Chadema yasema inachotaka kusema .. ICC

*TAARIFA KWA UMMA* TAARIFA inatolewa kwa umma kupitia vyombo vya habari kuwa Kurugenzi ya Mambo ya Nje na Mahuasino ya Kimataifa ya Chama ch...

*TAARIFA KWA UMMA*

TAARIFA inatolewa kwa umma kupitia vyombo vya habari kuwa Kurugenzi ya
Mambo ya Nje na Mahuasino ya Kimataifa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), inaitaka Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na watumishi wa
umma kwa ujumla, kujifunza kwa kile kilichotokea katika siasa za Kenya.
Imeripotiwa kuwa jumla ya watu wanne, wakiwemo wanasiasa wawili mashuhuri,
aliyepata kuwa mtumishi mwandamizi serikalini na mwandishi wa habari
wamepatikana na kesi ya kujibu, dhidi ya tuhuma zinazowakabili juu ya
uhalifu dhidi ya ubinadamu, wakituhumiwa kupanga na kuchochea vurugu baada
ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Mahakama ya kimataifa imetoa kuthibitisha kuwa wanasiasa wawili mashuhuri
wa Kenya, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha wa Kenya Uhuru Kenyatta,
aliyekuwa Waziri wa Elimu William Ruto, mwanahabari maarufu wa Kenya Joshua
arap Sang na Katibu wa Baraza la Mawaziri, Francis Muthaura.
Kurugenzi inapenda kuukumbusha umma kuwa tuhuma zinazowakabili watu hao
hadi kufikishwa Mahakama ya Kimataifa (ICC) chanzo chake kilikuwa ni
uchaguzi uliofanyika nchini Kenya mwaka 2007 ambapo kama ilivyo ada ya
serikali nyingi za Afrika zisizoamini katika uhusiano mkubwa kati ya
maendeleo na demokrasia, watawala hawakukiri kushindw ahata kama wananchi
walionesha kutowataka kupitia sanduku la kura.
Matokeo yake vurugu kubwa zilitokea nchini Kenya, zikihamasishwa na
wanasiasa kwa misingi ya ukabila. Watu wengi walipoteza maisha na mali za
mamilioni kuharibiwa. Matokeo ya uchaguzi huo yasingekuwa na utata iwapo
Tume ya Uchaguzi ingetenda haki kwa wananchi badala ya kuonekana ikilinda
maslahi ya chama tawala.
Na hivyo ndivyo inavyotokea hata hapa kwetu, kwa uwazi na kificho, hujuma
dhidi ya maamuzi na maoni ya watu kupitia sanduku la kura imefanywa na
watawala kuwa ni sehemu ya uchaguzi. Hivyo kusababisha sintofahamu kila
uchaguzi unapofanyika.
Kurugenzi ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa ya CHADEMA, inaitaka
serikali, chama kilichoko madarakani sasa, vyombo vya dola, mamlaka
mbalimbali na watumishi wengine wote wa umma, kupata funzo la kutosha kwa
kile kinachotokea katika siasa za Kenya, ambapo ni mwendelezo tu wa kile
kilichotokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, ambapo maoni ya watu
katika sanduku la kura hayakuheshimiwa.
Kurugenzi inataka yanayoendelea nchini Kenya yawe somo hapa Tanzania, kwa
sababu inajua namna ambavyo Serikali, CCM, vyombo vya dola na vyombo
vingine vya kimamlaka kama Tume ya Uchaguzi (NEC), Polisi na ambavyo
imekuwa ikifanya hujuma na hivyo kuzua vurugu katika uchaguzi. Ipo mifano
ya kutosha juu ya tuhuma hizi nzito ambazo zimekuwa zikiindama serikali
hapa nchini pamoja, chama kilichoko madarakani sasa na vyombo hivyo, tangu
kuanza kwa chaguzi zinazohusisha ushindani wa vyama vingi, mwaka 1995.
Mathalani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, kulidhihirika hujuma za wazi
katika baadhi ya majimbo mengi ambako CCM kilionekana kushindwa kuhimili
ushindani wa vyama vya upinzani, hususan chama mbadala nchini, CHADEMA,
ambapo katika kulazimisha matokeo yaliyo kinyume na maoni ya wananchi
kupitia sanduku la kura, kulizuka vurugu, zikisababishwa kwa makusudi na
watawala ili kutafuta mianya ya kuharibu matokeo ama zilizuka pale ambapo
wananchi walipoteza matumaini na vyombo vya utoaji haki na hivyo kudai
matokeo halali yatangazwe bila hila.
Mifano hai ni namna ambavyo mgombea wa ubunge wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga
Mjini, marehemu Phillip Shelembi Magadula alivyoporwa ushindi wake kwa kura
moja tu. Itakumbukwa namna ambavyo vyombo vya dola vilitumika kuwatisha
wananchi kwa kuwapiga mabomu, kuhakikisha mbunge wa CCM anatangazwa
mshindi, huku wananchi wakipinga vikali. Hila za katika kuchezea kura za
watu pia na kuwafanyia kila aina ya rafu wagombea wa CHADEMA, zilionekana
katika majimbo mengine kama Kigoma Mjini, Bukoba, Maswa Magharibi, na
majimbo mengine.
Katika majimbo mengine kama Nyamagana, Arusha Mjini, Ubungo, Kawe, Mbeya
Mjini, ni nguvu ya umma pekee, baada ya wananchi kuungana kudai matokeo
halali yatangazwe, ndiyo iliweza kunusuru waliokuwa wagombea wa CHADEMA
watangazwe washindi. Wananchi waliamua kufikia hatua hiyo baada ya kunusa,
kuhisi na kuona kila dalili za wagombea waliowataka na kuwapigia kura
nyingi za ushindi, kufanyiwa hujuma na watawala, kupitia vyombo vya dola,
NEC, chama tawala na serikali kwa ujumla.
Mbali ya matatizo katika nafasi ya ubunge katika uchaguzi huo wa mwaka
2010, kulikuwa na matatizo lukuki katika matokeo ya urais, ambapo ushahidi
bado unaonesha hadi leo namna ambavyo uhalali wake unapaswa kutiliwa
mashaka na mtu yeyote makini.
Kasoro hizo hasa katika ukusanyaji na ujumlishaji wa matokeo, ambapo
CHADEMA kupitia kwa aliyekuwa mgombea urais, Dkt. Wilbroad Slaa, iliwahi
kutoa mifano hai, kwa baadhi tu ya majimbo, zilitakiwa kuundiwa tume huru,
ili kutengeneza utengemano na mwafaka wa kitaifa kwa chaguzi zijazo, hasa
katika kuhakikisha haki inaonekana ikitendeka. Kurugenzi hii inaamini kuwa
ni haki inayoonekana ikitendeka ndiyo itajenga na kudumisha msingi imara wa
amani na utulivu kwa nchi yetu.
Lakini kasoro hizo zilizojitokeza katika matokeo ya nafasi ya urais kwenye
uchaguzi wa mwaka 2010, zilihanikizwa zaidi na ubovu wa sheria
zinazosimamia uchaguzi, ambapo hakuna kipengele kinachoruhusu matokeo hayo
kupingwa mahali kokote, mara baada ya Mwenyekiti wa NEC kumtangaza mshindi.
Hali hii mbali ya kumpatia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) mamlaka ya
Mungu mtu, pia inaminya haki na wajibu wa raia katika kuamua mstakabali wa
nchi yao. Kuendelea kuwepo kwa sheria za namna hii kusimamia chaguzi ni
kuendelea kuweka nchi hii rehani, katika zama hizi ambazo wananchi
wameamuka na wanatimiza wajibu wa kudai haki zao.
Kurugenzi pia inataka serikali, CCM na watumishi wengine wa umma wajifunze
kwa yale yanayoendelea nchini Kenya, ambako inadaiwa kuwa baadhi ya
wanasiasa na watumishi waliunda na kusaidia vikundi vya kufanya ghasia
wakati wa uchaguzi ili kutimiza matakwa yao binafsi na yale ya watawala. Hali
hiyo pia imekuwa ikionekana kwa wazi hapa nchini, hasa nyakati za uchaguzi.
Itakumbukwa katika uchaguzi wa mwaka 2010 na chaguzi zingine ndogo ndogo
kabla, ambapo CCM ilikuwa na vikundi vya vijana kupitia kile kinachoitwa
‘Green Guards’. CHADEMA ilitoa ushahidi wa namna ambavyo vijana hao
waliwekwa makambini na kupewa mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya kutisha na
kupiga wananchi, hasa baada ya CCM ilishindwa kabisa kushindana kwa hoja na
wagombea wa CHADEMA, hivyo kihoro za kupoteza ushawishi kwa wananchi na
madaraka ya kuongoza serikali, kikawa kiko wazi.
Kurugenzi inapenda kuukumbusha umma namna ambavyo mara kadhaa Green Guards
hao walipiga hata waandishi wa habari, ambao walikuwa wakiandika ukweli
hasa wa kile kilichokuwa kikijiri katika kampeni zote za vyama vya siasa
vilivyoshiriki uchaguzi mkuu, ambapo walionesha dhahiri CCM ilivyokuwa
inapoteza mashiko na uhalali katika maamuzi ya Watanzania juu ya chama gani
kwa sasa kinastahili kuongoza nchi, miaka hamsini baada ya uhuru.
Vikundi hivi vya CCM vinavyofanya ghasia na kusababisha fujo wakati wa
uchaguzi kwa nia ya kuwatisha wananchi wasifanye maamuzi sahihi kwa
kuchagua chama wanachokitaka, kutokana na sera bora, vimekuwepo kwa muda
mrefu sasa. Vimekuwa vikitumika kila vinapohitajika.
Vilitumika katika chaguzi ndogo za Kiteto, Busanda, Biharamulo na hata
katika uchaguzi mdogo wa hivi karibuni huko Igunga, mara zote katika maeneo
haya CHADEMA kama ilivyo kawaida yake kwa kuonesha umakini wa kiuongozi,
ilionesha kwa ushahidi yakinifu, mpaka kutaja na kuonesha maeneo ambayo
yalitumika kama makambi ya kuwafunzia vijana hao mafunzo ya kupiga watu.
Lakini hakuna hatua mabazo zimekuwa zikichukuliwa.
Kwa kujua kuwa CCM wameandaa vijana wa namna hiyo kwa nia ya kupiga,
kujeruhi na hata kuua watu, wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga,
wakajishtukia na kujikuta wakikurupuka, kutoa madai mazito juu ya kuwepo
kwa makomandoo kutoka nje ya nchi. Kitu ambacho mpaka leo aliyetoa madai
hayo, hawezi kuthibitisha na hivyo alipaswa akamatwe, ahojiwe na ikibidi
ashtakiwe kwa uchochezi.
Kurugenzi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inayakumbusha yote
haya kwa sababu kumekuwepo na hali ya kufanana hata kama si moja kwa moja,
kati yaliyojitokeza Kenya katika uchaguzi wao wa mwaka 2007 na kile ambacho
kimekuwa kikifanywa hapa nchini na serikali, CCM na baadhi ya vyombo vya
mamlaka kama vile NEC, Polisi na watumishi wengine wa umma katika kuminya
kuminya haki za watu na hivyo kutishia amani na utulivu wa nchi hii kwa
kiasi kikubwa.
Kurugenzi pia inazikumbusha mahakama nchini kutenda haki kwa haraka ili
kuepusha umma kuanza kutafuta haki kwenye vyombo vya kimataifa badala ya
vyombo vya ndani. Na katika kutimiza wajibu wake huo muhimu wa kikatiba kwa
jamii, mahakama zipiganie kufanya kazi kwa uhuru bila upenedeleo ili
wananchi wawe na imani nazo, maana wananchi wengi wa Kenya waliunga mkono
kesi ya ghasia na vurugu za baada ya uchaguzi mkuu 2007, ipelekwe kwenye
mahakama ya kimataifa kwa sababau walikuwa hawana imani na mahakama nchini
mwao.
Kurugenzi inasisitiza kuwa hili linapaswa kuwa fundisho kubwa kwa mahakama
zetu hapa nchini ili ziweze kutenda haki wakati wote bila upendeleo wala
kufuata maelekezo ya serikali, chama tawala au vigogo fulani katika
utumishi wa umma.
Uhuru huu kwa ni ya kutenda haki pia unapaswa kuonekana kwa vyombo vya
ulinzi na usalama ili viweze kudhibiti na kuzuia vurugu wakati wa uchaguzi.
Hata vurugu hizo zinapotokea basi vyombo hivi vinatakiwa kukamilisha
uchunguzi mapema ili kuzipatia mahakama ushahidi wa kutosha kufanya maamuzi
ya haki kwa wakati kwa kuwa haya ni makosa ya kijinai.
Mathalani mpaka sasa haieleweki kwa nini majalada yaliyofunguliwa polisi
kuhusu matukio ya Kiteto, Busanda, Biharamulo, Igunga (hususan juu ya kifo
cha Kada wa CHADEMA, Mbwana Masudi) mpaka sasa hayajakamilika. Hali imekuwa
hivyo hasa pale tuhuma zinakuwa kwa CCM na Viongozi wake.
Ni wazi kabisa kuwa kushindwa kwa mifumo mizima ya ndani ni kichocheo cha
kuingia kwa mifumo mbadala ya kimataifa kuanzia kwenye ngazi ya uchunguzi
mpaka mashtaka, kama ilivyotokea kwa wenzetu huko Kenya.
Kurugenzi pia inataka kuwa yaliyotokea Kenya yatufundishe sasa kujihadhari
kabla ya hatari, hasa kwa kufanya mabadiliko ya kimfumo wakati wa mchakato
wa katiba mpya ili kuwe na tume huru ya chaguzi za mwaka 2014 na 2015.
Lakini pia ni muhimu sana serikali ikazingatia maoni ya wananchi
mbalimbali, mmoja mmoja au taasisi zinazoamini katika maendeleo na
demokrasia kama CHADEMA, kuwa si lazima kila kitu kisubiri mchakato wa
katiba ambao unapaswa kuwa mwafaka wa kitaifa juu ya masuala mengi
mbalimbali, kutuweka pamoja kama taifa moja.
Mathalani hakuna tatizo lolote kama kweli serikali ya CCM inaamini katika
utendekaji wa haki kuwa ndiyo msingi imara wa amani na utulivu, kupeleka
mswada wa kubadili sheria zinazosimamia chaguzi mbalimbali na kuondoa
vipengele ambavyo kuendelea kuwepo kwake, kunaminya haki na kuhatarisha
amani yetu.
Lakini pia mchakato wa katiba mpya iwapo utaachwa uendelee kwa kutumia
sheria mbovu ya sasa ya mabadiliko ya katiba, nchi haitapata katiba mpya
bora ambayo wananchi wa Tanzania wanaiota na kuitaka. Iwapo itatokea
watawala kuwa wabishi na kuufanya mchakato huo kuwa wao badala ya
kumilikiwa na wananchi, itaweka mazingira mabovu ya uongozi wa nchi na
wananchi kujitawala na hususan kupitia chaguzi zijazo, hivyo kuweza
kuelekea njia ambayo wenzetu Kenya walilazimishwa na watawala wao kuipitia.
Hivyo, Kurugenzi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya CHADEMA
Inaitaka serikali kuifanyia mabadiliko ya msingi Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba ya Mwaka 2011, katika Mkutano wa Sita wa Bunge utakaoanza karibuni
kwa kuzingatia pia uzoefu wa kimataifa. Lakini wakati tukisubiri katiba
mpya, bado vyombo vya dola na vyombo vya kutoa haki hapa nchini vinapaswa
kuwajibika na kusimamia sheria za kitaifa na za kimataifa ili kuhakikisha
kwamba amani ya nchi inadumishwa kwa haki kuzingatiwa na kuonekana
ikitendeka.

*Imetolewa leo, Januari 26, 2012, na;*

* *

*Ezekia Wenje*

*Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa*

* *

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,287,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7054,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,739,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,9,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Chadema yasema inachotaka kusema .. ICC
Chadema yasema inachotaka kusema .. ICC
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2012/01/chadema-yasema-inachotaka-kusema-icc.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2012/01/chadema-yasema-inachotaka-kusema-icc.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy