MAKALA

                             MAKALA ya Uhuru
Desemba 9, 1961, Tanzania ilipata Uhuru  chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Je, Uhuru huu unamaanisha nini kwetu? Leo hii tunaweza kusimama kidete na kusema ni Uhuru wa kweli unaotuondoa kwenye utegemezi wa wakoloni tulioachana nao, unaotufanya tuamue mambo yetu wenyewe kama taifa, unaotuondoa kubughudhiwa na kuingiliwa na mambo kama magonjwa, njaa, upungufu wa umeme, umasikini na ujinga? Tupo huru kweli, hebu msikilize Beda Msimbe anavyochambua Uhuru wa Tanganyika na sasa Tanzania, ikiwa imepita kwenye awamu tatu, na sasa ya nne inaingia ngwe ya pili. Anaaangalia yote hayo na kushauri nini kifanyike zaidi ili Uhuru uwe wa kweli au kuuimarisha, furahia makala hii...


Gavana wa mwisho akisindikizwa melini na Julius Nyerere
Tanzanzania  ya miaka ya sasa inazungumza ufisadi zaidi kuliko hatga kuangalia historia yao na kuangalia wapi walipojikwaa na badakla yake wanaangalia wapi walipoangukia.Wakati mwalimu Nyerere anahutibia Bunge kwa mara ya kwanza baada ta Tanganyika kupata Uhuru alionesha wazi njia ya kufuata, sehemu kubwa ya njia hiyo ni kupata maendeleo ya kweli kibinadamu kama nchi kwa kupigana na maadui watatu ambao ni umaskini, ujinga na maradhi.

Kwa kauli yake hiyo alidhamiria kuonesha njia ya kuondokana na utegemezi na katika kipindi hicho kauli yake haikuwa Uhuru kazi ya Tanu bali ni Uhuru na Kazi.

Hata wakati wa kuangalia miaka mitano ya mwanzo ya uhuru mwaka 1965 historia iliandika mengi lakini mtu ambaye aliandika kauli tata zilizojadiliwa kwa kina ni Henry Bienen. Mwandishi huyu katika kitabu chake cha Tanzania: Party Transformation and Economic Development ilichotolewa na  Princeton Unmiversity Press mwaka 1967 alizungumzia kwa kina siasa za Tanzania na maendeleo yake.

Huenda maneno aliyoyasema wakati huo ingawa wachambuzi wenzake wa enzi hizo walisema maandishi yake yamepitwa na wakati kutokana na kutokea kwa Azimio la Arusha, ukiyatazama hutaweza kuyakana kwa leo wakati kilio cha Tanzania ni ufisadi na mipango ya maendeleo isiyotekelezeka au isiyokuwa endelevu.

Mwandishi huyo wa zamani alikuwa anazungumzia haja ya mipangilio ya kisiasa ya wazi ambayo juu yake ndipo mipango ya maendeleo inaweza kusukwa kwa ajili ya kusukuma mbele gudrudumu la maendeleo. Kwake yeye aliona wazi kwamba Tanzania haijapambanua mfumo wa kufuata katika kujenga uchumi wake na haiwezi kuwa rahisi kuendelea kutegemea mihimili ya kikoloni kupata maendeleo ya kweli. Mwandishi huyo alisema wazi kwamba pamoja na Tanu kuwa na uwezo wa kushawishi watu lakini shauri la kiuchumi lilikuwa ni dogo na kama vile halina mwelekeo wa kweli  kama taifa lilififishwa na uwezo mdogo wa kati ndani ya chama wa kubuni mipango na kuiweka katika utekelezaji wa kweli.

Shida kubwa ya hali hiyo kwa mujibu wa mwandishi huyo ilitokana na  uongozi sehemu kubwa kuanza mchakato wa kujineemesha na kuchukua vivazi vya wazungu waliondoka na kuachana na falsafa nzima ya kuutafuta uhuru.

Kuwepo kwa mwelekeo usioeleweka wa kijamaa kwa mfumo wa Mao na Marx  haukutoa nafasi kubwa ya mabadiko ya kasi kutokana na tofauti za matabaka. Hali ambayo ilijionesha na kusababisha kuzaliwa kwa Azimio la Arusha kasha kuwapo kwa Elimu ya kujitegemea na badaye ujamaa na maendeleo vijijini.

Huenda Bienen kutokana na Uamaerika wake alikosea kuzungumza jinsi mkanganyiko wa siasa na mchuano wa matabaka unavyomaliza nchi kwa kukosa msingi imara wa kisiasa wa kujenga miundo mbinu ya maendeleo kipindi hicho lakini upo ukweli wa leo kwamba taifa la Tanzania limerejea katika mchakato wa miaka hiyo ya mwanzo ya uhuru kutokana na kuchipuka kw amsuguano mwingine wa kitabaka ambapo wanajiotokeza watu ambao wanajijazia mali wanafanya hivyo kwa kuitafuna nchi kwa njia mbalimbali.

Pengine ni Nyerere ambaye alikuwa na  mabadiiko ya kifikira pale ambapo alianza kulidhibiti tabaka hili la watu wenye nacho na wenye uwezo wa kujilimbikizia mali kuacha kufanya hivyo kwa kufikiria shauri la Ujamaa na Azimio la Arusha.

Tukiwa katika mwaka  50  bado tunaweza kujiuliza kama kweli tuko huru, Kimsingi katika dunia hii ya mtandao Tanzania bado haijawa huru katika mambo yote ambayo Julius Nyerere Rais wa kwanza wa Tanzania aliyapigania; na katika msingi mbaya wa mawazo tunaweza kusema kwamba sehemu kubwa ya maendeeo ambayo yalipatikana miaka kumi baada ya Uhuru hayapo .

Tunachofanya sasa kama ukimtazama mtunzi mwingine wa mustkabali wa Tanzania Ibrahim Werrema John katika kitabu chake cha Tanzanians to the Promised Land ni kutibia sehemu ya juu ya jeraha wakati kidonda kwa ndani bado kibichi na huenda kikawa kinavunda.

Ukimsoma Werrema sehemu kubwa ya maandishi yake utagundua kuwa anasisitiza Watanzania kuliangalia taifa lao kwa namna nyingine kutokana na umaskini mkubwa kuendelea kuwapo, tofauti kubwa ya kipato, kudidimia kwa elimu  na tatizo la uadilifu na uongozi ambao ndio nyenzo muhimu katika kufanikisha njia isiyo ya kubahatisha au kudanganya ya uchumi ambao ndio unaweza kuleta maisha bora kwa wananchi.

Kitabu hiki ambacho kimehaririwa na  Jenerali Ulimwengu na Lisa Smith Holtz kimechambuo uongozi kuanzia enzi za Mwalimu Nyerere,Mzee Mwinyi, Benjamim Mkapa na kidogo Jakaya Kiwete.Mtunzi ana maswala ya msingi ambayo anataka watanzania kuyajadili nap engine  katika upofu aliulizia  ule ukali wa kijiwe cha mlimani cha kushawishi mawazo makali ya maendeleo imeishia wapi.

Kimsingi elimu ni mkombozi wa kwanza, lakini kwa taifa ambalo linategemea utaalamu wa sayansi katika kuchimba madini kutoka nje, elimu yetu ikiwa ni bora elimu badala ya elimu bora ambayo inaweza kumfanya mtu kujitambua na kutambua haki yake katika maisha haya bila kujali uchakachuaji  unaofanywa na wanasiasa uchwara.

Ni wazi mapungufu makubwa ya ushindani na kutaka watu kuwajibika kunafanya hata kujipanga kuwa na viwanda mama kuwa ni tatizo, taifa likibaki la wachuuzi zaid kama vile hatuna raslimali za kutufanya kuwa na sauti kubw aya kicuhumi duniani; lakini hiyo kama si mbaya watanzania wanakosa ule utashi  wa kuangalia hilo kwa undani na kulipatia ufumbuzi wa utamaduni unaokubalika wa kistaarabu duniani kwa kukomaa kwa demokrasia na kutambua haki ya mtanzania kwa taifa lake . Kila mtu anadhani si wajibu wake kuangalia mustakabali wa nchi, tunabaki si tu wachuuzi bali walalamikaji wakubwa!

Ukiangalia historia ya nchi hii unaona kwamba miaka ya awali ilikuwa na shida nkubwa lakini miaka sita baadaye kukawa na nia ya dhati ya kuangalia maendeleo ya wananchi hasa kwa kuleta nidhamu ya matumizi ya madaraka na pia kuweka wazi maendeleo ya nchi yanayozingatia watu na si vitu.

Lakini kwa nchi yenye uchumi mzuri , wakati ule katani ikiwa na heshima kubwa duniani na akiba nzuri ya fedha za kigeni, Tanzania ilishindwa kuwa na sera ambayo ingeliweza kusimama kidete katika vurugu za dunia na kuibuka na misingi imara na si kwa sababu ya ubaya wa sera baada ya Azimio la Arusha, bali kutokana na uongozi wenyewe kushindwa kutafsiri vyema kanuni walizojipangia za maendeleo kwa kuzingatia falsafa mpya yenye kujali maslahi ya watu na kuona aibu ya kujilimbikizia mali.

Lakini ni wazi kuwapo kwa umoja wa kitaifa ambao unatishiwa leo na masuala mapya  yanayoambatana na matabaka ya kijamii,pia ulisabaisha misingi nya uchumi kudharaulika na kubwa la kuzingatia ni amani na utulivu.

Ingawa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani zenye sifa za kuwa shwari kijamii na kisiasa, uchumi wake ni mtego mkubwa ambnao nunaweza baadaye kuleta maporomoko makubwa ya utamaduni wa uvumilivu uliopo kwa miaka 50 sasa.

Ukiangalia kimsingi Nchi hii inapoingia katika miaka 50 bado  juhudi za kuipeleka katika nchi ya maziwa haijapata mwelekeo hasa baada ya kufumuliwa kwa azimio la Arusha ambalo lina msingi mkubwa katika uadilifu na utumishi kwa umma; ni katika hili kizazi cha uhuru kilishuhudia utulivu wa kisiasa na kijamii uliotokana na kipato kuwa karibu sawa.

Tatizo kubwa la umaskini linalotokana na msingi duni wa uchumi wa taifa na kubaki kuwa taifa la kuagiza hata sindano na vijiti vya kusafishia meno kutoka nje,ndilo hasa linazaa hata myumbisho wa maadili ambapo rushwa zimetapakaa mpaka katika ngazi ya chini kabisa ya maisha, wajumbe wa nyumba kumi wakitaka elfu moja kukuandikia karatasi ya kwenda kupeleka shauri lako Polisi.

Tatizo la Tanzania kwa sasa ni shida katika uchumi wake ambao kuparaganyika kwake kunatokana na kukosekana kwa mipango inayofuatiliwa ya kutengeneza uchumi mdogo kwa lengo la kuuboresha uchumi mkubwa.

Kukosekana kwa uchumi imara kunaleta pia adha ya kuibuka kw a matatizo mengine kwa kuwa uchumi imara husaidia sana kuimarisha utendaji wa serikali. Kwa sasa japo tunasema tumep;iga hatua mbele ya kuangamiza ujinga, lakini shida kubwa ipo katika maradhi na umaskini na ndipo hapo unapojiuliza kama kweli ujinga umetoweka katika mazingira kama haya ya sasa.

Tatizo la maradhi linazidi kukua, malaria ukimwi vikiongoza na hata maradhik yanayozuilika yanatibuka na kutishia kama kweli fedha nyingi za serikali hazitayujmima katika kukabiliana na vitu ambavyo vingeliweza kuzuilika.

Swali la msingi la kujiuliza ni katika mazingira haya ya miaka 50 na mawazo yale yale na matatizo yale yale tuliyokuwa nayo wakati tunapata uhuru, kweli tunaweza kusogea mbele? Tukiw abado tunatawaliwa na kupokea misaada ya maendeleo, kweli hatuhatarishi uwezo wetu wa uhuru na kufuata wanayotaka wao hao wanatupa ruzuku yao?Si ajabu hata kuharibika kwa utamaduni wao wanatuvushia na sisi wakitutaka tuheshimu haki za binadamu pamoja na mashoga, na kuondokana na kanuni zinazozuia watu kuwa mashoga.

Nyerere alizungumzia kujilimbikizia mali akafikiria azimio la Arusha, lilileta jeuri kubwa,leo tunazungumzia mafisadi kama bidhaa iliyoletwa na Azimio la Zanzibar na tumevikwa na aibu kubwa katika kuwabana hawa walioibukia katika Azimio la Zanzibar.

Huduma za jamii bado . Ingawa zipo dalili za kuendeleo kupiga hatua kwa kukubali tulichokosea katika elimu na kujaribu kuiweka sawa kwa kuwa na jamii iliyoelimika kwa kuzingatia mpango wa maendeleo  (vision 2025).

Hatuwezi kuwa makini katika mali asili zetu iwe madini au mbuga kama hatuna elimu ya kutosha ya kuendesha mambo hayo sisi wenyewe au hata kama tukiwapa watu basi tujue nani anatuibia na nani anastahili kuwapo pale na tunamwangalia namna gani.

Kwa umri wa mtu miaka 50 hasa Afrika ni mzee mwenye busara lakini kwa taifa bado pengine linajivuta na kwa Tanzania mafanikio yaliyopatikana  katika jamii yanaonekana kutishiwa na mwenendo usiovumilika wa ufisadi na kutapanya mali  za umma kwa kuendekeza rushwa.

Pengine tunaweza kujidai kuwa tuko huru kama tutakuwa na uhakika wa sekta ya uchumi zaidi na kuhakikisha kwamba serikali inaendeshwa kwa kanuni na wafanyakazi wa serikali hawatumii vibaya madaraka yao na kusababisha matatizo kwa wananchi ambao waliwaweka pale ili kuwasaidia kuwaondolea matatizo yao.

Katika miaka 50  kuna kinachoonekana hasa kupunguza umbali na muda wa usafiri kati ya mikoa inayofanya Tanzania kutoka mji wa biashara wa Dare s salaam, Mwanza na Arusha. Barabara zimejengwa japo zinaharibika kutokana na kukosekana kwa busara zinazohitaji hasa fikira za matumizi ya reliu katika kubeba mizigo mizito.

Pengine jaribio la kufungua mikoa ya Tanzania inaweza kurekebisha hali ya uchumi, lakini kama tatizo la nishati litaendelea kutesa nchi hii kutokana na mipango isiyozingatia hali halisi ya mazingira, Tanzania ya sasa haitakuwa na tofauti na ile ambayo Mwalimu Nyerere aliichukua kutoka kwa wakoloni.
Nishati ni msingi wa uchumi wa kisasa, lakini kama hakuna maana yake hata viwanda mama haviwezi kuwapo na uimbaji wa sera usiotelekezekana ni sawa na kuwa na jeraha kubwa lilishonwa juu na ndani likaachwa bila dawa.

mwisho

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,288,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7077,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,739,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,10,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
static_page
Lukwangule Entertainment: MAKALA
MAKALA
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/p/makala.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/p/makala.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy