Wakati Tanzania ikiwa imevuka salama tarehe 25 Desemba huku kukiwa na utulivu wa kupigiwa mfano, kumeibuka mjadala mzito kufuatia kauli ya A...
Wakati Tanzania ikiwa imevuka salama tarehe 25 Desemba huku kukiwa na utulivu wa kupigiwa mfano, kumeibuka mjadala mzito kufuatia kauli ya Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi ambaye katika homilia yake, aliwaita waumini walioandika barua Vatican kumshitaki Padri Charles Kitima kuwa ni "malofa," "vibaraka," na "wasaliti," jambo ambalo limeleta taharuki miongoni mwa waumini wanaopigania amani na haki.
Kwa mujibu wa Sheria za Kanisa Katoliki, kila muumini ana haki ya kufikisha malalamiko yake kwa Baba Mtakatifu endapo anaona mwenendo wa viongozi wa chini unahatarisha imani au amani. Hatua yao ya kwenda kwa Papa Leo XIV imelenga kulinda Kanisa lisivutwe kwenye mivutano ya kisiasa inayoweza kuamsha machafuko nchini.
Hatua ya muumini kutafuta haki kwa Baba Mtakatifu siyo usaliti, bali ni utaratibu rasmi wa kanisa kuhakikisha sauti ya kila mwana-kondoo inasikika. Kitendo cha kiongozi kutumia madhabahu kudhalilisha haki hiyo kinatafsiriwa kama ukiukaji wa misingi ya unyenyekevu.
Kauli za Askofu Ruwa'ichi zinatolewa wakati kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, akisisitiza ujumbe wa amani na upatanishi akisisitiza kuwa:Kanisa linapaswa kuwa "daraja" la kuunganisha watu, siyo chombo cha kutenga au kukashifu,Viongozi wanapaswa kutofautisha kati ya mivutano ya kisiasa na huduma ya kiroho kwa waumini wote na Amani ya "kudumu na ya kidiplomasia" ndiyo msingi wa kutafuta haki yoyote ile.
Wakati waumini nchini Tanzania wakilinda amani kwa gharama yoyote, kauli za Askofu zinazodai "kutafuta haki" kwa kutumia lugha ya dharau zimeleta hofu ya kuchochea taharuki. Wazalendo wanahoji: Inawezekaje kudai haki huku ukiwaita waumini "malofa"? Historia inatufundisha kuwa amani inapotoweka, haki haiwezi kupatikana. Amani ya Tanzania ni tunu inayopaswa kulindwa kwa kauli za busara, siyo kwa kebehi madhabahuni.
Katika hali iliyoelezwa na wengi kama "mshtuko wa kiroho," kauli ya kumwita muumini "lofa," "kibaraka," na "msaliti" kwa sababu tu ametumia haki yake ya kikatiba na kidini kuelezea malalamiko yake, imetafsiriwa kama ukiukwaji wa misingi ya upendo na unyenyekevu aliyoacha Yesu Kristo.
Licha ya jitihada za wachochezi wa nje na ndani waliotamani kuona machafuko tarehe 25 Desemba, Watanzania wamezidi kuimarika katika umoja. Waumini sasa wanatoa wito kwa viongozi wao kufuata nyayo za Papa Leo XIV: kurejea kwenye lugha ya upendo, kuheshimu haki za waumini, na kuacha kuhusisha madhabahu na mivutano inayoweza kuhatarisha utulivu wa taifa.
Waumini wengi wamehoji: Ikiwa viongozi wa dini wanahubiri haki kila siku, ni kwa nini wanawanyima haki hiyo hiyo waumini wao wanapotaka kuwasiliana na mamlaka za juu (Roma) kuelezea hisia zao?
Inasikitisha kuona kuwa, wakati wananchi wanapambana kulinda taswira ya nchi, ndani ya nyumba za ibada maneno makali yanatumika kudhalilisha watu wenye maoni tofauti. "Huwezi kudai haki huku unatumia lugha ya kidikteta dhidi ya kondoo unaowachunga," alisema mmoja wa waumini aliyekwazwa na kauli hizo.
Wachambuzi wa mambo ya kiroho na wazalendo wamekumbusha kuwa Biblia inakataza lugha ya magomvi na inasisitiza utii kwa mamlaka.Warumi 13:1-2 inasisitiza kuwa mamlaka zote zimewekwa na Mungu, na anayezipinga anapinga agizo la Mungu. Aidha Mathayo 5:9 inasema heri wapatanishi, lakini kauli za kuwaita waumini "malofa" zinatajwa kama mbegu ya utengano inayoweza kuchochea vurugu badala ya amani.
Licha ya kuwepo kwa shinikizo na matarajio ya watu kama Mange Kimambi na washirika wake waliotabiri machafuko tarehe 25 Desemba, Watanzania wameonesha ukomavu. Hakuna chombo cha habari cha kimataifa kilichopata picha ya vurugu walizokuwa wakizisubiri.
Tanzania ni nchi ya amani. Kiongozi yeyote anayetumia jukwaa lake kuchochea chuki au kudharau utu wa Mtanzania kwa kuitwa "lofa," anapaswa kutambua kuwa zama za waumini kufuata mkumbo bila kuhoji zimepitwa na wakati. Watanzania wanataka viongozi wanaojenga madaraja ya amani, siyo wanaobomoa kwa lugha za kashfa.
Haki ya Kikanisa na Msimamo wa Papa Leo XIV
Waumini hao wanashikilia kuwa, kwa mujibu wa Sheria za Kanisa Katoliki, kila muumini ana haki ya kufikisha malalamiko yake kwa Baba Mtakatifu endapo anaona mwenendo wa viongozi wa chini unahatarisha imani au amani. Hatua yao ya kwenda kwa Papa Leo XIV imelenga kulinda Kanisa lisivutwe kwenye mivutano ya kisiasa inayoweza kuamsha machafuko nchini.
Msimamo wa Papa Leo XIV tangu ashike kiti cha Mtakatifu Petro mwezi Mei 2025 umekuwa ni:Kujenga madaraja ya amani na kuepuka lugha zinazobomoa umoja wa waumini,Kutofautisha huduma ya kiroho na harakati za kisiasa ambazo zinaweza kuleta mpasuko na kuhimiza diplomasia na unyenyekevu katika kutatua migogoro ndani ya nchi.
Hakuna Haki Bila Amani
Hoja kuu ya waumini wanaopingwa na Askofu Ruwa'ichi ni kwamba "Haki" haiwezi kupatikana kupitia lugha za kashfa au uchochezi wa vurugu. Wanahoji ni kwa nini madhabahu inatumika kuwashambulia waumini (malofa) ambao kimsingi ndio walengwa wakuu wa upendo wa Kristo.
Aidha baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki, wakiongozwa na Mackdeo Shilinde na Gerald Abel, wamejitokeza hadharani kupinga vikali kauli za Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, wakidai kuwa homilia yake ya Krismasi ilitawaliwa na lugha ya matusi, vitisho, na hukumu badala ya faraja.
Katika taarifa yao kwa umma iliyotolewa Desemba 27, 2025, waumini hao wamesisitiza kuwa matumizi ya mimbari kushambulia watu waliowasilisha hoja halali kwa Balozi wa Vatican ni ukiukwaji wa misingi ya Kikristo na maadili ya uongozi wa kiroho yanayopaswa kuongozwa na upendo na haki.
Waumini hao wamebainisha kuwa mimbari ni mahali patakatifu pa kuhubiri Neno la Mungu na kuimarisha mshikamano, na si jukwaa la kueneza chuki, hofu, au kuwavua waumini hadhi yao ya Ukristo hadharani kama alivyofanya Askofu Ruwa’ichi tarehe 25 Desemba.
Wamesema matumizi ya maneno mazito na ya udhalilishaji yanakwenda kinyume na mafundisho ya Yesu Kristo na mwelekeo wa amani na upatanishi unaosisitizwa na kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, tangu ashike kiti hicho Mei 2025.
Wakati vyombo vya habari vya kimataifa kama CNN na BBC vilivyokuwa vikisubiri kuona Tanzania inavurugika vikiambulia patupu, waumini hawa wanasisitiza kuwa amani ya Tanzania iliyoshinda tarehe 25 Desemba ndiyo inapaswa kulindwa na viongozi wa dini, badala ya kutoa kauli zinazoweza kutoa mwanya kwa maadui wa nchi kufanya vurugu.
Waumini wameeleza kuwa kuitwa "wasaliti" hakutawarudisha nyuma katika kutafuta ukweli. Wanasubiri majibu kutoka Vatican, wakiamini kuwa Papa Leo XIV, ambaye amekuwa akisisitiza amani duniani kote, atatoa mwongozo utakaorejesha nidhamu na utulivu ndani ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na kuondoa lugha za kebehi dhidi ya waumini wanyonge.

COMMENTS