ya kusaka washindi kwa kuchambua washiriki (nominee) ilianzia Desemba 1, 2010 mpaka Desemba 25 2010.
Katika mchakato huo Wadau kumi walifanikiwa kushinda katika shindano hili lililofanywa kwa kipindi cha takribani mwezi mmoja.
Washindi hao 10 walipatikana kwa kuchaguliwa kwa kura zilizopigwa na wadau na wapenzi wa tasnia ya hii kupitia tovuti ya www.filamucentral.co.tz,ikiwa wamechaguliwa kulingana na mafanikio na mchango wao katika tasnia ya filamu kwa mwaka wa 2010.
Dhumuni kuu likiwa ni kuwapa moyo na kutambua mchango wao katika kuimarisha na kuendeleza tasnia hii ambayo bado changa hapa Tanzania lakini yenye kukua kwa kasi.
Washindi hao 10 wanatokana na makundi (categories) kumi ambayo ni muigizaji bora chipukizi,muigizaji bora wa kiume,muigizaji bora wa kike,mchekeshaji bora,muandishi bora wa miswaada,kampuni bora ya usambazaji filamu,kampuni bora ya usambazaji wa filamu,kampuni bora ya utengenezaji wa filamu,muongozaji bora wa filamu na mtayarishaji bora wa filamu.
Washiriki (nominees) katika makundi haya walichaguliwa kutokana na ubora wa kazi zao kwa mwaka 2010.
Jumla ya kura zipatazo 13,142 ziliweza kupigwa kwa ujumla,ikiwa ni rekodi yenye kutia moyo na watu wa FilamuCentral waliwashukuru walioshiriki katika tukio hili adhimu katika tasnia ya Filamu hapa nchini.
Muigizaji wa filamu mahiri hapa nchini Ray Kigosi amejinyakulia tuzo/vyeti vitatu ambavyo ni tuzo ya utengenezaji bora wa kava za filamu,muongozaji bora wa filamu pamoja na kampuni yake tuzo ya utengenezaji bora wa filamu.
Steven Kanumba alikabidhi cheti cha Muigizaji bora wa Filamu pamoja na cheti cha mtayarishaji bora wa filamu
Athuman Mussa a.k.a Mwalubadu amejinyakulia cheti cha Mchekeshaji bora 2010.
Muigizaji wa filamu,Monalisa amekuwa muigizaji bora wa kike 2010.
Muigizaji bora chipukizi ni Hanifa Daudi maarufu kama Jenifer,ambaye ameigiza kwenye filamu ya This is it na Uncle JJ za Kanumba.
Mwakilishi wa FilamuCentral,Myovela Mfwaisa akizungumza kwa ufupi kuhusiana na tuzo hizo adhimu katika tasni ya filamu hapa nchini alisema zimelenga kuleta muwashawasha zaidi katika tasnia ya sinema hapa nchini.Picha zaidi tembelea hapa

Ujumbe wa Kibaki kwa Kikwete


Mjumbe maalum wa Rais Mwai Kibaki wa Kenya, Mhe.Robinson Njeru Githae akimkabidhi RaisDr.Jakaya Mrisho Kikwete ujumbe kutoka kwa Rais Kibaki ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Bwana Githae ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya jiji la Nairobi aliambatana na maofisa waandamizi kutoka ubalozi wa Kenya nchini Tanzania.

SOURCE:Freddy Maro

Konyagi na siku ya familia


Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (Konyagi), David Mgwasa (kushoto) akitoa zawadi ya cheti kwa mfanyakazi wa kampuni hiyo Bw. Mustafa Nassoro kwa kutumikia kampuni hiyo kwa miaka 30. Hafla hiyo iliyoambatana na siku ya wanafamilia wa Konyagi ilifanyika Kigamboni Dar es Salaam hivi karibuni.Anayeshuhudia katikati ni Mratibu wa Sherehe hiyo Bw. Ramadhani Njenje

SOURCE mtandao wa PR habari

Thursday, January 13, 2011

Haya kutoka hapa... tunasema... hii vipi imekaaje?


President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete with YARA Fertilizer Company Chief Executive Officer Jorgen Ole Haslestad cut a ribbon to signal the launch of a USD 20million fertilizer terminal by the Dar es Salaam port this afternoon. YARA is global fertilizer company with its headquarters in Norway and the new Dar es Salaam terminal will have a revolving storage capacity of 45,000 tons of fertilizer.

Hawa ndio waliokufa ajali ya Sumry Mikumi

WATU saba kati ya nane waliofariki katika ajali ya Basi la Sumry iliyotokea kwenye Barabara kuu ya Morogoro- Iringa , eneo la Kijiji cha Masimba , Tarafa ya Mikumi, Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wametambuliwa na ndugu zao na miili yao kuchukuliwa.
Ajali hiyo iliyotokea eneo hilo majira ya saa 9 alasiri jana, baada ya kugongana na Lori aina ya Fuso mali ya Kampuni ya Kutengeneza Pipi aina ya Ivory lililokuwa likitokea Mkoani Iringa kuekelea Dar es Salaam ilisababisha vifo vya watu wanane na kujeruhiwa watu 21 ambao walilazwa Hospitali ya St Kizito ya Mjini Mikumi.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoa wa Morogoro, Ibarahim Mwamakula, alithibitisha kutambuliwa kwa miili saba na kuchukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya shunguli za mazishi katika maeneo mablimbali.
Alisema ajali hiyo ilihusisha basi mali ya Kampuni ya Sumry aina ya Nissan lenye namba T333 BCX lilokuwa likotokea Mkoani Dar es Salaam kwenda Iringa na Lori hilo aina ya Fuso lenye namba T 317 ASR na kusababisha watu hao kufariki dunia papo hapo kati yao wanaume watatu na wanawake watano.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani maiti zilizotambuliwa ni ya Abdubakar Laiser ( 25) ambaye ni Ofisa Masoko na mkazi wa Sinza Jijini Dar es Salaam, Mariam K. Jaha ( 25) Mhasibu wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Iringa , Mboko Anyasime ( 31) Ofisa wa Mifugo , mkazi wa Iringa, Saddiq J. Lyimo ambaye ni mtumishi wa Bohari ya Taifa ya Madawa ( MSD) mkazi wa Jijini Dar es Salaam.
Aliwataja wengine waliotambuliwa na ndugu zao ni Heppy Afred Mwakonjombe ( 15) Mkazi wa Iringa , Vicent Mrema (35) mfanyabiashara na Mkazi wa Kimara Jijini Dar es Salaam, Doris John Lwungo ( 24) mkazi wa Ipogoro , Mkoani Iringa na Martin Cassian ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Idiogoya ya Mjini Iringa .
Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, kuwa mwili wa Martin Cassian hadi sasa bado umehifadhiwa Chumba cha maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kutokana kukosa ndugu wa kuutambua na kudhibitisha.
Hata hivyo alisema kuwa majeruhi wote 21 waliokuwa wamelazwa katika Hospitali St Kizito Mjini Mikimu waliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupatiwa matibabu na kupata nafuu

Wednesday, January 12, 2011

Mchango kuhusu Katiba Mpya

Katiba ya Marekani yenye miaka 200 imefanyiwa marekebisho mara 27 na mara ya mwisho ilifanyiwa marekebisho Mei 7,1992 kwa Rekebisho lililopendekezwa Septemba 25,1789.
Rekebisho la kwanza mpaka la 10 lilihusu haki za binadamu pamoja na haja ya kupasha na kupashwa habari na marekebisho yaliyobaki ambayo yalifanyika zamani pia yalihusu uawakilishi , dhamana yake na sheria.
Kimsingi pamoja na ukweli kuwa katiba ni msingi wa sheria mama kubadili katiba kiholela ni tatizo na mara nyingi watu wenye kuelewa mambo hutumia viraka kujazia maeneo ambayo yana upungufu.
Nimeamua kuchukau mfano wa Marekani kutokana na mazungumzo yanayofanyika nchini, majadiliano ambayo wakati wmingine yanaona yanaenda kasi na wengine wanaingia tu katika mkumbo bila kuelewa dhana nzima ya katiba,uwekaji viraka na pia maana nzima ya katiba mpya.
Wamarekani waliunda katiba yao ya kwanza polepole kwa makubaliano ya viongozi wa mataifa yaliyofanya Marekani lakini rasimu yao ilichukua muda kuandikwa na wala hawakuanza kuiandika mpaka wote waliohusika walikuwapo.
Ukiangalia simulizi unaposoma katiba ya Marekani utaona kwamba mkutano wa katiba uliofanyika katika Jumba la serikali(Independence Hall) mjini Philadelphia hapo Mei 14, 1787, kupitia vifungu vya katiba ulibidi kutoanza kutokana na ukweli kuwa wajumbe wa majimbo mawili tu walikuwa wamefika kwa ajili ya mkutano.
Mkutano uliahirishwa mpaka wajumbe wa majimbo saba walipofika Mei 25 mwaka huo.
Na katika majadiliano katikati ya Juni ilionekana dhahiri kwamba ile katiba ya mwanzo iliyokuwa inajadiliwa haifai na lazima itengenezwe mpya na kutoa muonekano mpya kabisa wa serikali.
Kipindi chote cha majira ya kiangazi kilitumika kuandika na kufuta na kuandika tena huku majadiliano yakiwa makali.
Mambo makubwa ambayo yalijadiliwa kwa muda mwingi ni serikali kuu iwe na mamlaka kiasi gani, watu wangapi wanatakiwa katika bunge (congress)na uwakilishi wa kila jimbo wakati suala la namna ya kuchaguliwa likitiliwa maanani.
Suala ilikuwa je wawakilishi hawa wachaguliwe na wananchi moja kwa moja au watokane na mabunge ya majimbo yao.
Walifikia mwisho na katiba ikatengenezwa lakini Wamarekani wenyewe wanasema katiba yao inatokana na ushirikiano,kukubaliana kutokukubaliana lakini ni katiba ambayo inaonesha mshikamano mkubwa wa uongozi na haja za wananchi.
Katiba kwa kuwa kimsingi ni kanuni au utaratibu wa uendeshaji wa taifa huru ambapo wananchi hutumia kwa ajili ya kuidhibiti serikali, bunge na Mahakama na kuhakikisha vyombo mvyote hivyo vinafanyakazi yake inayostahili ni kitu ambacho hakihitaji kukurupukiwa.
Ndani ya katiba kunazungumzwa mfumo wa maisha ambapo yenyewe inakuwa ndio sheria mama ya nchi.
Inapaswa ieleweke kuwa lengo kuu la katiba ni kutengeneza njia au mfumo ambao unastahili kuendeshwa na serikali kwa watu wake, kuelekeza ukomo wa mamlaka na utendaji wa mihimili ya dola.
Utengenezaji wa katiba unaweza kuwa ni kwa kuzingatia historia au bunge kutengeneza au kundi la watu kutengeneza na kupigiwa kura au watu kuzungumza lakini lazima iwepo rasimu.
Chochote kinachoweza kutokea katiba nzuri ni ile ambayo ni ndogo iliyozingatia mahitaji ya msingi ya jamii inayoeleza wazi mipaka ya kila kitu katika uendeshaji wa nchi na mamlaka zinazotolewa kwa nchi.
Katiba ya Marekani katika uhai wake imefanyiwa marekebisho ya msingi 27 na ikumbukwe kwamba hawa walitengeneza katiba yao baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Katiba ya Tanzania ambayo tayari imerekebishwa mara 14 haiwezi kuwa mbaya kuliko ya Marekani ambayo kwanza ilikuwa na historia tofauti.
India ambao walipata uhuru wao mwaka 1947 wameifanyia katiba yao marekebisho mara 50 na hawa hawana katiba nzuri zaidi ya Tanzania au mbaya zaidi ya Tanzania.
Kimtazamo ni rahisi lakini ni wazi kunatakiwa subira katika kutengeneza katiba mpya lakini kunahitaji mawazo na usahihi wa falsafa ya nchi hii kutengeneza viraka sahihi ili tuwe na mengine ya kufanya kuliko kujadili kitu ambacho wengi wetu hatuelewi.
Bado Marekani walitengeneza kundi la watu na mabadiliko yakafanyika kwa kupitia Bunge kwa kuridhia na yote unaona yanayoingizwa ni kukabiliana na mabadiliko yanayohitajika.
Pengine ni vyema wananchi wakatambua haja ya kutambua kilichopo katika katiba ya sasa na kuona ni namna gani wanaweza kushiriki katika mjadala huu na wala si wa siku moja, bali wa muda wa kutosha kuwawezesha kuchora ramani sawia ya uongozi wa nchi.

Nimefurahi ile mbaya.. Simba 2 Yanga 0

Kukaa kwangu kwa ofisi kumenipa raha kubwa kwani nilishuhudia jinsi simba ilivyoaanza taratibu kama tunafungwa vile kisha tukabadilika Mgosi akaweka kitu dak 33 Yanga akaweka kati na kisha dakika 71 Mkina akafanya vitu vyake na krosi zote hizo zimetoka kwa Ochan ahh ilikuwa maridadi, usiku poa na raha tele, hawa jamaa huwa wananikosesha usingizi.Mpira dakika 90 niliwaambia marafiki zangu unadunda nini Manji bwana.....yalikuwa manne yale mawili Manji kayatia mfukoni.. ha ha ha ...Pole Maganga Feruzi, Pole Padri wangu, pole news editor wetu na msaidizi wako, Pole mhariri wa habarileo na yule wa Jumapili na najua nyie washindani ha ha ha mpira unadunda poleni tu ...tutakutana tena si ligi bado ipo?Lakini hii imetoka na kombe la Mapinduzi letu ha ha ha Nimefurahi kama Msolopa alipofanikiwa kulinga ngazi kuu mpaka dakika ya mwisho ili wauaji wasimfikie Nyleptha...

Mustafa Hassnali atangaza kazi.. hizi hapa

Subject: VACANCY
(1) A young, creative, outgoing, dynamic and competent web designer is required (Part time); should be creative, committed to work under pressure, time and deadline oriented and should be able to work independently under minimum supervision.

(2)Are you crazy, creative, young , Organised, fun, Loves Life , Focus , Customer Satisfaction Oriented, never say Die Attitude, Bored of 9-5 Job...and Want to work as projects manager for Swahili fashion Week?

(3) Are you good at Numbers, can you Sell a Spear to a Maasai:? Are you Aggreessive and honest! SALES PERSON position is available.

(4) PR and MEDIA Manager

Send your CV to info@3http://www.facebook.com/l/061b2-B-f_XwUliLPTvlCSbh0WQ;61.co.tz

Kazi kwelikweli na Ras makunja Serbia
ILIKUWA hekaheka kubwa katika viwanja vya mji wa Belgrade nchini serbia wakati Kamanda Ras Makunja na Kikosi chake cha Ngoma Africa band aka FFU,kilipochambulia jukwaa na kuwaacha washabiki, wapenzi na wale waliofika kuwangalia wakisimamia vidole.
Hii kazi ilifanyika Januari 6,2011 mzaliwa wa Jijini Dar Kamanda Ras Makunja na mzimu wake wa dansi "Ngoma Africa Band"
Kwa maelezo zaidi burudika nao www.reverbnation.com/ngomaafricaband

NAIBU WAZIRI NDANI YA KITUO CHA REDIO ULANGA


Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri, akiwa katika studio za Kituo cha Redio Ulanga FM -91.2 , kilichoanza kufanya kazi kwa majaribio hivikaribuni. Kituo hicho kilichojengwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo.

Summry yaua Iyovi

KUNA habari kwamba basi la Summry limepata ajali majira ya saa 10 na watu wanane wamekufa.Ajali hiyo imetokea Iyovi huko Kilosa.
Source:Mdau

leo ilikuwa mapinduzi kule Zanzibar


THT wafanya vitu visivyokuwa vya kawaidaUZINDUZI wa albamu sita za wanamuziki wa Tanzania House of Talent (THT)umefanyika jana usiku .
Uzinduzi huo wa aina yake ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na watu maalumu 400 akiwamo Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na familia, Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Emanuel Nchimbi na wageni wengine mbalimbali.
Wasanii hao sita wakisindikizwa na wataalamu wa kudansi kutoka kundi hilo waliimba nyimbo zao zote live kwa kushirikiana na bendi ya Odama.
Wasanii waliozindua albamu zao ni Lina, Mataluma, Barnaba, Amini, Mwasiti na Ditto ambapo pia walisherehekea kutimiza miaka yao mitano.
Pichani mwasiti akiondoka sambamba na wachezadansi na picha nyingine wakiwa pamoja wazinduaji kwa picha zaidi nenda hapa

Tanzania yaona pengo la walionacho na wasionacho


NEW YORK-
Ikiwa ni miaka kumi imepita tangu kupitishwa kwa mpango mkakati wa utekelezaji wa Brussels, Ubelgiji uliolenga kuzikwamua nchi maskini kuliko zote duniani kutoka katika lindi la umaskini uliopindukia, hakuna hata nchi moja kati ya 48 iliyoweza kuhitimu na kuingia hatua ya pili.
Nchi hizo maarufu kama LDCs sasa zitakutana tena katika mkutano wake wa nne utakaofanyika jijini Istambul nchini Uturuki mwezi Mei, kwa lengo la, pamoja na mambo mengine kufanya tathimini ya kwanini katika miaka hiyo kumi hakuna hata nchi moja iliyohitimu.
Akizungumza wakati wa mkutano wa kamati maandalizi ya mkutano huo, uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ombeni Sefue,pichani, amesema mkutano huo ulenge katika kuibua mpango mkakati mpya wa utekelezaji wa Istambul wa kuongeza kasi ya kuzifanya nchi hizo maskini kuhitimu.
Akabainisha kuwa ingawa kila nchi imejitahidi kwa kiasi chake kutekeleza mpango mkakati wa Brussels lakini hali halisi inaonyesha kwamba hicho kilichofanyika hakitoshi na hivyo juhudi zaidi zinatakiwa.
Akaonya kwa kusema ni hali isiyokubalika kwamba, bado kuna kundi kubwa la watu ambao wanaishi katika hali ya umaskini wa kutupwa, huku idadi ya nchi maskini zaidi duniani haionyeshi kupungua kama ilivyotarajiwa.
“ Lakini linalotisha zaidi ni kuendelea kuongezeka kwa pengo kati ya walionacho na wasionacho ndani ya nchi na kati ya mataifa na mataifa na hii inatishia usalama na utulivu si tu wa nchi moja moja lakini pia usalama wa kikanda na kidunia” anasema Sefue.
“ Lazima tuwe na lengo moja huko Istambul, nalo ni namna ya kuzisaidia LDCs ziweze kuhitimu na kuondokana na hali hii ya kusikitisha. Mchakato mzima wa mkutano huo na matokeo ya mkutano huo, kwa namna yoyote ile yasiingiliwe na mambo mengine isipokuwa nini cha kufanya kuzikwamua nchi hizo”. akasema Balozi Sefue.
Mwakilishi huyo wa Tanzania amewaeleza wajumbe wa mkutano huo wa maandalizi kwamba Tanzania inajua nini inataka katika mkutano huo.
“ Sisi Tanzania tunajua nini tunachokitaka kijiri huko Instabul. Tunataka fursa ya uhakika ya kujiletea maendeleo, na tunataka kuwaalika washirika wa kweli watakaotusaidia kuondoa vikwanzo vinavyozifanya nchi maskini zisihitimu na kuingia katika hatua nyingine ya maendeleo”.
Akisisitiza kile amabacho Tanzania inakitarajia kama matokeo ya mkutano huo, Balozi sefue anasema pamoja na mambo mengine, kwanza ni kutolewa kwa tamko la kurejea upya utashi wa kisiasa wa ushirikiano wa kuhitimu kama lengo la msingi kutoka nchi za LDCs, kutoka nchi zilizoendela, zinazoinukia kiuchumi na zile zinazoendelea.
Kwa mujibu wa Balozi Sefue, Tanzania ingepeda katika mkutano huo itolewa taarifa fupi inayotathimini utekelezaji wa mpango mkakati wa Brussels, ikielezea mafanikio, kuna lipi la kujifunza, na cha muhimu zaidi lipi linawezekana, lipi haliwezekani kwa nini na kwa vipi.
Aidha Balozi Sefue anasisitiza kuwa, Tanzania inataka kuona katika mpango mkakati wa utekelezaji utakaoibuliwa Instambuli unajielekeza katika kutoa mwelekeo wa kile ambacho nchi zenyewe maskini zinataka kifanyike ndani ya kila nchi na kikanda na kiwango cha ushirikiano na misaada kutoka wadau wa maendeleo ,ili kuharakisha mchakato huo wa kuhitimu kutoka kundi la nchi maskini.
SOURCE:Ubalozi Tanzania UN

Tuesday, January 11, 2011

Wathamini MCC wasema fedha hazitoshi alaaa..


Wathamini wa kujitegemea (independent consultant) wanaofanya kazi chini ya shirika la Africare Tanzania, kutathimini mali za wananchi zinazotakiwa kufidiwa kupisha mradi wa ukarabati na uwekaji wa miundombinu mipya ya kusafirishia umeme kupitia Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) katika mikoa ya Iringa na Mbeya wamegoma kuendelea na shughuli zao.
Wamesema kwamba hawataendelea na kazi hiyo kutokana na kuchakachakuliwa kwa makubaliano.
Mmoja wa wathamini hao Fidelis Kisuku alisema, wakati wakipewa mafunzo kwa ajili ya kuwawezesha kutekeleza kazi hiyo mwishoni mwa mwaka jana walioahidiwa kulipwa Sh 70,000 lakini sasa wanakutana na kila hojiano kuwa sh 8000.
Taarifa yao inaonesha kwamba endapo kila mthamini atachukua taarifa za wananchi 177 wanaopaswa kufidiwa, ndani ya mwezi mmoja waliopewa kukamilisha kazi hiyo, watakuwa wamepata takribani Sh milioni 1.5 kwa malipo ya Sh 8,000, tofauti na Sh Milioni 2.1 kama watalipwa Sh 70,000 walizoahidiwa kwa siku.
Mkoani Iringa, wathamini hao wanatakiwa kuifanya kazi hiyo katika wilaya za Iringa Mjini, Iringa Vijijini, Makete, Mufindi na Njombe wakati mkoani Mbeya wanatakiwa kufanya kazi katika wilaya za Mbeya Vijijini na Mbeya Mjini.
Pichani baadhi ya wathamini wa kujitegemea wanaofanya kazi na shirika la Africare, wakiwa nje ya ofisi ya shirika hilo, mjini Iringa wakisubiri majibu kutoka kwa wakilishi wao, waliokuwa wakifanya mazungumzo na uongozi wa shirika hilo kuhusu posho waliyoigomea .

Monday, January 10, 2011

Patashika la nguo kuchanika! washabiki na Bongo Dansi nchini serbia


"Bongo Dance" limepata makoloni mapya ktk nchi za Serbia,Bosnia,Croatia na baltic
FFU wa Ngoma Africa wameuweka mziki wa Bongo ndani tufe la kimataifa!!!!
Bendi maarufu ya mziki wa dansi "Ngoma Africa band" aka FFU yenye makao yake nchini ujerumani,
Imeuhakikishia ulimwengu kwa mara nyingine kuwa "Bongo dansi" kutoka bongo tambarale ni fyagio la
kimataifa.Baada ya bendi hiyo na "Mzimu wake wa dansi" kutingisha jukwaa la maoenesho ya kimataifa
ya "Kunstendorf Film and music festival" yaliofanyika nchini Serbia kuanzia januari 5 hadi 10.
Kiongozi wa bendi hiyo Ras Makunja aka kamanda wa FFU,alikiongoza kikosi chake jukwaani siku 7 januari 2011
majira ya saa 6.00 usiku na kuanza kuungurumisha mdundo wa "Bongo Dance",ilichukua takribani dakika chache tu
mziki huo kutua katika masikio ya washabiki na hapo ndipo palipoanza kulipuka mshike mshike wa nguo kuchanika!
washabiki walijikuta wamepagawa akili,na kujimwaga uwanjani.baadhi ya watu walio udhuria walikuwemo viongozi wa
ngazi za juu wa serbia,nao walijukuta wameachia viti vya VIP na kujikuta wamejinganya kisawa sawa!walinzi wa vigogo hao walijikuta wana kazi kubwa ya ziada!
Onyesho hilo lilikuwa likirushwa hewani moja kwa moja na TV za Poland,Serbia,Montenegro,St.Petersburg,Bosnia,Croatia,pia TV hizo zilimuhoji Ras makunja,ambaye alikubali mihaliko mingine ya kutumbuiza nchini Poland,Serbia,Bosnia,Croatia na St.Petersburg,Urusi.
Vianzo vya habari vya nchi hizo zimemtaja Ras Makunja na mzimu wake Ngoma Africa band,kuwa mziki wao ni mdundo wa aina yake na unachezeka,CD za bendi hiyo zimeshaanza kupigwa katika vituo vya redio za nchi hizo.
Katika maonyesho hayo wanamziki wa ngoma africa band walikuwa wakilimudu jukwaa na kushambulia kama vile hawana akili nzuri,mpiga solo Chris-B aka "Mshenzi" alikuwa akifinya solo gitaa lake...na uku dansa wa ffu Dada Bedi La Bella Bella akienda sambamba na Ras Makunja kuhakikisha kuwa washabiki wanatolewa Knock Out.
Ras Makunja na bendi yake imekuwa ndio bendi ya kwanza ya kiafrika kutumbuiza nchini humo toka vita vimalizike,na washabiki wameukubali mziki wa Bongo Dance kutoka Bongo Tambarale kuwa ni moto wa nyikani.....
wasikilize ffu at www.reverbnation.com/ngomaafricaband
Source:Msemakweli

Kijana huyu mdogo mgonjwa anahitaji msaada


Tuombe msaada kuwasaidia wenzetu ambao ni
mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu...

Ninakuomba kama mtanzania mwenzangu tupeane hamasa ya kupendana na kusaidiana sio katika sherehe za starehe tuu, zaidi siku hizi tuzidishe kusaidiana katika shida maana sasa shida zinazidi siku hadi siku.

Katika pitapita zangu, nimekutana na mtoto huyu Abdully mwenye ulemavu wa viungo huko Kaole, Bagamoyo. Kula kwake kwa taabu, haongei, ingawa anacheka akifurahishwa, na kulia kwa kupiga kelele akiudhiwa au akiwa na maumivu ingawa hawezi kuelekeza maumivi yako wapi.

Cha kusikitisha, mama yake mzazi amemkimbia mtoto na mume, baba nae ameanza kukata tamaa ya mwanae kwa kukosa muelekeo na msaada (support). Baba (Bw. Hamoud) anaishi na mama yake mzazi ambaye ni mtu mzima mwenye matatizo ya kiafya, macho na thyrod eshafanyiwa upasuaji nk... sasa Bw Hamoud ameacha shughuli za kutafuta fedha za kukimu maisha ili aweze kumlea kijana Abdul (4) ananza asubuhi kwa kumuosha, kumlisha kifungua kinywa..... mchana kumlisha anakula kwa taabu maana ulimi hauzunguki sawa sawa kama vile umepooza, na koo halimezi vizuri.... jioni anamsafisha na kumlisha.... maisha yamekuwa duni, kwa hivyo hata malezi ya Abdul yamekuwa magumu mno...

Alishauriwa ampeleke hospitali ya CCBRT, nae baada ya kwenda hapo alishauriwa ampeleke kwa physiotherapy kila wiki, tatizo la Bw Hamoud ni usafiri kutoka Kaole hadi msasani CCBRT ni wa daladala na mtoto mwenye ulemavu wa viuongo si mchezo... mlemavu wa aina hii anaweza kuwa na haja kubwa au ndogo mahali popote wakati wowote hata mkiwa ndani ya daladala huduma yake ngumu hapo ni mtihani...

Hapo CCBRT wanaweza kushinda kutwa kabla ya kupata huduma kipindi hicho cha kusubiri mtoto amebebwa au kupakatwa, chakula hakuna, na pahala pa kumlaza aweze anaglau kunyoosha viuongo hakuna. wahudumu wanapita na kumuangalia hapo katika foleni bila kumpa tamaa au hata nasaha. Jioni usafiri wa wa kubanana ndani ya daladala kurudi Bagamoyo, pikipiki hadi Kaole.... Baba Abdul kaishiwa nguvu ameshindwa. Wapo Kaole wanasubiri hatma ya Mwenyezi Mungu.

Abdul amepewa ki "baiskeli" cha mtoto (push chair) na akiwekwa hapo lazima afungwe na khanga ndio akae kwa usalama na kwa sasa anabanwa hapo....

Hivyo basi Kama kuna wasamaria
wenye huruma na hali hii, wanaomba:

1. Wheelchair ya kawaida Abdul akae
kwa usalama na awe na nafasi viungo viwe huru
2. Ushauri kwa kiafya
3. Ushauri wowote, na msaada wowote
utakaoweza kutoa afueni kwa Abdul na baba yake Hamoud

mpigie simu Hamoud
+255 757 652449 na +255 787 771566
kwa msaada au ushauri. Juhudi za kufungua
akaunti maalumu zinafanywa kwa wenye
kutaka kumsaidia mtoto Abdully
Mdau Dar

wezi wa vocha za ruzuku wadakwa Moro

OFISA Mtendaji wa Kata ya Kibungo Juu, Tarafa ya Matombo, Wilaya ya Morogoro , Silvester Mpangwa na Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Chisundike , Kata ya Tawa, Jumanne Zuberi , wametiwa mbaroni na Polisi na baadaye kufikishwa Mahakamani kwa kutuhumiwa wizi wa vitabu vitatu vya Vocha za Pembejeo za Ruzuku , imefahamika.
Kutiwa mbaroni kwa Watendaji hao kulitokana na agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mwambungu , ni baada ya kufichuliwa na wenzao wanne waliokuwemo kwenye safari moja ndani ya gari la Serikali lilolobeba makasha wenye vocha hizo eneo la Kata ya Tawa , katika Tarafa hiyo .
Maofisa Watendaji hao bila aibu waliamua kuvichomoa kwa njia ya siri vitabu hivyo vilivyohifadhiwa kwenye kasha na kuvificha katika mikoba yao, huku wakifikiri kitendo chao hicho hakijabainiwa na wenzao waliokuwemo ndani ya gari hilo.
Akizungumza kutiwa mbarobni kwa watendaji hao na kufikishwa Mahakamani , mbele ya Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri, juzi , katika mkutano na wadau wa maendeleo wa Wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya , Said Mwambungu, alisema kuwa ndani ya gari hilo walikuwemo watendaji sita ambapo wawili ndiyo wakiochomoa vitabu na kuonwa na wezao wanne waliokuwemo katika safari hiyo.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya , kuwa wakati akipotelemka katika eneo la Tawa , watendaji wanne waliamua kuwabonyeza viongozi waliokuwAmo katika msafara huo kuhusu njama hizo za kuiba vitabu hivyo na walipobanwa na viongozi hao walikiri kuvichomoa vitabu hivyo .
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa , katika jaribio hilo lililoshindwa, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kibungo Juu alichomoa vitabu viwili vya vocha na kuviFicha , wakati Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Chisundike alichomoa kitabu kimoja hivyo kufanya vitabu hivyo kuwa vitatu.
Sakata za kuhujumiwa kwa mpango wa ugawaji wa vocha za ruzuku ulijitokeza kwa mara ya kwanza Wilaya ya Mvomero katika Kijiji cha Maharaka , Kata ya Doma, ambapo wakulima 219 kati ya 225 waliosaonishwa vocha hizo walipewa ‘mapoozeo’ya sh: 10,000 na kusamehe kuchukua mbegu na mbolea hizo.
Katika sakata hilo , Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Fatma Mwassa, Desemba 31, mwaka jana aliamuru kukamatwa kwa Wakala wa vocha za ruzuku wa Kata hiyo, Mtendaji wa Serikali ya Kijiji hicho , na viongozi wa kamati ya vocha ya Kijiji na watu wengine na kufikia idadi ya watu 14 kutiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani.
Hata hivyo kutokana na juhuma hizo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya , Januari 3, 2011 , aliamuakusitisha kwa muda zoezi la ugawaji wa vocha za ruzuku na kuagiza kuhakikiwa upya katika Wilaya zote na kuanza zoezi hilo upya , ambapo mawakala watakaobainika waliingia kupitian njia haramu wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria na wale waliowasaidia kupata tenda hizo.
Mkoa wa Morogoro katika mwaka huu wa fedha wa 2010/2011 umepata mgao wa vocha 422,118 , ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero imepata vocha 87,531, na Halmashauri nyingine vocha zake katika mabano ni pamoja na Kilosa (63,333), Morogoro vijijini ( 61,497, Mvomero ( 103,152), Ulanga ( 74,592) na Manispaa ya Morogoro ni 32,013.
Mwisho.

Mzee Cleopa David Msuya atimiza miaka 80


Former Prime Minister Cleopa David Msuya ,surrounded by his children and grand children, cuts a cake to mark his 80th Birthday during a colorful celebration held at Golden Tulip Hotel in Dar es Salaam last night. President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, retired President Ali Hassan Mwinyi, and former Prime ministers attended the ceremony.

HAPA NI JEI KEI TII MLALE


Naibu waziri wa Habari Utamaduni vijana na Michezo, Dkt. Finella Mukangara akitoa maelezo kwa viongozi wa JKT Mlale-Songea, baada ya kukagua Shamba la uzalishaji Mbegu bora za Mahindi la Ekari 200 lijulikanalo kama Embakasi. Mkuu wa kikosi hicho Major Abas Ahmed akifuatilia maelekezo ya Naibu Waziri.
source: JUMA NYUMAYO

warsha ya kuzungumzia filamu za Kitanzania

Saturday, January 8, 2011

nakutana na mwanafunzi mwenzangu miaka 35 baadae

BAADA ya miaka takribani 35 nimekutana na Mpogolo au tuseme Apolinari (Apolo) ambaye nilisoma naye shule ya msingi darajani sasa Gilman wakati nilipofika shule hiyo nikitokea shule ya Msingi Bumu, Mgeta Morogoro nilikokuwa naishi. Naam ni miaka mingi lakini jamaa alinikumbuka.
Alikuwa ndani ya taksi anayoiendesha T 643 AKP wakati aliponiita kaka nilipogeuka nikajikuta natazamana naye nilitamani niwe na kamera wakati huo lakini sikuweza kwani nilikuwa nimetoka tu kutarazaki nje ya ofisi mitaa ya Samora.
Tulishangilia sana kwani si kila mmoja yupo.

Siku ya Msanii Tanzania na BASATA


BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) baadaye mwaka huu linatarajiwa kuandaa tamasha kubwa la wasanii ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka likijulikana kama ‘Siku ya Msanii wa Tanzania’.
Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika ukumbi wa baraza hilo kila Jumatatu, Katibu Mtendaji wake,
Ghonche Materego alisema kwamba, tamasha hilo ambalo litakuwa likipambwa na burudani kemkem kutoka kwa wasanii wa sanaa mbalimbali hapa nchini, litakuwa ni maalumu kwa ajili ya kuenzi sanaa na kusisitiza kaulimbiu ya ‘Sanaa ni Kazi’ kwa vitendo.
“Katika kuhakikisha sanaa inakuwa kweli kazi na ajira kama ilivyo kaulimbiu yetu mwaka huu, watendaji wa BASATA wako katika maandalizi ya kuandaa tamasha la siku ya wasanii, ambalo tutawapa taarifa zake hivi karibuni. Katika tamasha hilo wasanii wetu watapata fursa za kuonyesha kazi zao na kushiriki kikamilifu,” alisema Materego.
Aliongeza kwamba tamasha hilo litakuwa ni mwanzo wa kuenzi wasanii wetu na kukuza sekta ya sanaa nchini, hasa ikizingatiwa itakuwa ni fursa kwa wasanii kujitangaza na kupanua mwanya wa masoko ya kazi zao.
Huku akiomba ushirikiano wa dhati kutoka kwa wadau mbalimbali, hasa wale wa sanaa, Materego aliongeza; “Tunataka wasanii wetu sasa waone faida ya kazi zao, wazalishe sanaa zenye ubora na zinazoweza kukubalika na kuvuta watu wengi. Hii ndiyo siri pekee ya kuwafanya wapate fursa ya kushiriki maonyesho na matamasha mbalimbali ya sanaa ndani na nje ya nchi, lakini pia kufanya kazi zao ziuzike”.
Awali akiwasilisha mada katika Jukwaa la Sanaa, iliyohusu ‘Mchango wa Matamasha ya Sanaa Katika Kukuza Ajira nchini Tanzania, aliyekuwa Mratibu Msaidizi wa onyesho maarufu hapa nchini la Sauti za Busara, Kwame Mchauru alisema kwamba, wasanii hawana budi kutengeneza sanaa zenye ubora na zenye asili ya Tanzania ili kuweza kupata fursa ya kushiriki maonyesho na matamasha mbalimbali ya ndani na nje ya nchini.

THT miaka mitano sasa


MAANDALIZI ya kusherehekea miaka mitano ya Nyumba ya Kuvumbua Vipaji Tanzania ‘Tanzania House Of Talent’ (THT), yamekamilika hivyo wadau wanatakiwa kukaa mkao wa kupata onyesho la aina yake ifikapo Januari 11 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Msemaji wa THT,
Kemmy Mutahaba, kiingilio siku hiyo kitakuwa sh 30,000 huku wakipanga kuwa na watu 400 tu katika ukumbi, hivyo mashabiki wametakiwa kuchangamkia kununua tiketi ili waweze kupata fursa ya kushuhudia tamasha hilo.
Mutahaba alisema mbali na maadhimisho ya miaka mitano, pia watazindua albamu sita kwa mpigo za wasanii wanaotamba hivi sasa, ambao ni Mwasiti, Amini, Dito, Barnaba, Lina na Mataluma.
Alisema licha ya kuzindua albamu zao wasanii hao, pia wataudhihirishia umma kwamba wao ni wakali kwa kuonyesha shoo ya aina yake siku hiyo.
Aliongeza kuwa mambo mengi mapya kuhusu THT yataanikwa siku hiyo.
Taarifa hii ni kutoka hapa

Mkunga wa jadi alalamika


Bibi wa Kijiji cha Kinda, ambaye ni mkunga wa jadi akitoa malalamiko yake kwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, juu ya kutuliwa kifuta jacho cha kazi yake na Idara ya Afya

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO