Bloga wa mtandao wa modewjiblog.com, Andrew Chale akiwa katika geti kuu la kuingilia ofisi za Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa zilizopo eneo la...
Bloga wa mtandao wa modewjiblog.com, Andrew Chale akiwa katika geti kuu la kuingilia ofisi za Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa zilizopo eneo la Mang'ula, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro, Tanzania.
TABIANCHI KUANGAMIZA HIFADHI
Na Mwandishi Wetu, modewjiblog
[TANZANIA] Zimebaki siku takribani 60, kuelekea mkutano mkuu wa 21 (COP21) wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya tabia Nchi (UNFCCC) unaotarajiwa kufanyika Paris, Ufaransa. Mkutano huo umepangwa kufanyika mwanzoni mwa Desemba mwaka huu.
Wakati mkutano huo unafanyika Taarifa za kitafiti zinaonesha kwamba katika nchi zitakazokumbwa na mabadiliko ya tabia nchi, Tanzania ni miongoni mwao hasa maeneo ya hifadhi za taifa na mbuga zake.
Imeelezwa kuwa idadi kadhaa za wanyama zitatoweka.
Hivi karibuni, mwandishi wa Makala haya, alitembelea Hifadhi kadhaa za taifa zilizo chini ya usimamizi wa Shirika la Hifadhi la Taifa, (TANAPA) za Udzungwa, Selous Game Reserve, Mikumi, Ruha, na Saadan na kufanya mazungumzo na wataalamu wa mabadiliko ya tabianchi kwenye idara za serikali na watu binafsi.
Eneo la kuingia katika Hifadhi na makao makuu ya hifadhi ya Udzungwa...
Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa:
Kwa mujibu wa tovuti ya Serikali Udzungwa ni miongoni mwa milima yenye Bayoanuwai nyingi iliyofunikwa na misitu.
Pamoja na uzuri wake Udzungwa ni miongoni mwa Hifadhi zilizo kwenye hatari ya kutoweka kutokana na kuwapo na mipango hafifu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Vyanzo vya ndani vinaeleza kuwa, ili kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabianchi, juhudi za haraka zinahitajika kuchukuliwa ikiwemo wasimamizi na wananchi wanaozunguka hifadhi kupewa elimu ya kutosha pamoja na mipango kazi ya mara kwa mara.
Bwana Ruambano Mnege (56) mkazi wa kijiji cha Msolwa katika eneo jirani na hifadhi ya Udzungwa anaeleza kuwa, hafahamu maana ya mabadiliko ya tabianchi, ila anachoelewa ni kuwa mambo yanabadilika pindi Mungu anapoamua.
"Mimi natambua Mungu anapoamua ndio mambo yanatokea. Suala la mabadiliko ya tabianchi kwa sie wa huku hasa wakulima hatutambui sana kwa sababu hatuna elimu ya kutosha” alibainisha Mnege akijibu maswali endapo wasimamizi wa hifadhi hizo kama wanawashirikisha wananchi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Kauli yake ni moja ya miongoni za kauli nyingi zinazoonesha watukutokuwa na elimu ya kutosha katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Hali hiyo pia inabainishwa ukataji miti hovyo pamoja na kuharibu vyanzo vya maji, kuchoma moto misitu pamoja na kuwinda wanyama.
"Kulikuwa na wanyama wakifika hadi kwenye mashamba yetu miaka ya nyuma. Lakini kwa sasa wanyama wale hawafiki kabisa kutokana na hali ilivyo huenda wamepotea” anaeleza Bi. Jonesia Simon mkazi wa Sanje ambapo anasema kutoonekana kwa wanyama hao kwa hivi sasa kumechangiwa na mabadiliko ya tabianchi kwani kulikuwa na wanyama waliokuwa wakifuata maji na wengine walikuwa wakifuata vyakula kwenye mashamba hayo lakini kwa sasa wametoweka kabisa.
Mwandishi wa makala haya, Andrew Chale wa modewjiblog.com akiwa katika eneo la Sanje, Udzungwa (Picha na modewjiblog team).
ramani inayoonyesha hifadhi hiyo ya Udzungwa..
Milima ya udzungwa ni hifadhi inayopatikana ndani ya Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro pamoja na upande wa Iringa. Milima hii ni makazi ya wanyama pori wa aina mbalimbali huku ikiwa na ukubwa wa kilometa 1990.
Udzungwa ni miongoni mwa hifadhi zenye hazina ya aina nyingi za mimea, ndege na wanyama ambao hawapatikani katika sehemu nyingine duniani.
Hifadhi iko umbali wa kilometa 350 kusini mwa Dar es Salaam, kilometa 65 kutoka katika Hifadhi ya Mikumi ambayo ni ya jirani kabisa.
Kati ya aina sita za jamii ya nyani wanaopatikana katika hifadhi hii, mbili hupatikana katika hifadhi hii pekee ambao ni : Mbega Mwekundu, wa Iringa (Iringa red colobus monkey) na aina ya pili ni Sanje Crested mangabey.
Huku kukiwa na aina mbalimbali za ndege kuna aina nne za ndege ambao hazikufahamika hadi katika miaka ya karibuni. Ndege hao ni Chozi bawa jekundu (rufous-winged sunbrid) na wengine wengi akiwemo kwale wa Udzungwa.
Hifadhi hii pia ni moja ya makazi makuu na muhimu ya ndege pori barani Afrika.
Picha ya juu Maporoko hayo na chini ni Mwandishi wa makala haya wa modewjiblog.com, Andrew Chale. (Picha na modewjiblog team).
Mwandishi wa makala haya wa modewjiblog.com, Andrew Chale akiwa katika eneo la awali la mapumziko baada ya safari ndefu ya kupanda mlima (Picha na modewjiblog team).
Maporomoko ya Sanje:
Ndani ya hifadhi hii pia kuna Mto Sanje ambao ni kivutio kikubwa sana. Mto huu una maporomoko ya maji yenye urefu wa mita zipatazo 170 yakianguka kupitia msituni na kusababisha ukungu bondeni.
Hata hivyo, mbali na kuwa na vitu vyote hivyo ndani ya hifadhi hii ya Udzungwa, Serikali na jamii inayozunguka hifadhi hii inawajibu mpana wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwani wasipochukua hatua hifadhi itatoweka na kila kitu chake.
Wanyama kutoweka:
Tovuti ya Serikali ya Makamu wa Rais (http://www.vpo.go.tz/news), imebainisha kuwa asilimia 34 ya ardhi ya Bara la Afrika iko katika hatari ya kugeuka jangwa kutokana na mabadiliko ya TabiaNchi.
Na kuongeza kuwa hali hiyo ya mabadiliko ya TabiaNchi itachangia kutoweka kwa asilimia kati ya 25 hadi 40 ya aina fulani za wanyama katika hifadhi Barani Afrika ifikapo mwaka 2020 na kwamba maeneo kame yataongezeka kwa asilimia 5 hadi 8 Barani Afrika ifikapo mwaka 2080.
Msemaji wa TANAPA:
Hata hivyo suala la mabadiliko ya tabianchi katika hifadhi za Taifa nchini bado halijapewa kipaumbele kikubwa hasa kwa wadau wa mabadiliko ya tabianchi ikiwemo wanahabari, wanaharakati wa mazingira na wananchi wanaoishi jirani na hifadhi.
Mwandishi wa makala haya akiwa katika view point ya maporomoko.
Taswira ya eneo la maporomoko ya Udzungwa inavyoonekana unapokuwa katika eneo la awali la View Point ndani ya Hifadhi hiyo ya Udzungwa.
eneo la maji yanayotoka kwenye maporomoko.
Miongoni mwa aina za ndege wanaopatikana ndani ya hifadhi hizo ya Udzungwa.
Miongoni mwa miti inayopatikana ndani ya misitu hiyo ya Hifadhi ya Udzungwa..
Miongoni mwa miti inayopatikana ndani ya Hifadhi hiyo ambayo hata hivyo bado inakabiliwa na changamoto kwa watu wasio na mapenzi mema kuvamia na kukata miti hiyo ya hifadhi kwa ajili ya shughuli za mbao na mambo mengine.
Miongoni mwa miti ambayo inapatikana ndani ya hifadhi hiyo ambayo ni dawa na pia ni miongoni mwa miti inayopendwa na wanyama hata hivyo ipo katika changamoto ya kutoweka...
Red Col wanaopatikana ndani ya Misitu hiyo ya Hifadhi ya Udzungwa..
Mwandishi wa makala haya wa modewjiblo, Andrew Chale akiwa katikati ya Hifadhi hiyo.
Misitu hiyo ya Udzungwa inavyoonekana..
Itaendelea ripoti sehemu ya Pili…
Makala haya yamefadhiliwa na kwa ufadhili wa Shirika la ( CFI) la nchini Ufaransa, chini ya mradi wa Medias 21 Africa & Asia.
COMMENTS