MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ameahidi kuchangia Sh Milioni 3 na pikipiki (bodaboda) kumi kwa chama...
MBUNGE
wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ameahidi kuchangia
Sh Milioni 3 na pikipiki (bodaboda) kumi kwa chama kipya cha bodaboda
kinachotarajia kuanzishwa kwa uratibu wa ofisi yake wakati wowote kuanzia sasa.
Azma
hiyo ikitimia manispaa ya Iringa itakuwa na vyama viwili tofauti vya madereva
hao vinavyoelezwa na baadhi ya wadau kwamba vitatofautiana kwa mitizamo yao
itikadi zao za kisiasa.
Chama
pekee kinachotambulika hivisasa ni kile Chama cha Bodaboda na Bajaj Iringa
kinachoelezwa kuwa na wanachama wengi ambao pia ni wanachama na wakereketwa wa
Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kinachotarajiwa
kuanzishwa kwa uratibu wa ofisi ya mbunge huyo kinatarajiwa kuwa na wanachama
wenye itikadi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mgawanyiko
wa madereva hao ulidhihirika juzi baada ya Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini
kufanya mkutano na baadhi ya madereva hao katika ukumbi wa Jumba la Maendeleo,
huku Mwenyekiti wa Chama cha Bodaboda na Bajaj Iringa, Mwambope Joseph naye
akifanya kikao na madereva wengine katika uwanja wa Mbwetogwa, mjini hapa.
Katika
mkutano wa Mwembetogwa, Joseph alimtuhumu Mchungaji Msigwa akisema anataka
kudhohofisha maslai ya madereva hao kwa kuwagawa kisiasa.
“Mchungaji
alinipigia simu Agosti 18 akinieleza kwamba anataka mkutano na madereva wa
bodaboda na tukakubalina kabla ya mkutano huo uliokuwa ufanyike kesho jumanne,
kulikuwa na haja akakutana na viongozi kwanza,” alisema.
Alisema
katika mazungumzo yao Mchungaji Msigwa aliahidi kuchangia Sh Milioni 10 kama
mchango wake katika harakati za bodaboda hao za kujileleta maendeleo yao.
Badala
ya kukutana na viongozi, Joseph alisema Mchungaji Msigwa aliitisha kinyemela
mkutano na madereva wa bodaboda na bajaj akiwa na ajenda ya kuwagawa.
Baada
ya kumaliza mkutano wao , Joseph na wanachama wake walikwenda kuhudhuria wa
Mchungaji Msigwa na katika mazingira yaliyodhihiri mgawanyiko wao yeye pamoja
na baadhi ya wanachama wake walizuiwa kuingia.
Wakimuomba
Mchungaji Msigwa awasaidie kuanzisha chama kipya, madereva waliohudhuria
mkutano wake walisema hawataki kuendelea na chama hicho kwa madai kwamba kina
muelekeo wa chama fulani cha siasa, taarifa zake za mapato na matumizi ni ngumu
kuzipata, viongozi wake ni wababe na hakifanyi mikutano kwa mujibu wa katiba.
Katika
utetezi wake, Joseph alisema tuhuma dhidi ya chama na uongozi wake sio za kweli
bali zinakuzwa ili kujenga chuki dhidi yake.
Mwambope
alisema chama hicho kilianzishwa kikiwa na wanachama 38 waliongia kwa ada ya
Sh3,000 kila mmoja, Agosti 31, mwaka jana..
Alisema
kwa mujibu wa katiba yao, mkutano mkuu wa chama hicho unakutana mara moja kila
mwaka na kwamba Agosti 31, mwaka huu watakutana kwa lengo la kutoa taarifa
mbalimbali za chama zikiwemo za mapato na matumizi.
Hata
hivyo Joseph alisema pamoja na kwamba manispaa ya Iringa ina madereva zaidi ya
1000 na wengi wao wakiwa wamesomeshwa udereva na mlezi wao, Salim Asas, chama
hicho kina wanachama 171 tu.
“Hao
ndio wenye haki na chama hiki, hao ndio wanaostahili kupata taarifa zote za
chama chao. Madereva wengine tunashirikiana nao kama ndugu na wadau tuliopo
katika sekta moja ya usafirishaji,” alisema.
Alisema
wengi wa madereva waliokutana katika mkutano wa Mchungaji Msigwa sio wanachama
wa chama hicho, hawajui katiba ya chama hicho na ndio maana wanatoa lawama
wasizozijua.
Akiitikia
ombi la madereva hao Mchungaji Msigwa alisema; “niko tayari kusaidia uanzishaji
wa chama kipya lakini ni lazima kiwe na viongozi waadilifu watakaokuwa
wanaitisha vikao na kutoa taarifa zote za chama zikiwemo za mapato na
matumizi.”
Alisema
hawasaidii madereva hao kwa lengo la kujinufaisha kisiasa, anafanya hivyo
kwasababu anafahamu kero zinazowasumbua madereva hao.
“Msikubali
mtumike, wala mimi msikubali niwatumie. Nitasaidia uanzishaji wa chama kipya
lakini niwahakikishie sitawaweka mfukoni. Na tukifanikiwa kuanzisha kingine,
msitoke na kwenda kuwafanyia fujo wenzenu. Vyama hivi ni vya hiari, kama
hukubaliani na taratibu zake jitoe na kajiunge na kingine,” alisema.
Alisema
atakipa chama hicho kipya sh Milioni 3 na bodaboda kumi sio kwa lengo la
kujihakikishia kura kwa vijana hao katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani bali
kwasababu anaguswa na matatizo yao.
“Mambo
ya Uchaguzi Mkuu wa mwakani maamuzi yako mikononi mwenu, nasema ya mwakani
mtajua wenyewe kama mnipe au msinipe, mimi nimewaita kutekeleza majukumu yangu
ya kibunge,” alisema.
Pamoja
na kuasaidia uanzishwaji wa chama hicho, Mchungaji Msigwa aliwataka madereva
hao kuzingatia taratibu za biashara yao ya usafirishaji.
“Zingatieni
kanuni, za usafirishaji, mimi kama mbunge ni lazima niwe fair, bodaboda, taxi,
daladala na maroli ni lazima wote wapate nafasi sawa kwa mujibu wa taratibu za
kufanya biashara yao, maana sisi wote ni watanzania, tukisema kazi hii iwe ya
bodaboda pekee yao mimi nitakuwa kiongozi mbaya,” alisema.
COMMENTS