Kongamano lafungwa kwa ahadi kubwa kubwa kwa wadau wa CHF , NHIF

HOTUBA YA KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII, BIBI BLANDINA NYONI KATIKA UFUNGAJI WA KONGAMANO LASABA LA WAANDISHI NA WAANDISH...

HOTUBA YA KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII, BIBI BLANDINA NYONI KATIKA UFUNGAJI WA KONGAMANO LASABA LA WAANDISHI NA WAANDISHI WAANDAMIZI LILIOFANYIKA TAREHE 28 HADI 29, 2011, MOROGORO.


• Mwenyekiti wa Kongamano Bw. Lauden Mwambona
• Makamu wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHFI), Bw. Kiwenge Ally Kiwenge,
• Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Emanuel Humba,
• Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,
• Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bw. Hamis Mdee,
• Wakurugenzi, Mameneja na Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,
• Wawakilishi wa Taasisi dada zilizo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
• Waratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii wa Mkoawa Morogoro,
• Ndugu wana habari,
• Wageni Waalikwa,
• Mabibi na Mabwana

Asalam Aleikum, Bwana Yesu Asifiwe.

Shukrani:
Ndugu Mwenyekiti wa Kongamano, Wajumbe wa Bodi ya Mfuko, Viongozi, Wahariri na Waandishi. Nianze kwa kutoa shukrani za dhati kwa kunialika kufunga Kongamano hili muhimu la Wahahari na Waandishi wa Habari ambalo lililenga kupata mrejesho kuhusu Hali halisi ya huduma za matibabu zinatotolew kupitia NHIF na CHF huko vijijini.
Utaratibu mliotumia wa kuwapa nafasi wanahabari kwenda vijijini ni mzuri na ningefurahi kuona unaendelezwa na kuigwa na taasisi nyingine pia. Kwa kuzingatia umuhimu wa kongamano hili, Wizara iliwaleta maafisa wake waandamizi ambao mmekuwa nao tangu jana na pia iliwasisitiza kuwepo na uwakilishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara. Nashukuru kwamba wote wamehudhuria kama tulivyoelekeza.

Taarifa za Utafiti na Majadiliano:
Ndugu Mwenyekiti na ndugu Wanahabari, nimetaarifiwa pia mmekuwa na kikao kizuri na mmejadili kwa kina masuala muhimu yanayogusa maeneo mbalimbali muhimu ikiwa ni pamoja na suala zima la upatikanaji wa dawa, hali ya vituo vya matibabu, matumizi ya fedha zinazotokana na mifuko ya uchangiaji, maadili ya watoa huduma, miundombinu na kadhalika.

Napenda niwashukuru nyote. mliofanya utafiti na nyote milioshiriki kikao hiki kwa kuchangia mada mbalimbali. Michango yenu imesaidia kuibua masuala na maeneo yanayokwamisha maendeleo ya sekta ya afya hasa utekelezaji wa Sera ya Mabadiliko katika Sekta ya Afya.

Ni dhahiri kuwa sekta ya afya inakabiliwa na jukumu kubwa la kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi hasa maeneo ya vijijini. Nina imani na matumaini makubwa kuwa kwa ushirikiano ambao mmekuwa mkiutoa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, tunaweza kabisa kuzipunguza (kama si kuzimaliza) baadhi ya changamoto zilizo ndani ya uwezo wetu. mfano suala la matumizi ya fedha zinazotokana na uchangiaji huduma za matibabu ngazi ya Halmashauri ambalo

Suala la upatikanaji wa dawa:
Ndugu Mwenyekiti na ndugu wanahabari, bila shaka kila mmoja wetu ameshuhudia mwenyewe jinsi gani suala la usimamizi na upatikanaji wa huduma ya dawa katika baadhi ya vituo vya matibabu linavyokatisha tamaa siyo tu wanachama wa NHIF na CHF, lakini Watanzania kwa ujumla. Hili ni suala ambalo sisi kama Serikali kwa upande wetu tunalitambua na tunalifanyia kazi katika maeneo yafuatayo:-
• Tunaendelea kuiimarisha Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ambayo ni chombo cha kimkakati cha Serikali.
• Tunaihimiza Sekta Binafsi washiriki katika kuagiza dawa na kufungua maduka ya dawa za Moto na Dawa Muhimu hasa vijijini, maeneo ambayo huduma hiyo inahitajika sana na kuna wanachama wengi wa Bima ya Afya;
• Tumeongeza kasi ya kusambaza kwa Maduka ya Dawa Muhimu (DLDM) kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) na kuuagiza Mfuko wa Bima ya Afya kuyasajili maduka hayo kila mara TFDA watakapokuwa wamemaliza kuyaidhinisha;

• Tulikwisha toa tamko Bungeni (wakati wa Bunge la Bajeti) kuwa fedha kiasi cha theluthi mbili (2/3) ya fedha zote zinazotokana na mifuko ya uchangiaji ya NHIF, CHF na Papo kwa Papo zitumike kununulia dawa. Kazi yetu sisi na nyingi iwe ni kuona azma hiyo inatekelezwa kwa vitendo ili wananchi wengi wanufaike na huduma hii.
• Kupitia MSD tumeanza utaratibu wa usambazaji wa Dawa hadi vituoni kule Tanga. Matarajio yetu ni kuona ni kwa namna gani utaratibu huu unaweza kuendelezwa kwa ufanisi katika mikoa mingine. Tuliamua katika mwaka huu wa fedha tuchukue mkoa mmoja kwa kila kanda.

Tunaamini kuwa hatua hiyo itasogeza karibu zaidi hudma za usambazaji wa dawa na hivyo kupunguza kero ya ukosefu wa dawa katika vituo vya matibabu. Tunawaomba wananchi na ninyi wanahabari kuwa macho na kuwa walinzi wa dawa hasa za Serikali ili zisivuje vituoni na kuangukia mikononi mwa watu wasio tutakia mema. Sisi kama Wizara tuko tayari kushirikiana na mwananchi yoyote katika suala hili. Kamati za Afya ziimarishwe ili wawe wasimamizi wa huduma za dawa maeneo yao.

Ubovu wa Miundo mbinu:
Ndugu Mwenyekiti, nimetaarifiwa pia Katika baadhi ya makala tulizozionanjana na leo zinaonyesha wazi kuwa hali ya vituo vya kutolea huduma ni mbaya, na kwa kweli kwa namna moja au nyingine hali hiyo inasababuisha hata wananchi wachache wanaokatwa mishahara yao kwa ajili ya NHIF na wale wanaochangia katika Mfuko wa Afya ya Jamii wakate tamaa ya kuendelea kuchangia. Hili nalo tutalifanyia kazi kupitia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi (MMAM) ili kuhakikisha kuwa kila kituo kinakuwa na hadhi inayostahili.


Katibu Mkuu akiongea leo jioni morogoro


Maadili ya Watumishi wa Sekta ya Afya:
Suala la maadili ya watendaji wa vituo vya matibabu mmelitaja katika taarifa zenu kama eneo lenye changamoto. Wito wangu kwenu na kwa wananchi wote ni kuwa watumishi wachache wasiofuata maadili wabainishwe ili hatua za kinidhamu zichukuliwe. Inawezekana kabisa watumishi hao wachache wanaweza kuathiri vibaya juhudi za Serikali za kutoa huduma bora kwa wananchi. Ni vyema pia pale watumishi wengine wanapofanya vizuri pia tutambue mchango wao. Si vizuri pia wananchi au wanachama wa Mfuko wa NHIF au wa CHF kuwa chanzo cha malumbano katika vituo vya matibabu. Hivyo wakati tunahimiza suala la maadili kwa Watumishi wa Sekta ya Afya ni vyema vilevile wananchi kwa upande mwingine wakazingatia maadili na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa watumishi wa sekta hii.

Suala la Elimu kwa Umma
Ndugu Mwenyekiti, tatizo kubwa linalochangia utekelezaji mdogo wa Sera na Miongozo ya Serikali ni elimu kwa walengwa. Kama mmesikiliza kwa umakini hoja zilizowasilishwa katika Kongamano hili nyingi zinabainsha uhaba wa elimu kuhusu Sera au huduma za NHIF au CHF kwa walengwa. Kukwama au kufanikiwa kwa utekelezaji wa mipango ya NHIF na CHF kunategemeana sana na uelewa wa wananchi kuhusu shughuli hizo. Naomba kwa kushurikiana na Idara nyingine zilizo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wekeni mikakati ya pamoja ya kuelimisha umma kuhusu haki na wajibu wa mdau ili linaptokea tatizo wananchi wajue ni nani wa kumwelekeea kidole.

Utafiti wa pamoja:
Napenda kumaliza kwa kusema kuwa baada ya kusikiliza taarifa hizi za utafiti, mimi nafikiri kuwa kuna haja ya kuwa na mkakati wa pamoja wa kufanya tafiti za mara kwa mara kwa kuwatumia wana habari ili tufikie mahali ambapo tunaweza kusema kwa uhakika kuwa changamoto za sekta ya afya zinafahaika na zinawekewa mikakati na nguvu za pamoja za kuzitatua.

Hitimisho:
Baada ya kusema hayo naomba sasa nitamke kuwa Kongamano letu la siku mbili limefungwa rasmi.

Asanteni kwa kunisikiliza.

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,308,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,243,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4976,habari dodoma,19,habari. dodoma,31,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,510,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,351,muziki na fasheni,6,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,2,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Kongamano lafungwa kwa ahadi kubwa kubwa kwa wadau wa CHF , NHIF
Kongamano lafungwa kwa ahadi kubwa kubwa kwa wadau wa CHF , NHIF
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjVDRuIpM5lmJz1QFfJIPSgRMfN9KB6oCChGGImiKxdsFZxWvAkxtypYLiFp2aiCMalqyzs3h-I7SsRM8F8OMQ7eJi45llmImFMlDPq51RUifh-QaWymofd9FeCxJZzNJG31jXPA-HrNrc8/s320/DSC05390.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjVDRuIpM5lmJz1QFfJIPSgRMfN9KB6oCChGGImiKxdsFZxWvAkxtypYLiFp2aiCMalqyzs3h-I7SsRM8F8OMQ7eJi45llmImFMlDPq51RUifh-QaWymofd9FeCxJZzNJG31jXPA-HrNrc8/s72-c/DSC05390.JPG
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2011/10/kongamano-lafungwa-kwa-ahadi-kubwa.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2011/10/kongamano-lafungwa-kwa-ahadi-kubwa.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy