1 HOTUBA YA WAZIRI KIVULI NA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI NDUGU KABWE ZUBERI ZITTO KUHUSU...
1
HOTUBA YA WAZIRI KIVULI NA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA
UPINZANI WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI NDUGU KABWE ZUBERI ZITTO KUHUSU MAKADIRIO YA
MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013
1.0 UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kanuni ya 99(7), toleo la mwaka
2007 na kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,napenda kuwasilisha maoni
ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mafungu ya
Wizara ya Fedha – Fungu 50 Wizara ya Fedha, Fungu 21 Hazina, Fungu 22 Deni la
Taifa na Fungu 23 Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali. Vile vile Fungu 10 Tume ya
Pamoja ya Fedha na Fungu 13 Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa
Ugaidi.
Mheshimiwa Spika, mafungu yote yaliyo chini ya Wizara ya Fedha yanaomba
kuidhinishiwa na Bunge lako tukufu jumla ya shilingi Bilioni 4,208 (trilioni
4.2) ili yaweze kutekeleza majukumu yake. Mafungu haya maombi yake ya Fedha ni
sawa na asilimia 28 ya Bajeti nzima ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2012/13.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha ndiyo msimamizi mkuu wa Uchumi wa nchi
ikitekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo, kusimamia ukusanyaji wa mapato ya
ndani na ya nje, kusimamia matumizi ya Serikali, kusimamia utendaji wa Taasisi
na Mashirika ya Umma, kusimamia manunuzi ya Serikali na Taasisi na Mashirika ya
2
Umma,
kusimamia Deni la Taifa na dhamana za Serikali, kutafuta suluhisho na kusimamia
mfumo wa kodi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kupambana na Fedha haramu.
Sambamba na hayo ni kusimamia na kutekeleza mpango wa kupunguza umasikini
nchini kupitia utekelezaji wa MKUKUTA II.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha na mafungu yote yaliyo chini yake ndio moyo
wa Serikali na hivyo ni lazima kuitazama Wizara hii kwa jicho kali na kutilia
mashaka kila jambo ambalo inalifanya ili kuhakikisha kuwa moyo huu hausimami
maana madhara yake ni kwa taifa zima na watu wake. Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni kupitia Waziri Kivuli wa Fedha inatekeleza wajibu huu kwa Uzalendo,
Uadilifu na kwa misingi ya Uwajibikaji. Tumetekeleza wajibu huu na tunaendelea
kuutekeleza bila kujali maneno na kuweka maslahi ya Taifa letu mbele ya kila
kitu kingine. Maslahi ya Taifa ni zaidi ya vyama vya siasa, mahala tunapotoka
au dini tunazoamini. Maslahi ya Taifa ni kwa ajili ya Watazania na hasa
Watanzania milioni 30 (The Bottom 30M) ambao bado wanaishi katika ufukara
mkubwa sana wakikosa huduma muhimu za jamii na wanaoishi vijijini ambapo hakuna
umeme, barabara hazipitiki na wanahangaika kutwa kutafuta maji safi na salama.
Maslahi ya Taifa sio faida ya wachache wenye kuishi mijini au wanasiasa
wanaotafuta ushawishi kwa umma bila kujali matakwa ya Umma. Watanzania wanyonge
wa vijijini wanajua maslahi yao ni nini. Wanajua kina nani wanapigania maslahi
ya Wanyonge. 3
2.0 MAPATO YA SERIKALI
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya mwenendo wa Uchumi ya mwezi Julai
(Monthly Economic Review, July 2012) iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania,
katika kipindi cha mwezi Juni Serikali iliweza kukusanya kiasi cha shilingi
bilioni 998.0. Hata hivyo matumizi halisi yalikuwa kiasi cha shilingi
bilioni 1,911.8 hali iliyopelekea kuwepo kwa nakisi baada ya kuondoa
msaada wa masharti wa masharti wa shilingi bilioni 400.2; nakisi hiyo
ililipwa kwa vyanzo vya ndani na nje.
Mheshimiwa Spika, taarifa hiyo ilionyesha kuwa mapato yote ukiondoa fedha
zilizokusanywa na Serikali za mitaa kwa mwezi Juni, yalikuwa kiasi cha shilingi
bilioni 887.5 ambacho ni zaidi ya asilimia 38.1 ya malengo
yaliyokuwa yamewekwa kukusanywa mwezi huo. Aidha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 753.3, kiasi ambacho ni zaidi ya
asilimia 22.3 ya malengo ya makusanyo kilichokuwa kimewekwa na mamlaka
hiyo. Makusanyo haya ni makubwa zaidi kukusanywa na TRA kwa mwezi mmoja tangu
Mamlaka hiyo ianzishwe.
Mheshimiwa Spika, katika makusanyo hayo ya mwezi Juni Mamlaka ya Mapato
Tanzania ilikuwa imejiwekea lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 242.4
kama kodi ya Mapato, lakini ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 366.0 kiasi
ambacho ni zaidi kwa asilimia 60.8 ya malengo yaliyokuwa yamewekwa. 4
Kambi ya Upinzani inapenda
kulikumbusha Bunge na Taifa kwamba katika Bajeti Mbadala iliyowasilishwa hapa
Bungeni tulisema kwamba TRA wanao uwezo wa kukusanya mpaka shilingi trillion
moja kwa Mwezi iwapo tutadhibiti misamaha ya kodi, tutakusanya kodi stahili
katika Sekta ya Madini na tutasimama kidete kuzuia ukwepaji kodi wa Makampuni
ya Kimataifa.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inaitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania
kuimarisha zaidi marekebisho yanayofanyika katika mfumo wa kodi ili kufikia
lengo tajwa la kufikia makusanyo ya zaidi ya asilimia 20 ya Pato la Taifa.
Mabadiliko kadhaa tunayoyafanya kwenye Sheria ya Fedha itakayosomwa hapa
Bungeni katika mkutano huu wa Bunge yana lengo hilo la kupanua wigo wa kodi na
hivyo kulifanya Taifa lijitegemee.
2.1 Mauzo ya Nje
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha kupitia Benki Kuu ya Tanzania inapaswa
kuhakikisha kuwa Akiba ya Fedha za Kigeni nchini inakuwa imara muda wote.
Biashara ya nje ndio inaingiza Fedha za kigeni nchini kwa hiyo ni eneo la
kutazama kwa makini na kuchukua hatua mwafaka. Taarifa ya mwenendo wa uchumi
kwa mwezi Julai iliyotolewa na Benki kuu inaonyesha kuwa jumla ya mauzo ya
Tanzania nje yalikuwa dola za kimarekani 7,990.0 milioni ukilinganisha
na kiasi cha dola 7,050.7 milioni kwa kipindi kama hicho kwa mwaka 2011
na hali hii ilisababishwa kwa kiasi kikubwa 5
kutokana
na kuongezeka kwa bei ya mauzo ya dhahabu. Hata hivyo Manunuzi yetu
kutoka nje yamefikia dola za Kimarekani 12,959 milioni.
Mheshimiwa Spika, taarifa hiyo inaonyesha kuwa mauzo ya dhahabu Nje kwa mwaka
2011 yalikuwa kiasi cha dola 2,330.7 milioni sawa na aslimia 56.7% ya
mauzo yote nje, wakati mauzo ya nje kutokana na bidhaa zilizozalishwa viwandani
yalikuwa na jumla ya dola 922.0 milioni sawa na asilimia 22.4% ya
mauzo yote ya nje. Aidha mauzo ya mazao mbalimbali kama Pamba, Katani, Korosho,
Chai, Kahawa na mengineyo yalikuwa na thamani ya dola 761.1 milioni kwa
kipindi hicho cha mwaka 2012.
Mheshimiwa Spika, taarifa hiyo imeendelea kuonyesha kuwa tuliagiza bidhaa
kutoka nje zenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 12,958.7. Katika
manunuzi hayo tuliyofanya mafuta peke yake yalikuwa na thamani ya dola za
Kimarekani milioni 3,586.1 ambalo ni ongezeko la asilimia 60.08% ukilinganisha
na kipindi kama hicho kwa mwaka 2011.
Mheshimiwa Spika, takwimu hizi zinaonyesha kwamba fedha zote za kigeni
zilizotokana na mauzo ya dhahabu, bidhaa za viwandani na Korosho zilitumika
kuagiza mafuta pekee yake! Hali hii ni mbaya sana kwa uchumi wa Taifa letu na juhudi
zote za kuongeza mauzo nje zinaliwa na uagizaji wa Mafuta ambao umepanda sana
katika siku za hivi karibuni. 6
Kambi Rasmi ya Upinzani inatambua kuwa kuanzia mwaka jana Serikali imekuwa
ikitekeleza mpango wa Umeme wa dharura ambao umepelekea matumizi makubwa ya
Mafuta. Hata hivyo ieleweke kuwa Mpango mzima wa Manunuzi ya Mafuta ya
kuendesha mitambo ya Umeme inaligharimu Taifa Fedha nyingi sana. Takwimu
zinaonyesha kuwa Serikali inapaswa kutumia zaidi ya shilingi 42 bilioni kila
Mwezi kuendesha mitambo ya dharura ya Umeme. Manunuzi yenyewe ya Mafuta yamejaa
mazonge ya ufisadi uliokithiri. Licha ya kutaka Spika aunde timu ya kuchunguza
ufisadi katika manunuzi ya Mafuta na licha ya Kamati ya Bunge kutaka Uchunguzi
wa kibunge kufanyika katika manunuzi haya bado hakuna hatua inayochukuliwa.
Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Mamlaka ya Manunuzi ya Umma PPRA kufanya
uchunguzi wa kina kuhusu manunuzi ya mafuta kuzalisha Umeme ambayo yanachoma bilioni
42 za Serikali kila Mwezi. PPRA hapaswi kufumbia macho manunuzi
yanayotafuna shilingi 1.4 bilioni kila siku na yanayoongeza manunuzi ya nchi
kutoka nje (imports) na hivyo kupoteza fedha za kigeni hovyo.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha ambayo ndio wizara mama ya PPRA kupitia Fungu
50, na ndio Wizara yenye kusimamia uchumi wa nchi kwa ujumla ituletee Bungeni
Taarifa ya Uchunguzi utakaofanywa na PPRA kuhusu manunuzi shilingi 1.4 bilioni
kila siku ya mafuta kuendesha mitambo ya kuzalisha Umeme. 7
2.3 Deni la Taifa.
Mheshimiwa Spika, Fungu 22 linaombewa jumla ya shilingi bilioni 2,735 ili
kuweza kulipa madeni ikiwemo deni la nje la shilingi bilioni 373 na trilioni
1.5 kama deni la ndani. Kwa mujibu wa taarifa ya mwenendo wa uchumi ya mwezi
Julai 2012, deni la nje la Taifa (external debt) mpaka mwisho wa mwezi Juni
2012 lilikuwa limefikia kiasi cha dola za Kimarekani milioni 10,354.6 kiasi
ambacho ni ongezeko la zaidi ya dola milioni 385.9 kwa kipindi kama
hicho mwaka 2011. Aidha katika kipindi hicho deni la ndani lilikuwa kiasi cha
shilingi bilioni 4,174.2. Kambi ya Upinzani Bungeni ina taarifa kwamba
takwimu hizi za Deni la Taifa hazihusishi dhamana ambazo Serikali imezitoa kwa
Mashirika ya Umma na Kampuni binafsi. Dhamana lazima katika siku za usoni ziwe
ni sehemu ya deni la Taifa maana tumeshuhudia sasa ambapo Kampuni nyingi
binafsi zimeshindwa kulipa mikopo iliyodhaminiwa na Serikali. Mfano ni malipo
ya deni lenye thamani ya shilingi bilioni 60 la kukodisha ndege ya Airbus kwa
Shirika la ATCL kutoka kampuni ya Wallis Traders ya Lebanon na Deni
lililochukuliwa na Kampuni ya Kiwira Coal and Power limited ambayo mbia wake
alishindwa kuendesha mradi wa Makaa ya Mawe Kiwira licha ya kudhaminiwa na
Serikali Mkopo kutoka kwenye taasisi za Fedha hapa nchini ambapo sasa Serikali
imepanga kulipa shilingi bilioni 40 katika Bajeti ya mwaka huu. 8
Mheshimiwa Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani haina tatizo na uhimilivu wa Deni la Taifa (Debt
sustainability) kwani tunajua kuwa mataifa makubwa yanakopa sana na yana uwiano
mkubwa wa Deni kwa GDP kuliko sisi. Tatizo letu ni namna ambavyo fedha za
mikopo zinatumika. Matumizi ya mikopo tunayochukua sio endelevu maana sehemu ya
mikopo hiyo hutumika kwa matumizi ya kawaida badala ya matumizi ya uzalishaji
au kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha.
Kambi Rasmi ya Upinzani
inaendeleza wito wake
wa kutaka Fungu 22 la deni la Taifa lifanyiwe ukaguzi maalum (Special Audit)
ili tuweze kujua mikopo hii tunayochukua kila wakati inatumika kufanyia nini?
Miradi iliyotekelezwa kutokana na Madeni ambayo Waziri wa Fedha aliitangaza
wakati wa kufunga mjadala wa Bajeti kuu ya Serikali ifanyiwe ukaguzi kutambua
ukweli na kuona thamani ya Fedha.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaendelea kuhoji kama tulivyohoji
mwaka 2011/2012 kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma. Katika fungu 21, kasma
229929, Serikali imetenga Shilingi bilioni 26.4 kwa ajili ya kulipa fidia kwa
mikataba mbalimbali ambayo Serikali imeingia. Hii inaonyesha kuwa Serikali
inatumia fedha nyingi sana kwa ajili ya mikataba iliyoingiwa na Mashirika ya
Umma na kuliletea hasara Taifa.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani pamoja na kutaka majibu kutoka kwa
serikali, bado tunataka kuwe na usimamizi thabiti 9
ili
kulinda fedha za umma zinazotumika kwenye Mashirika ya Umma, ambapo kumekuwa na
usimamizi mbovu sana na unaopelekea Taifa kupoteza fedha nyingi sana kutokana
na ubadhirifu katika Mashirika ya Umma. Hii ni kweli kwa Mashirika ambayo
Serikali inamiliki sehemu ya hisa.
2.5 MKOPO WA KUNUNUA
RADA ILIYOGUBIKWA NA UFISADI
Mheshimiwa Spika, sehemu ya Malipo ya Deni la Taifa ni Mkopo ambao Serikali
ilichukua ili kununua Rada kutoka kampuni ya BAE ya Uingereza. Suala hili la
rada limejadiliwa sana nchini kwa upande mmoja tu wa ufisadi wa kupandisha bei
ya Rada na hatimaye kurejeshwa kwa iliyoitwa chenji ya Rada. Hiyo ilikuwa ni
nusu tu ya ukweli kuhusu suala la Rada kwani Serikali ilikopa kiasi cha dola za
kimarekani 40 milioni kutoka Benki ya Barclays ya Uingereza kwa ajili ya
kununulia Rada. Mkopo huo ulikuwa na Riba ya asilimia 4.9 juu ya kiwango cha
riba zinazotolewa na Benki ya Dunia au IMF.
Kambi Rasmi ya Upinzani
inataka kujua kama mkopo huu umeshalipwa wote na jumla tulilipa kiasi gani cha
fedha. Ukilinganisha fedha iliyorejeshwa kama chenji ya Rada na Fedha ambayo
Tanzania iliilipa Benki ya Barclays (Principal amount na Interest), je chenji
ya Rada ilikuwa na thamani yoyote kifedha? Mjadala wa ununuzi wa Rada hauwezi
kuisha kwa kufurahia kurejeshewa chenji tu. Mjadala huu bado mbichi kabisa
kwani tunataka ukweli na ukweli mtupu uelezwe kwa umma na kuona 10
Taifa
lilipata hasara kiasi gani kwa ufisadi huu wa kimataifa na hatua stahiki za
kisheria kuchukuliwa dhidi ya wote walioingiza hasara kwa Taifa letu.
2.4 Kitengo cha
Udhibiti wa Fedha Haramu
Mheshimiwa Spika, taifa letu limekuwa na sheria nyingi ambazo ziliwahi kutungwa
kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la fedha haramu, rushwa na uhalifu
uliopangwa hapa nchini mwetu tangu tupate uhuru na hii inathibitishwa na uwepo
wa sheria zaidi ya 15 kuwahi kutungwa tangu uhuru (tazama kiambatanisho A).
Vile vile Bunge liliimarisha Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu mwaka 2011.
Hata hivyo bado nchi yetu imegubikwa na fedha chafu na hasa wizi katika Mabenki
hapa nchini. Wakati sheria ya Fedha haramu inayataka Mabenki kutunza kumbukumbu
sahihi za wateja, kumekuwa na matukio (yaliyoripotiwa na yasiyoripotiwa) ya
Wafanyakazi wa mabenki hapa nchini kushirikiana na baadhi ya wananchi kuiba
fedha za wateja na hasa wateja ambao wamefariki dunia na ndugu na jamaa zao
kutojua taarifa za kibenki za marehemu hawa. Serikali inapaswa kufahamu kuwa
wizi kwenye mabenki ni moja ya sifa mbaya sana ya mfumo wetu wa fedha na hivyo
kusababisha Benki kuweka riba kubwa sana ili kufidia ‘risk’ kama hizi za watu
‘kupiga’ amana za wateja kwenye mabenki. Kambi Rasmi ya upinzani inaitaka Wizara
ya Fedha kupitia Kitengo 11
cha
Udhibiti wa Fedha haramu kudhibiti wizi kwenye Benki za hapa nchini.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kupata maelezo ya kina juu
ya matatizo ya mtaji “Capital under pressure” yanayoikabili benki ya NBC na
hatua zilizochukuliwa na Serikali kama mmoja wa wanahisa dhidi ya mwanahisa
mwenye dhamana ya kuisimamia Benki hiyo (ABSA) kwa kushindwa kuisimamia kwa
umakini na hivyo kuiingiza katika matatizo hayo ya mtaji. Mheshimiwa Spika,
hivi sasa wanahisa (ambapo Serikali ni mmoja wao) wanapaswa kuongeza mtaji
katika benki ya NBC ili kuinusuru, Benki ambayo ni moja ya Benki kubwa kabisa
hapa nchini ambayo kama ingekuwa na usimamizi mzuri ingepaswa kujiendesha
yenyewe na kutoa gawio kwa wanahisa.
Mheshimiwa Spika, taarifa iliyotolewa na Benki Kuu ya Uswissi na kuchapishwa na
magazeti mbalimbali ya hapa nchini mwezi June, 2012 inanonyesha kuwa viongozi
wa Serikali pamoja na wafanyabiashara wakubwa wametorosha fedha zao katika
mabenki ya Uswissi kiasi cha shilingi bilioni 315.5. Habari zaidi zinaeleza
kwamba mabilioni haya yanatokana na ‘deals’ zilizofanywa na watendaji wa
Serikali na wafanyabiashara kadhaa kwenye sekta za Nishati na Madini. Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni imepata taarifa kuwa mmoja wa Viongozi wa juu kabisa
wa 12
Tanzania
na baadhi ya Mawaziri wa Serikali za awamu zilizopita ni miongoni mwa wamiliki
wa Fedha hizi. Sehemu kubwa ya Fedha zililipwa na Kampuni za utafutaji wa
Mafuta na Gesi katika Pwani ya Mkoa wa Mtwara zilizopewa mikataba kati ya mwaka
2004 na 2006. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa taarifa rasmi ya
hatua gani imechukua mara baada ya taarifa ile kutoka Benki ya Taifa ya Uswissi
ilipotolewa. Tunaitaka Serikali kuliambia Taifa hatua itakazochukua kurejesha
fedha hizi na nyingine zozote ambazo zimefichwa ughaibuni. Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni italazimika kuweka wazi taarifa na majina ya watu wenye
umiliki wa fedha katika Benki za nchini Uswissi iwapo Serikali haitatoa taarifa
rasmi kuhusu suala hili.
Mheshimiwa Spika, Aidha, kuna taarifa nyingine zinaonyesha jinsi ambavyo taifa
linaibiwa kupitia kesi mbalimbali ambazo Serikali imeshitaki au kushitakiwa
kwenye Mahakama za Kimataifa. Mfano mzuri ni Kesi ya IPTL na Standard Chartered
Bank ya Hong Kong ambayo imechukua muda mrefu bila kuisha na kuliingizia taifa
hasara kubwa sana. Tunapenda kufahamu ni kwa nini mpango wa kumaliza kesi hii
nje ya Mahakama hautekelezwi na vile vile mpango wa kugeuza Mtambo wa kufua
umeme wa IPTL kuwa wa Gesi kwa nini hautekelezwi?
Kambi Rasmi ya Upinzani
inataka kupata majibu
kuhusu mambo yafuatayo; 13
Kwanza,
fedha zilizoko kwenye Escrow Akaunti Benki Kuu za IPTL (Tegeta escrow)
zimefikia kiasi gani mpaka sasa, na usalama wa fedha hizo ukoje? Ikumbukwe
kwamba kuna uamuzi wa Bunge kwamba Fedha hizi zisitumike wala kutolewa mpaka
maamuzi kuhusu mtambo wa IPTL kufikiwa na hasa uamuzi wa kugeuza mtambo huu
kutumia Gesi Asilia.
Pili, Suala hili la
kesi ya IPTL limechukua muda mrefu sana na sasa ni wakati muafaka likamalizwa
nje ya mahakama kwa Waziri wa Fedha kukutana na pande zote za mgogoro huu ili
liweze kufikia mwisho.
2.6 Kampuni ya Oxford
University Press Tanzania Kufungiwa
Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 03 Julai 2012 Benki ya Dunia ilitangaza
kuifungia kampuni ya uchapishaji ya Oxford University Press Tanzania Ltd
(OUPTL) kutokana na vitendo vya rushwa ambavyo kampuni hiyo ilikiri
kuhusika kwake kwenye miradi mbalimbali ya elimu iliyokuwa inafadhiliwa na
Benki hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Spika, kampuni hiyo ilikiri kuhusika katika kuwahonga maafisa
mbalimbali wa Serikali katika mkataba wake wa kusambaza vitabu na kampuni hiyo
ilikubali kuilipa Benki ya Dunia kiasi cha dola 500,000 kama sehemu ya
makubaliano yake kutokana na kashfa hiyo. 14
Mheshimiwa Spika,
mamlaka ya manunuzi ya umma ilitangaza kuifungia kampuni hiyo hapa nchini kwa
kipindi cha miaka saba, wakati ambao tayari tulishawapa zabuni ya kusambaza
vitabu vilivyotokana na chenji ya rushwa ya Rada ambazo ziliamuliwa kuwa
zitaenda kununua vitabu.
Kambi Rasmi ya Upinzani
inaitaka Serikali
kuinyang’anya kampuni hii zabuni ya kuchapisha na kusambaza vitabu hivyo na
badala yake kazi hiyo yapewe makampuni ya ndani ya nchi. Tabia ya Serikali
kufanya kazi na Kampuni ambazo tayari zina dosari ama za kifisadi au kukiuka
sheria na maagizo ya Serikali inatoa picha mbaya kwenye uchumi. Hali kadhalika,
Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuwachukulia hatua maafisa wote wa
Wizara waliohusika katika “rushwa ya Oxford”.
3.0 Mishahara hewa
nchini
Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
kuhusu makadirio ya mapato na matumizi katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2012/2013, tulitaja kiasi cha shilingi
bilioni 91 ambazo zililipwa kama mishahara kwa watumishi hewa kama
ilivyoripotiwa na magazeti ya ‘The Daily News’ na ‘The Guardian’ ya
Machi 23, 2011.
1 http://www.corruptiontracker.or.tz/dev/index.php?option=com_content&view=article&id=151%3Aghost-workers-difficult-nut-to-crack&catid=18%3Acurrent-issues-&Itemid=51&lang=en
15
Mheshimiwa Spika, ripoti
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya tarehe 31 Machi, 2012
inaonesha kwamba kwa mwaka wa fedha 2010/2011 jumla ya shilingi 142,715,827.992
zililipwa kama mishahara kwa wastaafu, watumishi walioacha au kufukuzwa kazi na
watumishi wengine ambao hawakustahili. Aidha, ripoti hiyo imeonesha kiasi cha
shilingi 1,842,607,565.29 zilizolipwa kama mishahara hewa kwa mwaka wa fedha
2009/2010.
2 Tazama Ripoti ya CAG toleo la Kiingereza uk.37.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Fedha kwa kamati ya kudumu
ya Bunge ya fedha na uchumi ya tarehe 7 Agosti, 2012 ni kwamba uhakiki wa
watumishi uliofanyika mwezi Januari, 2012 kwenye Halimashauri 133 na kwenye
taasisi na wakala za Serikali 154 ulibaini majina 9,949 ya watumishi
wasiostahili kuwemo kwenye orodha ya mishahara. Idadi hii ya watumishi hewa ni
sawasawa na takribani idadi ya watumishi walioajiriwa katika sekta nzima ya
madini kwenye migodi ya dhahabu hapa nchini. Watumishi hewa wanaokaribia 10,000
ni wengi mno na inaonyesha dhahiri namna Serikali isivyo makini katika suala
hili ambalo linasababisha upotevu mkubwa wa Fedha za Umma.
Mheshimiwa Spika, Waziri wa Fedha alikiri mbele ya Kamati ya Fedha na Uchumi
kwamba mwezi Februari Serikali ililipa shilingi bilioni 5.1 kama mishahara
hewa. Hii maana yake ni kwamba Serikali 16
hutumia
zaidi ya shilingi bilioni 70 kila mwaka kwa watumishi hewa wa Serikali.
Mheshimiwa Spika, tunataka fedha hizi wanazolipwa watumishi hewa zitumike
kuwalipa walimu na madaktari madai yao kwani ni nyingi na zinatosha sana. Siku
zote sababu za Serikali kutotimiza matakwa ya wafanyakazi kwenye sekta ya Afya
na Elimu ni kwamba Serikali haina Fedha. Lakini hapa tunashuhudia Shilingi
bilioni 70 kila mwaka zikiteketea kulipa watumishi hewa ambao hawapo, hawafanyi
kazi na hivyo kufaidisha mtandao wa kifisadi ambao kwa vyovyote vile unaanzia
Wizara ya Fedha na Wizara ya Utumishi. Serikali inakosa vipi fedha za kulipa madai
ya Walimu na inapata za kulipa watumishi hewa? Serikali inakosa vipi fedha za
kulipa Madaktari na Manesi lakini inapata shilingi bilioni 70 kila mwaka kulipa
watumishi hewa?
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka mradi huu wa watumishi hewa wenye
mauzo (turnover) ya shilingi 70 bilioni kwa mwaka uvunjwevunjwe ili kupata
fedha za kulipa Walimu na Madaktari. Waziri wa Fedha asambaratishe mtandao huu
mwovu ambao sasa umeota mizizi kwenye Taasisi za Serikali. Vile vile Waziri
agawe kwa Wabunge taarifa ya uhakiki wa wafanyakazi wa Serikali na pia hatua
ambazo Serikali imechukua dhidi ya vinara wa mtandao wa watumishi hewa
Serikalini.
4.0 Benki Kuu ya
Tanzania-(BOT) 17
Mheshimiwa Spika, taasisi
hii ndiyo yenye dhamana ya kutayarisha na kusimamia sera za fedha na utendaji
mzima wa taasisi za fedha kwa ujumla. Katika kutekeleza hilo Benki Kuu ndicho
chombo kinachoweka miongozo kwa taasisi za fedha, taasisi za bima na taasisi za
hifadhi za jamii ili kuhakikisha fedha za wanachama katika taasisi hizo zinalindwa.
Mheshimiwa Spika, taasisi za fedha zimegawanyika katika sehemu kuu mbili,
ambazo ni tasnia ya benki (Banking industry) na tasnia ndogo ya
fedha (Microfinance industry). Tasnia zote hizi zinahudumia
wateja tofauti kwa kulingana na wanachojishughulisha nacho katika kuinua kipato
cha familia inayomtegemea, mteja yuko kwenye sekta binafsi au sekta rasmi ya
ajira.
Mheshimiwa Spika, Benki Kuu katika kutimiza wajibu wake inailazimu kutoa
vigezo vitakavyozingatiwa katika utoaji wa mikopo ili kukabiliana na wakopaji
ambao wanaweza kuwa na lengo la kuchukua fedha wakati hawana nia ya dhati ya
kurejesha mikopo yao.
4.1 RIBA KATIKA TAASISI
ZA FEDHA
Mheshimiwa Spika, tofauti kati ya viwango vya riba vinavyotozwa kwenye mikopo
na vile vinavyotolewa kwenye amana kama faida vimeendelea kuwa juu, licha ya
kuongezeka kwa ushindani katika sekta ya kibenki. Hii imechangiwa kwa kiasi
kikubwa na kukosekana kwa taarifa sahihi za wakopaji (credit reference
data bank) na 18
kutokuwepo
kwa taasisi ya utoaji wa taarifa sahihi za waombaji mikopo (Credit
Rerefence Bureau) nchini. Aidha, gharama kubwa za kufanya biashara
kutokana na miundombinu hafifu, nazo zimechangia kuongeza viwango vya riba
vinavyotozwa kwenye mikopo. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaomba taarifa ya
kuanzishwa kwa Credit Reference Bureaux kwa mujibu wa Sheria ya Benki na
Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.
4.2 Usimamizi Wa Tasnia
Ndogo ya Fedha (Microfinance Industry-MFI)
Mheshimiwa Spika, tasnia hii ndiyo inayoshughulika moja kwa moja na kundi kubwa
la Watanzania ambao hawako kwenye mfumo rasmi wa ajira kwa kuwapa mikopo midogo
midogo kwa shughuli rasmi au zisizo rasmi, ili kuhakikisha kuwa kipato cha
familia kinapanda na hivyo uchumi wa mwananchi mmoja mmoja unakua.
Mheshimiwa Spika, tasnia hii inalenga kuboresha maisha ya wananchi wa
vijijini na maeneo mbalimbali ya mijini. Tasnia hii inalenga kuboresha maisha
kwa wananchi mmoja mmoja au makundi (Saccoss) na benki jamii (vicoba) ambazo
zimekuwa na wanachama wengi wanaoendelea kujiunga ili kujikwamua kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, kukosekana kwa mdhibiti anayeelewa jinsi tasnia hii
inavyofanya kazi zake na aina ya wateja inaowahudumia ni 19
udhaifu
mkubwa unaosababisha tasnia hii kushindwa kukua. Kukosekana kwa udhibiti wa
sekta ndogo ya Fedha kunasababisha wananchi masikini kuumia sana. Mfano
tumeshuhudia namna Kampuni za kukopesha zinavyowafanya Walimu vijijini kuwa
masikini zaidi kwa kuweka riba kubwa sana. Hata hivyo Serikali imekaa kimya
bila kusaidia wanyonge hawa kwa kuchukua hatua madhubuti za kudhibiti na
kusimamia sekta hii. Mfano mzuri wa Serikali kushindwa kusaidia wanyonge ni
pale ambapo wannachi wengi sana kujikuta wamepoteza fedha zao kupitia ‘schemes’
kama vile DECI ambapo wananchi walikusanya zaidi ya shilingi bilioni 16 ambazo
mpaka sasa hata riba yake hatujui inakwenda wapi? Kungekuwa na Mamlaka ya
kusimamia sekta ya fedha kwa ajili ya wanyonge tusingeshuhudia unyonyaji huu.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuunda Mamlaka ya
Usimamizi wa sekta ndogo ya Fedha (Tanzania Microfinace Regulatory
Authority) hapa nchini badala ya Benki Kuu ya Tanzania ambayo ndiyo
msimamizi wa tasnia ya benki. Lengo ni kuhakikisha kuwa wananchi wa vijijini
wanaopata mikopo kutoka kwenye taasisi za Benki wanalindwa na dola. Mamlaka
italinda Haki za wanyonge dhidi ya ‘loan sharks’ na Wajibu wa wanyonge wenye
kuchukua mikopo.
Mheshimiwa Spika, kuundwa kwa chombo chenye mamlaka ya kusimamia taasisi ndogo
ya fedha ni lazima kutokana na ukweli 20
kwamba
kuna utofauti wa muundo baina ya mabenki na taasisi ndogondogo za fedha;
inakuwa ni vigumu kudhibiti riba na utoaji wa vigezo vya kifedha katika
kuhudumia wananchi na kutoa mikopo kwa wateja wa tasnia hizo mbili zilizo
tofauti kimuundo.
Mheshimiwa Spika, kuwepo kwa chombo chenye mamlaka pia itasaidia kuwa na Credit
Reference Bureau itakalokuwa na taarifa za wakopaji kutoka taasisi ndogondogo
za fedha tofauti na itakayosimamia wadaiwa wa mabenki na taarifa hizi
zitasaidia udhibiti wa wateja wa taasisi hizi kuchukua zaidi ya mkopo mmoja
kwenye taasisi tofauti tofauti ambapo hali hii husababishwa na ucheleweshaji wa
mikopo inayotolewa na taasisi hizi pamoja na uhafifu wa mikopo katika kumsaidia
mlengwa.
4.3 Mifuko ya Hifadhi
za Jamii
Mheshimiwa Spika, Mifuko ya Hifadhi za Jamii ni mojawapo ya sekta ambayo ina
uwezo mkubwa wa kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana wetu, kama uwekezaji
unaofanywa kwa kutumia mifuko hiyo utasimamiwa vizuri.
Meshimiwa Spika, inaonesha kwamba mifuko hii imekuwa ikikusanya michango ya
wanachama na kulipa wastaafu wanachama wa Mifuko hii vizuri. Kutokana na
maelekezo ya sheria mpya iliyoleta mjadala baina ya wafanyakazi na serikali juu
ya mabadiliko ya sheria na utoaji wa mafao kwa wafanyakazi, pamoja na Bunge 21
kutaka
mabadiliko ya sheria hiyo bado kuna haja ya kutazama namna mifuko ifanyavyo
kazi.
Kambi Rasmi ya Upinzani
inaitaka serikali
kuweka wazi utendaji wa Mifuko hii katika maeneo nyeti yafuatayo, kwanza Ukwasi
wake (Liquidity of the Social Security funds), pili Uwekezaji (Investments)
pia Risk Management reports. Taarifa katika maeneo haya hupelekwa na mifuko
kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma na kutokana na utaratibu
wa Kazi wa Kamati hii ya POAC ni vigumu wananchi wote kuona taarifa hizi ambazo
ni muhimu kuwa wazi kwa umma. Taarifa kama hizi zitaliwezesha Bunge kuelewa
kiwango cha usalama wa Mifuko hii na uwezo ziada (excess financial capacity)
kuendelea kutoa huduma zinazohitajika. Kama ilivyo kwa Mabenki, tunashauri
kuwa taarifa za robo mwaka za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ziwe zinatangazwa
kwenye magazeti yanayosomwa zaidi nchini ili wananchi na hasa wanachama wa
mifuko waone namna mifuko yao inavyofanya kazi.
Mheshimiwa Spika, aidha, kwa kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kipindi chote
imekuwa ikitoa ushauri katika sekta hii, hatuna budi kurudia ushauri tulioutoa
mwaka jana kama ifuatavyo:
“Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inapendekeza kwa Mifuko ya PSPF na PPF
kuangalia namna ya kuwekeza katika maeneo yanayochochea ukuaji wa uchumi na
hivyo kuzalisha ajira na 22
kupata wanachama zaidi. Maeneo kama uwekezaji kwenye Bandari
na Reli yanapaswa kuangaliwa kwani kutokana na Jiografia ya nchi yetu ni maeneo
yanayoweza kuzalisha faida kubwa sana. Tunaitaka Serikali ilieleze Bunge kuna
mipango gani katika Mashirika haya (PSPF na PPF) kuangalia maeneo mapya ya
uwekezaji katika miundombinu na hasa Bandari.
Mheshimiwa Spika, Mifuko ya hifadhi ya jamii imewekeza katika miradi ya ujenzi
wa nyumba nafuu kwa ajili ya wanachama wao na pia wanachi kwa ujumla.
Tunasisitiza Miradi hii isiwe Dar es salaam na Mwanza tu bali ienee nchi nzima
kama ambavyo mfuko wa PSPF umeanza.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani pia inashauri kwamba fao la Elimu ambalo
Mfuko wa PPF unatoa kwanza litolewe na Mifuko mingine pia lakini pia lipanuliwe
hadi kufikia elimu ya Chuo Kikuu. Fao hili la Elimu ambalo ni muhimu sana na
twapongeza mfuko wa PPF kwa kulianzisha ni fao ambalo litasaidia sana
kuhakikisha kuwa yatima ambao wazazi wao wanakuwa wamefariki wanapata uhakika
wa kuendelea na masomo. Fao hili liwe fao la lazima kwa mifuko yote nchini.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni bado inasisitiza ushauri wake kuwa Mifuko
yote ya Hifadhi ya Jamii ihamishiwe Wizara ya Kazi na Ajira kama Wizara
inayohusika na ‘social security’. Hoja hii inatiliwa nguvu na uhalisia kwamba
Mdhibiti wa Mifuko 23
(SSRA) yupo chini ya Wizara ya Kazi. Vile vile Wizara ya
Fedha kama mlipaji mkuu wa Pensheni asiwe na Taasisi hata moja ya Pensheni
chini yake ili kuweka ‘checks’.
Mheshimiwa Spika, Hali kadhalika hakuna sababu ya kuwa na utitiri wa mifuko
mingi kama ilivyo sasa. Ipunguzwe na kubakia na mifuko miwili tu, mmoja wa
wafanyakazi walio katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi na mwingine kwa
wafanyakazi wa sekta ya umma. Tunarejea pendekezo letu kwamba mifuko ya
NSSF na PPF iunganishwe kuwa mfuko mmoja kwa ajili ya sekta binafsi na sekta
isiyo rasmi na mifuko ya PSPF, LAPF na GEPF iunganishwe kuwa mfuko mmoja kwa
ajili ya kushughulika na wafanyakazi wa Sekta ya Umma”.
Mheshimiwa Spika, mojawapo ya vipaumbele vya Kambi Rasmi ya Upinzani kwa
mwaka 2012/2013 ni kupunguza misamaha ya kodi ya kutozidi asilimia moja ya GDP,
kutokana na Mapato mengi ya Serikali kupotea kwa sababu ya kutoa misamaha ya
kodi kwa wadau mbalimbali wanaotakiwa kulipa kodi, na ikizingatiwa moja ya
michango ya waziri akiwa mbunge tarehe 25/8/2011 alisema “kupunguza
misamaha ya kodi ya kutozidi asilimia moja ya GDP”. Kambi Rasmi ya
Upinzani inaamini waziri alikuwa na nia ya dhati na kukubaliana na Kambi Rasmi
ya Upinzani uwezekano wa jambo hili. Hivyo basi, ili kuonesha kuwepo kwa
dhamira ya kweli Kambi Rasmi 24
ya
Upinzani inataka waziri alijulishe bunge juu ya utekelezaji wa azimio hili.
6.0 MSAJILI WA HAZINA
NA BODI ZA MASHIRIKA YA UMMA
Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa mnamo mwaka 2010 Sheria namba 2 (the written
laws (miscellaneous amendments) No 2. ACT 2010 ilipitishwa na katika eneo la
kumi (part X) ilifanyia marekebisho sheria ya mashirika ya umma (the public
Corporations Act, CAP 257). Sheria hii ilisainiwa na Rais mnamo tarehe 20 Mei
2010.
Mheshimiwa Spika, katika mabadiliko hayo ya sheria ibara ya 20 na 21
ilibainisha bayana majukumu ya msajili wa hazina na ndipo iliweka majukumu yake
ya kazi kuwa ni kusimamia mashirika yote ya umma. Aidha, mabadiliko hayo
yalibainisha wazi kuwa msajili wa hazina hatakuwa mjumbe wa Bodi za mashirika
haya na wala hapaswi kushiriki kwenye vikao vya bodi vya mashirika haya kwani
yeye ni msimamizi mkuu wa mashirika hayo na anapaswa kusimamia utendaji kazi
wake.
Mheshimiwa Spika, pamoja na mabadiliko hayo ya sheria bado msajili wa hazina
amekuwa akihudhuria vikao mbalimbali vya bodi za Mashirika ya Umma kama mjumbe
jambo ambalo ni kinyume na sheria, na amekuwa akishiriki moja kwa moja kwenye
maamuzi ya bodi hizo jambo ambalo linamfanya kushindwa kutimiza wajibu wake wa
kuwa msimamizi kama ambavyo sheria inaelekeza 25
Kambi ya Upinzani inataka
kupata maelezo ya kina ni kwa nini hali hii imeendelea kuachwa iwe ilivyo kwa
msajili wa hazina kuendelea kuwa mjumbe wa vikao vya Bodi za mashirika ya umma
kinyume na sheria. Aidha tunataka kauli ya serikali kuhusiana na suala hili.
Mheshimiwa Spika, Kambi
ya Upinzani inapenda kupata maelezo ya Serikali kuhusu masuala yafuatayo.
Moja, Sakata la uuzwaji
wa hisa za Shirika la UDA umefikia wapi?
Pili, Serikali imefikia
wapi katika utungaji wa Sheria mpya ya Ofisi ya Msajili wa Hazina ili
kuimarisha usimamizi wa Mashirika ya Umma.
Tatu, Serikali imefikia
wapi katika pendekezo la kuifanyia marekebisho Shirika Hodhi la Mashirika ya
Umma (CHC) ili liweze kumiliki, kusimamia na kuziendesha hisa za serikali
katika Kampuni binafsi ambapo umiliki wa Serikali ni chini ya asilimia 50.
Pendekezo hili lilikuwa ni uamuzi wa Bunge na hivi sasa mwaka mzima umepita
bila Bunge kupatiwa taarifa yeyote kinyume na maelekezo yake.
Nne, Serikali imefikia
wapi katika utekelezaji wa Waraka namba moja wa mwaka 2012 kuhusu usimamizi na
uendeshaji wa Mashirika ya Umma na hasa mahusiano kati ya Mashirika ya Umma na
Wizara mama. Waziri wa Fedha kama msimamizi mkuu wa Mashirika ya Umma amechukua
hatua gani kuhakikisha falsafa ya ‘eyes on, hands off’ katika kusimamia
Mashirika ya Umma inatekelezwa 26
kikamilifu
na kuhakikisha Mashirika ya Umma yanaendeshwa kwa faida na bila kuingiliwa
ingiliwa na Wanasiasa?
7.0 Ofisi ya Takwimu ya
Taifa
Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (National Bureau of Statistics –
NBS) ilizinduliwa rasmi tarehe 26 Machi, 1999 kama Wakala wa Serikali
(Executive Agency) kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka
1997, (The Executive Agencies Act 1997) (Act No. 30 of 1997), na ndio chombo
rasmi kinachojihusisha na kutafuta, kuandaa na kusambaza takwimu hapa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, katika kupanga mipango ya maendeleo na kuandaa sera
mbalimbali za nchi husika, upatikanaji wa takwimu rasmi zinazotokana na Kanuni
na Mbinu za Kitaalamu iliyowekwa na Ofisi ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa (United
Nations Statistical Division) ni muhimu. Takwimu zote zilizo rasmi
duniani hutolewa na Ofisi za Takwimu za nchi husika kupitia Sheria za Takwimu
za nchi mbali mbali.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani imekua ikitoa Mapendekezo ya
kuboresha utendaji wa Ofisi ya Takwimu katika Nyanja mbalimbali na serikali
kutothubutu kuchukua mapendekezo hayo na kuyafanyia kazi. 27
Mheshimiwa Spika,
katika taarifa ya miaka hamsini ya wizara,taarifa inaonesha wizara kuwa na nia
ya kuboresha ofisi ya takwimu ya taifa kwa kuboresha miundombinu ya utoaji
takwimu nchini ,kuimarisha mfumo wa takwimu nchini (NBS), kutoa takwimu sahihi
na kwa wakati, kutokana na nia hii ya serikali Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka
serikali kuzingatia Ofisi ya Takwimu Kuwa na uhisiano wa moja kwa moja wa Ofisi
ya Takwimu ya Taifa na ngazi za Mikoa, Halmashauri za Wilaya, Kata na Vijiji
kurahisisha upatikanaji wa takwimu ili zisaidie katika kupanga mipango ya
maendeleo.
8.0 Mamlaka Ya
Mapato-TRA
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba Mamlaka
ya Mapato Tanzania ijenge uwezo wa kukagua mahesabu ya kikodi kwenye Kampuni za
Utafutaji wa Mafuta na Gesi, Kampuni za Madini na Kampuni za Simu ambazo uzoefu
unaonyesha kuwa katika maeneo haya kuna mbinu nyingi sana za kukwepa kodi.
Mheshimiwa Spika, kwa msisitizo mkubwa sana Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
inaitaka mamlaka ya Mapato Tanzania kushirikiana kwa karibu na Mamlaka ya
Mawasiliano nchini kukagua mapato ya Kampuni za simu na hasa kampuni ambazo
zinatoa huduma kwenye kampuni za Simu. 28
Mheshimiwa Spika, Katika
mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Mawasiliano kulikuwa na mjadala kuhusu namna
ambavyo wasanii wa Tanzania wanavyonyonywa mapato na Kampuni zinazotoa huduma
ya miito kwenye kampuni za simu. Bunge lako lilielezwa kwamba Biashara ya miito
kwenye simu ina thamani ya shilingi bilioni 43 kwa mwaka lakini msanii
anayetengeneza kazi zinazouzwa anapata asilimia 7 tu ya mapato hayo.
Mheshimiwa Spika, taarifa zaidi za ziada zinaonyesha kuwa kampuni ya On
Mobile yenye mkataba na Kampuni za Simu za Vodacom na Airtel kama ‘aggrigator’
wa miito ya simu yenye miziki ya wasanii hapa nchini hailipi kodi kutokana na
mapato yake. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa taarifa za kikodi
za kampuni hii na washirika wake na hatua ambazo Serikali imechukua dhidi yao.
Kambi ya upinzani inashauri pia kwamba Mapato yanayotokana na miradi kama hii
kwenye Kampuni za simu yawe ‘ring fenced’ na kutozwa kodi stahiki au kodi
maalumu.
9.0 Ofisi ya Mkaguzi
Mkuu wa Ndani-Internal Auditor General
Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mkuguzi Mkuu wa Ndani (Internal Auditor General)
iliyoanzishwa na mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2010 inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikileta migongano katika maeneo ya
kiutendaji na uwajibikaji, sheria haipo wazi juu ya upatikanaji wa mtaalam huyo
kama 29
inavyotakiwa
na sheria na 8 ya utumishi wa umma, kwa mfano kutangazwa kwa nafasi hizo na
waombaji kufanyiwa usaili.
Mheshimiwa Spika, pamoja na utata wa uteuzi wa mkaguzi wa ndani kama sheria
ya utumishi wa umma inavyoelekeza mkaguzi wa ndani anasimamiwa na Katibu Mkuu
Hazina (Paymaster General) ambaye naye ni mkaguliwa- kwa hiyo
kunakuwa na mgongano wa kimaslahi uhuru wa ofisi ya mkaguzi wa ndani inaweza
kukosa uhuru Kambi Rasmi ya Upinzani inaishauri serikali katika ofisi ya
Mkaguzi wa Ndani (Internal Auditor General office) ingepaswa iwe na bodi ambako
maalumu wangekuwa wanaripoti ili kuweka uhuru unaofaa.
Mheshimiwa Spika, wakaguzi wa ndani ni waajiriwa wa serikali na hufanya kazi
zao za ukaguzi kwa kipindi chote ambacho shughuli za serikali zikifanyika,
mfano; katika halmashauri wakaguzi hutakiwa kuwajibika kuanzia upokeaji wa
fedha kutoka hazina, hadi kutumika kwake, Kambi Rasmi ya Upinzani inahoji
serikali nini nafasi ya wakaguzi wa ndani kama ubadhirifu wa fedha za umma
umeendelea kuwepo kama ripoti za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
zinavyothibisha?
Mheshimiwa Spika, katika ushughulikiaji wa matumizi mabovu ya rasilimali za
umma serikali imekuwa legelege hasa pale taarifa 30
zinapotolewa
na wakaguzi wa ndani ambao hutoa taarifa mara kwa mara na seriakali kukaa
kimya, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka serikali kutambua umuhimu wa taarifa
hizi za wakaguzi wa ndani na kuhakiki inachukua hatua stahiki pasipo kusubiri
taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambazo ukaguzi wake hufanyika kwa
kuchelewa zaidi.
10.0 Utekelezaji wa
Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012 Pamoja na Mpango wa Maendeleo kwa Mwaka
2012/2013
Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya Wizara ya Fedha mwaka 2011/2012 fungu Namba
50 wizara ilitenga shilingi bilioni 659 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na
fedha zilizotumika hadi kufikia Juni 2012 ni shilingi bilino 402.7 ambapo fedha
za ndani zikiwa shilingi bilioni 78.65 sawa na asilimia 11.9 ya bajeti ya
maendeleo hivyo kutegemea fedha za nje katika kutekeleza miradi ya maendeleo
kwa asilimia 88.1. Kambi Rasmi ya Upinzani, pamoja na Seriliali kutokubali
kutumia mapato ya ndani zaidi katika kugharimia miradi ya maendeleo, I azidi
kushauri serikali kuwa na Makati wa dhati wa muda mrefu wa kuachana na
utaratibu wa kutegemea misaada ya nje. Mkakati huo ulenge kuiongezea mapato kwa
kutumia mbinu mbalimbali za kodi.
Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya 2012/2013 serikali imetenga shilingi
bilioni 546.51 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo 31
ambayo
ni pungufu kwa asilimia 18 ya bajeti ya mwaka 2011/2012 ambapo serikali
ilitenga shilingi bilioni 659. Katika bajeti ya 2012/2013 ni asilimia 19.3 tu
ya fedha za ndani ndizo zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo na asilimia
80.7 ya makadirio ni fedha za nje ikiwa ni mikopo ya kibiashara na misaada.
Kambi Rasmi ya Upinzani inahoji: ni maendeleo yapi ambayo serikali inadhamiria
kwa kutenga fedha ya maendeleo ambayo ni pungufu kwa asilimia 18 ya bajeti ya
mwaka jana?
Hitimisho
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inasisitiza umuhimu wa kuisimamia
vema Wizara ya Fedha katika kusimamia uchumi wa nchi. Tuna imani kwamba Waziri
wa Fedha ndugu William Mgimwa na Manaibu wake Mhe. Janeth Mbene na Mhe. Saada
Mkuya Salum wataweza kukabili changamoto tulizoainisha katika hotuba yetu na
kufanyia kazi mapendekezo ambayo tumeyatoa. Tumeona dalili za Wizara hii na
hasa Waziri na Manaibu wake kusikiliza katika masuala ya Kikodi hivyo, tuna
imani kwamba wataendelea kusikiliza.
Kambi Rasmi ya Upinzani
haitasita kutoa
ushirikiano kwa lengo la kuleta maendeleo katika nchi yetu. Hata hivyo,
tutakosoa kwa nguvu zetu zote na kuchukua hatua za kiuwajibikaji dhidi ya njama
zozote za kudhoofisha maendeleo ya Taifa na watu wake. Siku zote tutasimama
upande wa wanyonge na kuwasemea wasio na sauti, 32
Watanzania
milioni 30 wanaoishi vijijini na kwenye dimbwi la Umasikini (The Bottom 30M).
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani
naomba kuwasilisha.
……………………………………
Kabwe Zuberi Zitto (Mb)
Waziri Kivuli-Wizara ya
Fedha
12.08.2012
KIAMBATANISHO A.
Sheria mbalimbali
kuhusiana na fedha haramu
i.
the establishment of the Permanent Commission of Inquiry, or Ombudsman, 1966;
ii.
the Foreign Exchange Control Act 1966;
iii.
the Anti-Corruption Act 1971;
iv.
the establishment of an anti-corruption squad in 1975;
v.
the Economic Sabotage Act 1983;
vi.
the Economic and Organised Crime Act 1984;
vii.
the Proceeds of Crime Act 1991;
viii.
the Leadership Code (Declaration of Assets) Act 1995;
ix.
the appointment of the Presidential Commission of Inquiry into Corruption,
1996;
x. the BOT Circular to
Banking and Non-banking Financial Institutions, No. 8 of 2000, on Money
Laundering.
33
xi.
the Drugs and Illicit Traffic of Drugs Act 1995;
xii.
the Arms and Ammunition Act 1991;
xiii.
the Mutual Assistance in Criminal Matters Act 1991; and
xiv.
the Tanzania Intelligence and Security Act 1998.
xv.
The anti-money laundering Act, 2007
xvi. the anti-money
laundering (amendment) act, 2012
COMMENTS