Kutoka Kanisani Hadi Shambani: Simulizi ya Sista Aliyenolewa na Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi

Na Mwandishi Wetu, Laela Rukwa Katika kuta za utulivu za Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kanisa Katoliki kilichopo Laela, mkoani Rukwa, sauti ...



Na Mwandishi Wetu, Laela Rukwa

Katika kuta za utulivu za Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kanisa Katoliki kilichopo Laela, mkoani Rukwa, sauti ya shukrani imesikika kutoka kwa mtawa mmoja aliyepata fursa ya kipekee ya kujinoa kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi (Uanagenzi). 

Mtawa huyo, Sista Vestina Damian ambaye sasa amekuwa ishara ya matumaini na weledi, anasimulia jinsi mafunzo ya vitendo aliyoyapata yalivyomgeuza kutoka kuwa mwanafunzi wa nadharia na kuwa mtaalamu aliyepikwa vyema.

Maelezo hayo yalitolewa mbele ya Maofisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano wakiongozwa na Msemaji Mkuu wa Ofisi hiyo Revocatus Kassimba waliofika chuoni hapo kufuatilia utekelezaji wa mafunzo ya uanagenzi.

Sista Vestina Damian, akiwa mmoja wa wanufaika wa programu hiyo, alieleza kwa msisitizo namna mafunzo hayo ya uanagenzi yaliyochukua miezi minane yalivyomjengea weledi wa kitaalamu katika kilimo na ufugaji wa kisasa.

Alibainisha kuwa, kupitia mchanganyiko wa nadharia na vitendo, ameweza kujifunza mbinu za kisasa za kilimo cha umwagiliaji, matumizi sahihi ya mbolea, na mbegu bora zinazohimili mabadiliko ya tabianchi, maarifa ambayo sasa anayatumia kuifanya bustani na mashamba ya utawani kuwa mfano wa kuigwa katika eneo la Laela.

Upande wa mifugo, Sista huyo alieleza kuwa programu hiyo imemsaidia kuelewa kanuni za kitaalamu za ufugaji wa kisasa, ikiwemo ujenzi wa maboma bora, utayarishaji wa lishe mchanganyiko, na udhibiti wa magonjwa. 

Alibainisha kuwa maarifa hayo aliyopata yamemwezesha kusaidia jamii inayomzunguka na hivyo kukuza tija katika kilimo na ufugaji, jambo ambalo linaendana na dhamira ya Serikali ya kuongeza tija na uzalishaji ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi.



“Ujuzi huu umenipa heshima kubwa kwa jamii yanguj kwani umenipa uwezo wa kuhudumia watu wangu kwa weledi zaidi,” alieleza Sista Vestina Damian mbele ya maofisa hao na wanajamii wengine. 

Akiwa amevalia mavazi yake ya kitawa , Sista Vestina Damian anasifu uamuzi wa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) kwa kuweka mfumo unaoruhusu wananchi wa kada zote kupata ujuzi stahiki. Kwake, uanagenzi huo haukuwa tu mafunzo ya darasani, bali ulikuwa ni ukombozi wa fikra uliompa ujasiri wa kwenda kusimamia miradi ya uzalishaji inayolenga kuwasaidia wahitaji na jamii inayomzunguka.

"Naishukuru Serikali, namshukuru mama Samia  kwa kutupa fursa hii sisi wananchi wake, bila kujali nafasi zetu," anasema Sista Vestina Damian huyo kwa unyenyekevu. 

Alisisitiza katika shukurani zake kuwa ujuzi alioupata chuoni Laela ni hazina itakayotumika kuimarisha ustawi wa jamii kwa ujumla, huku akitoa rai kwa Serikali kuendelea kutanua wigo wa programu hiyo ili kuwafikia vijana na wahitaji wengi zaidi katika maeneo ya pembezoni.

Chini ya kaulimbiu isemayo “Nguvukazi yenye Ujuzi Stahiki kwa Ajira Endelevu,” Serikali imeweka bayana dhamira yake ya kupunguza pengo la ujuzi linalowakabili vijana wengi nchini. Programu hii inalenga kuleta mabadiliko ya kifikra na kiuchumi kwa kutoa mafunzo yanayoakisi mahitaji halisi ya soko la ajira, yakijikita katika mchanganyiko wa nadharia na vitendo.

Uzinduzi wa awamu ya nane ya programu hii, umefanyika Machi 8 mwaka huu.Uendelevu wa programu unakuja wakati ambapo nchi inajipanga kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, ikihitaji nguvukazi yenye ushindani wa kimataifa. Katika awamu hii, Serikali imewekeza rasilimali nyingi kuwafikia vijana 5,746 nchi nzima.

Mafunzo yanatolewa kupitia vyuo 46 vilivyosambaa katika mikoa 25 ya Tanzania Bara, ambapo vyuo 29 ni vya Serikali na 17 ni vya sekta binafsi (ikiwemo Chuo cha Laela).

Programu hii ya uanagenzi ni sehemu ya mikakati ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano katika kuhakikisha kuwa nguvukazi ya Taifa inapata stadi muhimu za kuajirika au kujiajiri, hivyo kuchochea ukuaji jumuishi wa uchumi kuelekea mwaka 2050.


COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,405,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,275,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,2,Habari,6507,habari dodoma,38,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,688,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,370,muziki na fasheni,19,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,6,SAYANSI ANGA,7,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Kutoka Kanisani Hadi Shambani: Simulizi ya Sista Aliyenolewa na Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi
Kutoka Kanisani Hadi Shambani: Simulizi ya Sista Aliyenolewa na Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjUtaHtmGn085ilRvFs8tW0iWzOgSP1Uhjuf2lISrNkmaFW5mNuwstpwleklrAhmXbscfWPrVjivDGRfJU4wA9rTfw2RiECPGeMCwuZXUYcun98cXlw6aLS1rP-ETaZe5__oJNxMaU2FV2maxG4xi5H3kEHbD_sIeFyJbGR5bSD0hUYouKDHXGpH-DlGbyN/s320/sista.jfif
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjUtaHtmGn085ilRvFs8tW0iWzOgSP1Uhjuf2lISrNkmaFW5mNuwstpwleklrAhmXbscfWPrVjivDGRfJU4wA9rTfw2RiECPGeMCwuZXUYcun98cXlw6aLS1rP-ETaZe5__oJNxMaU2FV2maxG4xi5H3kEHbD_sIeFyJbGR5bSD0hUYouKDHXGpH-DlGbyN/s72-c/sista.jfif
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2026/03/kutoka-kanisani-hadi-shambani-simulizi.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2026/03/kutoka-kanisani-hadi-shambani-simulizi.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy