HA ha ha Shemeji, mbona utateseka. Angalia usijiapize unaweza kufa lazima nije na kuna siku nitakuja bila kualikwa, na ukiona nimef...
HA
ha ha Shemeji, mbona utateseka. Angalia usijiapize unaweza kufa lazima nije na
kuna siku nitakuja bila kualikwa, na ukiona nimefika na mkeo hayupo jua nini
nitakachofuata, itakuwa kama leo. Kwaheri. Hayo ndiyo maneno ambayo alisema
Kibua wakati akijilamba kwa utamu aliouonja wa shemeji yake kwa Semie, Je nini
kinaendelea?...
Semei
akiwa amechukia kabisa na huku uso umemuiva kwa kushindwa kujua amfanye nini
Kibua, huku akijenga taswira ya hasara katika uchumba wake kwani alitambua
kwamba mara zote Kibua hutekeleza tishio lake, alianza taratibu kushuka milima
kwa njia ile ile aliyokuwa ameijia.
Kibua
kwa upande wake alimtazama kwa nyodo jinsi alivyokuwa akishuka akifurahi jinsi
alivyomuweza. Alitabasamu.
Kibua
kwa namna fulani alikuwa binti ambaye anapenda kuudhi watu hasa wale ambao
wamemfanyia visa vinavyomnyima raha na kwa Semei alikuwa amekamilisha
alichotaka, lakini kumuumiza zaidi ni alitaka lazima amfumanie na mchumba wake
katika kitanda chake, kukomesha ngebe zake.
Alimfuatilia
mpaka alipoingia Dawilo, akiwa mdogo katika macho, aligeuka na kuelekea katika
chumba chake. Alikitazama chumba kile kisha akaamua kuanza kupanga nguo zake
katika sanduku lake la mbao kwani alijua ima faima safari ya kwenda mjini
ilikuwa imeiva.
Hakujua
anatakiwa kufanyakazi ya aina gani, lakini alijua kitu kimoja tu kwamba mama
yake alikuwa anataka aondoke pale ili aweze kupata raha, manake, hakuwa na raha
kutokana na jinsi yeye alivyokuwa akiendesha maisha yake.
Alimfikiria
huyo mjomba wake ambaye mara zote hajui kama ni mjomba wake kweli au baba yake.
Alikuwa ni mtu ambaye akimwangalia hawezi kumtazama moja kwa moja hadi siku alipogombezwa na mama yake kwamba si
vyema kumwangalia mtu mzima kwa macho ya juu juu.
Alipomaliza
kukunja nguo na kuziweka katika sanduku alichukua maji akayainjika na baada ya
kuchochea kuni na kupata moto aliipua na kuingia nayo chooni , muda wa kujisafi
ulikuwa umefika hakutaka kulala na janaba la mtu.
Mwaka
ni 1975, Kibua alikuwa amebadilika kidogo na alikuwa ni mtu ambaye huwezi kumtambua. Alikuwa amekwenda juu
kidogo, lakini hakuwa mrefu ki hivyo. Alikuwa na umbile ambalo sasa imekuwa
taabu hata pale alipokuwa anasoma.
Ahh
nilisahau kukusimulia kwamba Kibua aliondoka nyumbani kwao siku ile ile
aliyogombana na Semei. Kulikuwa na gari
la kahawa lililotoka Kibuko ambalo lilipitia
karibu na kwao na kumsubiri Masarawe. Kama si mama yake asingeliondoka
pale kwani yeye kama walivyokuwa Waluguru wengine wa huko mlimani gari la
kahawa kwao lilikuwa ni mauaji, lilikuwa ni la mumiani.
Baada
ya kupata lifti ile hadi Morogoro alichukua gari la Bin Klebu mpaka Dar es
Salaam ambapo alisubiriwa na mjomba wake ambaye alikuwa amefanana naye sana.
Aliishi pale kwa muda kabla ya kupata kazi za ndani katika nyumba moja ya mfanyakazi wa Serikali iliyopo Kijitonyama.
Ni
katika nyumba hii ndipo alipopata nafasi ya kuanza kusoma, hakuwa na kichwa
kibaya, alikuwa na kichwa kizuri. Kisa cha kuanza kusoma hakikuwa kizuri sana
kama unavyofikiria kwamba eti alimpata msamaria na kumwingiza shule la hasha,
ilikuwa ni sehemu ya makubaliano kati ya baba mwenye nyumba na yeye.
***
"Hapa
sisi tunaishi wawili tu, mtoto wetu yupo
masomoni Chuo Kikuu Makerere na hatumtarajii kurejea hapa mpaka miaka miwili
ipite, lakini la maana ni kuwa nyumba hii inahitaji msaidizi," alisema
baba mwenye nyumba huku mkewe akiwa anaangalia.
Baada
ya kupewa maelezo hayo na kukabidhiwa chumba chake cha kulala nje ya jengo
hilo, sehemu ya kota za wafanyakazi, Kibua alianza kazi zake na hakuwa mvivu.
Kwanza
akiwa na mke wa mwenye nyumba alijifunza utamaduni wao hasa katika kula na
mambo yao mengine. Alikuwa na muda mfupi sana wa kujifunza hasa chakula
anachokipenda baba mwenye nyumba, chakula ambacho kilimpa dhiki kwelikweli
kukitengeneza. Mama mwenye nyumba alikuwa na muda mwingi wa kumwelekeza mpaka
akakijua kwani alikuwa likizo.
Muda
haukupita, Kibua alikuwa anajua kujibu simu, japo kwa Kiswahili, akajua ratiba
ya nyumba ile, akawa msaada mkubwa kwa mke wa mwenye nyumba, aliyekuwa na utu
uzima fulani hivi.
Baba
mwenye nyumba ambaye alikuwa na urefu wa futi sita na inchi mbili hivi
aliyejengeka katika umbile la uanariadha akiwa hana tumbo linalosababishwa na
ukosefu wa mazoezi, sura ya duara, maji ya kunde hakuwa bazazi vile lakini
baada ya miezi mitatu wakati akiwa nyumbani wiki moja bila mkewe kuna kichaa
kilimpata.
Aliondoka
pale na kwenda ofisini kwake na baada ya kumaliza kazi, alikwenda klabu Msasani na kujipatia kilevi. Baada ya muda
wakati akiwa katika bia yake ya Tusker ya
pili, akafika binti mmoja anayemfahamu.
"Ahh
Richard upo hapa."
"Si
unaniona"
"Toka
umeoa Richard ndio basi tena."
"Duhh!
unakumbuka sasa miaka 24 na mtoto anamaliza chuo kikuu, Mariana lazima uwe na
wazimu."
"Nina
wazimu kidogo nimekuona hapa, nimekumbuka kila kitu. Dahh mwanamke mwenzangu
lazima awe anajidai."
"Kwani
wewe ulikatazwa?"
"Ilikuwa
lazima nisome, na wewe ulikuwa unanichanganya ningebaki dakika zaidi ya mia
pale siku ya mwisho nilikuwa siendi kusoma."
"Mhh.
"
"Kwanini
ulikimbilia kuoa?"
"Nilihitaji
mtu wa kunisaidia katika matatizo yangu."
"Matatizo
yako, wewe ulikumbwa na matatizo gani?"
"Yale
uliyokuwa umeyasaidia kuyatengeneza. Kulala wawili haikuwa rahisi na hasa
ulipoamua kuondoka, tena bila kuaga nakuja kwenu haupo."
"Ulinichanganya
wewe nikawa sina la kufanya. Narudi hapa nakutafuta haupo naenda mahali nasikia
jina lako, natafuta habari zako naambiwa umeshaoa na una mtoto wa miaka 10
nikakimbilia Msumbiji."
"Ndio
umerejea nini?"
"Wapi
nikampata mtu akanipeleka Namibia, tumerejea hapa ninachofanya sikijui hii siku
ya tatu nakuja hapa."
"Hukijui
unachokitaka ? Hii ajabu sana haiwezi kutoka kwa Mariana."
"Mariana
wako amebadilika. Amekua lakini bado nakumbuka ulivyokuwa mtundu. Je nina
nafasi?"
"Nafasi
kwa mke wa mtu, tena mwambata wa kijeshi. Haa milio ya risasi bado
naikumbuka."
"Unapendeza
Richard. Sijakusahau. Ulinifanya niwe na amani sasa sina, niliondoka kwa
kukuogopa kwani ninapokuwa karibu nawe nahangaika sana, lakini sasa najua woga
wangu umenikosesha amani na furaha."
"Wewe
unayesema au mwingine."
"Ulijua
kuunga wali kwa tui la nazi. Ulijua hili la tatu , hili la pili na hili la
kwanza. Ulijua muda Richard, ulijua kuivisha. Ulijua mpaka aina ya ukoko
unaoutaka ukajua utandu unakaa muda gani. Na kila ninapokuwa na baba wa mtoto
wangu wewe ndiwe umejaa. Niondolee laana uliyoniwekea,"
"Nikuwekee
laana? Mimi au?"
"Haiwezekani
umenipa nini wewe. Mpaka miaka inapita lakini nakuona katika fasheni ile ile
tu. Hapa nilipo nishaharibikiwa. Nikuongeze bia."
"Hapana.
Nataka kuwa na akili zangu."
"Kwani
huwa zinachomoka?"
"Hii
pombe wewe si chai wala maji ya kunywa."
"Bado
man of Principle," alitabasamu, tabasamu lililomkera sana Richard ambaye
bila kujijua alikuwa nyuma miaka 20, mara tu baada ya kumaliza Tambaza.
Mwanamke wake wa kwanza kumpenda kikwelikweli.
"Tuache
hayo mbona unakuja ulevini?"
Itaendelea
COMMENTS