TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Septemba 26, 2012 KAMATI YA UCHAGUZI TFF YATUPA RUFANI YA WARUFANI IRFA Kamati ya Uchaguzi ya Shir...
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Septemba 26, 2012
KAMATI YA UCHAGUZI TFF YATUPA RUFANI YA WARUFANI IRFA
Kamati ya Uchaguzi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana
(Septemba 25 mwaka huu)
kusikiliza rufani iliyowasilishwa mbele yake na warufani
Mussa H. Mahundi, Abou O.
Sillia na Alex Mgongolwa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya
Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Iringa (IRFA) iliyoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kubatilisha matokeo ya
uchaguzi wa IRFA uliofanyika Septemba 8 mwaka huu Mufindi,
Iringa, na kuomba
uchaguzi huo ufanyike upya kwa kuendeshwa na kusimamiwa na Kamati
ya Uchaguzi ya TFF.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deogratias Lyatto, baada ya
kupitia maelezo ya
warufani na warufaniwa, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imejiridhisha
kuwa rufani
iliyowasilishwa mbele yake na Mahundi, Sillia na Mgongolwa ilikosa sifa
ya kuwa rufani kwa mujibu
wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, Ibara ya 8(2),
Ibara ya 21(3) na 24(2).
Kwa kutozingatia matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama
wa TFF, Kamati ya
Uchaguzi ya TFF imetupa rufani hiyo.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF
imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya IRFA kuchukua hatua dhidi
ya Abuu Changawa kama
ilivyoainishwa kwenye Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF,
Ibara ya 28(6) kwa
kuingilia mchakato wa uchaguzi wa IRFA siku ya uchaguzi.
SHUKRANI KWA WADAU SERENGETI BOYS
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) linawashukuru wadau waliofanikisha kwa
njia mbalimbali ziara ya
timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17
(Serengeti Boys)
iliyofanyika hivi karibuni katika mikoa ya Mbeya na Njombe.
Wadau hao ni Chama cha
Mpira wa Miguu Mbeya Mjini (MUFA) chini ya Mwenyekiti wake
Suleiman Haroub, Kaimu
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Njombe
(NJOREFA), Stanley
Lugenge, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) na Chama
cha Mpira wa Miguu Wilaya
ya Njombe (NDFA).
Wengine ni Chama cha
Mpira wa Miguu Wilaya ya Makambako (MDFA), Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Morogoro
(MRFA), na klabu za Mbozi United, Kyela United, Tanzania
Prisons na Mbeya City.
Serengeti Boys inaendelea
na kambi yake jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya
kwanza ya mchujo ya
michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 dhidi
ya Misri itakayochezwa
Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
KAMSHINA MMOJA AONDOLEWA KWENYE LIGI
Kamati ya Ligi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana
(Septemba 25 mwaka huu)
kupitia ripoti za mechi 21 za Ligi Kuu ya Vodacom ambazo
zimeshachezwa mpaka sasa,
na kuzifanyia uamuzi wa kikanuni ikiwemo kumuondoa
Kamishna mmoja.
George Komba
aliyekuwa Kamishna kwenye mechi namba 20 kati ya Simba na Ruvu Shooting
ameondolewa kwenye orodha
ya makamishna wa ligi kutokana na upungufu uliojitokeza
katika ripoti yake.
Klabu ambazo zimeandikwa
barua za onyo ni African Lyon kwa kwenda uwanjani na jezi
tofauti na zile
ilizoonesha kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (pre match
meeting), Mtibwa Sugar
kwa kuchelewa kuwasilisha leseni za wachezaji wake wakati wa
mechi na Ruvu Shooting
kwa ushangiliaji uliopita kiasi kwenye mechi yao dhidi ya
Simba.
Kamati pia imethibitisha
kadi nyekundu ya Emmanuel Okwi kwa kumpiga kiwiko Kessy
Mapande wa JKT Ruvu,
hivyo kwa mujibu wa Kanuni ya 25(1)() anakosa mechi tatu na
kulipa faini ya sh.
500,000. Mchezaji huyo atakosa mechi namba 20, 27 na 80.
Kwa upande wa waamuzi,
Ronald Swai ameandikiwa barua ya onyo kutokana na upungufu
alioonesha kwenye mechi
kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Wamiliki wa viwanja vya
Mkwakwani, Tanga na Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya
wameandikiwa barua ya
kuvifanyia marekebisho viwanja vyao katika maeneo mbalimbali
yenye upungufu ikiwemo
uzio wa kutenganisha wachezaji na washabiki.
Mchezaji Faustin Lukoo wa
Polisi Moro ambaye kwa mujibu wa ripoti ya mwamuzi
aliyemtoa nje kwa kadi
nyekundu alimtukana mchezaji mwenzake kwenye mechi dhidi ya
African Lyon na Katibu wa
Oljoro JKT aliyemwaga maji kwenye chumba cha timu ya
Polisi Moro, masuala yao
ni ya kinidhamu, hivyo yamepelekwa Kamati ya Nidhamu na
Usuluhishi kwa ajili ya
hatua zaidi.
Kwa klabu ambazo timu zao
mpaka sasa zinacheza mechi bila kuwa na logo ya mdhamini,
suala hilo limepelekwa
kwa wadhamini Vodacom kwa vile wenyewe ndiyo wanaogawa vifaa
hivyo.
TENGA KUKUTANA NA WAANDISHI KESHO SAA 6
Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga atakutana na
waandishi wa habari kesho
(Septemba 27 mwaka huu) saa 6 kamili mchana. Mkutano huo
utafanyika kwenye ukumbi
wa mikutano wa TFF.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)
COMMENTS