WANAFUNZI wawili wakazi wa wilaya ya Makete ambao wameungana kiwili wili ni miongoni mwa wanafunzi waliofaulu vizuri mtihani wakitaifa wa da...
WANAFUNZI wawili wakazi wa wilaya ya Makete ambao wameungana kiwili wili ni miongoni mwa wanafunzi waliofaulu vizuri mtihani wakitaifa wa darasa la saba ambao matokeo yake yalitangazwa jana.
Wanafunzi hao ni Consolatha Mwakikuti na Maria Mwakikuti ambao wote wamepata alama 151 huku wakitofautiana katika somo la Maarifa ya jamii kwa Consolatha kupata alama 29 na maria kupata alama 25, Sayansi Maria amemzidi Consolatha kwa kupata alama 31 kwa 29 kama ilivyo katika somo la kingereza ambalo Maria pia amemzidi Consolatha kwa kupata alama 36 kwa 34.
Jitihada za madaktari wa ndani na nje wa kuwatenganisha watoto hao hazikuweza kufanikiwa kwa kile ambacho kimekuwa kikielezwa kwamba endapo wangetenganishwa ni lazima mmoja wapo au wote wawili wangefariki dunia.
Akitangaza matokeo ya jumla ya mtihani huo ya mkoa wa Iringa (sasa mkoa wa Iringa na Njombe), Mwenyekiti wa kikao cha kuchuja majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani, Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Getrude Mpaka alisema mkoa wa Iringa umeendelea kushika nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo hayo.
Alisema kuwa mkoa wa Iringa umeongeza kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 59.65 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 63.01 cha watahiniwa wote 44,275 mwaka huu kutokana na kazi nzuri na ushirikiano uliofanywa na viongozi wa elimu kata, wilaya na mkoa katika kuongeza jitihada za kupambana na changamoto mbali mbali ndani ya sekta ya elimu.
Alisema katika matokeo hayo Manispaa ya Iringa imeongoza ikifuatiwa na Mufindi, Njombe mji, Njombe, Makete, Ludewa , Iringa na Kilolo ikishika nafasi ya mwisho kimkoa japo imepanda katika ufaulishaji kwa mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana.
Hata hivyo alisema mkoa wa Iringa umeendelea kuwa na changamoto kubwa ya wanafunzi kutofanya mtihani kutokana na utoro ambapo wanafunzi 566 ya watahiniwa wote walishindwa kufanya mtihani huo mwaka huu ikilinganisha na mwaka 2009 ambao wanafunzi 816 pia hawakufanya mtihani huo.
Mbali na Southern Highlanda na Brooke Bond, Mpaka alizitaja shule zingine zilizoingia katika tano bora kwa kufanya vizuri zaidi katika mtihani kuwa ni pamoja na Livingstone (Njombe mji), Star (Iringa mjini) na St.Dominic Savio (Iringa mjini).
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Iringa, Salum Maduhu alisema kwa ujumla kiwango cha ufaulu ndani ya mkoa wa Iringa kwa mwaka huu kimezidi kuongezeka japo changamoto kubwa ni idadi ya wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza kushindwa kufika mwisho.

COMMENTS