Warembo wanaojianda kwa ajili ya shindano la Miss Ilala 2008 watachangia damu kwenye benki ya damu muhimbili siku ya Jumatatu 23/06/2008 saa...
Warembo wanaojianda kwa ajili ya shindano la Miss Ilala 2008 watachangia damu kwenye benki ya damu muhimbili siku ya Jumatatu 23/06/2008 saa tano asubuhi.
Warembo wameamua kuchangia damu kama shughuli mojawapo ya kijamii na kwa nia ya upendo wa kuokoa maisha ya watu wote wanaohitaji msaada.
Waandaaji tunaungana na warembo wetu kwa uamuzi mzuri walioufikia na sisi tutakuwa bega kwa bega kutachangia damu siku hiyo.
Aidha tutatumia siku hiyo kuhamasisha upimaji wa afya zetu ili kusaidia jamii kupambana na ugonjwa wa ukimwi na kuelimisha jamii umuhimu wa kujilinda na maambukizo.
Pia tunawaomba watu wote wenye upendo kuungana Mrembo anayemaliza muda wake Ratifa Warioba na Miss Ilala siku hiyo ya jumatatu tuchangie damu kwa ajili ya ndugu zetu wanaoteseka kwa magonjwa mbalimbali.
Warembo wanaendelea na maandalizi kambini ndani ya hoteli ya Oceanic Resort iliyoko Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Warembo wanaendelea kufanya maandalizi ya nguvu kila mmoja akijitahidi kuelewa zaidi ya mwenzake ili kuhakikisha kwamba ananyakua taji la Miss Ilala 2008.
Kambi hiyo ina jumla ya warembo 15 ambao wanajifua vyema kuwania taji la Miss Ilala 2008 na baadae mmoja wao kunyakua taji la Miss Tanzania .
Warembo walioko kambini ni Aneth John, Lulu Kessy, Dotto Gasper Msoka, Joy Mzava, Magreth John Chacha, Anne Jacquaeline Jonathan, Irene Joseph Mgonja, Christine Adrian Sigala, Fatuma Suleiman, Joyce Yohana, Adelqueen Method Nanjozi, Herieth Froyd Kibambe, Roseleen Malisa, Sylvia Mashuda, na Nelly Kamwelu Ahmadi.
Mashindano ya ,mwaka huu ya kumtafuta Mrembo wa Ilala yanakwenda sambamba na kuadhimisha miaka kumi ya mafanikio ya miss Ilala.
Warembo watatu wa Miss Ilala katika kipindi hicho wameisha shinda taji la miss Tanzania, Warembo watatu nafasi ya pili na warembo wawili nafasi ya tatu. Warembo hao ni Hoyce temu, Jackline ntuyabaliwe (Klyne), na Anjela Damas nafasi ya kwanza.
Aminatha Keita, Mbiki Msumi na verdiana Kamugisha nafsi ya pili wakati nafasi ya tatu ya miss Tanzania ni Nargis Mohamed na Diana Muhere.
Mwaka huu mchuano ni mkali na kuna tambo za mara kwa mara miongoni mwa warembo kuhusu nafasi zao katika mashindano ya miss ilala mwaka huu.
Mwaka huu tunao warembo ambao tambo zao wanazielekeza kwenye kufanya vizuri miss World ingawa hata mataji ya Miss Ilala na Miss Tanzania hawajayapata.
Shindano la kumpata Miss Ilala 2008 litafanyika siku ya ijumaa 27/06/2008 kwenye bwawa la kuogelea ndani ya ukumbi mpya wa City Garden Club iliyoko Gerezani zamani ikijulikana Railways Club.
Mwaka huu Miss Ilala imedhaminiwa na Vodacom Tanzania, Redds Premium Cold, Channel ten, Ben Expeditions, Clouds Fm, Tahfif School & Supplies ltd, Oceanic Resort na Fabak Fashions.
Imetolewa na:

Gasper Baltazary
Mratibu Miss Ilala 2008
Pichani ni mmoja wa washiriki wa Miss Ilala ambaye amepeperusha vyema jina mpaka leo Jackline ntuyabaliwe aka Klyne.
COMMENTS