Ambao hawajarejesha fomu kuwania Urais CCM ni 9

Ikiwa leo ni siku ya mwisho kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kurudisha fomu kwa ajili ya mchakato wa kuteuliwa kupeperusha be...


Ikiwa leo ni siku ya mwisho kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kurudisha fomu kwa ajili ya mchakato wa kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama ni wanachama 33 wamefanikiwa kurudisha fomu hizo makao makuu ya CCM.

Jumla ya wanachama 42 walichukua fomu hizo ambapo walitakiwa kuwa na wadhamini 450 ambao watapatikana katika mikoa 15 ikiwemo mikoa mitatu ya Zanzibar.

Ni wanachama tisa waliobaki ambapo wanatakiwa kurejesha fomu hizo ambapo mwisho wake ni saa 10 kamili jioni.

Wagombea hao ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na teknolojia, January Makamba, Mbunge wa Sengerema William Ngeleja, Godwin Mwapongo, Balozi Patrick Chokala, na Peter Nyalile.

Wengine ni Ritha Ngowi, Helena Elinewinga, Anthony Chalamila and Sonoko Banda. Hata hivyo katibu wa Sekteratieti Organaizesheni  wa CCM, Mohamed Seif Khatib alisema hakuna adhabu kwa mtu ambaye atashindwa kurudisha fomu.

Miongoni mwa wanachama waliorudisha fomu jana ni Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa.

Lowasa alisema amedhaminiwa na wadhamini 879,000 na kutaka wote wanaomtuhumu kwa ufisadi kuacha mara moja.

Alisema ikiwa atateuliwa kuwa Rais atahakikisha anatumia raslimali zote kwa faida za Watanzania.

Alisema kwa bahati mbaya watu ambao wanakosa hoja, wamekuwa wakiwatuhumu wenzao kwa vitu ambavyo havina ukweli wowote.

“Nataka nitumie nafasi hii kwa wale wote ambao wamekuwa wakinituhumu kwa miaka kadhaa sasa na kunihusisha na suala zima la rushwa kuwaambia waache mara moja kwani hakuna hata chembe ya ukweli wa maneno hayo” alisema.

Alisema kwa yeyote mwenye ushahidi wa tuhuma hizo za kipuuzi, autoe, aeleze kwa ushahidi rushwa yoyote inayomhusu.

“Aseme nimechukua rushwa lini, kwa nani, kwa lipi na kwa kiasi gani” alisema Pia alisema tofauti na maeneo yanayosemwa kwamba amehonga hakuna mdhamini yoyote aliyehongwa.

“Hayo ni maneno ambayo ni upuuzi tu na wanaonituhumu kwa ufisadi waache mara moja.” Alisema.

Alisema majungu kwake sasa yametosha na ikiwa atateuliwa basi ataongoza nchi kwa haki.

Alisema maelfu ya wana CCM walijitokeza kumdhamini  katika mikoa yote aliyofika .

“Mafanikio haya ya awali ni ishara njema kuelekea hatua zilizobaki na kwa uwezo wa mwenyezi Mungu na kwa ushirikiano kwa pamoja tutavuka daraja ili hatimaye kuwatumikia kwa utumishi uliotukuka nikiwa Rais wa awamu ya tano” alisema.

Alisema ana shahuku kubwa kuunganisha uwezo wa kila Mtanzania katika kupambana na umaskini wa nchi,umaskini wa watu siyo amri ya Mwenyezi Mungu kwani kwa pamoja raslimali tulizonazo kwa bidii,
maarifa na ufanisi zaidi ili kuutokomeza umaskini.

“Ni lazima sasa tufike mahali tuseme imetosha, majungu yametosha, upotoshwaji umetosha, rushwa imetosha na kwa pamoja tunaweza kukomesha haya, tutayakomesha kwa kusimamia ukweli, uadilifu, uaminifu na kutenda kwa haki” alisema.

Hata hivyo waandishi wa habari hawakupewa nafasi ya kumuuliza maswali kutokana na muda aliokuwa ametengewa kuisha.

Dk Asha Rose Migiro
Mwanachama mwingine aliyerudisha fomu jana ni Dk Asha-Rose Migiro ambaye alisema hayuko tayari kuzungumza na waaandishi wa habari.

Eldefonce Bilohe
Pia Mkulima kutoka Kigoma, Elfonce Bilohe naye alirejesha fomu akikishukuru chama kwa demokrasia iliyoionyesha.
Bilohe alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurudisha fomu.
Alisema yeye ni mkulima lakini amepata nafasi ya kushiriki katika kinyang'anyiro hicho kitendo ambacho kweli kimeonyesha kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi.
Akizungumzia zoezi la kutafuta wadhamini amesema limeenda vizuri na amekabidhi idadi ya wadhamini waliohitajika kutoka katika mikoa 15 kama chama kilivyotaka.
Alisema alikutana na changamoto ya kuombwa rushwa.
“Changamoto kubwa sana ambayo nimekutana nayo katika kuwapata wadhamini ni baadhi ya watu kuniomba kitu kidogo kama maji ya kunywa” alisema

Waziri Nyalandu
Mwingine wa CCM aliyerudisha fomu jana ni Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu .
Akizungumza na waandishi wa habari alisema ana imani na Watanzania na yupo tayari kuhakikisha CCM inashika dola  mwaka 2015.
Alisema kila alipokuwa akipita ameona watu wakiwa na mapenzi makubwa na chama chao na hiyo ni ishara kuwa bado wana imani na chama chao. Akizungumzia kuhusu umoja uliopo katika Taifa alisema alisema  kuwa ni lazima kuhakikisha tunu hiyo inalindwa na kuenziwa na kusisitiza kuwa
ni lazima kupiga vita ubaguzi wa aina yoyote.

Luhaga Mpina
Kwa upande wake mbunge wa Kisesa  Luhaga Mpina alisema ametembelea mikoa 17 na kusema zoezi lililenda vizuri.
Alitoa ushauri kwa CCM kuweka mdahalo kwa wagombea wote wa nafasi ya urais ili kujua nini ambacho watakifanya kwa Watanzania.
kusema kuwa hana presha na wagombea 42 ambao wamekwishachukua fomu na anaamini kuwa itashinda.
Alisema anaamini jina lake litakuwwepo katika tatu bora kwa wale watakaoteuliwa na chama.

Malick Malupu
Mwanachama mwingine aliyerudisha fomu ni Malick Malupu, mwanafunzi wa shahada ya uzamili ya utumishi wa umma Chuo kikuu cha mzumbe alirudisha fomu  aliwataka wagombea wenzake kuwa
makini na wapambe wao kwani wanaweza kusababisha mtafaruku au mgongano
baina yao.
Alisema kama kuna mtu anamuabudu mgombea aachane na chama.
“Ukiona mtu anakatwa jina lake akalalamika ujue ameingia kwa hujuma au kwa njia ya ubatili pamoja na kutoa rushwa” alisema

Dk Hamisi Kingwangala
Mbunge wa Nzega Dk Hamisi Kingwangala naye alirudisha fomu na kusema amefanikiwa kupata wadhamini kama ilivyo agizo la chama. Alisema atahakikisha anashughulikia suala la rushwa na ufujaji wa fedha za umma.

Hadi taarifa hii inaandikwa wagombea ambao wamerudisha fomu na wanasuburi kuingia kwenye mchakato wa kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa Rais Oktoba 25, mwaka huu ni Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta, Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal, Makongoro Nyerere, Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli, Waziri wa Kilimo na Ushirika Stephen Wassira, Balozi Ali Abeid Karume, Waziri wa Mifugo Dk Titus Kamani na Boniface Ndengo,
Wengine mi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe, Profesa Sospeter Muhongo, Balozi Amina Salum Ally, Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani, Leonce Mulenda, Waziri asiye na Wizara maalum Profesa Mark Mwandosya, Waziri Mkuu Mizengo Pinda Pia wamo Waziri wa Afrika Mashariki Dk Harrison Mwakyembe, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa.

Wengine ni Waziri wa Katiba na sheria Dk Asha Rose Migiro, Monica Mbega , Dk Mwele Malecela, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe,  Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.

 Wengine ni Mbunge wa Nzega, Mbunge wa Nzega Dk. Hamis Kigwangala, Dk Hans Kitine,  Balozi Augustino Mahiga,na mkulima kutoka kijiji cha Mjimtala Kasulu Kigoma, Eldefonce Bilohe,
Pia Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina, Amos Siyantemi, Mwanafunzi wa Chui Kikuu Mzumbe, Amos Robert na Maliki Malupu.

Source: Sifa Lubasi, Dodoma


COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Ambao hawajarejesha fomu kuwania Urais CCM ni 9
Ambao hawajarejesha fomu kuwania Urais CCM ni 9
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2015/07/ambao-hawajarejesha-fomu-kuwania-urais.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2015/07/ambao-hawajarejesha-fomu-kuwania-urais.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy