Marekani yavutiwa na Zanzibafr

    MAREKANI imeeleza kuvutiwa kwake na mafanikio yaliopatikana katika miradi inayoiendesha hapa Zanzibar na kuahidi kuunga mkono miradi m...

   
MAREKANI imeeleza kuvutiwa kwake na mafanikio yaliopatikana katika miradi
inayoiendesha hapa Zanzibar na kuahidi kuunga mkono miradi mengine ikiwemo miradi
mipya ya Changamoto ya Milenia (MCC) awamu ya pili  baada ya  Tanzania kufanikiwa
katika awamu hiyo ambapo Zanzibar nayo itafaidika. 
 
Maelezo hayo yametolewa leo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Alfonso
Lenhardt akiwa na ujumbe wake wakati walipokuwa na mazungumzo na Rais wa  Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu mjini Zanzibar.
 
Balozi huyo alieleza kuwa Marekani inathamini sana uhusiano na ushirikiano uliopo
kati yake na Zanzibar na kusisitiza kuwa itaendelea kuiunga mkono katika kuhakikisha
miradi ya maendeleo inayoisimamia ukiwemo mradi mkubwa wa umeme inafanikiwa.
 
Katika maelezo yake, Balozi huyo alisifu juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar katika kupambana na Malaria pamoja na kuimarisha sekta zake za
maendeleo huku akieleza jinsi hatua zinazochukuliwa na Ubalozi wake katika
kuitangaza Zanzibar nchini mwake kutokana na amani na utulivu uliopo ikiwa ni
miongoni mwa hatua za kuutangaza utalii wa Zanzibar.
 
Katika mazungumzo hayo, Balozi  Lenhardt alitoa nafasi kwa wajumbe aliofuatana nao
ambao ni Wakurugenzi wa Miradi mbali mbali inayoendeshwa na Marekani nchini Tanzania
kutoa ufafanuzi wa miradi wanayoisimamia hapa nchini.
 
Kwa upande wa mradi wa MCC, Mkurugenzi Mkaazi wa Mradi huo nchini Tanzania Bwana
Karl Fickenscher, alieleza  maendeleo yaliofikiwa katika  mradi mpya wa umeme kutoka
Ras Kiromoni hadi Fumba ambapo tayari ulazaji waya umeshakamilika na uwekaji nguzo
pamoja na uwekaji waya kutoka Fumba hadi mtoni umefikia hatua nzuri na kueleza
mategemeo ya kazi za mradi huo kumalizika mwishoni mwa mwezi ujao.
 
 
 
 
Aidha, Mkurugenzi huyo alieleza maendeleo yaliofikiwa katika ujenzi wa barabara
zenye urefu wa kilomita 35 huko kisiwani Pemba na kusisitiza kuwa suala la ubora wa
barabara hizo limezingatiwa sana ili ziweze kutumika kwa muda mrefu.
 
Pia, alisisitiza kuwa hivi sasa ni wakati muwafaka kwa Zanzibar kuunda timu
iliyoimara kwa kushirikiana na ndugu zao wa Tanzania Bara katika kutekeleza miradi
ya awamu ya pili ya MCC baada ya kufanikiwa kutokana na vigezo vilivyowekwa na MCC.
 
Nae Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani USAID, Bi Sharon Cromer alieleza
kuwa  Shirika hilo limeweza kupata maendeleo makubwa katika kuiunga mkono Tanzania
ikiwemo Zanzibar katika kusimamia na kuendesha shughuli mbali mbali za kiuchumi na
kijamii ikiwemo uzazi wa mpango, Malaria, uundaji wa Sera, Kilimo, Utumiaji wa
Raslimali, Elimu, Lishe,Uhifadhi wa Mazingira pamoja na Utalii.
 
Alieleza kuwa hivi sasa Shirika hilo limo katika kutekeleza mikakati ya miaka mitano
katika kuimarisha misaada juu ya sekta hizo wanazozishughulikia ambapo pia wana
dhamira ya kuendeleza mafunzo ya uongozi kwa sekta mbali mbali.
 
Nae Mkurugenzi Mkaazi wa Huduma za kujitolea za Wamarekani “US Peace Corps-
Tanzania’, Bi Elizabeth O’ Malley, alielezea maendeleo yaliofikiwa katika sekta
mbali mbali ambazo Marekani imekuwa ikisaidia kwa kuleta wafanyakazi wa kujitolea na
kushiriki katika kutoa misaada kwenye sekta za maendeleo ikiwemo elimu.
 
Kwa upande wa sekta ya elimu Mkurugenzi huyo alieleza kuwa hivi sasa tayari wako
walimu wane kisiwani Pemba wanafundisha lugha ya Kiengereza na bado ameahidi kuleta
wafanyakazi wa kujitolea wakiwemo walimu wa sayansi hasa hisabati katika skuli mbali
mbali za Unguja na Pemba.
 
Mwakilishi wa Mpango wa Rais wa Marekani wa Dharura kwa Maradhi ya Ukimwi (PEPFAR),
Bwana  Brian Rettmann alisifu jitihada za Tanzania ikiwemo Zanzibar katika kupambana
na Ukimwi pamoja na Malaria.
 
Kutokana na juhudi hizo, Mwakilishi huyo alieleza haja ya kuongeza jitihada katika
maeneo ambayo wanasaidia ikiwemo miradi ya kifua kikuu, uendeshahji wa tafiti kwa
miradi mbali mbali. Aidha, alieleza kuwa Mpango huo utaimarishwa zaidi ili uweze
kuleta mafanikio kupitia hospitali Kuu ya MnaziMmoja.
 
Nae Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Moahmed Shein  kwa upande wake alimueleza Balozi huyo
pamoja na ujumbe aliofuatana nao kuwa Zanzibar inathamini sana ushirikiano kati yake
na Marekani pamoja na juhudi zake za kuunga mkono miradi ya Zanzibar.
 
Aidha, Dk. Shein alimpongeza Balozi huyo wa Marekani nchini Tanzania kwa juhudi
 anazozichukua katika kuhakikisha Zanzibar inaendelea kuungwa mkono na nchi hiyo.
 
Dk. Shein pia, aliwapongeza wajumbe hao aliofuatana nao kwa usimamiazi mzuri wa
miradi mbali mbali pamoja na shughuli za maendeleo wanazozitekeleza hapa nchini
pamoja na zile ambazo wameahidi kuzitekeleza.
 
Pamoja na hayo, Dk. Shein aliahuidi kuwa Zanzibar itaendelea kuiimarisha miradi yote
inayoungwa mkono na Marekani na kuahidi kuunda timu iliyoimara na uzoefu katika
kusimamia kwa umakini zaidi miradi ya awamu ya pili ya MCC nchini. 
 
Dk. Shein alitoa pongezi kwa Balozi huyo kwa kuendelea kuitangaza vyema Zanzibar na
kumueleza kuwa licha ya matokeo ya uvunjifyu wa amani yaliosababishwa na vikundi vya
watu wachahe  yaliotokea hapa nchini bado Zanzibar ni salama. 
 
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822  
  E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4817,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Marekani yavutiwa na Zanzibafr
Marekani yavutiwa na Zanzibafr
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhIB929zsnIvr_6_EgldQ1xVAPWfF-DpONkarqXUM_iwiSl42pslaG2NcWlaLiFOSOtZiZHyQNjVxfGflIaZboMfBOp12IJJac_LFE0ouVCgkNBjEcm7iVWZhDXoOhX9Fk5obdHqjBVG1Of/s320/DK+SHEIN.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhIB929zsnIvr_6_EgldQ1xVAPWfF-DpONkarqXUM_iwiSl42pslaG2NcWlaLiFOSOtZiZHyQNjVxfGflIaZboMfBOp12IJJac_LFE0ouVCgkNBjEcm7iVWZhDXoOhX9Fk5obdHqjBVG1Of/s72-c/DK+SHEIN.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2013/01/marekani-yavutiwa-na-zanzibafr.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2013/01/marekani-yavutiwa-na-zanzibafr.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy