CCM YAWASAMBARATISHA UKAWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, YAZOA MAELFU YA VITI BILA KUPIGWA Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aki...
CCM YAWASAMBARATISHA UKAWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, YAZOA MAELFU YA
VITI BILA KUPIGWA
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya
viongozi wa CCM baada ya kuwasili katika mkutano wa kufunga kampeni za
Uchaguzi wa serikali za Mitaa za Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, leo jioni
Wana CCM wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
Wananchi wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
Nape akiwa Jukwaa Kuu pamoja na viongozi wa CCM baada ya kuwasili kwenye
mkutano huo
Lwiza Mbutu akiongoza bendi ya Twanga Pepeta kutumbuiza baada ya kuwasili
Nape kwe ye mkutano huo
Twanga akionyesha uhodari wa kuchezambele ya mza kuu
Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abilahi Mihewa akisalimia wananchi wa
Jimbo la Ilala waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa kufunga
kampeni za serikali za mitaa
Kada wa CCM Haji Manara akiwasalimu wakazi wa Jimbo la Ilala wakati wa
mkutano huo. wa kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa
uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru ambapo aliwaambia
wananchi hao kuwa jimbo la Ilala ni sehemu salama sana kwa CCM kwa kuwa
jimbo hilo lina historia ya CCM
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida akisalimia
wananchi wa Jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo wa kufunga kampeni za
uchaguzi wa serikali za mitaa jimbo la ilala uliofanyika kwenye makutano ya
mtaa wa Kongo na Faru.
Mbunge wa Jimbo la Ilala Azani Zungu akilonga jukwaani, ambapo aliwataka
watendaji wa serikali kuacha kuwabunghudhi mamalishe wa jimbo hilo kwa kuwa
ni eneo la biashara tu, hivyo watendaji hao watengeneze mazingira mazuri
badala ya timua timua ya mara kwa mara
Nape akihutubia kwenye mkutano huo
Nape akihutubia wananchi kwenye mkutano huo na ifuatayo ni habari kamili ya
alichosema
Na Bashir Nkoromo
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa
kesho, kikiwa kimeshajizolea maelfu ya nafasi ambazo wagombea wake wamepita
bila kupingwa.
Akihutubia kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi huo,
katika Mtaa wa Mtambani B, Kata ya Jangwani, jimbo la Ilala jijini Dar es
Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, kulingana na
takwimu CCM imepita bila kupingwa katika vijiji 2708, mitaa 644, na
vitongoji zaidi ya 26,300.
Alisema, CCM imeweza kupita bila kupigwa baada ya vyama vya upinzani
kushindwa kusimamisha kabisa wagombea na maeneo mengine kuweka wagombea
ambao walionekana kukosa sifa za kugombea baada ya kuwekewa pingamizi.
Nape alisema, hatua hiyo ya CCM kuingia kwenye uchaguzi huo ikiwa na mtaji
mkubwa wa nafasi ambazo wagombea wake amepita bila kupingwa ni dalili
tosha kwamba chama kitavibwaga vibaya vyama vya upinzani kuliko uchaguzi
uliopita mwaka 2009.
"Uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa CCM iliibuka na ushindi wa asilimia
96, sasa kutokana na dalili za mapema, uchaguzi wa safari hii sina shaka
kabisa kwamba wapinzani tutawapiga kwa ushindi wa asilimia mia moja",
alisema Nape.
Nape aliupongeza uongozi wa CCM katika jimbo la Ilala, baada ya
kumthibitibishia kwamba katika kipindi chote cha kampeni jimbo hilo
wamekuwa wakifanya kampeni za kistaarabu na wanao uhakika wa
kuibuka na ushindi kwa asilimia mia moja baada ya uchaguzi.
"Sina shaka kabisa kwamba hapa Ilala tutashinda kwa kishindo, mnastahili
kupata pongezi kutoka makao makuu kutokana na mlivyoendesha kampeni,
hongereni sana.". alisema Nape.
Alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kushinda lakini itafanya kazi ya
ziada ya kuhakikisha wapigakura waliojiandikisha wanapata fursa ya kwenda
kupiga kura bila kubughudhiwa na watu ambao huandaliwa na vyama vya
upinzani kufanya fujo ili kuzuia watu wasijitokeze kupiga kura.
"Nasema bila kificho, vijana wa CCM kama mtamuona mtu yeyote anajaribu
kufanya fujo wakati wa upigaji kura mshughulikieni kidogo kabla ya
kumpeleka polisi, maana watu wa aina hii wanabaka demokrasia, lazima
waadabishwe". alisema Nape na kuongeza.
"Vijana wa CCM lazima tuwe shupavu, maana kujifanya wanyonge unyonge huu
hautatusaidia chochote, na hili mimi sihamasishi fujo na si wa kwanza
kulisema hata Mwenyekiti wetu wa CCM alishasema kwamba unyonge basi. Sasa
mimi hapa napigilia msumari tu".
Nape aliwataka wananchi wa Ilala na Watanzania kwa jumla kuchagua wagombea
wa CCM, kwa kuwa ana uhakika ndio watakao watumikia vizuri.
Aliwataka viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi huo wa serikali za
mitaa kuhakikisha wanawatumikia wananchi, hasa kwa kusimamia kuondoa kero
zao na kusimamia misingi ya kuboresha mazingira ya shughuli mbalimbali
zikiwemo za biashara kama za mamalishe na machinga.
Nape alisema, CCM, itaendelea kusimamia na kutetea haki za wananchi hasa
walio wanyonge na si kwa sababu ya kutaka kura ila kwa sababu ni wajibu
wake kama chama kilichopewa ridhaa ya kutawala nchi.
Katika mkutano huo, Nape aliwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali katika
Mtaa huo wa Mtambani B, akiwemo mgombea wa nafsi ya Ueneyekiti wa mtaa huo,
Gungu Tambaza.
*...Sasa endelea na picha zaidi za mkutano huo*
Nape akimkaribisha jukwaani Gungu Mohamed Tambaza, mgombea wa Uenyekiti
mtaa wa Mtambani B ili kuomba kura kwa niaba ya wagombea wenzake wa jimbo
la Ilala wakati wa mkutano huo wa kufunga kampeni za serikali za mitaa
uliofanyika leo kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.
Nape akimsikiliza Gungu Mohamed Tambaza akiomba kura
Kada wa CCM Khamis Mkotya akimpongeza Nape wakati wa mkutano huo
Nape akimpongeza Haji Manara
Mkotya na Zungu
Mkotya na makada wengine wa CCM wakifuatilia
Shamrashamra uwanjani baada ya mkutano. Picha zote na Bashir
Nkoromo-theNkoromo Blog
COMMENTS