Tanzania mwenyeji Doha Dialogue Oktoba 2026

Na Beda Msimbe  BSKY Media Tanzania inatarajia kuweka historia mpya kwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa ...




Na Beda Msimbe  BSKY Media


Tanzania inatarajia kuweka historia mpya kwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, utakaofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 6 Oktoba 2026 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 

Mkutano huu wa kiwango cha juu kimataifa unatazamiwa kuwakutanisha wajumbe na viongozi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, Baraza la Ushirikiano wa nchi za Ghuba ambazo ni Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Qatar, Kuwait, Oman na Bahrain, pamoja na Jordan na Lebanon (GCC+), huku ukiwa na lengo kuu la kuimarisha ushirikiano katika kusimamia uhamaji wa nguvu kazi na kukuza ajira zenye staha. 

Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.   

Akizungumzia maandalizi na umuhimu wa mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Clement Sangu, amesema kuwa mkutano huo unakuja kufuatia mafanikio ya mkutano wa kwanza uliofanyika jijini Doha, Qatar, tarehe 21 hadi 22 Mei 2024, ukihusisha nchi 33 zikiwemo nchi 25 za Afrika na nchi za Ghuba pamoja na Jordan na Lebanon.

 Katika mkutano huo wa kwanza, Tanzania ilishiriki kikamilifu kupitia ujumbe ulioongozwa na Wizara yenye dhamana ya Kazi na Ajira, ambapo Doha Declaration iliweka msingi thabiti wa kuendeleza majadiliano na ushirikiano huo kila baada ya miaka miwili. 

 Waziri Sangu amefafanua kuwa maeneo muhimu yatakayojadiliwa katika mkutano huu wa Dar es Salaam ni pamoja na uimarishaji wa mikataba ya ajira baina ya nchi na nchi (Bilateral Labour Migration Agreements), uoanishaji wa ujuzi wa wafanyakazi na mahitaji halisi ya soko la ajira, na ujenzi wa mifumo ya uhamaji wa nguvu kazi inayoweza kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji mapya ya soko la ajira lenye staha. 

Aidha, mkutano huo utatoa fursa ya kimkakati kwa Tanzania kuimarisha nafasi yake katika mijadala ya kimataifa kuhusu uhamaji wa nguvu kazi, kupanua fursa za ajira nje ya nchi, kulinda haki za wafanyakazi wahamaji, na kuongeza ushindani wa nguvu kazi ya Kitanzania huku ukichangia katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.  

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeelezwa kuendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha uhamaji salama na wenye tija kwa wafanyakazi wahamaji kupitia mikataba ya kimataifa na nchi za Ghuba, kuunganisha wafanyakazi wahamaji na fursa za ajira katika nyanja mbalimbali kama vile kilimo, mifugo, utabibu, ujenzi, uhandisi, udereva, upishi na huduma za majumbani. 




Hatua nyingine ni pamoja na kuweka utaratibu wa kusajili na kusimamia wakala binafsi wa ajira kwa kuzingatia sheria na viwango vya kimataifa, kuweka mifumo ya kuwezesha rasilimali fedha kwa wafanyakazi kugharamia mahitaji muhimu, na kuimarisha mifumo ya kidijitali ikiwemo Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Soko la Ajira unaolenga kuboresha uajiri na ulinzi wa wafanyakazi wahamaji.  

Waziri Sangu amesisitiza kuwa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue ni fursa ya kipekee ya kugeuza ahadi na makubaliano kuwa hatua za vitendo na matokeo yanayopimika, akibainisha kuwa Tanzania inaamini kupitia ushirikiano thabiti kati ya Afrika na GCC+, mkutano huo utaimarisha uhamaji salama, rasmi, wa haki na endelevu, kufungua milango ya ajira kimataifa kwa Watanzania, na kujenga misingi ya ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi zinazopeleka na zinazopokea wafanyakazi.

Mkutano huo unafanyika huku idadi ya watanzania wlaiopo nchi za nje kwa kupitia mifumo ya serikali  wanakadiriwa kufikia elfu 15 kuanzia mwaka jana hadi mwaka huu na kwamba mipango zaidi ikiwa inasukwa ya ajira zaidi.

Katika kikao hicho na waandishi wa habari Waziri Sangu pia  amesema kwamba hivi karibuni watatangaza ajira 600 za wahandisi na mafunbdi mchundo.

Aidha alisema kwamba traifa linazidi kupata heshima kutokana na nguvu kazi inayoenda nje kujua wajibu wake kujituma na kuwa na nidhamu. Anasema hayo ni matokeo ya utaratibu mzima wa kuweka mazingira sawa na kuwezesha watanzania kutafuta kazi zenye staha ughaibuni.

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,473,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,318,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7677,habari dodoma,41,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,27,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,7,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,775,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,21,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,10,SAYANSI ANGA,16,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Tanzania mwenyeji Doha Dialogue Oktoba 2026
Tanzania mwenyeji Doha Dialogue Oktoba 2026
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgbEOoT-9N8yLwlOuVavFkhr5Qs5q3cQ25urnd2zBkk2ghj7MQ73qG7jxuq9rtmECNwwppiHtktzPouz2sohqjup0TRX80v-nuX3NF4-hW0aVbOpzWNouN_qdaEWO2x1FEOtC1VngJg_de2iANU3nykF1I1f_AKr0SQdshW_J8jzP6sviYPJPfqv-3c_c19/s320/sangu%20doha.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgbEOoT-9N8yLwlOuVavFkhr5Qs5q3cQ25urnd2zBkk2ghj7MQ73qG7jxuq9rtmECNwwppiHtktzPouz2sohqjup0TRX80v-nuX3NF4-hW0aVbOpzWNouN_qdaEWO2x1FEOtC1VngJg_de2iANU3nykF1I1f_AKr0SQdshW_J8jzP6sviYPJPfqv-3c_c19/s72-c/sangu%20doha.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2026/09/tanzania-mwenyeji-doha-dialogue-oktoba.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2026/09/tanzania-mwenyeji-doha-dialogue-oktoba.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy