Hili ni bango ndani ya uwanja wa taifa na halisemi uwongo WAKONGWE wa soka nchini Yanga na Simba jana waliwekeana heshima baada ya kutoka sa...
Hili ni bango ndani ya uwanja wa taifa na halisemi uwongo
WAKONGWE wa soka nchini Yanga na Simba jana waliwekeana heshima baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo, yanaifanya Yanga iendelee kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi moja, kwani sasa ina pointi 39 na Simba ina pointi 38.
Hata hivyo, matokeo hayo yanaweza kuisaidia zaidi Simba ambayo imecheza mechi pungufu kulinganisha na Yanga, Simba ina mechi 17 na Yanga jana ilicheza mechi yake ya 18.
Katika mechi hiyo iliyokuwa ikioneshwa moja kwa moja na chaneli ya Supersports, Simba walikuwa wakali katika safu ya ushambuliaji, huku Yanga wakiwa imara kwenye ulinzi.
Kwa mujibu wa takwimu za Supersports, karibu muda wote wa mchezo Simba ilikuwa ikimiliki mpira ‘ball possession’ kwa asilimia 69 na Yanga asilimia 31.
Yanga ndio iliyokuwa ya kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 56 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na Stephano Mwasika.
Penalti hiyo ilitolewa na Mwamuzi Oden Mbaga wa Dar es Salaam baada ya Juma Nyosso wa Simba kumchezea vibaya Davies Mwape wa Yanga.
Mwasika alipiga penalti hiyo kwa mguu wake wa kushoto iliyokwenda kutikisa nyavu za kwenye kona ya kulia mwa goli, na kumuacha kipa Kaseja akienda kushoto mwa goli.
Kuingia kwa bao hilo kulifanya timu zote kuzidisha mashambulizi ambapo dakika ya 74 mfungaji bora wa msimu uliopita, Mussa Hassan Mgosi aliipatia Simba bao la kusawazisha.
Hata hivyo Mwamuzi Mbaga alilikataa bao hilo, akidai halikuwa bao, lakini alilikubali dakika chache baadaye baada ya kuambiwa na mmoja wa waamuzi wake washika vibendera kwamba lilikuwa bao na pia kuona marudio ya picha kwenye runinga iliyopo uwanjani.
Mgosi alifunga bao hilo kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Emmanuel Okwi na kuwa ‘wamoto’ mikononi mwa kipa wa Yanga Yaw Berko ambapo aliutema ndipo mfungaji alipouwahi na kuupiga kuelekea golini ambapo ulivuka mstari wa goli na kutoka nje, hapo ndipo kulipokuwa na mzozo na Mwamuzi Mbaga kukataa si bao kabla ya kulikubali kwa msaada wa mshika kibendera.
Katika dakika hizo, Kocha wa Simba, Patrick Phiri alitolewa nje baada ya kuingia uwanjani kuamua wachezaji wake waliokuwa wamemzunguka Mbaga wakilalamikia bao.
“Mimi nashangaa kwanini nimetolewa nje wakati nilichokuwa nakifanya ni jambo zuri tu kuwazuia wachezaji wangu walivyokuwa wanamzonga mwamuzi,”alisema Phiri alipohojiwa na Supersports.
Aidha katika mechi ya jana, mchezaji Mbwana Samatta alikosa mabao mengi ambapo mengine alikuwa karibu na kipa lakini alishikwa na kitete na kupiga juu ama nje.
Baadhi ya mabao aliyokosa Samatta ni lile la dakika ya 26, dakika ya 38, na dakika ya 42. Na Amri Kiemba alikosa bao dakika ya 40.
Na kwa upande wa Yanga Mwape alikuwa mkosaji wa mabao kadhaa jana hasa lile la dakika ya 85, ambapo kipa wa Simba Kaseja alifanya kazi ya ziada kuokoa shuti lake ambalo lilikuwa likielekea kwenye nyavu, lakini Kaseja ambaye kwa siku za hivi karibuni mashabiki wake walipoteza imani naye alipangua shuti hilo.
Naye Jerryson Tegete aliyeifunga Simba katika mechi ya kwanza alikosa bao katika dakika ya 88, lakini sekunde chache baadaye Kocha Sam Timbe alimtoa na nafasi yake kuchukuliwa na Iddi Mbaga.

Source:Habarileo
COMMENTS