USANIFU wa bwawa la Kidunda ambalo litakuwa mhimili wa kuhakikisha kwamba maji katika mto Ruvu yanakuwapo kipindi chote cha mwaka na kuzalis...
USANIFU wa bwawa la Kidunda ambalo litakuwa mhimili wa
kuhakikisha kwamba maji katika mto Ruvu yanakuwapo kipindi chote cha mwaka na
kuzalisha umeme wa megawati 20 umekamilika na vitabu vya zabuni vipo tayari kwa
ajili ya matangazo ya kumpata mkandarasi.
Aidha imeelezwa kuwa mkandarasi wa uchimbaji wa visima virefu vya Kimbiji na Mpera amepatikana na kazi ya kuchimba visima 20 katika maeneo hayo itaanza Julai mwaka huu.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakati akiwasilisha hotuba yake ya bajeti kwa mwaka 2013/2014 jana.
Alisema miradi hiyo ni sehemu ya mpango wa dharura kwa ajili ya Dar e s salaam wa kuboresha huduma ya maji katika jiji la dare s salaam na miji ya Kibaha na Bagamoyo.
Mpango huo umelenga kuongeza wingi wa maji kutoka lita milioni 300 za sasa hadi lita milioni 756 kwa siku, kuboresha usambazaji maji, kupunguza upotevu wa maji yasiyolipiwa, kubiresha utendaji wa Dawasa na Dawasco kuongeza maduhuli na kuongez auwezo wa uondoshaji maji taka kutoka asilimia 10 za sasa hadi asilimia 30.
Kuhusu mradi wa Kidunda ambapo shughuli za uzalishaji umeme utatekelezwa na Tanesco chini ya makubaliano yaliyosainiwa kati ya Dawasa na Tanesco Novemba 2012, Waziri amesema kwamba wananchi watakaohamishwa ili kupisha ujenzi wa bwawa hilo wataanza kulipwa Mei mwaka huu.
Ujenzi wa bwawa hilo utaanza mara baada ya wananchi kumaliza kulipwa fidia.
Akizungumzia kimbiji na Mpera Waziri maghembe ambaye alisema kwamba uthamini wa maeneo yote ya mradi yenye ekari 7,300 umefikia shilingi bilioni 27, serikali inakisia kupata maji lita milioni 260 kwa siku ifikapo mwaka 2014.
Waziri pia alizungumzia upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu,upanuzi wa mradi wa maji wa ruvu Chini na ukarabati na upanuzi wa mfumo wa kusambaza majisafi.
Aidha kwenye miradi mingine ya kuboresha huduma ya maji kwa ushirikiano na shirika la maendeleo la Ubelgiji na Umoja wa Nchi za Ulaya umefikia asilimia 60. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Juni mwaka huu.
Mradi huo unaendeshwa katika maeneo tofauti ya maeneo tofauti ya Temeke,Ilala na Kinondoni.
NOTA BENE
-Uharibifu wa mazingira chanzo cha mto Ruvu haukuangaliwa kabisa. Hiki nakiita kituko kwa kuwa kama hakuna udhibiti katika chanzo cha mto Ruvu unatarajia kuwa na maji kweli.
-Chanzo cha mto ruvu watu wanavuna madini na wanayachenjua kwa kutumia zebaki hili nalo inaonekana wataalamu hawalijui.
-je tunahitaji mradi maalumu wa kuja kurekebisha chanzo cha mto Ruvu?
aksanteni sana

COMMENTS