TANGAZA NASI LEO

Friday, January 27, 2012

KUGAWA MAGARI 75 KATIKA SEKRETARIETI ZA MIKOA NA HALMASHAURI


Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kupitia Programu ya Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa inapeleka Magari 75 katika Sekretarieti za Mikoa 13 na Halmashauri 62 ili kuwawezesha Wakaguzi wa ndani pamoja na wataalamu washauri katika Sekretarieti za Mikoa hiyo kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Programu ya Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa inalenga kupeleka Madaraka ya kisiasa, majukumu, rasilimali fedha na rasilimali watu kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Magari haya yatawasaidia Wakaguzi wa ndani wa halmashauri na Sekretarieti za Mikoa kufanya ukaguzi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri zote nchini na hivyo kuongeza ufanisi na uwajibikaji miongoni mwa watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Ni matarajio yetu upatikanaji wa vitendea kazi hivi vitatusaidia kudhibiti ubadhirifu wa fedha katika Halmashauri zetu na kuhakikisha miradi inayotekelezwa katika halmashauri zetu inafikia malengo yaliyokusudiwa.

Napenda kutoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa shughuli za ukaguzi wa ndani zinaimarishwa na kupewa kipaumbele katika mipango yao.

IMETOLEWA NA

Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb)
WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI

0 comments: