Serikali ya Mapinduzi ya imetangaza bajeti ya fedha kwa mwaka 2013-2014 huku ikiweka kipaumbele dira ya maendeleo ya 2020 pamoja na m...
Serikali ya Mapinduzi ya imetangaza bajeti ya fedha kwa mwaka 2013-2014 huku ikiweka
kipaumbele dira ya maendeleo ya 2020 pamoja na mpango wa
kuimarisha uchumi na
kupunguza umasikini MKUZA
kama ndiyo kipaumbele cha kuleta maendeleo.
Akiwasilisha bajeti ya
Serikali kwa mwaka 2013-2014 hapo katika Baraza la
Wawakilishi,Waziri wa
Nchi Ofisi ya rais anayeshughukilia Fedha Uchumi na Mipango ya
Maendeleo Omar Yussuf
Mzee alisema hali ya uchumi ya Zanzibar imezidi kuimarika na
kufikiya asilimia 7.5
kutoka 6.7 katika mwaka 2012.
Alisema kwa mwaka wa
fedha 2012-2013 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatarajia
kutekeleza miradi minne
katika sekta ya maji safi na salama,afya pamoja na ajira na
elimu.
Mzee alisema katika
utekelezaji wa miradi hiyo Serikali imetenga jumla ya sh.Bilioni
113.2,huku akiitaja sekta
ya Afya imetengewa sh.Bilioni 23.9,sekta ya Maji safi na
salama imetengewa
sh.Bilioni 55.4 pamoja na ajira kwa vijana zimetengwa jumla ya
sh.1.1.
--uchumi wapanda kwa asilimia 7.5
---mishahara yatengewa bilioni 17.5 nyongeza.
--kodi uwanja wa ndege na hoteli kupanda.
---misamaha sasa kudhibitiwa.
---mfumuko wa bei sasa washuka
Alisema kwa mwaka wa
fedha 2013-2014 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatarajiwa
kutumia jumla ya
sh.Bilioni 658.5 ikilinganishwa na bajeti iliyopita ya mwaka
2012-2013 ya jumla ya
sh.648.9.
Akifafanua alisema bajeti
hiyo asilimia 50 inategemea makusanyo ya vyanzo vya mapato
vya ndani vinavyokusanywa
na taasisi za kukusanya mapato nchini Bodi ya mapato na
Mamlaka ya kodi nchini
TRA.
Alisema katika mwaka
2013-2014 ukusanyaji wa mapato ya Serikali yanatazamiwa
kufikiya asilimia 21.3 na
kufikiya sh.Bilioni 324.6.huku ZRB ikiwekewa malengo
kukusanya sh.171.7 na TRA
kukusanya jumla ya sh.Bilioni 147.9.
Mzee alisema Serikali
inatazamiwa kukusanya mapato katika vyanzo vyake vya ndani
jumla sh.bilioni 333.7.
Alisema katika mikakati
ya kuhakikisha Serikali inakusanya mapato yake
vizuri,Serikali
itadhibiti misamaha ya kodi ambayo ilikuwa ikilikosesha taifa zaidi
ya sh.Bilioni 12.6
Mzee alisema unafuu wa
misamaha kwa asilimia 100 utatolewa kwa ofisi za kibalozi na
miradi inayotokana na
wafadhili wa washiriki wa miradi ya maendeleo.
Alisema taasisi nyengine
unafuu utatolewa kwa asilimia 80 na asilimia 20 iliyobaki
ndiyo itakayolipiwa
kodi.ambapo alisema hatua hiyo itaongeza mapato kwa sh.Bilioni
4.56.
Mapema Mzee alisema
serikali inakusudia kuzifanyia marekebisho viwango vya kodi kwa
ajili ya kuongeza mapato
na kuacha utegemezi kutoka kwa wafadhili na washiriki wa
maendeleo.
Alizitaja kodi
zitakazofanyiwa marekebisho na kupanda ikiwemo ada ya bandari kwa
wasafiri wa baharini na
uwanja wa ndege pamoja na ushuru wa stempu na kodi za leseni
ya udereva.
Alisema ada ya viwanja
vya ndege itapanda ili kufikiya viwango vya nchi za Afrika ya
mashariki dola za
kiimarekani 35 na kufikiya 40kwa mtu na hivyo kusaidia mapato na
kufikiya sh.Bilioni 1.2
Aidha kodi za mahoteli
zinatazamiwa kufanyiwa marekebisho ili kudhibiti ukwepaji wa
kodi unaofanywa na
wamiliki wa mahoteli wasiokuwa waaminifu wakati wanapofanyiwa
ukaguzi.
Aidha Mzee Serikali
inakusudia kudhibiti na kupambana na magendo ya mafuta nchini
ambapo mashirikiano
yamefikiwa kati ya TRA pamoja na ZRB na Mamlaka ya mapato ya
Kenya.
Mapema Mzee aliwataka
wananchi kujtokeza kwa wingi kutoa maoni yao katika mchakato
wa marekebisho ya katiba
kwa njia ya amani na kuepuka fujo.
Alisisitiza na kusema
kwamba Muungano wa Tanganyika ulioasisiwa na viongozi wawili
hayati Abeid Amani Karume
na Mwalimu Nyerere ndiyo kielelezo cha taifa la Tanzania.
'Nawaomba wananchi wa
Zanzibar kutoa maoni katika mchakato wa katiba ya Tanzania kwa
njia ya amani na
utulivu....Muungano wetu ndiyo kielelezo cha taifa hili huku
umuhimu wake ukionekana
kwa kila pande'alisema.
Alisema uchumi wa
Zanzibar itaendelea kuimarika kama wananchi watatunza na kulinda
amani na utulivu katika
sekta muhimu ikiwemo ya utalii.
Akizungumzia kuhusu maslahi ya wafanyakazi,Mzee alisema ahadi ya
rais wa Zanzibar
katika kuimarisha maslahi
ya wafanyakazi wote bado ipo pale pale.
Alisema katika
bajeti ya mwaka wa fedha 2013-2014
Serikali imetenga jumla ya
sh.Bilioni 17.5 kwa ajili
ya maslahi ya wafanyakazi ikiwemo nyongeza ya mishahara.
'Katika bajeti hii
tumetekeleza ahadi ya rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la
Mapinduzi dk.Ali Mohamed
Shein katika kuimarisha maslahi ya wafanyakazi wote
nchini'alisema.
Aidha Mzee aliitaja
bajeti ya mwaka wa fedha 2013-2014 kuwa ni bajeti nafuu kwa
wananchi baada ya
serikali kufamnikiwa kukamilisha miradi mbali mbali ikiwemo wa
nishati ya umeme kutoka
Ras kilomoni Tanzania Bara hadi Fumba na ule wa Pemba hadi
Tanga.
Alisema kukamilika kwa
miradi hiyo kumeleta unafuu mkubwa kwa wananchi ikiwemo
kutumia nishati ya umeme
kwa maendeleo ya taifa.
Khatib Suleiman,habarileo
Zanzibar
COMMENTS