MKONO NYUMA YA VURUGU LA ZANZIBAR NA MALENGO YAKE-KUTOKA DARUISLAM BLOG

Kutoka Lukwangule Katika pitapita yangu nilipata ujumbe huu katika mtandao wa http://daruislam.blog.com . Mimi ni mtu tu katika maisha...


Kutoka Lukwangule
Katika pitapita yangu nilipata ujumbe huu katika mtandao wa http://daruislam.blog.com. Mimi ni mtu tu katika maisha ya dunia lakini wenye  akili na wasio na akili wana haki ya kusoma maandiko na kuyatafakari kwa kina nini maana yake. Mungu amewapa nafasi hizo.Nayaweka katika chapisho ndani ya bango hili bila kuhariri naamini  walionazo na wasionazo wanaweza kuangalia nini na kama wao mni wasomaji wa falsafa za plato,Aristotle na Yesu watajua kwanini nimeweka chapisho hili.
Lukwangule

MKONO NYUMA YA VURUGU LA ZANZIBAR NA MALENGO YAKE

Vurugu zilizotokea karibuni na kuchukuwa siku kadhaa ndani ya Zanzibar
zilizopelekea kuchomwa baadhi ya makanisa, kufungwa barabara, kuchomwa kwa
baadhi ya maduka ya ulevi (baa) na kusitisha kwa kiasi fulani shughuli za
kiuchumi na kijamii kiasi cha kulifanya Jeshi la Polisi kutawanya watu kwa
mabomu ya machozi na kufanya doria sehemu kubwa ya mji zilipangwa na
kuratibiwa kwa malengo maalum na kuna mkono mrefu nyuma yake.

Kabla ya kuelezea malengo na mkono nyuma ya vurugu hili, amma mkono wa
ndani au mkono wa nje. Kwanza, tuangalie baadhi ya viashiria
vinavyodhihirisha kwamba vurugu hizi ni mchezo wa kuigiza:

Kwanza, Jumuiya ya Uamsho ni rafiki mkubwa wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa
Zanzibar na Raisi wa Zanzibar, kiasi cha Jumuiya hiyo kuandaa dua maalumu
kuiombea dua serikali hiyo na Raisi wake.

Pili, licha ya Uamsho kufanya mihadhara yake viwanjani, lakini pia imekuwa
ikitumia misikiti kwa harakati zake mbali mbali katika vugu vugu hili. Kama
vile dua na itikafu. Mmoja katika msikiti mkubwa unaotumika kwa harakati
zake ni Msikiti Munawwara Kidongo chekundu. Msikiti ambao uko katika mikono
ya serikali.

Tatu, mihadhara ya Jumuiya ya Uamsho inayotoa kauli kali dhidi ya muungano
na kuhamasisha watu wawe tayari hata kufa kutetea nchi yao imekuwa
ikiendelea kwa muda mrefu kwa baraka zote za Serikali ya Umoja wa Kitaifa
Zanzibar. Na Serikali iliwapatia kibali cha miezi sita kufanya mahubiri
hayo. Kwa jina la kutoa elimu ya uraia.

Nne, idara ya serikali ya Waqfu ambayo ndio yenye dhamana ya kuratibu
masuala ya dini ya Kiislamu yakiwemo mahubiri ya Kiislamu hususan viwanjani
ililamika kuhusu mihadhara hiyo na kutaka kuisitisha lakini inaonekana
ilishindikana.

Tano, Waziri dhamana katika Ofisi ya Makamo wa Pili wa Raisi Zanzibar,
bwana Mohammed Aboud awali alitoa taarifa ya kujikosha serikali na
kutangaza kusitisha mihadhara hiyo. Hali iliyopelekea baadhi ya wakuu wa
mikoa hususan Pemba kutangaza kuzuia mihadhara hiyo katika maeneo yao,
lakini mihadhara iliendelea kama kawaida, kana kwamba inaonekana waliagizwa
na serikali kuu waachie mihadhara hiyo iendelee.

Sita, Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar pamoja na wakereketwa muhafidhina wa
CCM walionekana kukerwa na mihadhara hiyo pamoja na matamko makali dhidi ya
muungano yanayotolewa katika mihadhara hiyo, na walianzisha kampeni maalumu
kwa kushirikiana na wakereketwa wenye nguvu kama Borafya Silima na Mbaraka
Shamte kwa lengo la kujibu na kukabiliana na wimbi la mihadhara hiyo, huku
wakijigamba kwamba watakwenda sambamba na Jumuiya ya Uamsho, kwa kuwafuata
kila mahali inapofanyika mihadhara yao kuvunja na kubomoa athari yao. Cha
kushangaza! si muda mrefu Jumuiya hiyo ya CCM na wakereketwa wake pia
waliacha kampeni yao, kana kwamba walitakiwa wasitishe.

Saba, siku ya Jumamosi Mei 26 yalipofanywa maandamano na Uamsho yalifanywa
bila ya kibali na yalipewa ulinzi kamili na jeshi la Polisi bila ya
kudhuriwa wala kukamatwa viongozi wala waandamanaji na hawakupata pingamizi
yoyote.

Nane, kitendo na mazingira ya kumkamata kwa kumnyakuwa Ustadh Mussa Juma
ambae hakuwa mstari wa mbele sana kama wengine katika mihadhara wala katika
maandamano kilifanywa akiwa msikitini ili kiguse hisia za Waumini.
Ikikusudiwa kuchochea fujo na kupatikana uhalali wa vurugu, na ili
ipatikane fursa ya kuongeza vitendo vya vurugu zaidi, kama kuchoma makanisa
ili kukuza ukubwa wa vurugu na kuonekana kuna mgogoro na tatizo kubwa ndani
ya Zanzibar. Kazi ya kuchoma makanisa yumkin kwa kiasi kikubwa walipewa
wakereketwa wa kundi la vijana muhafidhina wa CCM wa maskani. Wakioneshwa
kwamba lengo la mkakati huo ni kuimaliza Uamsho. Vijana hawa wa CCM kama
walivyo Uamsho ni wenye jazba wasiokuwa na upeo wa mambo wala uchambuzi wa
kisiasa, kwa hivyo wakalibeba jukumu hilo bila ya kurudi nyuma. Ilhali
lengo kuu la mkakati huo wa kuchoma makanisa ni kukuza ukubwa wa vurugu na
kuonekana kuweko kiwango kikubwa cha mgogoro.

Tisa, namna Polisi walivyokabiliana na tukio lenyewe pia ni usanii wa wazi.
Kwanza, Kamishna wa Polisi Zanzibar alitamka wazi kwamba viongozi
waliochochea vurugu watakamatwa kwa gharama yoyote. Cha kushangaza!
Hakukuwa na kiongozi yoyote wa mstari wa mbele aliyekamatwa au kufanywa
msako mkali kama tulivyozoea. Pia namna Polisi walivyokuwa kwenye vurugu
hili, hakuna kiudhati aliyejeruhiwa au kuuwawa kama tulivyozoea namna
Polisi wa hapa wanapokabiliana kwa ukali wa kuruka mipaka na vurugu hususan
zenye kufungamana na siasa.

Hivi ni baadhi ya viashiria kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar
inaelewa fika kila kinachotendeka na kukibariki kuanzia vugu vugu la
mihadhara ya Uamsho hadi kuripuka vurugu.

*Nani nyuma ya vurugu hili, na nini malengo yake?*

Hapa kuna misukumo miwili mikubwa. Msukumo wa ndani na msukumo wa nje. Kwa
upande wa ndani, vurugu hizi ni shinikizo la baadhi ya wanasiasa wakubwa wa
CCM Zanzibar wakiungwa mkono na baadhi ya wanasiasa wa CUF Zanzibar
wanaofangamana kwa uzalendo wao wa ‘uzanzibari’. Japo kwamba CUF nyuma ya
pazia inaonekana kupinga vuguvugu hili, kwa kuwa ajenda ya vuguvugu la
Uamsho ni kuvunja kabisaa.. Muungano, ilhali sera ya CUF ni kuwepo serikali
tatu. Lakini kimsingi CUF imeshakufa na imebaki kuwa tawi la CCM. Na zaidi
hakuna matumaini kisiasa kwa CUF kupata serikali ya Muungano kuweza
kutekeleza sera yake hiyo. Kwa hivyo, sera yake juu ya Muungano na sera
nyenginezo zinabakia kuwa nadharia tu. Hivyo si ajabu CUF Zanzibar kwa
hisia zao za kizalendo wakadandia mkondo wa vugu vugu hili. Lakini kutokana
na nafasi za wanasiasa hao katika serikali na katika vyama vyao na kulinda
maslahi yao binafsi wanakosa ujasiri wa kuonekana wazi wazi. Aidha, wale
waliomo ndani ya CCM nao hawana ushujaa katika vikao vyao halali vya chama
kutoa duku duku lao kiudhati kuhusu Muungano, zaidi ya kusema ‘ndio
nakubaliana’ na kuahidi ‘kulinda Muungano’. Kwa hivyo, kundi hili wamehisi
watumie fursa ya kuyadandia majukwaa ya dini ya Kiislamu. Kwa kuwa wakaazi
wa Zanzibar kiasili wana hisia ya dini yao ya kiislamu, ili kuweza kuvutia
watu na wafuasi wengi zaidi katika vugu vugu hili bila ya kuzingatia chama
chochote. Pia kauli mbiu inayotumika na Uamsho ya kutaka kura ya maoni juu
ya mustakbali wa Muungano imetumika ili ionekane kuwa kinyume kabisa na
vyama vyote vya kisiasa vilivyopo. Lengo ni kuonesha na kupeleka ujumbe kwa
CCM taifa na serikali yake ya Muungano kwamba hali si shwari tena kutoka
kwa raia wenyewe wa Zanzibar. Ili kwa haraka matatizo mbali mbali
yanaotokamana na Muungano yakiwemo suala la uchimbaji na umiliki wa mafuta
yatatuliwe kabla hali haijawa ya kutisha zaidi!. Kimsingi Raisi wa sasa wa
Zanzibar si mtu shupavu kama alivyokuwa Dk. Salmin Amour kuweza kuwa na
misimamao mikali ya kizalendo. Lakini yumkin waliomzunguuka wameweza
kufanikiwa kumchochea kuhusu maslahi ya Zanzibar hususan katika suala la
uchimbaji wa mafuta ambao ni mtaji mwanana kisiasa. Ikumbukwe kwamba suala
la uchimbaji wa mafuta ya Zanzibar limekuwa na mjadala mkali miongoni mwa
wanasiasa na wananchi jumla, kiasi cha kuweza kuwaunganisha wanasiasa wa
Zanzibar na raia jumla kuunga mkono vugu vugu la Uamsho, kwa lengo la
kuzidisha shinikizo kwa Serikali ya Muungano kulitazama upya. Inawezekana
pia kwa kiasi kikubwa katika vugu vugu hili kumuhusisha raisi mstaafu
aliemaliza muhula wake. Katika zama zake, aliyekuwa Waziri wake wa Nishati
(Mansour) alikuwa akitamka waziwazi kwa maneno makali kuhusu uchimbaji wa
mafuta na gesi ya Zanzibar kwamba utabakia kuwa milki ya Zanzibar. Kitu
ambacho ni kinyume na mawafikiano ya Muungano. Waziri Mansour alidiriki
kutoa kauli hizo kali ilhali Raisi Amani si kwa nafasi yake ya uraisi, wala
Unaibu Mwenyekiti wa CCM hakuthubutu kumchukulia hatua za kumzuia wala
kumuadhibu. Pamoja na hayo Raisi huyu mstaafu ana shauku kubwa ya kumtakasa
baba yake kwamba alikuwa na nia safi juu ya suala la Muungano.Kampeni
ambayo inapata nguvu vya kutosha kila uchao. Kinyume na alivyokuwa
akichukuliwa huko awali kwamba ni msaliti aliyeuza Zanzibar kwa Tanganyika.
Pamoja na sababu hiyo pia wimbi hili ni ujanja wa kujificha kufeli kwa
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar kinyume na matarajio ya raia.

*Msukumo wa nje. *

Kwa upande mwengine wa msukumo wa nje. Vuguvugu hili linatokamana na
Marekani. Ukizingatia kwa makini kauli ya balozi wa Marekani ndani ya
Tanzania Alfonso E. Lenhardt, baada ya vurugu hili alitamka: *“Tunatambua
umuhimu wa kuwepo mjadala wenye nguvu ndani ya umma, na tunahamasisha wadau
wote kuuendeleza kwa utaratibu wa amani na kidemokrasia”*.

*
*

Akikusudia wahusika na wadau wa qadhia hii waketi na walimalize jambo hili
kidemokrasia na kwa maridhiano. Katika kauli hii kunadhihirika kiashiria
cha mkono wa dola hiyo. Marekani inaelewa fika sera ya Muungano ya CCM
kwamba ni serikali mbili kuelekea serikali moja, sasa iweje waketi kujadili
qadhia hii na wahusika wengine? Marekani ndio msimamizi kwa kiasi kikubwa
wa Afrika Mashariki baada ya kumnyan’ganya bwana wa asili wa ngome hii
yaani Uingereza. Licha ya Marekani kufanikiwa kujenga himaya na ushawishi
mkubwa Afrika ya Mashariki, bado inakabiliwa na upinzani mkubwa na
changamoto kadhaa kutoka bwana huyo wa asili wa eneo hili (Uingereza). Hili
hudhihirika katika upinzani mkubwa wa vyama vyao ndani ya nchi hizi. Kwa
mfano, Chama cha ODM nchini Kenya chini ya Odinga ni chama cha Marekani,
ilhali chama cha PNU cha Kibaki kiko chini ya Uingereza. Marekani
ilikabiliwa na hali ngumu sana katika uchaguzi uliopita ndani ya Kenya
kutokana na ujanja wa kisiasa wa Uingereza. Hadi ikalazimika kugawana
ngawira na keki ya Kenya na mwenzake Uingereza. Hali hiyo mpaka sasa ni
tofauti na Tanzania. Licha ya Uingereza kwa kupitia Chadema kuota mizizi,
bado chama cha CCM ambacho ni chama cha Marekani kinaendelea kushikilia
hatamu ndani ya Serikali ya Muungano. Na Marekani imefanikiwa kufanya
mkakati kabambe wa kumakinisha athari yake ndani ya Zanzibar na kumkatisha
tamaa kabisa Uingereza kwa kuunganisha chama chake kilichokuwa uwanjani CCM
na chama chake cha akiba/reserve (CUF). Hata hivyo, Marekani imejifunza
kutoka siasa za Kenya, lau haikuwa makini zaidi ndani ya Tanzania, amma
itafika mahala ipoteze kabisa ushawishi wake na maslahi yake au italazimika
kugawana ngawira na Uingereza. Hali itakayomugharimu kupungua athari yake
au kupoteza kabisa nguvu, maslahi na ushawishi wake katika nchi hii. Kwa
hivyo, hali inavyoendelea Tanzania kwa Chama cha Muingereza (Chadema)
kinachoungwa mkono pia na Jumuiya ya Ulaya hususan Ujerumani, kinaonekana
kila siku kumakinika na kupata watu wengi ndani ya Tanzania hususan Bara,
kiasi cha hata baadhi ya vigogo wa chama cha CCM, ambao bila ya shaka
wanaounga mkono Uingereza kutishia kutoka CCM na kuingia ndani ya Chadema.
Hali hiyo inaifanya Marekani kutokuwa na raha juu ya mwenendo wa siasa za
Tanzania ikiwemo Zanzibar. Kwa hivyo, vuguvugu hili la Uamsho Zanzibar ni
mchezo wa Marekani kupitia CCM kiujanja, kwa kutumia baadhi ya vikundi vya
Kiislamu ndani ya Zanzibar, amma kwa kujijua au kwa kutojijuwa kutokana na
kukosa kwao uweledi mpana wa kisiasa na fikra thabiti ya Kiislamu. Marekani
imejifunza kwamba baadhi ya vikundi vya Kiislamu ndani ya Tanzania hufanya
kazi nzuri ya kufikia malengo yake ikiwemo kukiokoa chama chake cha CCM
kinapokuwa katika shimo la maangamizi kwa kubanwa koo na Chadema. Kama
ilivyodhihirika katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga. Wakati huo
takriban vikundi vingi vya Kiislamu vililitumia tukio la kuvuliwa mtandio
Mkuu wa Wilaya Fatma Kimario na wakereketwa wa Chadema kama ni ushahidi wa
chama hicho kuwa ni adui wa Waislamu. Huku vikundi hivyo hivyo vya Kiislamu
vilijitia upofu wa tukio kubwa ovu lililofanywa na CCM wakati huo huo,
kufanya dua ya pamoja baina ya Waislamu na Wakiristo kuwaombea waathirika
wa ajali ya Mv. Spice Zanzibar. Unapoyapima matukio mawili haya yaliyotokea
wakati mmoja kwa mujibu wa ‘hukmu za Kiislamu’ licha ya kuwa yote ni maovu,
lakini la CCM ni ovu zaidi. Sasa iweje vikundi hivi kwa hili la CCM vibakie
kimya cha mfu? Na kwa upande wa baadhi ya vikundi vilivyopo Zanzibar
vilifanya kazi nzuri kwa gharama ndogo wakati wa kupiga kampeni ya Marekani
ya kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar.

Katika vugu vugu hili linaloendelea la Uamsho Marekani hailengi tu, kuunda
serikali tatu katika Muungano, bali ikiwezekana, lakini kwa njia za busara
kuiondoa kabisa Zanzibar katika Muungano. Japo kwamba si jambo jepesi,
litakalogharimu Zanzibar gharama za mambo ya ubalozi na mengineyo pia
kugharimu Tanganyika kulitangaza upya kimataifa dola lao jipya. Na lau
haitowezekana Marekani inadhamiria walau kuweka serikali tatu kwa lengo la
kuumega muungano kidogo kidogo mpaka kuuhitimisha kabisa. Kwa sababu,
kuitoa Zanzibar katika Muungano ni jambo la usalama na utulivu zaidi kwa
maslahi ya Marekani ya uchimbaji wa mafuta ya Zanzibar hata kuliko kuwapo
serikali tatu. Na pia salama kwake amma ikiwa Bara kinatawala chama chake
cha CCM au kikishinda chama cha Uingereza (Chadema). Utaona, japo kwamba
sera ya Uingereza (Chadema) kidhahiri katika suala la Muungano ni serikali
tatu, lakini inawezekana huo ni mtego tu wa Uingereza ambao Marekani
inaonekana kuung’amua. Yumkin, lau Chadema kinapata ushindi Tanganyika,
Uingereza inaweza ikaigeuza ghafla sera hiyo kiasi cha kuirejesha tena
Zanzibar katika mikono ya Uingereza kutokana na kuwepo rasilmali ya mafuta.
Karibuni Mbunge mwenye nguvu wa Chadema Zitto Kabwe alikaririwa akisema
kwamba masuala ya mafuta na gesi hayakupaswa kuwa katika mambo ya Muungano.
Kauli hiyo ya kijanja ni dhihirisho ya kukita siasa za Muingereza ndani ya
Chadema. Siasa ‘za unachosema kinyume na unachoamini na kukitendea kazi’.

Marekani na maafisa wa juu wa CCM wanajua kinachoendelea katika vuguvugu la
Uamsho na vurugu zilizojiri, wanajaribu kuonesha kwa ufundi sana kwamba
hili ni suala linalotokamana na wazanzibari wenyewe bila ya mkono wa nje,
kama lilivyoonyeshwa suala la muwafaka baina ya ‘Karume na Seif’
lililopelekea kuzaliwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Dhamira ya kuonesha
hivyo ni kuwafanya muhafidhina ndani ya CCM waweze kuikubali hali hiyo
kidogo kidogo na kuanza kulainika kidogo kidogo tayari kwa mabadiliko.

Kwa ufupi, Marekani inalenga kwa mkakati wa vuguvugu la Uamsho kama mbinu
ya kufikia kujihifadhi na kujilinda dhidi ya Uingereza, pia ipate kuikomba
kwa raha, salama na utulivu rasilmali ya mafuta ndani ya Zanzibar. Huku
Marekani akijifanya kijanja kuwaridhisha wazanzibari kwamba wanajitawalia
mambo yao wenyewe kikamilifu nje ya Muungano, dhana iliyojaa ndani ya vifua
vyao.

*Matarajio*

Baada ya vurugu hili Serikali ya Umoja wa Kitaifa kuwa mkali mdomoni,
lakini laini kivitendo kwa Uamsho, viongozi wake na vurugu lililotokea.
Tayari ZBC (Shirika la Utangazaji Zanzibar) katika Tv wanaonesha picha za
matokeo ya vurugu hili, na hitimisho la kipindi hicho humalizia: *‘iliyopita
si ndwele tugange ijayo’* Pia mihadhara itabanwa kidogo, na hatimae
kuruhusiwa kama kawaida. Baadhi ya kesi zilizofunguliwa dhidi ya walioleta
vurugu zitafutwa na kufa kifo cha kawaida, serikali italipa gharama za
uharibifu wa makanisa na mali nyenginezo, na Marekani kiufundi kidogo
kidogo itahamasisha mabadiliko ili kuandaa mazingira ya kufikia lengo lake.
Na viongozi wa juu wa CCM wataonekana kukemea qadhia hii kijanja kwa ukali,
kana kwamba hawana habari ya kinachoendelea.

*Hitimisho*

Kwa hakika, kuchanganyikiwa kwa ndugu zetu katika umma kunatupa moyo wa
fedheha na masikitiko makubwa. Lau ingekuwa aibu ya kifamilia tu
tungeinyamazia mambo yakesha! Lakini kwa kuwa tunabeba qadhia ya umma,
hulazimika tuuonye na kuuonesha njia. Katika mwezi kama huu wa Rajab mwaka
1342 Hijri sawa na mwanzoni mwa mwezi wa Machi mwaka 1924 miladi, ndio
wakati waliodiriki makafiri kwa uadui mkubwa kuimaliza dola ya mwisho ya
Kiislamu (Khilafah Uthmania). Miongoni mwa silaha ya hatari waliyoitumia
makafiri hao kufikia lengo hilo ni fikra hii wanayoishadidia leo Uamsho,
fikra ya ubaguzi/ aswabia. Fikra ya watu kujifunga, kujilabu na kujitukuza
kwa mujibu wa maeneo yao wanayoishi au walipozaliwa, badala ya kujinasibu
kama sehemu ya umma mtukufu wa Kiislamu ulioenea duniani kote. Hatimae,
Waarabu wakaona wana mambo yao kama Waarabu, na Waturuki kama Waturuki.
Haikumalizia hapo, katika Waturuki wakajitukuza wengine kundi la Wakurdi,
na Waarabu nao ardhi zao zikakatwa vijinchi telee…. hadi nyengine ni aibu
hata kuziita nchi kamwe! Lau Umma wetu ungejifunga vilivyo na hukmu za
Kiislamu na manhaj sahihi ya Kiislamu usingeweza kamwe kuingia ndani ya
mtego kama hii ya makafiri.

Tunamuomba Allah *Ta’ala *katika mwezi huu mtukufu wa Rajab ainue ufahamu
wa umma wetu ujifunge kidhati na manhaj ya Mtume wetu (SAAW) katika kuleta
mageuzi ya kweli ili tuweze kurejesha tena izza/nguvu yetu kwa kurejesha
tena dola yetu ya Kiislamu ya *Khilafah Rashidah* kama alivyobashiri
kipenzi chetu SAAW.



18 Rajab 1433 Hijri 04/06/2012 Miladi

*
Tembelea mtandao wetu www.daruislam.blog.com*

*Shukran*

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: MKONO NYUMA YA VURUGU LA ZANZIBAR NA MALENGO YAKE-KUTOKA DARUISLAM BLOG
MKONO NYUMA YA VURUGU LA ZANZIBAR NA MALENGO YAKE-KUTOKA DARUISLAM BLOG
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2012/06/mkono-nyuma-ya-vurugu-la-zanzibar-na.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2012/06/mkono-nyuma-ya-vurugu-la-zanzibar-na.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy