HomeHabari

HISTORIA YAANDIKWA UTEKELEZAJI MRADI WA CHUMA

📌 Ni Mradi wa Dola Milioni 77 kwa Maendeleo ya Viwanda Nchini 📌 Utafiti Waonesha Uwepo wa Tani Milioni 101 za Chuma 📌 Dkt. Bite...

📌 Ni Mradi wa Dola Milioni 77 kwa Maendeleo ya Viwanda Nchini 📌 Utafiti Waonesha Uwepo wa Tani Milioni 101 za Chuma 📌 Dkt. Biteko Ahimiza Wananjombe Kutumia Fursa za Mradi 📌 TANESCO, REA Wapewa Siku 5 Kushauri Namna ya Kufikisha Umeme Vijiji 10 Ludewa Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Tanzania imeandika historia mpya ya matumizi ya rasilimali zake kufuatia kusainiwa kwa utekelezaji wa mradi wa uchimbaji wa chuma wenye thamani ya dola milioni 77. Mradi huo ambao utatekelezwa katika eneo la Maganga Matitu Wilayani Njombe unatarajiwa kuchochea maendeleo ya viwanda nchini na hivyo kukuza uchumi wa nchi. Akizungumza Agosti 2, 2024 mkoani Njombe mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Uchimbaji Madini ya Chuma Maganga Matitu kati ya Shirika la Maendeleo la Taifa NDC na Kampuni ya Fujian Hexingwang Industry Tanzania .Co.Ltd. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema mafanikio hayo yametokana na jitihada za Serikali kuchochea matumizi sahihi ya rasilimali kwa manufaa ya Watanzania. ‘‘ Mhe. Rais amekuwa muumini wa kuikaribisha sekta binafsi iweze kushiriki kwenye uchumi wa nchi yetu ili tupate kodi na ajira kwa vijana wetu. Mradi huu na mingine mtaona dhamira yake ya kuona chuma kinachimbwa na kinapatikana,” amesema Dkt. Biteko. Anasisitiza ‘‘Ndio maana haikushangaza kulipa fidia bilioni 15 ili kupisha mradi wa Liganga na Mchuchuma ambao ndio mradi mkubwa katika bara la Afrika tunaoutegemea. Nataka niwahakikishie watu wa Ludewa na Njombe mambo mengi zaidi yanakuja tuendelee kumuombea Rais Samia.” Pia ameipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa usimamizi katika hatua iliyofikiwa. Aidha, Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali imekuwa ikijenga madaraja na miradi mingine mikubwa kwa kutumia chuma kutoka nje ya nchi ilihali kuna utajiri mkubwa wa chuma kwenye ardhi ya Tanzania. Ametoa wito kwenye miradi mingine yote inayotekelezwa nchini na kusema kuwa Watanzania wanataka kuona rasilimali zilizopo kwenye maeneo yao zinaleta maana kwenye maisha yao na kuwa utaratibu wa kuwa na rasilimali eneo fulani au kuchimbwa lakini sherehe za utiaji asaini mikataba au uzinduzi zinafanyika Dar es salaam au Dodoma kuwa si sawa ni lazima kwenda kwa wananchi wenyewe na kufanya jambo hilo kwa. ‘‘ Niwaombe wawekezaji muwe na hakika kuwa hakuna hasara mtakayopata katika kuwekeza Tanzania kwa sababu nchi yetu ina mazingira mazuri ya kibiashara na mahali tunapodhani kuna changamoto Mhe. Rais amekuwa akiunda kamati ili kurekebisha kasoro ndani ya mifumo ya Serikali, mtakumbuka kuna wakati haki jinai ilikuwa inalamikiwa na aliunda kamati na mapendekezo yake yanafanyiwa kazi na sasa ameunda tume ya kupitia malalamiko ya kodi, ’’amebainisha Dkt. Biteko. Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kufanya utafiti na kuwasilisha mapendekezo ya namna ya kufikisha umeme katika vijiji 10 vilivyopo pembezoni mwa Ziwa Nyasa eneo lenye milima wilayani Ludewa. ‘‘ Nimekuja na wataalamu kutoka TANESCO na REA na nitaomba Mkuu wa Mkoa tupate mwakilishi kutoka Ludewa nataka tuunde timu ili tukapitie upya vijiji kisha tujadiliane na kukubaliana namna ya kufikisha umeme katika vijiji hivyo kama ni kwa kujenga njia kubwa ya umeme au kuweka gridi. Kazi ianze Jumatatu na ndani ya siku tano nipate majibu tujenge kwa namna gani.’’ Amesema Dkt. Biteko. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exhaud Kigahe amesema kuwa mwaka 2023, Rais Mhe. Dkt. Samia alilipa fidia ya takribani shilingi bilioni 15 kwa wananchi waliopisha maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo na mwaka 2020 aliahidi kutekelezwa kwa shughuli za uchumi ili maeneo yote ya uwekezaji yaweze kufanikiwa na sasa anamitiza ahadi yake. ‘‘ Uhakiki wa taarifa za mashapo uliofanyika mwaka 2020 katika mradi huu wa Maganga Matitu umeonesha uwepo wa mashapo ya chuma tani milioni 101 na utekelezaji wa mradi huu utaongeza mnyororo wa thamani utakaokuza uchumi wa viwanda sasa utawezesha Serikali kuokoa fedha za kigeni zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kuagiza chuma kutoka nje ya nchi.’’ Amesema Mhe. Kigahe. Naye, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo (NDC), Dkt. Nicolous Shombe amesema kuwa mradi huo wa kuzalisha chuma wa Maganga Matitu ni mradi mdogo ukilinganisha ule wa Mchuchuma na Liganga ambao tangu kuamuliwa kutekelezwa mwaka 2007 hadi kufikia hatua ya sasa ni takribani miaka 17. ‘‘ Sasa tunaenda kutekeleza mradi huu ambao Serikali itakuwa na asilimia 36 mwekezaji kutoka nchini China atakuwa na asilimia 64, kwa kiasi kikubwa katika mradi huu Serikali inaenda kuhusika moja kwa moja kulingana na muundo wake wa menejimenti na bodi,’’amesema Dkt. Shombe. Ameongeza ‘‘ Mradi huu utazalisha chuma ghafi ambacho kitatumiwa na vyuma vingine na hivyo tutakuwa na uchumi shindani kwa kuzalisha vyuma vitakavyotumika katika miradi mikubwa ya miundombinu. Katika mradi huu tunatarajia kuwekeza zaidi ya dola milioni 77.45 ambazo ni fedha za mtaji kutoka kwa mwekezaji na uzalishaji utaanza mwaka 2027, wananchi 385 watalipwa fidia kabla ya mwezi Januari ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 4.25.’’ Vilevile, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Fujian Hexingwang Industry Tanzania .Co.Ltd. Bw. Ix Xsinda amesema kuwa Kampuni yake imewekeza nchini kwa miaka nane na kuwa inamiliki kiwanda cha nondo kilichopo Mkuranga mkoani Pwani. ‘‘Namshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali kwa ujumla kwa kuniamini ili niweze kufanya uwekezaji huu, kwa upekee nawashukuru NDC kwa kuhakikisha nafanikiwa kuwekeza katika mradi nawahakikishia wananchi wa Njombe kwamba nitawekeza katika mradi huu kama tulivyokubaliana katika mkataba kwa sababu Mhe. Rais na Serikali yake wamenipa imani kubwa. Nitaanza utekelezaji baada ya kusaini mkataba huu na taratibu zingine kukamilika.’’ Amemaliza Bw Xsinda. Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa Mkoa wake utahakikisha unaweka mazingira rafiki kwa wawekezaji watakaowekeza mkoani humo Mwisho.
Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,313,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,246,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,Habari,5016,habari dodoma,20,habari. dodoma,31,habaria,1,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,514,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,352,muziki na fasheni,6,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,2,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,2,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: HISTORIA YAANDIKWA UTEKELEZAJI MRADI WA CHUMA
HISTORIA YAANDIKWA UTEKELEZAJI MRADI WA CHUMA
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2024/08/historia-yaandikwa-utekelezaji-mradi-wa.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2024/08/historia-yaandikwa-utekelezaji-mradi-wa.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy