MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya-NHIF- umepanga kuhudumia asilimia 45 ya Watanzania wote ifikapo mwaka 2015 baada ya marekebisho ya sheria kufanyika.
Kauli hiyo imetolewa leo asubuhi katika mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Deogratias Ntukamazina wakati akizungumzia Siku ya Bima ya Afya itakayofanyika Jumatatu.
Kwa sasa mfuko huo unahudumia asilimia 5.2 ya Watanzania wote wengi wao wakiwa ni watumishi wa serikali na wakala wa serikali.
Mwenyekiti huyo wa Bodi amesema kwamba lengo kubwa la uwapo wa Mfuko kama wa Bima ya Afya ni kuhudumia wananchi wengi hasa wale wenye mahitaji maalumu, lakini kwa sasa wanashindwa kutokana na sheria.
Akizungumzia Siku ya Bima ya Afya ambayo mwaka huu inaadhimishwa wakati Mfuko unatimiza miaka saba, amesema pamoja na kuitambulisha Bima ya Afya kwa umma, shughuli za upimaji wa afya na ushauri, maelezo ya kiutendaji ya mfuko huo na shughuli nyingine za afya na utoaji vitambulisho zitafanyika.
Pichani ni Mwenyekiti Ntukamazina akizungumza huku Mkurugenzi wa mfuko huo akisikiliza kwa makini picha hii na mdau Yusuf Bad wa TSN leo asubuhi viwanja vya Mwalimu nyerere Kilwa road, dar es salaam.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO