WATU milioni 15.4 waishio vijijini watapata huduma ya maji kufuatia utekelezaji wa mpango maalumu wa kuleta matokeo ya haraka ukataohitaji...
WATU milioni 15.4 waishio vijijini watapata huduma ya maji kufuatia
utekelezaji wa mpango maalumu wa kuleta matokeo ya haraka ukataohitaji kiasi
cha shilingi trilioni 1.45.
Mpango huo wa miaka mitatu unaosema tekeleza
sasa kwa matokeo makubwa utaanza mwaka huu hadi mwaka 2016.
Hayo yamo katika bajeti ya wizara ya mji iliyomwa Bungeni Jumatano na Waziri wake Prof Jumanne Maghembe.bajeti hipo gereji ikifanyiwa marekebisho.
Prof Maghembe ambaye alikuwa anaelezea hali halisi ya raslimali , mgawanyo na namna serikali inavyojitahidi kufikisha maji salama kwa watu wengi zaidi vijijini, alisema kwamba program hiyo imejikita zaidi vijijini kutokana na ukweli kuwa watu wengi wanaishi huko.
Kwa utekelezaji huo serikali inatarajia kuongeza idadi ya wananchi wanaopata huduma hiyo maji nchini asilimia 57 za sasa hadi asilimia 75 ifikapo mwaka 2015.
Waziri Maghembe alisema katika program hiyo maalumu yenye lengo la kukabiliana na uchakavu na usimamizi duni wa miradi imelenga kuongeza idadi ya vituo vya kuchota maji na kupanua miundombinu iliyopo, kukarabati na kujenga miradi mipya.
Alisema katika hotuba hiyo kuwa jumla ya miradi 1,810 inatarajiwa kutekelezwa.
Aidha amesema program hiyo itaboresha usimamiziwa miradi ya maji ngazi za jamii kwa kuunda na kuimarisha vyombo vya watumia maji na kuweka mazingira mazuriwa matengenezo ya miradi ya maji.
Kauli hiyo ambayo imo katika tarifa ya kamati iliyosomwa na Makamu mwenyekiti wa kamati Said Nkumba imetaka ziada hiyo ili kuendeleza program ya kupeleka maji vijiji kumi, kw akuongeza viwili au vitatu katika kila halmashauri, kujenga miundombinu ya kuwasambazia maji wananchi kutoka katika mabwawa yaliyojengwa katika wilaya kame.
Aidha fedha hizo pia zilitarajiwa kuchimba visima virefu vya maji, kujenga na kukarabati miundombinu chakavu na kusanifu mradi wa Ugala, Urambo na kaliua mkoa wa Tabora.
Waziri wa Maji akizungumzia miradi ambayo serikali inaifanyia kazi kupunguza adha alizungumzia mradi wa maji katika miji kadhaa ikiwamo Tabora,Dodoma,Singida mjini, Morogoro mjini,Mbeya, Manispaa ya Iringa na Mradi wa maji Songea mjini.
Aidha alizungumzia miradi ya maji katika miji mikuu ya mikoa mipya ya Mpanda, njombe na bariadi. Katika miji hiyo kutajengwa matangi ya maji, kuchimba visima na ulazaji wa mabomba.
Akizungumzia miradi ya kitaifa waziri Maghembe alisema serikali kwa kushirikiana na benki ya kiarabu ya maendeleo ya afrika Badea na mfuko wa maendeleo wa Saudiaitatekeleza mradi wa maji safi wa Mugango/Kiabakari/Butiama. Mradi huo utagharimu dola za Marekani milioni 30.69 na kunufaisha watu elfu 80.
Imeelezwa kuwa usanifu wa mradi huo utaanza Agosti mwaka huu na kuanza kujengwa Machi mwakani.
Wakati huo huo kambi rasmi ya upinzani imeitaka serikali kuongeza bajeti ya wizara ya maji na kukabiliana na ufisadi mkubwa na wa kutisha katika miradi mbalimbali ya maji hapa nchini.
Msemaji mkuu wa kambi ya upinzani wizara ya maji na umwagiliaji Cecilia Paresso alisema mabomba ya m china yamekuwa bila maji .
Prof Maghembe aliomba bunge liidhinishe jumla ya shilingi 398,395,874,000 kwa ajili ya matumizi ya wizara ambapo kati ya fedha hizo matumizi ya kawaida ni sh 18,952,654,000 ambapo sh 13,319,877,000 mishahara ya watumishi na sh 5,632,777,000 ni fedha za matumizi mengine.
Jumla ya bajeti ya maendeleo ni sh 379,443,220,000 ambapo kati ya hizo sh 138,266,164,000 ni fedha za ndani na241,177,056,000 ni fedha za nje.

COMMENTS