MO APATA TUZO NYINGINE, ADHIHIRISHA TAMAA YA KUWATUMIKIA WATANZANIA
HomeHabari

MO APATA TUZO NYINGINE, ADHIHIRISHA TAMAA YA KUWATUMIKIA WATANZANIA

Mfanyabiashara maarufu ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akitembea kwenye 'Red Carpet' m...

Mfanyabiashara maarufu ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akitembea kwenye 'Red Carpet' mara baada ya kuwasili katika hotel ya Hilton Sandton jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwenye hafla ya utoaji tuzo iliyoandaliwa na jarida maarufu la Forbes na kutunukiwa tuzo ya "Forbes Africa Person Of the Year 2015".(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Modewjiblog team

MFANYABIASHARA na mtu mwenye taasisi ya kusaidia jamii, Mohammed Dewji maarufu kama Mo ametunukiwa tuzo ya jarida maarufu la Forbes ya "Forbes Africa Person Of the Year 2015" katika hafla iliyofanyika Novemba 27 mwaka huu jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Mfanyabiashara huyo pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises T Ltd (MeTL Group) kampuni iliyoanzishwa na na baba yake katika miaka ya 1970 ambayo sasa imekua na kujikita katika viwanda vya nguo, usagaji nafaka, utengenezaji wa vinywaji baridi, usindikaji wa mafuta ya kula, usindikaji wa chai na kuendesha mashamba ya mkonge ambapo tayari anashea ya asilimia 40 ya soko.

Mo ametwaa tuzo hiyo kwa kuwashinda watu watano mashuhuri barani Afrika. Watu hao ni Nkosazana Dlamini Zuma, mke wa Kwanza wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma. Mama huyo kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU). Mwingine ni Rais wa sasa wa Nigeria, Muhammadu Buhari aliyetambuliwa kutokana na kuanzisha vita dhidi ya rushwa nchini mwake.

Aidha wapo Arumna Otei, mchumi mahiri raia wa Nigeria ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia. Pia alikuwemo Mwandishi maarufu wa vitabu wa Nigeria, Chimanda Ngozi Adichie ambaye moja ya vitabu vyake vinaelezea picha halisi ya Afrika inavyofikiriwa duniani.

Akitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa kwa tuzo hiyo Mo, alisema anatoa tuzo hiyo kwa vijana wa Kitanzania kwani ndio nguvu kazi inayobeba uchumi wa nchi.

Mo ambaye kampuni yake ya MeTL inaongoza kwa kutoa ajira nchini, ikiwa imetoa ajira 26,000 kote katika viwanda vyake 31 vilivyopo nchini na katika mataifa matano ya Afrika, alisema amefurahishwa na tuzo hiyo ambayo anaitoa kwa vijana kwa kutambua pia wajibu mkubwa walionao katika kukabiliana na umaskini.

IMG_3317

Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akifurahi jambo na baadhi ya wageni waalikwa nje ya ukumbi wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyoandaliwa na jarida la Forbes.

Alisema ajira 26,000 zimegusa watu wengi nchini na kwamba ana matumaini makubwa ya siku za usoni kutoa ajira zaidi kutokana na biashara zake kuendelea kukua.

"Heshima yangu kubwa haitokani na utajiri, maana kama utajiri wako hauna msaada wala kugusa watu masikini hauna maana yeyote, hivyo basi heshima hii ni kutokana na kwanza bidhaa zangu kugusa maisha ya watu kila siku kuanzia sukari na majani ya chai asubuhi pamoja na unga wa ngano, lakini pia chakula cha mchana kwa unga wa sembe, mafuta ya kupikia na maji ya kunywa, bidhaa zote hizo za Mohammed Enterprises zinagusa maisha kila nyakati katika siku.

"Nina viwanda 31 ambavyo vimekuwa vikitengeneza bidhaa za Kitanzania na kuziuza kwa Watanzania kwa bei yenye unafuu mkubwa, mathalani tunauza maji kwa bei chini ya dola moja kwa shilingi za Kitanzania 200, hakuna hata Ulaya, nina kiwanda cha khanga na vitenge ambacho malighafi zake zote ni za Kitanzania, hivyo kuna kusaidia serikali kwa kulipa kodi ipasavyo, lakini pia kusaidia moja kwa moja ajira za Watanzania walio wengi ambao tatizo lao kubwa katika kundi la vijana ni ajira"

Alitumia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza baba yake kwa kumwita mjasiriamali shujaa ambaye alitoka kuanzia dereva wa malori baada ya kuhitimu kidato cha nne mwishoni mwa miaka ya 1960 hadi kufikia ubilionea. Alisema alipata maono ya utajiri hasa kutoka kwa baba yake huyo aliyekuwa akimshirikisha biashara tangu akiwa mdogo.

“Mwanaume mwenye ndoto huhitaji mwanamke mwenye maono. Na nimebarikiwa mwanamke ambaye kwa miaka 15 amekuwa akinipa sapoti isiyoyumba.

IMG_3362

Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akibadilishana 'Business card' na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo.

“Saira, nina shukurani nyingi kwako kwa kuwa nguzo ya familia yetu, mama wa heshima kwa watoto wetu watatu,” alisema Mo kwenye hafla hiyo.

Kwa utulivu, Mo alisema: “Baba, zawadi kubwa ambayo ulinipa katika maisha yangu ni muda wako, na kwa hilo nitakuwa mwenye deni la shukurani kwako siku zote za maisha yangu.”

Mo ambaye moyo wake wa binadamu ulimfanya awanie uwakilishi Jimbo la Singida Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kushinda nafasi hiyo na hivyo kuwawakilisha wanasingida kuanzia 2005 na 2015 amesema maisha ni changamoto kubwa inayobadilishwa kwa utumishi wenye nia ya dhati kwa umma.

Alisema alipowania uwakilishi alikuwa na sababu: “Nilikuwa na umri wa miaka 24, nilikwenda Singida kutoa heshima kwenye kaburi la marehemu babu yangu. Sikuwa nimefika huko tangu nilipoondoka nikiwa na umri wa miaka mitatu.

“Nilipokuwa njiani, nilimuona mzee akiwa na maji yenye rangi ya njano, machafu ambayo aliyatumia kwa kunywa. Nilishangaa, maana hali ile sikuwahi kufikiri kama ipo vile. Kipindi hicho nilikuwa nimemaliza Chuo Kikuu cha Georgetown, Marekani.”

Mo anasema kuwa aliingiwa na hisia kutaka kujua nini hasa alichokuwa anahitajika kufanya, alimfuata yule mzee aliyekuwa na maji yale, alipozungumza naye, aliwazungukia watu wengine na kuridhika kuwa ile ndiyo hali halisi, hapo ndipo fikra ya kwa nini agombee ubunge ilipoanzia.

Anasema kuwa baada ya kujiridhisha hivyo, alirudi kwa mzee wa kwanza, alizungumza naye na kumuuliza ni kwa nini shida ile ilikuwa haizungumzwi kwa upana katika mamlaka husika.

IMG_3434

Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji pamoja na ujumbe wake alioambatana nao kutoka Tanzania.

“Nilipojitambulisha yule mzee alisema anamkumbuka babu yangu, kisha akanishauri nigombee ubunge, alinisisitiza mno ili nisaidie kuondoa lile tatizo la watu wa Singida kunywa maji machafu,” alisema Mo.

Anaeleza kuwa alipokuwa njiani kurejea Dar es Salaam, alilifikiria tatizo hilo kwa mapana zaidi, akalifanyia utafiti na kubaini kwamba katika kila watu 10, watatu walikuwa wakipoteza maisha kutokana na maradhi yanayosababishwa na maji machafu.

Anaendelea kusema kuwa aligundua kuwa Singida kulikuwa na tatizo kali la maji safi na salama. Anasema kuwa alibaini uwepo wa tatizo la elimu kuhusu matatizo ya maji.

Jambo lingine ambalo anasema aliligundua ni uwepo wa tatizo la huduma za afya. “Niliwafikiria watoto wangu, jinsi ninavyowapenda, na namna ambavyo kila mzazi anavyompenda mwanaye. Nilipingana na hali kuwa watoto wa Uingereza na Marekani wamependelewa zaidi. Maisha ni sawa bila kujali chochote,” anasema Mo.

IMG_3359

Sehemu ya ujumbe kutoka Tanzania uliombatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji kwenye hafla hiyo.

“Niliona lazima nitimize wajibu wangu. Kutimiza malengo yangu ya kusaidia jamii, kufanikiwa katika biashara. Mambo hayo mawili hisani na biashara nimeyaweka pamoja na ndiyo maana nimefika hapa leo, tunajivunia sana kuitwa METL nembo ya Watu. Katika miaka yangu 10 kama mbunge, nimefanya mabadiliko mengi. Nilikuwa na sababu ya kupata mkopo nafuu wa dola milioni 35, ambao ulisababisha kuwekwa kwa miundombinu ya maji safi na salama Manispaa ya Singida.

“Niliitumia MeTL, tuliweza kudhamini shughuli nyingi za maendeleo ya kijamii. Kuhusu elimu, nilifanikisha kujenga shule 15, zikawa 17, kabla ya hapo tulikuwa na shule mbili tu. “Kuhusu huduma za afya, hapa nimshukuru mke wangu kwa jitihada zake. Alikuwa Mwenyekiti wa taasisi ya Tumaini la Maisha ambayo imekuwa ikisaidia watu wengi, hasa watoto dhidi ya maradhi ya saratani.”

IMG_3469

Burudani mbalimbali zikiendelea ukumbini hapo.

IMG_3548

Mkurugenzi Mtendaji wa Jarida la Forbes Afrika, Sid Wahi akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa. Kulia ni Head of Events wa ABN Productions, Alexander Leibner.

DSC_4663

Mwanzilishi na mchapishaji wa jarida la Forbes Afrika, Bw. Rakesh Wahi ( wa pili kushoto) akikamkabidhi Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji (wa pili kulia) tuzo ya Heshima Barani Afrika "2015 Forbes Africa Person of the Year" iliyotolewa na Jarida la Forbes Afrika kwa kutambua mchango wake katika kusaidia jamii ikiwemo kutoa ajira kwa zaidi ya watu 26,000 nchini na mambo mengine yanayoigusa jamii. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Forbes Afrika, Sid Wahi (kulia) na MEC Panyaza Lesufi kutoka kitengo cha elimu, Gauteng Province (kushoto).

IMG_3780

Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa kwa tuzo, alisema anatoa tuzo hiyo kwa vijana wa Kitanzania kwani ndio nguvu kazi inayobeba uchumi wa nchi.

IMG_3776

IMG_3825

MO akiteta jambo na Mchumi mahiri raia wa Nigeria ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Arunma Oteh (kulia) ambaye walikuwa pamoja kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hiyo ambapo pia alimpongeza sana.

IMG_3849

Pichani juu na chini MO akiendelea kupongezwa na wadau mbalimbali walioalikwa kwenye hafla hiyo.

IMG_3866

IMG_3875

Pongezi kwa MO zikiendelea kutolewa.

IMG_3889

IMG_3857

MO katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Jaguar Land Rover ambao ni miongoni mwa wadhamini wa sherehe za tuzo hizo.

IMG_3940

MO katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Makampuni ya MeTL Group, Vipul Kakad mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.

IMG_3925

Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na Shemane Amin wakipitia moja ya taarifa iliyowavutia kwenye jarida la Forbes Afrika.

IMG_3911

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Jaguar Land Rover ya Afrika Kusini wakipozi kwenye 'Red Carpet'.

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,313,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,246,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,Habari,5017,habari dodoma,20,habari. dodoma,31,habaria,1,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,514,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,352,muziki na fasheni,6,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,2,SAYANSI ANGA,2,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,2,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: MO APATA TUZO NYINGINE, ADHIHIRISHA TAMAA YA KUWATUMIKIA WATANZANIA
MO APATA TUZO NYINGINE, ADHIHIRISHA TAMAA YA KUWATUMIKIA WATANZANIA
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/11/IMG_3351.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2015/11/mo-apata-tuzo-nyingine-adhihirisha.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2015/11/mo-apata-tuzo-nyingine-adhihirisha.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy