Jamani nambieni huyu anayeshiriki Miss Leisure World huko China anayeonja chai ya Suzhou (wa pili kutoka kulia) ni nani walahi ? Hata sijui nani maskini lakini picha hii ninayo. Jamani wadau nani kapeleka mtu huko anaweza kunambia huyu nani na anafanya nini hasa?

Nimeambiwa na mdau mmoja kwamba kuna washiriki wapatao 76 kutoka nchi 70 duniani ambao ni warembio haswaaa wakimsaka Miss Leisure World hii si miss Universe. Mbona nimechanganyikiwa Lukwangule, wadau huu ndio unaitwa msaada katika tuta lakini si kwa dizaini ya Mbagalkka unaweza kuvunja miguu.

Hili ni shindano la kwanza na tayari tuzo ya kwanza ya kutabasamu (Miss Smile),imeshanyakuliwa na Sarah Katrina Miñoza wa Ufilipino. Uholanzi na Venezuela waliibuka wapili na watatu.Sarah Katrina Miñoza ana miaka 23.

Mshindi wa shindano hili anaondoka na kitita cha dola 10,000 na taji.
Waandazi wamesema Miss Leisure 2008 atapatikana Juni 27, 2008.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO