TANGAZA NASI LEO

Friday, January 27, 2012

Kifo cha kiongozi wa Seven Survivor Band, Juma Mpogo


Busara Promotions imeshtushwa na kusikitishwa na kifo cha kiongozi wa bendi ya Seven Survivor , Juma Mpogo a.k.a. General Lupozi.
Juma alifariki dunia Jumapili ya Januari 22. Ameacha mke na watoto wawili. Alikuwa ndiye mtunzi mkuu, mwimbaji na mpiga kinanda wa bendi hiyo.
Seven Survivor (pichani) ni moja ya bendi zilizopo jijini Dar es Salaam inayoongoza katika upigaji wa muziki aina ya Mchiriku, ni muziki maarufu na unaopendwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Hata hivyo bendi hiyo imethibitisha ushiriki wake mwaka huu hata baada ya kuondokewa na kiongozi wao, pia bendi hiyo itapambana na Jagwa Music Jumamosi , Februari 11 katika mpambano wa Mchiriku utakaoitwa Nani Zaidi?

0 comments: