Temeke imekuwa timu ya kwanza kupata tiketi ya kucheza nusu fainali kwenye michuano ya mwaka huu ya Copa Coca-Cola baada ya kuing’...
Temeke imekuwa timu ya
kwanza kupata tiketi ya kucheza nusu fainali kwenye michuano
ya mwaka huu ya Copa
Coca-Cola baada ya kuing’oa Mjini Magharibi kwa mikwaju ya
penalti.
Mechi hiyo ya kwanza ya
robo fainali imechezwa leo asubuhi (Julai 10 mwaka huu)
Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, Dar es Salaam ambapo hadi dakika 90 za kawaida
zinamalizika timu hizo
zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Mjini Magharibi ndiyo
walioanza kupata bao dakika ya 79 lililofungwa na Salum Maulid
wakati Abdul Hassan
aliisawazishia Temeke dakika ya 90.
Waliofunga penalti kwa
upande wa Temeke ni Baraka Ntalukundo, Khalid Mwendakamo,
Mohamed Dikougwa na Abdul
Hassan wakati aliyekosa ni Anwar Kilemile. Waliokosa kwa
Mjini Magharibi ni
Abdulrahman Mohamed na Salum Maulid wakati waliofunga ni Alawi
Kombo na Salum Shukuru.
Katika nusu fainali,
Temeke itacheza na mshindi wa mechi ya robo fainali kati ya
Kinondoni na Mwanza
itakayochezwa kesho asubuhi (Julai 11 mwaka huu) Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam.
Robo fainali ya pili ya
michuano hiyo kati ya Mara na Morogoro ilitarajiwa kuchezwa
leo jioni kwenye uwanja
huo huo. Mechi nyingine ya robo fainali itakayowakutanisha
Dodoma na Tanga itachezwa
kesho jioni.
EL SALAM WAU, ATLETICO
ZAWASILI KUWANIA KOMBE LA KAGAME
El Salam Wau ya Sudan
Kusini na Atletico ya Burundi zinatarajiwa kuwa timu za kwanza
kuwasili nchini kushiriki
michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe
la Kagame).
Michuano hiyo inaanza
kutimua vumbi Jumamosi (Julai 14 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam
ikishirikisha timu kumi na moja akiwemo bingwa mtetezi Yanga na
makamu bingwa Simba.
Kikosi cha El Salam Wau
ambacho kitawasili kesho alfajiri (Julai 11 mwaka huu) kwa
ndege ya Ethiopia
Airlines kikitokea Juba kupitia Addis Ababa, Ethiopia kikiwa na
wachezaji 18 na viongozi
saba.
Wachezaji wanaounda
kikosi hicho ni Khamis Leone Uso Wani (nahodha), Adheil Bugwic
Jongkor Bugwic, Edward
Joram Simon Julio, Fidel Andrea Fides Fas, Ismael Musa Juma
Ismael, James Anei
Matheli Anei, Jervas Ayo Abdalla Ayak, Khamis Doshama Ulama Andel
na Meki Sultan Berema
Kuku.
Wengine ni Moga Emmanuel
Androga, Mubarak Mohammed Saleh Omer, Ndili Rabeh Nasir
Hozi, Nizir Rihan Taban
Talib, Oliver Paul Kangi Akok, Rabie Mohammed Abubakar
Hassan, Rufino Joseph
Uras Ambros, Santino Makuei Uyu Upio, Thomas Rufino Thomas
Diakon.
Nayo Atletico inatarajiwa
kuwasili kesho (Julai 11 mwaka huu) kwa usafiri wa
barabara. Timu hiyo inakuja
kwa usafiri wa basi lake ambalo pia italitumia kwa muda
wote itakapokuwa kwenye
mashindano.
Wakati El Salam Wau
itafikia kwenye hoteli ya Rungwe iliyoko maeneo ya Kariakoo,
Atletico itakuwa Lunch
Time Hotel iliyoko Mabibo.
Timu zinazotarajiwa
kuwasili keshokutwa (Julai 12 mwaka huu) ni Mafunzo ya Zanzibar
kwa boti saa 9 alasiri,
Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (RDC) itatua
saa 1.20 usiku kwa Kenya
Airways. Timu nyingine itakayowasili siku hiyo jioni ni URA
ya Uganda.
WATANGAZAJI KWA ‘SCREEN’
KUBWA KOMBE LA KAGAME
Wakati wa michuano ya
Kombe la Kagame itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kuanzia Julai 14-28 mwaka
huu, screen kubwa iliyoko uwanjani itatumika kwa matangazo
ya biashara na ujumbe
mbalimbali kwa washabiki watakaoshuhudia mechi hizo.
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) linakaribisha kampuni na wadau
mbalimbali wanaotaka
kuweka matangazo yao wakati wa michuano hiyo itakayoshirikisha
klabu kumi na moja kutoka
ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
Muda wa kurushwa
matangazo hayo yanayotakiwa kuwa kwenye mfumo wa DVD ni kabla ya
mechi kuanza, wakati wa
mapumziko na baada ya mechi. Matangazo hayo yanatakiwa kuwa
ya sekunde 60 (dakika
moja) au sekunde 30 (nusu dakika).
RAMBIRAMBI MSIBA WA MWENYEKITI
FAM
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo
cha Mwenyekiti wa Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Fabian Samo
kilichotokea leo asubuhi
(Julai 10 mwaka huu).
Samo ambaye Novemba 13
mwaka jana alichaguliwa kwa kipindi cha pili mfululizo kuwa
Mwenyekiti wa FAM katika
uchaguzi uliofanyika wilayani Rorya alikuwa amelazwa
Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Dar es Salaam akisumbuliwa na maradhi ya figo.
Taratibu za mazishi ya
Samo ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu
(Internal Audit
Committee) ya TFF ikiwemo siku atakayozikwa bado zinafanywa na
familia yake.
Samo alitoa mchango
mkubwa katika maendeleo ya mpira wa miguu mkoani Mara na
Tanzania kwa ujumla, vitu
ambavyo vilichangia kuchaguliwa kwake tena kuiongoza FAM.
Msiba huo ni pigo kwa
familia ya Samo, FAM, TFF na mchezo wa mpira wa miguu kwa
ujumla nchini kutokana na
mchango na mawazo aliyotoa kwa kipindi chote alichokuwa
kiongozi.
TFF inatoa pole kwa
familia ya marehemu Samo, FAM, jamaa na marafiki na kuwataka
kuwa na uvumilivu katika
kipindi hiki cha msiba huo mzito. Pia TFF itatoa ubani wa
sh. 200,000 kwa familia
ya marehemu kama rambirambi zake.
Mungu aiweke roho ya
marehemu Samo mahali pema peponi. Amina
KOZI YA MAKOCHA WA
GRASSROOTS
Kozi ya makocha wa mpango
wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu
(wasichana na wavulana)
wenye umri kuanzia miaka 6-12 imeanza leo (Julai 10 mwaka
huu) kwenye ukumbi wa
Msimbazi Center, Dar es Salaam.
Wakufunzi kutoka
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ndiyo wanaoendesha
kozi hiyo iliyofunguliwa
na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Angetile Osiah.
Kozi hiyo itakayomalizika
Julai 15 mwaka huu inashirikisha washiriki 35, na
mwendelezo wa ile ya
awali iliyofanyika Desemba 14-17 mwaka jana jijini Dar es
Salaam.
Gouinden Thandoo kutoka
Mauritius ni mmoja wa wakufunzi wa Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA)
wanaoendesha kozi hiyo.
Source:Boniface Wambura
Ofisa Habari
COMMENTS