RAIS Jakaya Kikwete amesema wakati umefika kwa taasisi za kimataifa za fedha kuanza pia kufuatilia kwa makini uchumi wa nchi kubwa na tajiri...
RAIS Jakaya Kikwete amesema wakati umefika kwa taasisi za kimataifa za fedha kuanza pia kufuatilia kwa makini uchumi wa nchi kubwa na tajiri duniani, kama njia ya kuepukana na misukosuko katika uchumi wa dunia.
Rais Kikwete aliyasema hayoJuni 10, mjini London, Uingereza wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliohutubiwa na viongozi wa nchi 10 za Jumuiya ya Madola waliokuwa wanakutana mjini hapa, kujadili mageuzi katika taasisi za kimataifa.
Akizungumza baada ya wakuu hao kumaliza kikao chao kwenye Jumba la Marlborough mjini London, Rais Kikwete alisema ni dhahiri kuwa yanahitajika mageuzi makubwa katika taasisi za kimataifa ukiwamo Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya fedha.
Rais Kikwete alieleza kuwa badala ya taasisi hizo, hasa Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia (WB) kujihangaisha wakati wote kusimamia uchumi wa nchi masikini na zinazoendelea, wakati umefika kwa taasisi hizo kuelekeza nguvu zake kwa uchumi wa nchi tajiri.
“Ni dhahiri kuwa matatizo ya karibuni ya kunyumba kwa uchumi wa dunia kumetokana na ukweli kuwa chumi za nchi tajiri hazisimamiwi na zinajiendesha zenyewe na hii ni hitilafu kubwa,” alisema.
Alisema kuwa kama ungekuwapo utaratibu wa kutoa tahadhari mapema katika mfumo wa sasa wa uchumi wa dunia, ni dhahiri kuwa yaliyotokea majuzi yasingeweza kutokea.
“Inawezekana vipi kiasi cha Dola za Marekani bilioni mia tano kutoweka bila habari katika mfumo wa uchumi wa nchi tajiri?” aliuliza Rais Kikwete wakati wa mkutano huo wa waandishi wa habari.
Alisema kama kweli IMF na WB zingekuwa zinasimamia uchumi wa nchi tajiri, hasa za Uingereza na Marekani, ni dhahiri kuwa tusingepata hali ya kuyumba kwa uchumi wa dunia kama ilivyotokea. Alisema uchumi wa nchi tajiri zinapoyumba, uchumi wa nchi zote duniani, pia zinakumbana na dhoruba kubwa.
Viongozi wengine waliohutubia mkutano huo wa waandishi wa habari ni Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown ambaye alikuwa Mwenyekiti wa wakuu hao 10 wa Jumuia ya Madola, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Bharrat Jagdeo wa Guyana, Rais Maumoon Gayoom wa Visiwa vya Maldives na Rais Mahinda Rajapaksa wa Sri Lanka.
Wengine ni Waziri Mkuu wa Tonga, Dk. Feleti Sevele; Waziri Mkuu Patrick Manning wa Trinidad na Tobago, Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia, Najib Tun Razak na Makamu wa Rais wa Ghana, Alhaj Aliu Mahama.
Waziri Mkuu wa Mauritius, Dk. Navinchandra Ramgoolam hakuhudhuria mkutano huo wa waandishi wa habari kwa sababu aliwahi kuondoka Uingereza kurejea nyumbani baada ya kumalizika kikao hicho.
Wakuu hao wa Jumuia ya Madola walikutana London kwa siku mbili ili kujadili jinsi jumuiya hiyo inavyoweza kuhamasisha mageuzi katika taasisi za kimataifa, ukiwamo Umoja wa Mataifa, IMF na WB.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Brown alisisitiza kuwa wakuu hao katika kikao hicho, wamekubaliana kuwa wakati umefika kufanya mageuzi makubwa katika taasisi za kimataifa kwa sababu mifumo ya sasa ya taasisi hizo haiziwezesha taasisi hizo kukabiliana na changamoto za karne ya 21.

Rais na viongozi wenzake katika mkutano wa London.Picha na Ikulu
COMMENTS