JEETU Patel anayetajwa kuwa kinara wa ufisadi kwa kuchota Sh bilioni 133 kwenye akaunti ya madeni ya nje (EPA) iliyoko Benki Kuu (BoT) pamoj...
JEETU Patel anayetajwa kuwa kinara wa ufisadi kwa kuchota Sh bilioni 133 kwenye akaunti ya madeni ya nje (EPA) iliyoko Benki Kuu (BoT) pamoja na wenzake tisa jana wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kuibia benki hiyo.
Wengine waliofikishwa mahakamani ni Devendra Vinodbhai Patel na Amit Nandy, Ketan Chohan, Johnson Lukaza, Bahati Mahenge, Davies Kamungu, Godfrey Mosha na Manase Mwakale anayeshitakiwa na mke wake Eddah Mwakale ambaye ni mwanamke pekee katika kesi hiyo ya kifisadi.
Jeetu ambaye jina lake halisi ni Jayantkumar Chandubahi Patel katika moja ya kesi anazokabiliwa nazo, anashitakiwa kwa pamoja na Devendra Vinodbhai Patel na Amit Nandy.
Kwenye shitaka hilo washitakiwa wanatuhumiwa kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo, kuiba na kujipatia Sh Bilioni 2.6 kwa kutumia kampuni yao ya Bencon ya Jijini Dar es Salaam.
Wanadaiwa waliiba fedha hizo baada ya kudanganya kuwa kampuni ya Matsushita Electric Trading Company iliwapa jukumu la kulipwa fedha hizo kupitia kampuni yao ya Bencon International Ltd.
Washitakiwa hao pia kwa pamoja wanashitakiwa kula njama, kughushi, kuiba na kujipatia tena Sh Bilioni 7.9 kwa kutumia kampuni hiyo ya Bencon International Ltd. Katika wizi huo washitakiwa hao wanadaiwa kudanganya kuwa walipewa jukumu la kulipwa fedha hizo na kampuni ya Maruben Corporation ya Japan wakati wanajua kuwa si kweli.
Hakimu Euphamia Mingi alisema dhamana kwa washitakiwa ziko wazi ila kila mshitakiwa anatakiwa kuweka mahakamani nusu ya fedha anazodaiwa kuiba na wadhamini wawili na mmoja kati yao awe ndugu wa karibu wote watasaini hati ya dhamana.
Washitakiwa hao pia wanatakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiria mahakamani, wanatakiwa wasisafiri nje ya mkoa hadi kwa ruhusa ya mahakama. Sharti lingine ni kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi wataripoti kwa mwendesha mashitaka na pale wanapokuwa na matatizo wadhamini wao watalazimika kwenda kutoa taarifa mahakamani.
Jeetu pia anashitakiwa katika kesi nyingine na Ketan Chohan na Amit Nandy ambao wanadaiwa kuiba Sh bilioni 3.3 kwa kutumia kampuni ya Navy Cut Tobacco Tanzania Limited.
Walidanganya kuwa wameruhusiwa na kampuni ya Matsushita Electric Trading Company ya Japan walipwe fedha hizo. Kesi hiyo inasikilizwa na Mkazi Neema Chusi na maamuzi ya dhamana yao yatatolewa leo.
Kinara huyo wa ufisadi pia anashitakiwa kwa wizi wa Sh bilioni 3.9 ambazo aliiba kwa kutumia kampuni ya Bina Rosorts Ltd kwa kudanganya kuwa walipewa mamlaka ya kulipwa fedha hizo na kampuni ya C. Itoh & Company Ltd ya Japan.
Katika shitaka hilo anashitakiwa kwa pamoja na wenzake Devenra Vinodbhai Patel na Nandy kesi hiyo iko mbele ya hakimu mkazi Richard Kabate.
Katika shitaka lingine Jeetu anashitakiwa kwa wizi wa Sh bilioni 4.9 kwa kushirikiana na Devenra na Nandy. Wote wanatuahumiwa kufanya wizi huo kwa kutumia kampuni Maltan Mining Company Ltd wakidanganya kuwa wameruhusiwa na kampuni ya Marubeni Corporation ya Japan walipwe fedha hizo na BoT.
Mtuhumiwa mwingine aliyefikishwa mahakamani jana ni Johnson Lukaza ambaye naye anatuhumiwa kula njama, kughushi, kuwasilisha hati ya uongo, kuiba na kujipatia Sh bilioni 6.3.
Mtuhumiwa huyo na mwenzake aliyetajwa kwa jina la Mwesiga Lukaza ambaye hakuwepo mahakamani wanadaiwa kufanya wizi huo Desemba 2005. Dhamana kwa mshtakiwa iko wazi ila mshitakiwa anatakiwa kuweka mahakamani nusu ya fedha anazodaiwa kuiba na wadhamini wawili na mmoja kati yao awe ndugu wa karibu wote watasaini hati ya dhamana.
Mshitakiwa pia anatakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahakamani, anatakiwa asisafiri nje ya mkoa hadi kwa ruhusa ya mahakama. Sharti lingine ni kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ataripoti kwa mwendesha mashitaka na pale anapokuwa na matatizo wadhamini wao atalazimika kwenda kutoa taarifa mahakamani.
Wengine ambao walifikishwa mahakamani hapo ni Bahati Mahenge, Davies Kamungu, Godfrey Mosha na Manase Mwakale anayeshitakiwa na mke wake Eddah Mwakale ambaye ni mwanamke pekee katika kesi hiyo ya kifisadi.
Washitakiwa wanatuhumiwa kuiba Sh milioni 855. 4 ambazo waliiba kwa kutumia kampuni ya Changanyikeni Residential Complex Ltd baada ya kuwasilisha nyaraka za kughushi BoT wakionyesha kuwa kampuni hiyo mkurugenzi wake Samson Mapunda ndiye aliyetoa idhini ya kulipwa fedha hizo.
Watu hao pia walishitakiwa kwa wizi wa Sh bilioni 1.2 mbali ya BoT baada ya kutumia kampuni ya Changanyikeni Residential Complex Ltd wakidai kuwa wamepewa mamlaka ya kulipwa fedha hizo na kampuni ya Marubeni Corporation ya Japan. Uamuzi wa dhamana yao utatolewa kesho na hakimu Victoria Nongwa.

COMMENTS