Richard Burton na Elizabeth Taylor wakiigiza Cleopatra napicha nyingine Taylor katika uzee wake na nyingine katika ujana wake Muigizaji Eliz...

Richard Burton na Elizabeth Taylor wakiigiza Cleopatra napicha nyingine Taylor katika uzee wake na nyingine katika ujana wake
Muigizaji Elizabeth Taylor ambaye alishawahi kuolewa mara nane huku wanaume wawili wakimuoa mara mbili baada ya kutalikiana naye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79 kutokana na tatizo la moyo.
Muigizaji huyu ambaye inaaminika kuwa mmoja wa magwiji wa uigizaji wenye kipeo cha juu wa sasa aliyepitia moja ya studio za zamani za Hollywood (MGM) amefariki leo na mara ya mwisho alitibiwa katika hospitali ya Los Angeles mwezi uliopita baada ya kupata tatizo la moyo.Alianza kufanya shughuli ya uigizaji akiwa na umri mdogo kwenye miaka ya 1940 .
Muigizaji huyu ambaye ni Mwamerika mwingereza alizaliwa mjini London Februari 27, 1932 nana kwa ujumla amekuwa ni mtu mwenye matatizo ya kiafya kila mara.
Elizabeth au Liz ambaye alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka 2009 alipata tuzo mbili za Oscars kwenye miaka ya 1960 kutokana na uigizaji wake katika sinema za Who's Afraid of Virginia Woolf na Butterfield 8 .
Msemaji wake Sally Morrison amesema kwamba muigizaji huyo alifariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center baada ya kukumbwa na ugonjwa wa moyo.Imeelezwa kuwa alikufa huku watoto wake wakiwa pamoja naye hospitalini.
Mcheza sinema huyo imeelezwa kuwa alikuwa amelazwa hospitalini kwa wiki sita sasa.
Taylor alianzia uigizaji akiwa mtoto amecheza zaidi ya sinema 50.Pamoja na kuishi maisha ya kujiachia mwanamama huyu katika miaka ya baadaye alikuwa msemaji wa masuala ya kijamii hasa ukimwi kazi ambayo ilimpatia tuzo maalumu ya oscar mwaka 1993.
Pamoja na kuleta kiwi kubwa na gumzo la kutosha kuhusu maisha yake anatambulika vyema kwa jinsi alivyotumia maisha yake hasa kule kuolewa mara mbili na muigizaji sinema Richard Burton aidha katika mwaka 1975 hadi 1976 alikuwa akiishi na balozi wa Iran nchini Marekani Ardeshir Zahedi.Na wakati wa uhusiano wao wote wawili walikuwa wameachna na wenzi wao wa ndoa.Waliachana baada ya kiongozi wa Iran Mfalme Reza Pahlavi klumshawishi Zahedi kuachana na Taylor.
Hizi ndizo ndoa zake:Conrad "Nicky" Hilton (6 Mei 1950 – 29 Januari 1951) (wakachana) Michael Wilding (21 Februari 1952 – 26 Januari 1957) (wakaachana) Michael Todd (2 Februari 1957 – 22 Machi 1958) (kifo kiliwatenganisha) Eddie Fisher (12 Mei 1959 – 6 Machi 1964) (waliachana) Richard Burton (15 Machi 1964 – 26 Juni 1974) (waliachana) Richard Burton (10 Oktoba 1975 – 29 Julai 1976) (waliachana) John Warner (4 Desemba 1976 – 7 Novemba 1982) (waliachana) Larry Fortensky (6 Oktoba 1991 – 31 Oktoba 1996) (waliachana)
Mwanamke huyu aliingia katiba tiba ya ulevi miaka ya 1980

COMMENTS