Baadhi ya Waislamu, kutoka Jumuiaya ya Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu Morogoro wakiwa wameketi chini barabarani karibu na Ofisi ya Mkuu wa ...
Baadhi ya Waislamu, kutoka Jumuiaya ya Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu
Morogoro wakiwa wameketi chini barabarani karibu na Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Morogoro, wakiwa na mabango yaliyoandikwa ujumbe ' Majengo ya
Serikali Ardhi ya Kanisa J.K. Thibitisha " Lazima Kieleweke"
Maandamano hayo yalifanyika leo mjini hapa baada ya sala ya Ijumaa.
Mamia ya Waislamu wa Morogoro wakiwemo Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu wameandamana hadi Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha madai yao mbalimbali yakiwemo ya kupinga mfumo Kristo ndani ya Serikali.
Maandamano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi na Vijana wa
Kiislamu Mkoa wa Morogoro, yalianza mara baada ya swala Ijumaa
kutoka Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro eneo la Msamvu , kupitia
katikati ya mitaa ya Manispaa ya Morogoro hadi nje ya Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa .
Askari wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU)Mkoa wa Morogoro wakijenga
uwigo kwa ajili ya kuwazuia waandamanaji waislamu wa Jumuiya ya
Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu Morogoro leo karibu na Ofisi za Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro.
Hivyo pamoja na kufikisha risala hiyo, wameipa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
siku 21 kuanzia Januari 20, mwaka huu kuyashughulikia madai ya
Waislamu wa Mkoa wa Morogoro na kupatia uvumbuzi wa kudumu ,
vinginevyo watayashughulikia wao wenyewe.
Wakati maaandamano hayo kijumuisha baadhi ya wasilamu wengine njiani ,
Polisi Mkoa wa Morogoro chini ya Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa,
Joseph Rugira, waliwahi kuziba njia karibu na Ikulu ndogo yakiwemo na
Makazi ya Mkuu wa Mkoa sambamba na lango la kuingilia Jengo la Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Hata hivyo wakati maandamano hayo wakisika kasi kwa waislamu hao
kubeba mabango yaliyoanzidikwa ‘ Kupinga mazira mfumo kristo Tanzania’
‘ No Peace without justice ‘ pia walibeba mabango yaliyoandikwa kwa
vitambaa yakiwa na ujumbe ‘ Majengo ya Serikali Ardhi ya Kanisa . JK
Thibitisha …lazima kieleweke’ na ‘ Pasipo haki hakuna usawa’.
Azma ya kufanyika kwa maandamano hayo ni kushinikiza Serikali
kuuondoa mfumo kristo , kudhulumiwa , kunyanyaswa na ukandamizaji wa
wanafunzi wa Kiislamu mashuleni, Vyuoni na kubakizwa nyuma kwa
makusudi katika elimu , ajira na maeneo mengine mbalimbali na kupewa
majina mabaya kama magaidi ili kuhalalisha dhuluma dhidi ya Waaislamu.
Pamoja na kurupushani hizo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo,
Rugira, aliwataka Waandamanaji hao kuteua wawakilishi watano
wataowasilisha risala yao kwa Mkuu wa Mkoa na wao wabakie wakisubiri
kupatwa majawabu.
Askari wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU)Mkoa wa Morogoro wakijenga
uwigo kwa ajili ya kuwazuia waandamanaji waislamu wa Jumuiya ya
Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu Morogoro leo karibu na Ofisi za Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro.
Hatua hiyo iiliafikiwa na Waaislamu hao, na waliwateua wawakilishi
watano kupeleka ujumbe katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa , ambapo pamoja na
kufika Ofisi hiyo, Mkuu wa Mkoa alikuwa safarini na wao wakimtaka
Ofisa Elimu wa Mkoa ili asikilize madai yao.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mgeni Baruani, aliazimika kutoka
nje ya lango kuu walipokuwa wameketi waandamanaji hao ili kusikiliza
risala yao iliyosomwa na Shehe Mohammed Mohammed , ambaye pia alikuwa
ni Mratibu na Msemaji wa Maandanano hayo.
Katika risala yao, walidai kuwa Serikali ya Tanzania haiwathamini
Waislamu wala kujali shida zao , pamoja na sauti za vilio na hivyo
kutoa tamko la kuitaka Serikali kuu na Mkoa iwachukulie hatua za
kisheria wanafunzi , walimu , watendaji wanaongoza kuleta migogoro ya
Kidini Shuleni na sehemu za kazi.
Hata hivyo katika mambo yao sita ni kuwa watapambana wenyewe
watakapoona wanadhulumiwa katika kutetea haki kwa vile ni wajibu wa
waislamu kufanya hivyo na kwamba huo ndiyo msimamo wao wa kuueneza
nchini kote hadi pake Serikali itakapoonesha kujali na kudhamini
waislamu.
Baadhi ya wanawake wa Kiislamu wa kutoka Jumiya ya Wanafunzi na Vijana
wa Kiislamu Morogoro, wakiwa kwenye maandamano yaliyoandaliwa na
Jumuiya hiyo ijulikanayo kwa kifupi –TAMSYA, kama walivyokutwa katika
barabara ya Boma kuelekea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Akizungumza baada ya kupokea risala ya madai yao, Katibu Tawala wa
Mkoa huo, Baruani, aliwataka Waislamu hao kuwa watulivu na kwamba Mkuu
wa Mkoa mara atakaporejea atakabidhiwa ili kuyapitia na yenye kuhitaji kuchukua hatua zaidi ya kuwasilisha kwa Rais Jakaya Kikwete.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Rugira, ambaye
pamoja na safu yake walijitahidi kuzungunza na baadhi ya viongozi wa
Maandamani hayo kuwataka watulize jazba na baada ya kuwasilisha kilio
chao aliwataka watawanyike kwa amani na utulivu.
Hata hivyo kabla ya kutawanyika walimtaka Kaimu Kamanda huyo wa
Polisi, kuwaachia wenzao watatu waliokamatwa kwa madai ya vinara wa
maandamano hayo na dai lao lilikubaliwa na kuwawachia Siamini Said,
Athuman Seba na mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika
mara moja.
Magari ya Polisi yakiwa na Askari yakipita katikati ya barabara ya
kwenda Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, baada ya waandamanaji hao
ambao ni Waislamu wa Jumuiya ya wanafunzi na Vijana wa Kiislamu
kutakiwa kusongea mbele ili wasililize majibu ya hoja zao kutoka kwa
Uongozi wa Mkoa , leo.
Lakini Waislamu hao walitaka Jeshi la Polisi limlipe fidia mmoja wao
aliyetambuliwa kwa jina la Mgeni Athumani aliyepasukiwa na bomu
sehemu ya kichwani na kusababisha majeraha.
Hata hiviyo Waislamu hao mara baada ya kuwasilisha madai yao walitii
agizo la kuwataka kutawanyika eneo la Ofisi za Mkuu wa Mkoa na
waliodoka kwa amani majira ya saa kumi jioni kurejea kuendelea na
shughuli zao nyingine.
COMMENTS