Ikulu yainanga Tanzania Daima.. Ndege ya Rais

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Gazeti la Tanzania Daima la leo, Jumatano, Januari 25, 2012, kwenye ukurasa wake wa kwanza limechapisha habari...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Gazeti la Tanzania Daima la leo, Jumatano, Januari 25, 2012, kwenye ukurasa wake wa kwanza limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Ndege ya JK utata: Iko nje kwa miezi miwili. Serikali yakwama kuilipia.”

Miongoni mwa yaliyoandikwa kwenye habari hiyo ni pamoja na “Ukata unaiokabili Serikali umesababisha kukwama kuilipia ndege hiyo maalum ya Rais…Ndege ya Rais mahususi kwa ajili ya safari za namna hiyo imezuiliwa nje baada ya Serikali kukwama kulipia gharama za matengenezo yake…Kutokuwepo kwa ndege hiyo, kumesababisha Rais Kikwete na ujumbe wake wa watu 14, ulioondoka nchini jana kwenda Davous, nchini Sweden kuhudhuria mkutano wa dunia wa uchumi, kuondoka na ndege ya Shirika la Ndege la Qatal”.

Limeendelea Gazeti hili la Tanzania Daima kudai kuwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa ndege hiyo ya Rais gharama za safari hiyo ya Rais zimeongezeka na ziara hiyo ya Rais ya siku nne kuhudhuria mkutano huo itagharimu kiasi cha shilingi milioni 300.

Aidha, Gazeti hili linadai kuwa mkutano huo hauna tija kwa taifa, kwamba Rais Kikwete amehudhuria mikutano hiyo mara nyingi lakini hakuna faida iliyopatikana kwa taifa.

Kwa hakika, maandishi na kauli hizi za ovyo na zisizokuwa za kweli za Gazeti la Tanzania Daima zinalenga kuupotosha umma wa Tanzania bila sababu za msingi na hivyo kuusababishia umma chuki isiyokuwa na msingi kwa Rais. Katika kuuelezea umma ukweli wa safari hiyo ya Mheshimiwa Rais Kikwete tunapenda kutoka ufafanuzi ufuatao:

Kwanza, kama tulivyoeleza, kwa usahihi, katika taarifa yetu kwa vyombo vya habari jana jioni, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekwenda katika mji/kijiji cha Davos, nchini Uswisi kuhudhuria Mkutano wa World Economic Forum (WEF) unaoanza leo. Rais Kikwete hakuwenda katika mji wa Davous, nchini Sweden kama linavyosema Gazeti hili. Aidha, Rais Kikwete na ujumbe wake umesafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Qatar na siyo Qatal kama linavyoripoti Tanzania Daima.

Pili, Serikali haijakwama, kwa sababu zozote zile, kulipia matengenezo ya kawaida (routine maintenance) ya Ndege ya Rais. Hili limefafanuliwa vizuri na ipasavyo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali, Rubani Kennan Paul Mhaiki jana.

Isipokuwa ni vyema kuongeza kuwa matengenezo ya ndege hiyo yalimalizika juzi tu, Jumatatu, Januari 23, mwaka huu, wakati ndege hiyo ilipofanyiwa safari ya majaribio (test flight) kule Savannah, Georgia, Marekani na wala siyo miezi miwili iliyopita kama linavyodai Tanzania Daima. Hivyo, madai kuwa ndege hiyo imezuiliwa nje kwa miezi miwili sasa kwa sababu ya Serikali kushindwa kulipia gharama za matengenezo ni porojo tu zisizokuwa na msingi.

Tatu, ni vigumu kujua Gazeti la Tanzania Daima limepata wapi habari kuwa safari hiyo ya siku nne inagharimu kiasi cha sh. milioni 300. Ukweli ni safari ya Mheshimiwa Rais Kikwete na ujumbe wake ni ya siku nane, kama tulivyoeleza jana, ambako atahudhuria mikutano ya WEF na ule wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili Jumamosi, Januari 28, 2021. Hivyo, si kweli kwa Gazeti hili kudai kuwa nauli tu na matumizi ya safari ya Mheshimiwa Rais ni shilingi milioni 300 kwa siku nne tu.

Nne, Tanzania Daima linadai kuwa safari za Mheshimiwa Rais mjini Davos hazina tija na wala faida yoyote. Huu pia ni uongo mwingine wa dhahiri wa Gazeti hili. Tunapenda kukumbusha faida chache tu zilizotokana moja kwa moja na Mheshimiwa Rais Kikwete kushiriki mikutano ya WEF kama ifuatavyo:

(a) Moja, ni kubuniwa na kupitishwa kwa Mpango Kabambe wa Uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania wa Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT) uliozinduliwa wakati wa WEF mwaka jana. Mpango huu utakaotekelezwa kwa pamoja na sekta binafsi na sekta za umma kwa kushirikisha Serikali ya Tanzania, Mashirika ya Kimataifa, Makampuni ya Kimataifa unalenga kuleta faida zifuatazo:

(i) Uwekezaji wa kiasi cha dola za Marekani bilioni 3.4 katika kilimo cha Tanzania na kuongeza uzalishaji wa kilimo hicho mara tatu katika miaka 20 ijayo.
(ii) Kuchochea uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara kwenye eneo ya hekta 350,000.
(iii) Kutengeneza kiasi cha ajira 420,000 za kudumu.
(iv) Kuwatoa kwa namna ya kudumu kiasi cha watu milioni mbili katika umasikini.
(v) Kuleta usalama wa kudumu wa chakula kwa kuhakikisha kinapatikana chakula cha kutosha kwa Tanzania na nchi za jirani.
(vi) Kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, barabara, reli, nishati na bandari katika eneo lote la Mradi wa SAGCOT.
(vii) Kuwahakikishia wakulima masoko ya mazao yao, kuwawezesha kupata dhana za kisasa, na kuwaanzishia mifumo ya kisasa ya umwagiliaji.
(viii) Kuingizia wakulima mapato ya kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.2 kila mwaka.

(Kiasi cha dola za Marekani milioni 50 zinaendelea kuingizwa katika mfuko wa uanzishwaji wa Mpango wa SAGCOT utakaotelekezwa kwa kuanzia katika maeneo ya Sumbawanga (Rukwa), Ihemi na Ludewa (Iringa), Kilombero (Morogoro), Mbarali (Mbeya), na Rufiji (Pwani)

(b) Pili, ni uwekezaji kabambe wa kiasi cha dola za Marekani milioni 20 katika mfumo wa upakuaji wa mbolea kwenye Bandari ya Dar es Salaam unaofanywa na Kampuni ya Yara International, moja ya makampuni makubwa zaida ya uzalishaji wa mbolea duniani.

Yara International ni mmoja wa washirika wakubwa katika SAGCOT na uwekezaji wake unalenga kuhakikisha kuwa Tanzania na hata majirani wanapata mbolea ya kutosha kwa ajili ya kuimarisha kilimo.

(c) Tatu, mikutano ya WEF ni shughuli moja inayomwezesha Kiongozi wa Nchi kukutana na kufanya mazungumzo na wakubwa wote duniani – wawe wa siasa, wa biashara, wa uchumi, wa uwekezaji, wa kijamii – katika jitihada zake za kuitangaza Tanzania kama kituo muhimu cha uwekezaji.

Katika siku tatu zijazo, kwa mfano, Mheshimiwa Kikwete miongoni mwa watu wengine atakutana na Bwana Bill Gates wa Bill&Bellinda Foundation, Naibu Waziri wa Uchumi, Nishati na Kilimo wa Marekani Bwana Robert Hormats, Rais wa Benki ya Dunia Bwana Bob Zoellick, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Australia Bwana Kevin Ruud, Mkuu wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani Bwana Raj Shah, Mtendaji Mkuu wa Benki ya ABSA Bi. Maria Ramos, na Waziri Mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra.

Tunapenda kumalizia kwa kusisitiza, kwa mara nyingine tena, kuwa ni vyema Gazeti la Tanzania Daima lijiridhishe na usahihi na habari zake kabla ya kuzichapisha kama inavyoelekeza misingi mikuu ya uandishi wa habari na weledi wa kazi hiyo. Uandishi wa habari za uongo unaleta hofu na kuanzisha uzushi usiokuwa na sababu zozote miongoni mwa wananchi na hiyo siyo kazi ya uandishi wa habari.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

25 Januari, 2012

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,287,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7054,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,739,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,9,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Ikulu yainanga Tanzania Daima.. Ndege ya Rais
Ikulu yainanga Tanzania Daima.. Ndege ya Rais
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2012/01/ikulu-yainanga-tanzania-daima-ndege-ya.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2012/01/ikulu-yainanga-tanzania-daima-ndege-ya.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy