TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali imepanga kununua mbolea yote tani 150,000 inayozalishwa kwenye kiwa...
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali imepanga kununua mbolea yote tani 150,000 inayozalishwa kwenye kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara ikiwa ni sehemu ya uendelezaji wa kilimo nchini.
Akizungumza alipokitembelea kiwanda hicho leo (Ijumaa Juni 13, 2008), Pinda alisema ununuzi huo utafanywa na kampuni ya Mbolea nchini (TFC) na Serikali itadhamini mkopo wa ununuzi.
Mbolea hiyo itakayogharimu kiasi cha Sh. Bilioni 60 itanunuliwa kwa awamu na itasambazwa kwenye mikoa kabla ya msimu ujao wa kilimo ili iwahi na itumiwe kikamilifu, alisema.
"Tunataka tuwe na kiasi cha uhakika cha mbolea hapa hapa nyumbani kabla ya kuhangaika na mbolea kutoka nje…Watanzania tunatumia mbolea kidogo sana hivyo inabidi tuongeze kiwango ili tuvune zaidi," aliongeza.
Akitoa mfano wa matumizi kidogo ya mbolea nchini, Waziri Mkuu alisema wakati wastani wa matumizi ya mbolea Tanzania ni kilo 8 kwa eka moja, Malawi ni kilo 27 na Afrika Kusini ni 53.
Wakati wastani wa uzalishaji nchini ni tani moja kwa eka, Malawi ni tani 3 na Afrika Kusini ni tani 6 kwa eka hiyo hiyo, alisema.
"Siyo kweli kwamba udongo wetu ni mzuri na hatuhitaji matumizi ya mbolea…wenzetu hao wa Malawi na Afrika Kusini wanavuna zaidi kwa eka kwa sababu wanatumia mbinu za kisayansi kwa kutumia mbolea," aliongeza.
Waziri Mkuu alisema inashangaza kuona mbolea ya Minjingu inagombaniwa na Kenya na Afrika Kusini, lakini Watanzania wenyewe hawashughuliki nayo badala yake wanategemea mbolea ya kuagiza kutoka nje ambayo ni ghali zaidi.
Alisema ameridhishwa na ubora wa mbolea ya Minjingu baada ya kuthibitishwa kwa utafiti wa kisayansi na kwamba kuna unafuu wa bei yake kwa vile inapatikana hapa hapa nchini ilinganishwa na ile ya kuagiza kutoka nje.
Waziri Mkuu alito changamoto kwa viongozi, hasa Wakuu wa Mikoa, kuhakikisha kuwa mbolea inasambazwa vizuri katika kila mkoa na wananchi wanahamasishwa juu ya uzuri wa matumizi yake.
Kiwanda cha Mbolea cha Minjingu kilikuwa ni mali ya umma lakini kilishindwa kufanya kazi na kikatelekezwa kabla ya kubinafsishwa. Hivi sasa kinafanya kazi na kinazalaisha wastani wa tani 150,000 kwa mwaka. Kina mpango wa kuongeza uzalishaji hadi tani 200,000 kwa mwaka.
Mbolea hiyo aina ya "phosphate" huchimbwa kutoka ardhini na asili yake ni mabaki ya kinyesi na mifupa ya ndege aina ya Flamingo. Inaaminika kuwa kuna kiasi cha tani milioni 10 za mbolea hiyo ardhini katika eneo la Minjingu.
Zamani "phosphate" kutoka Minjingu ilikuwa inatumika kama malighafi ya kutengenezea mbolea kwenye kiwanda cha mbolea cha Tanga.
Waziri Mkuu alitumia mapumziko ya Bunge linaloenelea na kikao cha bajeti mjini Dodoma kutembelea kiwanda cha Mbolea cha Minjingu.
Baada ya kutembelea Minjingu, Waziri Mkuu alitembelea makao makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) mjini Arusha na kuzungumza na menejimenti ya Shirika hilo.
Kesho (Juni 14, 2004), kabla ya kurejea Dodoma, ataanzisha matembezi ya kupanda mlima Kilimanjaro katika eneo la kupandia mlima la Machame Gate kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano ya ugonjwa wa UKIMWI.
Waziri Mkuu anafuatana na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mhe. Jeremiah Sumari; Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Asha Kigoda.
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM
Ijumaa Juni 13, 2008

COMMENTS