Hofu inaua, lakini wakati mwingine tahadhari ni jambo la muhimu kuchukua, ndio maana waswahili wakasema ukikumbuka simba wakati hujafunga ml...
Hofu inaua, lakini wakati mwingine tahadhari ni jambo la muhimu kuchukua, ndio maana waswahili wakasema ukikumbuka simba wakati hujafunga mlango basi ufunge mapemaa! Majuto mjukuu.
Katika safu hii siku za nyuma, tuliwahi kutoa hoja ambayo ilikuwa pana tu, kuhusu TBC. tuliipongeza RTD kwa kutunza na kulinda utamaduni wetu na tukaihitimisha hoja hiyo kwa kuiomba TBC mpya iulinde. Mpaka sasa hakuna kilichoharibika na mambo yote yako kwenye mstari. Wakati wa amani ndio mzuri kuimarisha ulinzi, pengine hii ndio sababu inayonisukuma leo hii.
Inawezekana ni hofu yangu tu! Kurudia kulizungumzia jambo ambalo tulikwisha lisema hapo awali, lakini safari hii ninazo sababu. Sababu ambazo ninafikiri ni za msingi za kufanya hivi. Safari hii siwapongezi TBC lakini ninawatahadharisha kuhusu kile ninachokihisi na kile kinachosemwa mitaani kuhusu Shirika hili la Utanganzaji la Taifa.
Wakati naijadili hoja hii ninajua kuwa vipo vilevile hapa nchini vyombo vingine vya habari lakini ninazo sababu maalumu za kwa nini ninaiongelea TBC.
TBC ni chombo cha utangazaji cha taifa tofauti na mtu binafsi ambaye anaweza kuwa na maslahi yake binafsi ya kwa nini kaanzisha chombo chake, anaweza pia kuwa na mapenzi yake binafsi ya nini kipewe kipaumbele katika matangazo ya kituo chake. Mtu chake na pia uhuru si ndio huu.
Shirika hili kwa sasa lipo katika mchakato wa uboreshaji. Nani hajaona? Wanapendeza na vipindi kwa kweli ni vizuri. Mpaka sasa kwa kweli kazi ni nzuri, nzuri mno na wala hatungoji mpaka watu wafariki ndio tusema walilifanyika kazi nzuri shirika hili. Sisi tunasema mapema, wasikie na wajue. Tuna imani kuwa kauli za kuwaunga mkono zitawapa nguvu. Tunajua kuwa hujafa hujaumbika lakini hatuombei hayo na mungu apishie mbali na vile vile wimbo mbaya haulei mwana. Watu wawe na fikra chanya. Tusifu inapobidi na kukosoa inapobidi.
Hoja yangu katika TBC ni kuhusu vipindi vya sanaa na utamaduni vya TBC . Huko nyuma vilishakuwepo vipindi vingi vya sanaa, lugha na utamaduni kama tumbuizo asilia, mama na mwana, asilia salamu, ngoma zetu, michezo ya Radio, mahoka, maneno hayo, mwanamuziki wa wiki nk. Katika gazeti la uhuru kulikuwa na kolamu ya Radioni leo ambapo vipindi vyote vilionekana vizuri.
Sasa hivi tupo katika ulimwengu mwingine kabisa tofauti na ule wa zamani. Ulimwengu wa sasa ni ule unaoitaka TBC ijiimarishe na kuhimili sio tu mikiki ya ushindani lakini pia ya kukifanya chombo hiki kijitegemee. TBC inayo changamoto kubwa ya kuwianisha mambo matatu ambayo ni kujiimarisha kiushidani, kujitegemea na kuyashika makundi yote ya rika zote (wazee na vijana) na vilevile kuendeleza urithi wa taifa hili katika nyanja za sanaa, lugha na utamaduni.!
Katika mabadiliko kama haya TBC inayo mipango ya mageuzi ya kuongeza idhaa zake. Hili si jambo geni hasa kwa upande wa Radio kwa sababu huko nyuma TBC ilishawahi kuwa na idhaa ya Taifa, idhaa ya Biashara pamoja na idhaa ya nje ambayo ilikuwa ya ukombozi. Mungu bariki wamekumbuka moja ya studio zake na kuipa jina la ukombozi. Tatizo niloliona mimi ni kuwa baadhi ya wadau wanaona kuwa vipindi vya sanaa na utamaduni pengine havina wasikilizaji au watazamaji? Nao wana hofu kama mimi lakini hofu zetu zinapishana.
Tahadhari ninayoitoa ni jinsi gani wamejipanga kujiimarisha katika soko na kuvutia watazamaji bila kuathiri vipindi vya sanaa na utamaduni. Katika hali ya sasa kundi kubwa la watazamaji kwa vyovyote litakuwa ni la vijana. Katika hili TBC imetenga muda mrefu wa muziki usiku katika kipindi cha Boda 2 boda ambapo kuna muziki wa kizazi kipya.
Kuna wakati mheshimiwa Rais alishawahi kusema kuhusu kipindi cha ulimwengu wa kiswahili kuonyeshwa usiku uliokomaa. Pamoja na yote nafikiri mnajua kuwa watu wazima wengi RTD ndio radio waliyoizoea na bahati nzuri au mbaya hawajapata radio yenye ladha inayofanana wabadilishe.
Vipindi vilivyokuwa vina malengo ya kukuza kiswahili hata kama ndani kulikuwa na maudui mengine vimepungua. Kuna kipindi mfano cha Maneno Hayo kulichokuwa kinatoa ujumbe kwa njia ya fasihi simulizi. Watu walikipenda sana lakini kikauawa hata kabla TBC haijaundwa.
Zamani TBC ilikuwa na kikundi cha maigizo cha RTD kina marehemu mzee Jongo, Rajab Hatia na kina mama hambiliki kikundi hiki kilikuwa kinalipwa posho na RTD. Sasa hivi vitu hivi havipo, imebaki twende na wakati na changamoto na vyenyewe kukiwa na ratiba nyingine ya mchana kama wakati huu wa bunge huwezi kujua vinasikika saa ngapi!
Naizungumzia TBC Radio na Televisheni kwa sababu ndio vyombo pekee ya utangazaji ambavyo naweza kujinafasi navyo na wahusika wakasikia kilio, pongezi au lawama zangu. Hivi ni vyetu. Kwa ajili yetu. Vyombo hivi wengine ndivyo vilivyotulea. Na ninaweza kusema kwa sauti kubwa kwamba vilichangia sana kukuza maadili kwa watu wa rika langu wakati tunakuwa. Watu wanashangaa kuporomoka kwa maadili kwa baadhi ya vijana wa sasa. Pamoja na mambo mengine vyombo vyetu vya utangazaji vimechangia.
Juzi hapa wakati wa tuzo za filamu mlimsikia Mheshiwa Naibu waziri wa Habari utamaduni na michezo akiwalipongeza baraza la sanaa la Taifa BASATA kwa kuzikemea baadhi ya bendi za muziki kwa kuvaa nguo zilizostahili, baadhi ya televisheni zinaonyesha nyimbo ambazo mavazi ya wasanii hayafai. TBC isifike huko.
Mpaka leo hii TBC imevuka mabonde na vilima na nina uhakika kuwa hata mageuzi haya TBC itayavuka. Wanaosema watu hawatazami au kusikiliza vipindi vya sanaa na utamaduni nani amewambia? Wamefanya utafiti? Ni watu wa mijini au vijijini? Jamani tusifike huko. Mimi sioni kama kuna chombo kingine cha utangazaji wenye dhamira ya dhati ya kuendeleza sanaa na utamaduni wa mtanzania zaidi ya TBC.
Mageuzi yaje, sawa! Cha msingi ni kuwa yasimamiwe vizuri. TBC ikumbuke kuwa yenyewe ndio inalo jukumu la msingi kwa Taifa hili. Jukumu ambalo pengine si la lazima sana kwa vyombo vingine. Ni kwa kuzingatia hilo ndio msingi wa hoja yangu ya leo uliposimamia. Kama tumeshindwa kuimba na kucheza ngoma zetu, basi tusishindwe hata kuwarithisha watoto wetu kupitia vipindi vya Radio na Televisheni. Vinginevyo kizazi kijacho kitakuwa watanzania kwa kuzaliwa lakini watakuwa raia wa nchi ngingine kwa kauli na matendo yao.
Hoja hii ni ya maganga Feruzi anayeandikia The Football, huenda wahusika wakaona mantiki kwanini mdau wenu ameamua kuwapa hapa. Ni changamoto au vipi?

COMMENTS