baadhi ya watoto wanaolelewa na vituo hivyo JESHI la Polisi Mkoani Dodoma limeviweka chini ya ulinzi vituo vitatu vya kulelea wato...
baadhi ya watoto wanaolelewa na vituo hivyo |
Kufuatia sakata hilo watu 115 wakiwemo watoto walikutwa wakiishi katika vituo hivyo.
Kwa mujibu wa majirani wa vituo hivyo watoto
hao walikuwa wakipatiwa mafundisho ya dini ya kiislam na kareti na wametoka
katika mikoa 14 nchini huku asilimia kubwa ya watoto hao wakitoka katika Wilaya
ya Kondoa mkoani Dodoma.
Juzi saa sita na nusu usiku polisi walifika katika eneo la kwanza na kukuta watoto 63 kati yao 46 wana umri chini ya miaka 18 ambapo wadogo kabisa wana umri chini ya miaka sita.
Kwenye kituo cha pili walikutwa watoto 40 ambapo kati yao walikuwa na umri chini ya miaka 18 ni 12 ambapo katika kituo cha tatu walikutwa watoto saba wenye umri chini ya miaka 18 walikuwa watano.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime alisema watoto idadi ya watoto waliokutwa katika vituo hivyo vitatu ni 63 na wenye umri wa miaka 18 -25 ni 52.
Alisema watoto hao wote ni wa kiume na wanatoka katika wilaya mbalimbali, ambapo Kondoa wanatoka watoto 50, Dodoma Mjini, Chamwino na Mpwapwa jumla yake watoto 26 na waliosalia wanatoka katika mikoa ya Kagera, Dar es Salaam, Kilimanjaro, Zanzibar, Tanga, Tabora, Singida,
pwani Lindi, Mtwara Geita, Mwanza na Manyara.
Pia watoto hao walikutwa wakiwa wamechanganywa bila kujali umri katika mazingira ambayo kiuhalisia ni hatarishi.
“Uchunguzi unaendelea na yoyote atakayeguswa na ushahidi kuwa amekiuka sheria atafikishwa mahakamani ikiwemo wazazi waliowaruhusu watoto. watoto hao kuwa katika uangalizi ambao si wa kutosha kama sheria ya watoto inavyotaka” alisema.
Kamanda Misime alisema Polisi pia wanachunguza ili kufahamu vijana hao walikuwa wakifundishwa kitu gani na kama walikuwa wakihudhuria shule kulingana na umri wana na sheria za nchi zinavyoelekeza.
Baadhi ya majirani
wakizungumza jana sharti la kutotajwa majina yao walisema wanashangazwa uwepo
wa kituo hicho ambacho kina idadi kubwa ya watoto.
Wengine walionesha kushangazwa na kituo hicho ambacho muda mwingi watoto huonekana wapo peke yao bila uangalizi wowote.
Walisema walianza kuwaona watoto hao tangu mwaka jana.
“Mwanzoni tuliona kama kawaida lakini kadri siku zinavyokwenda tunashangaa mambo yanayoendelea, watoto hawa muda mwingi unawaona wapo peke yao,wale wakubwa ndio wanaopika chakula kikishakuwa tayari wanaitana kisha wanakaa katika makundi makundi kula chakula” alisema.
"Yaani hapa hawa watoto wanaishi peke yao..,hawana muangalizi yeyote..,walimu wao wakishamaliza kuwafundisha tu ..,wanaondoka."alisema mkazi mmoja wa jirani na nyumba hiyo kwa sharti la kutotajwa jina lake
Mkazi huyo alisema,kinachoshangaza zaidi ni wakati ambao watoto hao hucheza michezo ya kupigana huku wakionesha kama wanafanya mazoezi.
"Kuna wakati utaona wanacheza mchezo wa kupigana...,sijui wanaita kareti...,yaani wanavyokuwa wanacheza...,wanaonekana kama wanafanya mazoezi fulani hivi..,na hapo kwa mimi binafsi ndipo panaponitia hofu."
Mkazi mwingine anayoishi jirani na kituo hicho alisema,yeye hashangai kuwepo kwa watoto hao kwenye nyumba hiyo,isipokuwa alisema,hali ya mazingira katika nyumba hiyo siyo ya kuridhisha.
"Watoto kuwepo katika kituo hicho siyo shida,changamoto iliyopo katika kituo hicho ni mazingira...,kwa kweli mazingira ni mabaya na machafu hayafai kuwaweka watoto hao..,hii inaweza kuwasababishia mlipuko wa magonjwa yakiwemo ya kuhara."
Vile vile mkazi huyo alisema,pia kituo hicho hakijakidhi hatua ya kutunza watoto hao kwa kuwa hakuna msimamizi maalum wa kuwafundisha masuala ya nidhamu na kusababisha watoto hao kutokuwa na nidhamu kama Dini ya kiislamu inavyotaka.
Pia watoto hao wamekuwa wakilala chini kwenye mikeka na wengine hutandika nguo huku kukiwa na magodoro machache.
Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo,Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajab alisema hakuna dhambi yoyote kwa watoto hao kulelewa katika kituo hicho na akisema hayo ni mafunzo katika madrasa ambayo harakati zake zilianza zamani ulimwenguni kote.
"Madrasa zilianza zamani... polisi haina Mamlaka ya kufunga madrasa labda kama watakuta kuna tatizo lolote la kuhatarisha amani."alisema sheikh Rajab.
Kuhusu suala la kusoma shule,sheikh huyo alisema kuwa suala hilo linamuhusu mzazi na mtoto wake.
"Suala la mtoto kwenda shule ama kutokwenda hilo linamhusu mzazi na mwanawe,maana yeye ndiye anayeamua ampeleke mwanae kwenye taaluma gani...,ya dini ama ya kidunia,”
Kuhusu mazingira ya eneo hilo kutoridhisha Sheikh Rajab alisema,hawezi kulizungumza suala hilo kwa kuwa kuna wanamazingira wanaopaswa kuliona na kulizungumzia.
"Mimi Siwezi kuzungumzia suala la Mazingira... wanamazingira wapo na wao ndio wanaopaswa kulizungumzia suala hilo..,kama hayaridhishi basi waambiwe na kupewa muda wa utekelezaji ...,wasipotekeleza ndipo hatua zichukuliwe." alisema Sheikh Rajab.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Nkuhungu aliyefahamika kwa jina moja la Ponela alisema,alikuwa akiwaona watoto katika nyumba hiyo lakini hakuuliza chochote kwani aliamini ule ulikuwa ni uhuru wa Kuabudu.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Betty Mkwassa alisema amesikitishwa na hali ya mazingira waliyokuw wakiishi watoto hao.
“Lazima sheria ichukue mkondo wake” alisema.
Akihojiwa jana
Katibu wa Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata) Hassan Kuzungwa alisema baraza
limesikitishwa sana na uwepo wa vituo hivyo.
Tangu walikuwa wakisali wakifanya mazoezi huku wakijitenga na majirani wanaowazunguka.
COMMENTS