KAULI YA AWALI KUHUSU TAMKO LA CCM DHIDI YA CHADEMA

Nimejulishwa na vyanzo vyetu kuwa msemaji wa CCM amefanya mkutano na wanahabari na kutoa madai mbalimbali ya uzushi kwa CHADEMA ...





Nimejulishwa na vyanzo vyetu kuwa msemaji wa CCM amefanya mkutano na wanahabari na
kutoa madai mbalimbali ya uzushi kwa CHADEMA baada ya CHADEMA kuendelea  kutekeleza
mikakati na mipango yake ya kuwaunganisha watanzania kupitia falsafa ya ‘nguvu ya
umma’ katika kuchangia vuguvugu la mabadiliko (M4C) katika maeneo mbalimbali nchini.
Nitatoa tamko kamili na kueleza hatua za ziada baada ya kupata taarifa iliyotolewa
kwa ukamilifu, hata hivyo kwa kuwa tayari baadhi ya vyombo vya habari vimetaka kauli
ya awali naomba kueleza machache:
Kuibuka huku kwa CCM na kufanya propaganda chafu ni ishara ya kwamba CCM inaumizwa
na namna ambavyo watanzania wanajitokeza kuunga mkono CHADEMA kwa hali na mali hivyo
CCM sasa inatapatapa  kujaribu kudhibiti wimbi la mabadiliko kwa kutumia siasa
chafu. Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete anapaswa kueleza watanzania iwapo
mikakati hiyo michafu ina baraka zake na za serikali anayoiongoza kwa kurejea pia
madai yaliyotolewa na Waziri wa Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Steven Wassira
kuwa CHADEMA itasambaratishwa katika kipindi cha mwaka mmoja kwa mbinu mbalimbali.
CCM kwa kuwa imekuwa  na kawaida ya kufanya usanii kuhalalisha fedha haramu kama
ilivyofanya kwenye chaguzi zilizopita baada ya viongozi waandamizi wa CCM na makada
wake kuchota fedha za chafu kifisadi kama zile za kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya
Nje (EPA) na vyanzo vingine vichafu na kuzisafisha kupitia harambee za hadaa
zilizofanywa na CCM kwa nyakati mbalimbali; inataka kuichafua CHADEMA inayopata
fedha kutoka vyanzo halali kwa njia za wazi ili kukatisha tamaa umma wa watanzania
unaochangia vuguvugu la mabadiliko.
Viongozi wa CCM wameamua kujidanganya, kuidanganya Serikali yao na kujaribu
kuwapotosha watanzania lakini CHADEMA inatambua kwamba watu wachache wanaweza
kudanganyika kwa muda mchache lakini si watu wote wakati wote; na kwamba watanzania
wa leo kwa uwingi wao hawawezi kudanganyika na uzushi wa kijinga wa CCM.
Ni ukweli ulio wazi kwamba CHADEMA imekuwa ikifanya harambee kwa uwazi kwa nyakati
mbalimbali katika kumbi na katika mikutano ya hadhara ikiwemo ya vijijini ambapo
michango hutolewa kwa uwazi, aidha michango kwa njia ya simu inaweza kufuatiliwa na
kuthibitisha bila shaka yoyote kwamba watanzania wameamua kuchangia mabadiliko ya
kweli.
Madai ya CCM kuwa CHADEMA imepokea au itapokea mabilioni ya shilingi kutoka mataifa
ya nje ni ya uzushi na narudia kwa mara nyingine tena kuitaka CCM itaje majina ya
serikali, taasisi ama makampuni ya nje ambayo CCM inadai kwamba CHADEMA imepokea
mabilioni ya shilingi katika siku za karibuni au inatarajia kupokea.
Badala ya CCM kuisingizia CHADEMA ilipaswa CCM ieleze watanzania orodha ya vigogo wa
Serikali inayoongozwa na wanachama waandamizi wa CCM ambao wanaelezwa kuwa na
akaunti nchini Uswisi na nchi zingine wakituhumiwa kupewa fedha za kifisadi kutoka
kwa makampuni ya utafutaji wa mafuta, gesi asili pamoja na uchimbaji wa madini.
CCM ilipaswa ieleze watanzania sababu za kuendelea kusuasua kujivua magamba ya
ufisadi kinyume na maazimio ya CCM yaliyofikiwa baada ya msukumo wa CHADEMA kutaja
orodha ya mafisadi kwa kuwa kati ya mafisadi hao ni pamoja na viongozi wa CCM
walioiingiza nchi katika mikataba mibovu.
Ikumbukwe kwamba madai haya si mapya kutolewa na CCM, yaliwahi kutolewa na
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Sophia Simba mara baada ya uchaguzi
mkuu wa 2010 akidai kuwa CHADEMA imepokea fedha kutoka mataifa ya ulaya kwa ajili ya
kufanya maandamano ya kuiondoa CCM madarakani.
Itakumbukwa kwamba wakati huo nilimtaka ataje nchi hizo na kueleza kusudio la
kumchukulia hatua zaidi na kwa upande mwingine niliyataka mataifa hayo ya Ulaya
yatoe kauli kuhusu madai hayo. Izingatiwe kwamba mataifa hayo yalikanusha madai hayo
ya CCM na Sophia Simba hakuna madai hayo dhidi ya CHADEMA.
Nimeelezwa kuwa CCM imetoa madai mengine ya uzushi kuwa CHADEMA inapewa mabilioni
toka nje kwa kuwa nchi imegundua rasilimali za mafuta na gesi na kudai kuwa fedha
hizo ni kwa ajili ya kuiweka nchi rehani.
Madai haya yaliwahi kutolewa pia kwa Katibu wa CCM wa Fedha na Uchumi Mwigulu
Nchemba na nikamtaka Waziri wa Mambo ya Nje Benard Membe kutaja nchi hizo na
mikataba hiyo hata hivyo mpaka sasa hakuna kiongozi yoyote wa CCM na Serikali
aliyejitokeza kutaja CHADEMA imepokea au itapokea mabilioni kutoka nchi gani na kwa
mikataba gani.
CCM inatoa madai hayo kuhamisha mjadala baada ya CHADEMA wa uongozi bora, sera
makini, mikakati sahihi na oganizesheni thabiti kuwa mstari wa mbele katika kutetea
rasilimali za taifa na watanzania kutambua kwamba taifa letu litaepushwa kutumbukia
kwenye laana ya rasilimali kwa kuiondoa CCM madarakani katika chaguzi za mwaka 2014
na 2015 na kuichagua CHADEMA.
CCM na Serikali yake ndiyo imekuwa kinara wa kupokea fedha kutoka nje kwa kisingizio
cha misaada na kuingia mikataba mibovu na mataifa ya nje pamoja na makampuni ya
kigeni na kuachia mianya ya uporoji wa rasilimali za nchi na CHADEMA imeanika hali
hii kwenye orodha ya mafisadi kwa kutaja majina ya viongozi waliohusika kwenye
mikataba ya madini na tutaendelea kufanya hivyo hata katika masuala ya mafuta na
gesi ambayo tayari vigogo wa Serikali inayoongozwa na CCM wameshaanza kuingia
mikataba mibovu na kuingiziwa fedha katika akaunti zao za nje ya nchi.
Hivyo, badala ya CCM kutoa madai ya uzushi kuhusu CHADEMA kuingia mikataba na
serikali au makampuni ya nje, CCM ieleze watanzania imechukua hatua gani mpaka sasa
juu ya viongozi na wanachama wake waliongia mikataba mibovu kwenye rasilimali muhimu
nchini ikiwemo madini, mafuta, gesi na maliasili zingine za taifa letu na kutoa
mikataba hiyo hadharani ili watanzania waweze kuchukua hatua za kufanya mabadiliko
ya kweli.
Hivi karibuni Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM alisema kwamba serikali
inayoongozwa na CCM haitarudia makosa ya kuachia mianya ya ufisadi kwenye gesi;
hivyo CCM ilipaswa wakati huu kuwaomba radhi watanzania kwa ufisadi uliofanyika
kwenye madini na rasilimali nyingine na kuishukuru CHADEMA kwa kuendelea
kuwaunganisha watanzania wakati wote kusimamia mabadiliko ya kweli.
CCM badala ya kutishia kuwa ina mikataba inayoihusu CHADEMA ingetoa mikataba hiyo na
hali hii ya CCM inayoongoza Serikali kudai CHADEMA kufanya mikakati, mipango na
shughuli iliyo kinyume cha sheria bila vyombo vya dola kuchukua hatua ni ishara ya
CCM kukiri wazi kuwa chama legelege chenye serikali legelege kimeshindwa kuongoza
nchi na badala yake kimejikita katika propaganda chafu.
CHADEMA tangu kuanzishwa kwake imekuwa na mikataba ya makubaliano ya ushirikiano
(MOU) na vyama rafiki vya ndani ya Afrika na duniani na makubaliano hayo yamekuwa
yakifikiwa kwa uwazi ikiwa ni sehemu ya CHADEMA kuwa na mtandao wa kitaifa na
kimataifa na hayajawahi kuhusisha wala hayatawahi kuhusisha CHADEMA kusaidiwa
mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kufanya kazi zake kama inavyodaiwa na CCM.
CHADEMA kimekuwa chama kiongozi kwa nyakati mbalimbali kueleza viwango cha matumizi
yake ya fedha na vyanzo vya fedha husika huku kikitegemea kwa kiwango kikubwa
michango ya wanachama na wapenzi wa chama hapa nchini pamoja na kutumia kwa ufanisi
ruzuku inayotolewa kwa vyama vya siasa.
CCM imekuwa na kawaida ya kutoa madai ya uzushi wakati mwingine yakiambatana na
kutoa nyaraka za kughushi inazodai kuwa ni za CHADEMA. Ikumbukwe kwamba wakati wa
uchaguzi wa mdogo wa Igunga, CCM ilitoa madai ya uzushi kuwa CHADEMA inafadhiliwa na
nchi za nje ikiwemo kupewa mafunzo ya ugaidi na kudai kuwa tayari magaidi
wameingizwa na CHADEMA toka nje katika uchaguzi huo; hata hivyo katika mwenendo wa
kesi ya uchaguzi ya Igunga Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama aliyetoa madai hayo
alitoa ushahidi mahakamani kwamba CHADEMA haijawahi kuleta magaidi bali kauli hizo
za CCM zilikuwa ni za siasa za uchaguzi.
Hivi karibuni, CCM imeghushi waraka mwingine na kuusambaza kile ilichodai kuwa ni
maazimio ya  kamati kuu ya CHADEMA ya kupanga migomo ya walimu, madaktari na mipango
mingine ya kuhujumu serikali; hata hivyo waraka huo ulidhihirika wazi kuwa ni wa
kughushi.
Mikakati yote hiyo michafu hupangwa na CCM mara kwa mara wakati ambapo CHADEMA
inaanza operesheni Sangara na mikakati mingine ya kuleta mabadiliko nchini na
kujipanga kuiondoa CCM madarakani kama ilivyo sasa ambapo CHADEMA inaendelea na
operesheni katika mkoa wa Morogoro hivyo watanzania wanapaswa kuipuuza CCM na
kuendelea kujiunga CHADEMA na kuchangia mabadiliko kwa hali na mali mpaka kieleweke.


John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
12/08/2012

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,288,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7077,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,739,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,10,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: KAULI YA AWALI KUHUSU TAMKO LA CCM DHIDI YA CHADEMA
KAULI YA AWALI KUHUSU TAMKO LA CCM DHIDI YA CHADEMA
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2012/08/kauli-ya-awali-kuhusu-tamko-la-ccm.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2012/08/kauli-ya-awali-kuhusu-tamko-la-ccm.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy